TPCC Annual Report 2008.indd - HeidelbergCement
TPCC Annual Report 2008.indd - HeidelbergCement
TPCC Annual Report 2008.indd - HeidelbergCement
Create successful ePaper yourself
Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.
Tanzania Portland Cement Company Ltd, Annual Report 2008

Mara baada ya Mahakama Kuu kutoa uamuzi mwezi Oktoba 2006 kwa kuipa ushindi Kampuni katika kesi ya uvamizi

wa ardhi iliyowahusisha watu 933, walalamikiwa walikata rufaa ambayo bado inashughulikiwa na Mahakama ya Rufaa.

Hatua hii imeizuia Kampuni kuchukua na kutumia ardhi yake na hivyo kufanya upanuzi wa machimbo ya mawe kuelekea

kutowezekana kutokana na makazi ya wavamizi hao kuwa karibu mno na eneo la machimbo.

Kinyume na ahadi za awali, Serikali iliondoa kabisa ushuru wa ziada kwenye saruji inayoagizwa kutoka nje kuanzia Julai

2008. Kabla Kampuni haijaamua kuwekeza katika mradi wa upanuzi wa kiwanda na baada ya kuombwa kutoa msi-

mamo wake juu ya ushuru huu, Serikali ilitamka wazi kuwa sera yake ni kupunguza ushuru huo wa ziada kwa asilimia 5

kila mwaka hadi mwaka 2010 utakapofikia aslimia 25 na kiwango hiki hakingeshuka tena. Kutabirika kwa mazingira ya

biashara ni muhimu kwa wawekezaji katika kufanya maamuzi yao na mabadiliko ya sera juu ya ushuru wa ziada ambayo

yalifanywa na Serikali mwezi Julai 2008 hayaendani na dhana hii ya kutabirika.

Kampuni imeingia mikataba na wasambazaji wa gesi asilia kwa kipindi kiachoishia Juni 2014 kwa mahitaji yote ya nishati

hii kwa ajili ya kiwanda kipya pia.

Usitawi wa Wafanyakazi

Uhusiano kati ya Uongozi na Wafanyakazi

Uhusiano kati ya uongozi na wafanyakazi unalindwa na mkataba wa hiari kati ya Kampuni na Chama cha Wafanyakazi

wa Viwanda na Biashara (TUICO) na ulisainiwa upya mwezi Desemba 2008 kwa kipindi cha 2009-2010.

Huduma za Matibabu

Huduma za matibabu hutolewa bure kwa wafanyakazi na familia zao.

Usalama Viwandani

Kampuni inatimiza masharti yote yaliyowekwa kisheria kuhusu mazingira salama ya kufanyia kazi.

Mafunzo

Shughuli za mafunzo zimekuwa zikiendelea sanjari na mafunzo yanayolenga kuijua vema technologia ya kisasa ya uende-

shaji wa kiwanda kipya.

Mishahara

Viwango vya mishahara ya wafanyakazi hurekebishwa kila mwaka kwa kuzingatia uwezo wa kifedha na baada ya ma-

jadiliano kati ya TUICO na Uongozi wa Kampuni. Viwango vya mishahara ya 2008 vilikubaliwa na kuanza kulipwa mwezi

Januari 2008. Katika Mwaka husika, wafanyakazi wote wa kudumu walikuwa na mishahara isiyopungua TZS milioni tatu.

Mafao ya Wafanyakazi

Wafanyakazi wa kudumu ni wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa Mashirika ya Umma (PPF) wakati wale wenye

mikataba ya muda maalumu ni wanachama wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF). Kampuni huchangia asilimia 15 ya

mshahara kwa kila mwanachama wa PPF na asilimia 10 ya jumla ya mshahara na marupurupu mengine kwa kila mwana-

chama wa NSSF. Pamoja na kuchangia kwenye hii mifuko miwili, Kampuni inaugharamia mpango wa tatu wa pensheni

kwa ajili ya kuboresha mafao ya uzeeni ya wafanyakazi wote kwa kuchangia asilimia 10 ya mshahara wa kila mfanyakazi.

Isitoshe, mkataba wa hiari kati ya TUICO na Kampuni umeongeza malipo mengine kwa mfanyakazi anayestaafu ambayo

hutegemea urefu wa utumishi wa mfanyakazi husika hadi wakati anapostaafu. Pia, wafanyakazi hupata saruji kama tuzo

ya utumishi wa muda mrefu katika vipindi maalumu vilivyoainishwa kwenye mkataba wa hiari.

24