TPCC Annual Report 2008.indd - HeidelbergCement

TPCC Annual Report 2008.indd - HeidelbergCement TPCC Annual Report 2008.indd - HeidelbergCement

heidelbergcement.com
from heidelbergcement.com More from this publisher
18.01.2013 Views

Tanzania Portland Cement Company Ltd, Annual Report 2008 Taarifa ya Wakurugenzi kwa Mwaka ulioishia 31 Desemba 2008 Wakurugenzi wanayo furaha kuwasilisha taarifa yao pamoja na hesabu zilizokaguliwa kwa mwaka ulioishia 31 Desemba 2008. Shughuli kuu Shughuli kuu ya Kampuni ni uzalishaji, usambazaji na uuzaji wa saruji. Wajibu wa Wakurugenzi Kwa mujibu wa Sheria ya Makampuni Na.12 ya mwaka 2002, ni wajibu wa wakurugenzi kuandaa hesabu za Kampuni kila mwaka zenye kutoa hali halisi ya Kampuni kifedha mwishoni mwa kila kipindi. Wakurugenzi wanathibitisha kwamba katika kutayarisha hesabu ambazo zinaonyesha hali halisi ya Kampuni kila wakati, wametumia sera na kanuni za kiuhasibu zinazohakikisha kuwa hesabu zinakidhi matakwa ya viwango vya kimataifa vya utayarishaji hesabu na taarifa za fedha. Hesabu zimeandaliwa kwa kuzingatia kuwa Kampuni itaendelea kufanya shughuli zake kwa muda mrefu ujao. Wakurugenzi wanawajibika kutunza vitabu na nyaraka za kiuhasibu zenye kuonyesha hali halisi na sahihi ya Kampuni na kuhakikisha kuwa hesabu zinazotayarishwa zinaendana na matakwa ya Sheria ya Makampuni Na.12 ya mwaka 2002. Wanawajibika pia kuhakikisha kwamba mali zote za Kampuni ziko katika hali ya usalama na kuweka mifumo ya udhibiti wa shughuli za Kampuni inayofanya kazi ya kuzuia au kugundua wizi, ufujaji au makosa kuwa rahisi. Wakurugenzi Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wakati huu ambao wamekuwa wajumbe katika kipindi chote cha mwaka 2008 ni hawa: Bw. Jean-Marc Junon Mfaransa Mwenyekiti Bw. Klaus Hvassing Mnorwei Mjumbe Bw. William Mlaki Mtanzania Mjumbe Bw. George Fumbuka Mtanzania Mjumbe Bw. Daniel Gauthier Mbeljiji Mjumbe Bw. Arne J. Selen Mnorwei Mjumbe mbadala wa Daniel Gauthier Bw. Ola Schippert Mswedi Mjumbe Wajumbe wote wa Bodi siyo watendaji katika Kampuni, isipokuwa Bw. Klaus Hvassing ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji. Wakurugenzi Wanahisa Bw. William Mlaki ana hisa 49,927 katika Kampuni 22

Malipo kwa Wakurugenzi Tanzania Portland Cement Company Ltd, Annual Report 2008 Malipo kwa huduma ya ukurugenzi katika Kampuni katika mwaka 2008 yalikuwa kama ifuatavyo:- TZS Mwenyekiti 1,000,000 kwa mwaka Kila mkurugenzi 600,000 kwa mwaka Pia, kila mkurugenzi alilipwa posho ya dola 1,200 kwa kila kikao cha Bodi au Kamati ya Ukaguzi alichohudhuria. Katika mwaka husika, malipo ya namna hii kwa wakurugenzi yalikuwa TZS 46,883,304 (2007:TZS 25,919,680). Tathmini ya Biashara Mauzo mwaka 2008 yaliongezeka kwa aslimia 4 ikilinganishwa na mwaka 2007. Uzalishaji wa klinka ulishuka kwa asil- imia 6, hali iliyosababishwa na haja ya kusimamisha mitambo mara kwa mara kupisha kazi za ujenzi wa kiwanda kipya. Taarifa kamili ya mapato kwa mwaka husika inapatikana ukurasa wa 28 wa taarifa ya hesabu Uwezo wa Kulipa Wakurugenzi wamefanya tathmini ya kina juu ya hali ya kifedha ya Kampuni ikiwa ni pamoja na madeni ya muda mfupi na muda mrefu. Kwa misingi ya tathmini hii ambayo imefanywa kwa kuzingatia mpango wa biashara uliopo, kanuni za kimataifa za uhasibu na matakwa ya Sheria ya Makampuni Na.12 ya 2002, wakurugenzi wameridhika kwamba Kampuni ina uwezo wa kuendesha shughuli zake bila matatizo yoyote. Shughuli za Biashara na Makampuni yenye Uhusiano Kampuni huagiza malighafi, vipuri na mahitaji mengine ya uzalishaji kwa bei ambazo hufikiwa kwa misingi ya kawaida ya kibiashara, kutoka Scancem International ANS ambayo inamiliki asilimia 69.25 ya hisa zote za Kampuni. Maelezo ya kina ya shughuli zinazofanywa na watu au makampuni yenye uhusiano yako aya ya 29 ya taarifa ya hesabu Masuala ya Mazingira Ukarabati mkubwa wa mitambo ya uzalishaji ambao umefanyika kati ya mwaka 2002 hadi 2006 umesaidia sana ku- punguza kutimka kwa vumbi hapa kiwandani. Mfumo wa Udhibiti wa Mazingira umeandaliwa katika mwaka 2008 na mchakato umeanza ili Kampuni ipate cheti cha Ubora cha ISO 14001 katika mwaka 2009. Matukio Muhimu Soko la saruji nchini Tanzania liliendelea kukua katika mwaka 2008. Kampuni iliweza kuzalisha na kuuza saruji nyingi zaidi kuliko wakati wowote katika historia yake. Ili kukidhi mahitaji ya soko, TPCC iliendelea kuagiza klinka kutoka nje ya nchi kuziba pengo katika uzalishaji wa bidhaa hiyo. Mradi wa upanuzi wa kiwanda umeendelea kama ilivyopangwa na kwa gharama kama zilivyo kwenye bajeti. Ujenzi wa mtambo mpya wa kusaga na kupakia saruji ulikamilika mwezi Agosti na kukabidhiwa rasmi mwezi Oktoba 2008 na hivyo kuongeza uzalishaji wa saruji maradufu kutoka tani kama 700,000 kwenda tani 1,400,000 kwa mwaka. Mtambo wa kuzalisha klinka unatarajiwa kukabidhiwa rasmi katika robo-mwaka ya pili ya 2009. 23

Malipo kwa Wakurugenzi

Tanzania Portland Cement Company Ltd, Annual Report 2008

Malipo kwa huduma ya ukurugenzi katika Kampuni katika mwaka 2008 yalikuwa kama ifuatavyo:-

TZS

Mwenyekiti 1,000,000 kwa mwaka

Kila mkurugenzi 600,000 kwa mwaka

Pia, kila mkurugenzi alilipwa posho ya dola 1,200 kwa kila kikao cha Bodi au Kamati ya Ukaguzi alichohudhuria. Katika

mwaka husika, malipo ya namna hii kwa wakurugenzi yalikuwa TZS 46,883,304 (2007:TZS 25,919,680).

Tathmini ya Biashara

Mauzo mwaka 2008 yaliongezeka kwa aslimia 4 ikilinganishwa na mwaka 2007. Uzalishaji wa klinka ulishuka kwa asil-

imia 6, hali iliyosababishwa na haja ya kusimamisha mitambo mara kwa mara kupisha kazi za ujenzi wa kiwanda kipya.

Taarifa kamili ya mapato kwa mwaka husika inapatikana ukurasa wa 28 wa taarifa ya hesabu

Uwezo wa Kulipa

Wakurugenzi wamefanya tathmini ya kina juu ya hali ya kifedha ya Kampuni ikiwa ni pamoja na madeni ya muda mfupi

na muda mrefu. Kwa misingi ya tathmini hii ambayo imefanywa kwa kuzingatia mpango wa biashara uliopo, kanuni za

kimataifa za uhasibu na matakwa ya Sheria ya Makampuni Na.12 ya 2002, wakurugenzi wameridhika kwamba Kampuni

ina uwezo wa kuendesha shughuli zake bila matatizo yoyote.

Shughuli za Biashara na Makampuni yenye Uhusiano

Kampuni huagiza malighafi, vipuri na mahitaji mengine ya uzalishaji kwa bei ambazo hufikiwa kwa misingi ya kawaida ya

kibiashara, kutoka Scancem International ANS ambayo inamiliki asilimia 69.25 ya hisa zote za Kampuni. Maelezo ya kina

ya shughuli zinazofanywa na watu au makampuni yenye uhusiano yako aya ya 29 ya taarifa ya hesabu

Masuala ya Mazingira

Ukarabati mkubwa wa mitambo ya uzalishaji ambao umefanyika kati ya mwaka 2002 hadi 2006 umesaidia sana ku-

punguza kutimka kwa vumbi hapa kiwandani. Mfumo wa Udhibiti wa Mazingira umeandaliwa katika mwaka 2008 na

mchakato umeanza ili Kampuni ipate cheti cha Ubora cha ISO 14001 katika mwaka 2009.

Matukio Muhimu

Soko la saruji nchini Tanzania liliendelea kukua katika mwaka 2008. Kampuni iliweza kuzalisha na kuuza saruji nyingi

zaidi kuliko wakati wowote katika historia yake. Ili kukidhi mahitaji ya soko, TPCC iliendelea kuagiza klinka kutoka nje ya

nchi kuziba pengo katika uzalishaji wa bidhaa hiyo.

Mradi wa upanuzi wa kiwanda umeendelea kama ilivyopangwa na kwa gharama kama zilivyo kwenye bajeti. Ujenzi wa

mtambo mpya wa kusaga na kupakia saruji ulikamilika mwezi Agosti na kukabidhiwa rasmi mwezi Oktoba 2008 na hivyo

kuongeza uzalishaji wa saruji maradufu kutoka tani kama 700,000 kwenda tani 1,400,000 kwa mwaka. Mtambo wa

kuzalisha klinka unatarajiwa kukabidhiwa rasmi katika robo-mwaka ya pili ya 2009.

23

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!