TPCC Annual Report 2008.indd - HeidelbergCement
TPCC Annual Report 2008.indd - HeidelbergCement
TPCC Annual Report 2008.indd - HeidelbergCement
Create successful ePaper yourself
Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.
Maelezo mafupi ya Mwenyekiti

Tanzania Portland Cement Company Ltd, Annual Report 2008

Mwaka 2008 ulikuwa wenye changamoto nyingi na pia wenye mafanikio makubwa kwa Kampuni ya Saruji Tanzania

(TPCC). Kwa ujumla, katika mwaka huu, tulishuhudia muendelezo wa ukuaji wa soko la saruji, kuanza kwa uzalishaji

kutoka kwenye kiwanda kipya sanjari na mafanikio makubwa kifedha.

Hali ya Uzalishaji na Mauzo

Uzalishaji na mauzo ya saruji katika mwaka 2008 yalikuwa

makubwa kuliko wakati wowote katika historia ya Kampu-

ni ambapo kulikuwa na ongezeko la asilimia 4 ikilinganish-

wa na mwaka uliotangulia. Soko la saruji liliendelea kukua

katika ukanda mzima wa Afrika Mashariki ingawa kasi ya

ukuaji ilikuwa chini kidogo ukilinganisha na mwaka 2007.

Katika nusu ya kwanza ya mwaka 2008, mahitaji ya saruji

katika eneo lote la Afrika Mashariki yalikuwa makubwa

kuliko uwezo wa uzalishaji, hali ambayo inafanana na ile

iliyokuwepo mwaka 2007. Hata hivyo, hali ya upatikanaji

wa saruji nchini Tanzania ilianza kuwa nafuu baada ya

kinu kipya na.4 kuanza uzalishaji katika robo-mwaka ya

mwisho ya 2008 na kufanya uwezo wa uzalishaji wa TPCC

kuwa maradufu ikilinganishwa na uwezo wa awali. Kam-

puni iliendelea kutoa kipaumbele katika kutosheleza soko

la ndani ya nchi.

Utendaji kifedha

Mauzo yaliongezeka kwa aslimia 24 ikilinganishwa na

mauzo ya mwaka 2007 ingawa faida kabla ya gharama

za kifedha na kodi iliongezeka kwa asilimia 18 tu. Faida

baada ya kodi ya mapato ilifikia TZS.35 bilioni ikiwa ni juu

kwa asilimia 16 ikilinganishwa na faida ya mwaka uliotan-

gulia.

Bei za mahitaji yanayopatikana nchini na yale yanayo-

agizwa kutoka nje ziliongezeka kwa kasi kubwa katika

mwaka huu. Pia, uzinduzi wa mtambo mpya kusaga na

kupakia saruji uliongeza mahitaji ya malighafi (clinker)

kutoka nje ya nchi na kusababisha ongezeko la gharama za

uzalishaji.

Uraia Mwema

Kampuni inaamini katika kuendesha shughuli zake kwa

misingi ya uwajibikaji, utawala bora na uraia mwema. Tu-

natambua na kukubali wajibu wa kutekekeleza majukumu

yetu kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo Seri-

kali, katika ukuaji endelevu wa uchumi wa nchi, kuweka

mazingira mazuri na salama ya sehemu za kazi, kuboresha

maslahi ya wafanyakazi na kuwapa kipato cha kuridhisha

wamiliki (wenye-hisa) wa Kampuni

TPCC na sekta nzima ya uzalishaji saruji hutoa mchango

mkubwa kwenye uchumi wa nchi kwa kulipa kodi sta-

hiki, kuleta ajira, kuboresha technolojia, kushiriki katika

mipango mbalimbali ya maendeleo ya jamii na kufanya

shughuli mama ya uzalishaji wa saruji inayohitajika katika

shughuli za ujenzi nchini.

Matarajio

Kuparaganyika kwa mifumo ya uchumi duniani kumeu-

weka uchumi wa nchi za Afrika Mashariki katika wakati

mgumu na mashaka makubwa pia. Tunadhani kwamba

kushuka kwa hali ya uchumi duniani kutaathiri sekta nzima

ya ujenzi hapa nchini na nchi jirani, yakiwemo mahitaji ya

saruji.

Hata hivyo, ujenzi wa kiwanda kipya unaiweka TPCC

katika hali nzuri kiushindani katika kukabiliana na hali

ngumu soko inayotarajiwa kujitokeza. Baada ya kufanikiwa

kuzindua kinu kipya na mtambo wa upakiaji mwishoni

mwa mwaka 2008, Kampuni sasa iko kwenye mchakato

wa uzinduzi wa tanuru jipya. Mafanikio ya uzinduzi huu

yataiweka TPCC katika hali ya kutohitaji kuagiza malighafi

(clinker) kutoka nje na hatimaye kuleta nafuu ya gharama

za uzalishaji.

Thamani ya Hisa katika Soko

Bei ya hisa moja ya TPCC katika soko ilikuwa TZS 1,600

mwishoni mwa mwaka 2008 na hivyo kufanya thamani ya

Kampuni kuwa TZS 288 bilioni. Thamani hii ni ongezeko

la asilimia 40 juu ya thamani iliyokuwepo mwishoni mwa

mwaka 2007 wakati bei ya hisa moja ilikuwa TZS. 1,140.

Kampuni ilikuwa na wamiliki wa hisa kama 11,500 mwis-

honi mwa mwaka 2008.

Gawio

Bodi inapendekeza gawio la TZS 70 kwa hisa kwa mwaka

2008 ikilinganishwa na gawio la TZS 43 kwa hisa kwa

mwaka 2007 ambalo ni ongezeko la asilia 63. pendekezo

hili la gawio ni sawa na asilimia 36 ya faida yote ya mwaka

baada ya kodi ya mapato.

5