You also want an ePaper? Increase the reach of your titles
YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.
UTANGULIZI

Karibu Mkoa wa Simiyu. Mwongozo wa Uwekezaji wa mkoa wa Simiyu

umeandaliwa sambamba na sera ya uwekezaji ya Tanzania. Unaainisha

fursa za uwekezaji zinazopatikana katika mkoa wa Simiyu. Vile vile

unaendana na dira ya mkoa wa Simiyu kama ilivyoelezwa na Mheshimiwa

Rais wa Jamhuri ya Muungano Dr. John Pombe Magufuli wa Tanzania

mnamo tarehe 11, Januari 2017, na umeandaliwa kulingana na mifumo

ya kimaendeleo ya kitaifa kama vile Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025 na

Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano 2016-2021 (FYDP II).

Mwongozo huu wa uwekezaji unatoa taarifa za uwekezaji kwa makampuni

ya uwekezaji ya hapa nchini, ya nchi za nje na watu binafsi. Vile vile,

Mwongozo unaainisha rasilimali na kubainisha fursa za uwekezaji zilizopo

katika mkoa wa Simiyu ili kuchochea biashara, maendeleo na ukuaji wa

uchumi. Pia Mwongozo unadhamiria kukuza uwezo wa ushindani wa

Mkoa wa Simiyu katika maeneo ambayo Mkoa una fursa za kiuchumi.

Madhumuni mengine ni kukuza uwezo wa uzalishaji katika sekta muhimu

za msingi ili kuleta maendeleo endelevu yatakayochangia kukua kwa pato

la jumla la Taifa na ustawi wa mkoa wa Simiyu.

Kwa hiyo, mkoa wa Simiyu na wilaya zake na Serikali za Mitaa: Bariadi,

Busega, Itilima, Maswa, na Meatu wamedhamiria kutoa kipaumbele katika

uwekezaji na kutoa huduma stahiki na motisha za kuvutia kwa wawekezaji

katika Mkoa. Zaidi ya hayo, Ofisi ya Mkoa wa Simiyu na mamlaka zake

za Serikali za Mitaa wataandaa mipango mwafaka na mazingira bora ya

uendeshaji na ya kibiashara na watakuwa wanapatikana wakati wote ili

kutoa maelezo zaidi kuhusu fursa zilizopo kwa wawekezaji wenye nia ya

kuwekeza.

Napenda kulipongeza Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP)

kwa msaada wa kifedha na utaalamu, pia Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na

Kijamii (ESRF) kwa kuandaa Mwongozo huu. Napenda pia, kuwashukuru

MWONGOZO WA UWEKEZAJI MKOANI SIMIYU | iii