Create successful ePaper yourself
Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.
za umeme za vimiminika, photovoltaic na joto la jua. Pia vinajumuishwa

matanki ya upozaji wa maziwa yaliyofunikwa na majarikeni ya alumini

yanayotumika kwa ajili ya kuhifadhi na kukusanya maziwa katika viwanda

vinavyotoa kila siku; huduma za shambani za maandalizi ya ardhi, ulimaji,

upandaji na uvunaji.

Vikwazo vya Ushuru wa Uingizaji: Ushuru wa uingizaji ambao hutozwa

katika pembejeo zinazoingizwa nakumika kwa ajili ya kuzalisha bidhaa kwa

ajili ya kupelekwa nje na bidhaa zinazouzwa katika taasisi kama vile Umoja

wa Mataifa nchini Tanzania hurudishwa.

Utengenezaji chini ya dhamana: Viwanda vyote vilivyosajiliwa

kutengeneza bidhaa chini ya dhamana kwa madhumuni ya usafirishaji nje

vinasamehewa ushuru wa uingizaji na kodi nyingine katika zana zilizotumika

kutengenezea bidhaa hizo.

Miundombinu ya kiuchumi: Barabara, reli, usafiri wa anga na bahari,

vifaa vya bandarini, mawasiliano ya simu, huduma za benki na bima.

Utalii: Katika utalii, hasara hupelekwa mbele. Hata hivyo, kampuni zenye

hasara za kudumu kwa miaka mitatu mfululizo zinatozwa 0.3% ya mapato

ya mwaka. Magari ya 4WD yaliyoundwa na kutengenezwa kwa ajili ya

madhumuni ya mtalii yanasamehewa ushuru wa kuingiza, kulingana na

kukidhi vigezo vilivyowekwa na Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Vilevile, vifaa vya hotelini, ambavyo vimenakshiwa au kuchapwa au

kuwekwa logo ya hoteli iliyoingizwa na hoteli yenye leseni kwa matumizi

yake vinasamehewa ushuru wa kuingiza.

Motisha kwa Wawekezaji wa Kigeni:

Hakikisho la Uwekezaji na Utatuzi wa migogoro: Uwekezaji nchini

Tanzania unahakikishwa dhidi ya utaifishaji na kunyang’anywa. Tanzania ni

mwanachama wa kituo cha kimataifa kwa ajili ya Utatuzi wa Migogoro ya

Uwekezaji (ICSD) na Wakala wa Hakikisho la Uwekezaji Unaohusisha nchi

nyingi (MIGA).

MWONGOZO WA UWEKEZAJI MKOANI SIMIYU | 43