24.03.2017 Views

MWONGOZO WA UWEKEZAJI MKOANI SIMIYU

mwongozo-simiyu

mwongozo-simiyu

SHOW MORE
SHOW LESS

Create successful ePaper yourself

Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.

inajumuisha Wilaya za Bariadi, Busega na Itilima, zenye topografia ya kupanda

na kushuka zenye udongo mfinyanzi na udongo wa juu mweupe. Kiasi cha

mvua ni baina ya mm 700 - 900. Shughuli kuu ya kiuchumi katika kanda

hii ni pamoja na kilimo cha mazao hasa mahindi, mtama, pamba, muhogo

na ufugaji. Kanda ya pili inajumuisha Wilaya ya Meatu yenye topografia ya

kupanda na kushuka na kupindapinda upande wa Mashariki wenye udongo

mfinyanzi wenye rutuba. Kanda hii ina mmomonyoko mbaya wa udongo

unaopunguza kilimo cha mazao. Kiasi cha mvua kwa kawaida ni chini ya mm

700 chenye tabia isiyotabirika. Kilimo cha mazao na ufugaji ndiyo shughuli

kuu za kiuchumi katika eneo hili. Mazao makuu yanayolimwa katika eneo hili

ni pamoja na mtama, pamba na mahindi. Kanda ya tatu inajumuisha Wilaya

ya Maswa yenye topografia ya kupanda na kushuka na ya kupindapinda.

Ardhi yake ni ya udongo wa Usukumani maarufru kwa jina la mbuga, udongo

mfinyanzi mweusi wa tifutifu ambao ni mzuri kwa kilimo cha mpunga. Mazao

mengine yanayolimwa katika eneo hili ni pamoja na mahindi, mtama na

pamba. Kanda hii ina kiasi cha mvua kisichoaminika kati mm 700 hadi mm

800 kwa mwaka. Eneo hili ni maarufu pia kwa shughuli za ufugaji.

Kielelezo 1.1: Ramani ya Mkoa wa Simiyu

6 | MWONGOZO WA UWEKEZAJI MKOANI SIMIYU

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!