24.03.2017 Views

MWONGOZO WA UWEKEZAJI MKOANI SIMIYU

mwongozo-simiyu

mwongozo-simiyu

SHOW MORE
SHOW LESS

You also want an ePaper? Increase the reach of your titles

YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.

Zifuatazo ni miomgoni mwa sababu za kuwekeza Mkoa wa Simiyu

• Mkoa huu unafaa kwa uwekezaji kwa sababu ya hali nzuri ya hewa,

ambayo ni nzuri kwa utalii, kilimo na ufugaji. Amani na utulivu wa

kisiasa ambavyo hujenga mazingira ya usalama pamoja na kiwango

cha chini cha uhalifu ni vivutio vingine vya kumfanya mtu awekeze

katika mkoa huu. Wawekezaji hawana haja ya kuwa na wasiwasi

kuhusu usalama wa mali zao watakazowekeza katika mkoa huu. Zaidi

ya hayo, wananchi wake ni wachapakazi na wanazo stadi za kutosha

za ukulima wa kisasa.

• Kwa mujibu wa matokeo ya sensa ya Taifa ya mwaka 2012, idadi

ya watu mkoani Simiyu ilikisiwa kuwa 1,591,000. Ukiwa mkoa mpya

wenye maeneo yenye uwezekano wa kuwekeza ni wazi kuwa idadi ya

watu inaongezeka kila siku na kwa hiyo upanuzi wa huduma za kijamii

na uchumi unahitajika.

• Pato la kila mtu katika mkoa huu ni shilingi 510,023/- ukiwa ni

miongoni mwa mikoa yenye watu wa kipato cha uchumi wa kati

katika nchi. Kilimo kimeendelea kuwa ndiyo shughuli kuu ya kimaisha

na kiuchumi ya Mkoa wa Simiyu. Sekta hii inachangia asilimia 75 ya

uchumi wa Mkoa huu na inaajiri kiasi cha asilimia 80 ya wananchi

katika Mkoa huu. Mazao makuu ya biashara yanayolimwa ni pamba,

karanga na alizeti. Mazao makuu ya chakula ni mahindi, mtama,

mpunga, viazi vitamu, ulezi na muhogo.

• Usafiri wa kuunganisha mkoa huu na mikoa mingine na ukaribu wake

na nchi za jirani ni jambo jingine muhimu linalowavutia wawekezaji

katika mkoa huu.

• Wawekezaji wanakaribishwa kuwekeza katika viwanda vya pamba.

Mtu anapozungumzia uzalishaji wa pamba nchini Tanzania, mtu huyo

atakuwa anazungumzia pamba ya Maswa katika Mkoa wa Simiyu.

Kwa mujibu wa takwimu, hadi sasa mkoa wa Simiyu ndiyo Mkoa

unaoongoza katika uzalishaji wa pamba nchini Tanzania ukizalisha zaidi

ya tani 150,000 za pamba yenye mbegu kwa mwaka. Wawekezaji

wanakaribishwa kuwekeza katika kilimo cha pamba na viwanda vya

kuchambulia pamba na shughuli nyinginezo.

MWONGOZO WA UWEKEZAJI MKOANI SIMIYU | 3

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!