12.04.2023 Views

Kupinga ya Kiprotestanti

You also want an ePaper? Increase the reach of your titles

YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.

Kupinga ya Kiprotestanti

Sura 13. Katika Uholandi na Scandanavia

Katika Uholandi ukali wa Papa ukaleta haraka upinzani. Miaka mia saba kabla ya Luther,

askofu wa Roma kwa uhodari akashitakiwa na maaskofu wawili, waliotumwa kuwa mabalozi

huko Roma, wakajifunza tabia ya kweli ya “jambo takatifu la askofu”; “Unakaa mwenyewe

ndani ya hekalu la Mungu; baada ya mchungaji unakuwa mbwa mwitu kwa kondoo, ... lakini

ulipashwa kuwa mtumishi wa watumishi, kama upendavyo kujiita mwenyewe, unatumaini

kuwa bwana wa mabwana. ... Unaleta haya kwa amri za Mungu.”

Wengine wakatokea katika karne zote kukariri kukataa huku. Biblia ya Wavaudois

ilitafsiriwa katika lugha ya Kijeremani. Wakatangaza “kwamba hapo kulikuwa faida ndani

yake; hakuna mizaha wala uongo, wala mambo ya michezo, wala udanganyifu, bali maneno

ya kweli.” Ndivyo waliandika rafiki za imani ya zamani tangu karne ya kumi na mbili.

Sasa wakati wa mateso ya kanisa la Roma ikaanza; lakini waaminifu wakaendelea

kuongezeka, kutangaza kwamba Biblia ni mamlaka pekee ya haki katika dini na kwamba

“hakuna mtu anayepashwa kushurutishwa kuamini, bali angepashwa kusadikishwa kwa njia

ya mahubiri.”

Mafundisho ya Luther yakapata katika Uholandi watu wa juhudi na waaminifu kwa

kuhubiri injili. Menno Simons, mtu wa elimu mkatoliki na aliyetakaswa kwa upadri, alikuwa

mjinga kabisa wa Biblia na hakuisoma kwa ajili ya hofu ya upinzani wa ibada ya dini. Kwa

ondoleo la zambi akajitahidi kunyamazisha sauti ya zamiri, lakini bila manufaa. Baada ya

wakati akaongozwa kujifunza Agano Jipya; hili pamoja na maandiko ya Luther ikamletea

kukubali imani ya matengenezo. Kwa mda kitambo akashuhudia mtu aliyeuawa kwa sababu

alibatizwa mara ya pili. Jambo hili likamwongoza kujifunza Biblia kwa ajili ya ubatizo wa

watoto wadogo. Aliona kwamba toba na imani vinahitajiwa kuwa sababu ya ubatizo.

Menno akatoka kwa kanisa la Roma na akajitoa wakfu kwa kufundisha maneno ya ukweli

aliyokubali. Katika Ujeremani na Uholandi kundi la washupavu likatokea, kuharibu kanuni

na adabu, na kuendelea kufanya maasi. Menno kwa nguvu zake zote akapinga mafundisho ya

uongo na mashauri ya ushenzi ya washupavu. Kwa miaka makumi mbili na tano akapitia

Uhollande na upande wa kaskazini ya Ujeremani, kutumia mvuto mkubwa sana, kufananisha

katika maisha yake mwenyewe mafundisho aliyofundisha. Alikuwa mtu wa haki, mpole na

mtulivu, mwaminifu na mwenye bidii. Hesabu kubwa ya watu wakageuka sababu ya kazi

zake.

Katika Ujeremani Charles V alikomesha Matengenezo, lakini watawala wakasimama

kama boma juu ya utawala wa ukaidi wake. Katika Uhollande mamlaka yake ilikuwa kubwa

sana. Amri za mateso zikafuatana kwa upesi. Kwa kusoma Biblia, kuisikia ao kuihubiri,

kumwomba Mungu kwa siri, kukataa kusujudu mbele ya sanamu ao kuimba Zaburi ilikuwa

azabu ya kifo. Maelfu waliangamia chini ya Charles na Philip II.

93

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!