MAKALA YA BIASHARA YA HEWA UKAA
Ndugu wananchi ni jukumu letu kuhifadhi Misitu kwa Maendeleo ya jamii zetu na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi - Tanzania. Ndugu wananchi ni jukumu letu kuhifadhi Misitu kwa Maendeleo ya jamii zetu na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi - Tanzania.
14 MAKALAHABARILEO, IJUMAA JANUARI 15, 2021Na Budoya NillaHEWA ya ukaa ni biasharapoa na inalipa.Mtu akisikia sentensihiyo kwa mara ya kwanzaanaweza asielewe kitu lakiniukisoma makala haya hadimwisho, bila shaka utaelewa.Kazi kubwa unayotakiwakufanya ili uweze kufanya biasharahii ni kuhifadhi misitu ya asiliiliyo katika eneo lako na kutunzamazingira yako, basi. Misitu ya asiliina uwezo mkubwa wa kufyonzana kuhifadhi hewa ukaa na hewasumu.Ukiwa na misitu hii, ili ufanikishehilo lazima uzuie uharibifukwa maana ya kuhakikisha hakunaukataji miti hovyo, hakuna kufyekamiti, kuchoma misitu na kuzuiakufanya shughuli zingine hatarishikwa uhifadhi wa misitu ikiwemokufyeka misitu kwa ajili ya kufuguamashamba mapya au kuigeuzamalisho ya mifugo.Badala yake matumizi yamisitu yanatakiwa yawe endelevusambamba na kupanda miti mbalimbali katika maeneo yako. Ukiwezakufanya hayo utakuwa sasana uhakika wa kuvuna hewa ukaana kufanya biashara.Pengine unaweza kujiuliza, jebiashara hii ni kama biashara yamahindi au biashara nyingine?Kwamba mtu anaweza kupanda nakuvuna mahindi na kuuza sokoni?Hapana sivyo.Katika biashara hii, mhusikiaanachotakiwa kufanya ni kuhifadhimisitu ya asili iliyo katika eneolake, basi.Kwa hatua hiyo, taasisi ya CarbonTanzania watamtafutia watejaduniani wanaotoa ruzuku kwawanaofaya uhifadhi huo.Biashara hii imeingia katikaMkoa wa Katavi, hususani katikaHalmashauri ya Wilaya ya Tanganyikana tayari wananchi 21,000katika vijiji vinane walio katikahalmashauri hiyo wamenufaika namradi wa hewa ukaa.Hii ni baada ya kuivuna na kulipwakiasi cha shilingi milioni 380kupitia Carbon Tanzania chini yamradi uitwao Ntakata MountainsRedd Plus Project.Wananchi katika wilaya hiyowamezuia uharibifu wa misituwaliyoihifadhi ili iwasaide kutunzamazingira ikiwemo kufyonza hewaukaa na hewa sumu iliyo katikaanga la nchi yetu na nje ya nchi.Kutokana na uhifadhi huo, vijijihusika vimevuna jumla ya tani82,000 za hewa ukaa na kuiuza kwathamani ya shilingi 250,000,000.Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Juma Homera akishiriki upandaji mitikutunza mazingaira.Biashara ya hewa ukaainavyowanufaisha KataviMwakilishi wa Carbon Tanzania, Frank Kweka akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Juma Homerahundi yenye thamani ya Sh milioni 225 fedha inayotokana na mauzo ya hewa ya ukaa.Pamoja na uvunaji wa tani hizo,mauzo yake hayajafikia hata nusuya tani 270,000 ambazo bado hazijauzwa.Tarehe 2/5/2020 na 12/11/2020kiasi cha Sh milioni 130 zilitolewakama motisha na wadau mbalimbali wa uhifadhi kwa vijiji kablaya kupata wateja na vyeti vya uuzajiwa hewa ukaa na kugawanywakulingana na makubaliano yamradi.Makubaliano hayo yanabainishakuwa asilimia 10 ya fedha zinazopatikanazinaenda kwenye Halmashauriya Wilaya ya Tanganyikaili kugharimia shughuli za usimamizimazingira wakati asilimia 90zinagawiwa kwenye vijiji vilivyokatika mradi ambao unakadiriwakuwa na hekta 230 katika msitu waTongwe Magharibi.Fedha hizo zinatarajiwa kutimikakatika miradi ya maendelao yakijamii na kiuchumi kwa wananchikama vile ujenzi wa madarasa,utengenezaji wa madawati,kujenga vituo vya afya na miradiya kuwaletea wananchi nishati yaumeme.Inaelezewa kuwa ikiwa hewaya ukaa itauzwa kwa wingi na ukamilifuwake uliopo katika misituya vijiji hivyo, kuna uwezekano wavijiji hivyo kulipwa shiligi bilionisita na hivyo wananchi wanatakiwakuendelea kuhifadhi misitu nakutunza mazingira. Miti isikatweovyo wala kuchomwa, waepukekilimo cha kuhamahama na ufugajiusiozingatia tija.Vijiji vilivyonufaika na mauzoya hewa ukaa ni Lugonesi, Mwese,Lwega na Bujombe. Vijiji vinginevilivyo katika mradi wa mauzo yahewa ukaa ni Kapanga, Mpembe,Kagunga na Katuma. Baadhi yavijiji hivyo viko katika Kata yaMwese, Tarafa ya Mwese na vijijivingine viko Kata ya Kasekese.Carbon Tanzania ndio taasisiinayowezesha vijiji hivyo kupatamasoko ya hewa ukaa ipatikanayokatika misitu ya hifadhi za vijiji namaeneo ya malisho.Je, biashara hii ilianzaje? Ilianzabaada ya vijiji vinane kuwekwakwenye mpango wa matumizi boraya ardhi kwa maana ya kupimwamaeneo yao na kuyatenga kamavile eneo la hifadhi ya misitu, eneola kilimo, eneo la makazi, mifugo,huduma za jamii na kadhalika.Yaani wananchi kupitia mkutanowao wa kujiji wanajipangianamna ya kutumia ardhi yaoiliyopimwa kwa faida yao.Matumizi bora ya ardhi ndiochanzo cha mradi wa hewa ya ukaakwa maana ya kutenga maeneo yahifadhi ya misitu na kuilida sawia.Mradi wa Ntakata MountainsRedd Plus Project unalenga kuhifadhimisitu ya asili na kulindabayoanuai zote muhimu hasa zilizohatarini kutoweka ikiwemo sokwe.Mradi pia umejikita katikakukabiliana na mabadiliko yatabianchi, kutunza vyanzo vyamaji, kutunza wanyamapori na kuwawezeshawananchi walio katikavijiji venye uhifadhi wa misitu asilikunufaika na mauzo ya hewa ukaa.Mashuleni wanafuzi hufundishwakwamba sisi binadamuhupumua hewa ya ukaa na baadayehewa hiyo hufyonzwa na mitina kuhifadhiwa kwenye miti naardhini lakini sisi binadamu huvutahewa ya oksijeni inayotolewa namimea.Mbali na hewa tunayopumua,anga letu limejaa hewa ukaa zinazozalishwana shughuli mbalimbaliza mwanadamu hususani viwanda.Uchomaji wa mimea pia husababishahewa ukaa kwenda angani kwanjia ya moshi.Uzalishaji mkubwa wa hewaukaa (kaboni) angani huchocheaathari ya jotogesi na kusababishamabadiliko ya tabianchi.Ongezeko la viwango vya hewaya ukaa na gesi nyingine anganizinazotokana na shughuli za binadamuhusababisha pia kiwango chajoto duniani kuongezeka.Mabadiliko haya yana maanagani? Mabadiliko haya yana maanaya kuongezeka kwa joto duniani,kuwa na misimu ya mvua isiyoaminika,kupata mvua chache aunyingi zinazosababisha mafuriko,utabiri wa majira kuwa mgumuna mvua kunyesha nje ya misimuiliyozoeleka.Hali hii huleta athari katikakilimo, uzalishaji wa chakulakupungua kwa sababu ya uhabawa mvua au mafuriko yanayozoamazao na ongezeko kubwa la joto,milipuko ya magonjwa ya mimeana wadudu waharibifu wa mazaowanaweza kusambaa hata maeneoambayo awali hawakuwepo.Ongezeko la joto duniani limesababishakuyeyuka kwa theluji katikancha za dunia na kusababishaongezeko la kima cha maji baharini.Kimsingi, kasi ya mwanadamukuongeza hewa ukaa angani nikubwa kuliko uwezo wa duniakufyonza gesi hiyo.Ukataji wa misitu kwa sababumbalimbali hupunguza uwezo waardhi kuhifadhi hewa ya ukaa, tunapochomamafuta kwa kuendeshamagari yetu na wakati mwingie kuzalishaumeme kwa njia ya mafutapia tunaongeza hewa ukaa angani.Kwa kuwa kasi ya ongezeko lahewa ukaa angani ni kubwa, kituambacho ni hatari kwa maisha yamwanadamu mintarafu suala lamabadiliko ya tabianchi, wataalamuwamefanya tafiti na kubainikuwa njia moja wapo katika kukabilianana mabadiliko ya tabianchini uhifadhi wa misitu ya asili.Misitu ya asili ina uwezomkubwa wa kutumia hewa ya ukaana hewa sumu kama chakula chake.Misitu ya asili iliyopo katikaHalmashauri ya Tanganyika nimiongoni mwa misiti iliyo nauwezo wa kuchangia katika sualala kabiliana na mabadiliko ya tabianchi.Wananchi mkoani Katavi,watanzania na Waafrika kwa ujumlahatuna budi kuhifadhi misituna kutunza mazingira yetu kwamanufaa yetu na vizazi vilivyo.Tuendelee kutunza mazingira yetukwa kupanda miti mbali ikiwemoya matunda kwa ajili matumizimbambali sambamba na kufyonzahewa ukaa kwa manufaa yetu.Mwandishi wa makala haya niOfisa Habari Mkuu, Ofisi ya Mkuuwa Mkoa wa Katavi.
14 MAKALA
HABARILEO, IJUMAA JANUARI 15, 2021
Na Budoya Nilla
HEWA ya ukaa ni biashara
poa na inalipa.
Mtu akisikia sentensi
hiyo kwa mara ya kwanza
anaweza asielewe kitu lakini
ukisoma makala haya hadi
mwisho, bila shaka utaelewa.
Kazi kubwa unayotakiwa
kufanya ili uweze kufanya biashara
hii ni kuhifadhi misitu ya asili
iliyo katika eneo lako na kutunza
mazingira yako, basi. Misitu ya asili
ina uwezo mkubwa wa kufyonza
na kuhifadhi hewa ukaa na hewa
sumu.
Ukiwa na misitu hii, ili ufanikishe
hilo lazima uzuie uharibifu
kwa maana ya kuhakikisha hakuna
ukataji miti hovyo, hakuna kufyeka
miti, kuchoma misitu na kuzuia
kufanya shughuli zingine hatarishi
kwa uhifadhi wa misitu ikiwemo
kufyeka misitu kwa ajili ya kufugua
mashamba mapya au kuigeuza
malisho ya mifugo.
Badala yake matumizi ya
misitu yanatakiwa yawe endelevu
sambamba na kupanda miti mbali
mbali katika maeneo yako. Ukiweza
kufanya hayo utakuwa sasa
na uhakika wa kuvuna hewa ukaa
na kufanya biashara.
Pengine unaweza kujiuliza, je
biashara hii ni kama biashara ya
mahindi au biashara nyingine?
Kwamba mtu anaweza kupanda na
kuvuna mahindi na kuuza sokoni?
Hapana sivyo.
Katika biashara hii, mhusikia
anachotakiwa kufanya ni kuhifadhi
misitu ya asili iliyo katika eneo
lake, basi.
Kwa hatua hiyo, taasisi ya Carbon
Tanzania watamtafutia wateja
duniani wanaotoa ruzuku kwa
wanaofaya uhifadhi huo.
Biashara hii imeingia katika
Mkoa wa Katavi, hususani katika
Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika
na tayari wananchi 21,000
katika vijiji vinane walio katika
halmashauri hiyo wamenufaika na
mradi wa hewa ukaa.
Hii ni baada ya kuivuna na kulipwa
kiasi cha shilingi milioni 380
kupitia Carbon Tanzania chini ya
mradi uitwao Ntakata Mountains
Redd Plus Project.
Wananchi katika wilaya hiyo
wamezuia uharibifu wa misitu
waliyoihifadhi ili iwasaide kutunza
mazingira ikiwemo kufyonza hewa
ukaa na hewa sumu iliyo katika
anga la nchi yetu na nje ya nchi.
Kutokana na uhifadhi huo, vijiji
husika vimevuna jumla ya tani
82,000 za hewa ukaa na kuiuza kwa
thamani ya shilingi 250,000,000.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Juma Homera akishiriki upandaji miti
kutunza mazingaira.
Biashara ya hewa ukaa
inavyowanufaisha Katavi
Mwakilishi wa Carbon Tanzania, Frank Kweka akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Juma Homera
hundi yenye thamani ya Sh milioni 225 fedha inayotokana na mauzo ya hewa ya ukaa.
Pamoja na uvunaji wa tani hizo,
mauzo yake hayajafikia hata nusu
ya tani 270,000 ambazo bado hazijauzwa.
Tarehe 2/5/2020 na 12/11/2020
kiasi cha Sh milioni 130 zilitolewa
kama motisha na wadau mbali
mbali wa uhifadhi kwa vijiji kabla
ya kupata wateja na vyeti vya uuzaji
wa hewa ukaa na kugawanywa
kulingana na makubaliano ya
mradi.
Makubaliano hayo yanabainisha
kuwa asilimia 10 ya fedha zinazopatikana
zinaenda kwenye Halmashauri
ya Wilaya ya Tanganyika
ili kugharimia shughuli za usimamizi
mazingira wakati asilimia 90
zinagawiwa kwenye vijiji vilivyo
katika mradi ambao unakadiriwa
kuwa na hekta 230 katika msitu wa
Tongwe Magharibi.
Fedha hizo zinatarajiwa kutimika
katika miradi ya maendelao ya
kijamii na kiuchumi kwa wananchi
kama vile ujenzi wa madarasa,
utengenezaji wa madawati,
kujenga vituo vya afya na miradi
ya kuwaletea wananchi nishati ya
umeme.
Inaelezewa kuwa ikiwa hewa
ya ukaa itauzwa kwa wingi na ukamilifu
wake uliopo katika misitu
ya vijiji hivyo, kuna uwezekano wa
vijiji hivyo kulipwa shiligi bilioni
sita na hivyo wananchi wanatakiwa
kuendelea kuhifadhi misitu na
kutunza mazingira. Miti isikatwe
ovyo wala kuchomwa, waepuke
kilimo cha kuhamahama na ufugaji
usiozingatia tija.
Vijiji vilivyonufaika na mauzo
ya hewa ukaa ni Lugonesi, Mwese,
Lwega na Bujombe. Vijiji vingine
vilivyo katika mradi wa mauzo ya
hewa ukaa ni Kapanga, Mpembe,
Kagunga na Katuma. Baadhi ya
vijiji hivyo viko katika Kata ya
Mwese, Tarafa ya Mwese na vijiji
vingine viko Kata ya Kasekese.
Carbon Tanzania ndio taasisi
inayowezesha vijiji hivyo kupata
masoko ya hewa ukaa ipatikanayo
katika misitu ya hifadhi za vijiji na
maeneo ya malisho.
Je, biashara hii ilianzaje? Ilianza
baada ya vijiji vinane kuwekwa
kwenye mpango wa matumizi bora
ya ardhi kwa maana ya kupimwa
maeneo yao na kuyatenga kama
vile eneo la hifadhi ya misitu, eneo
la kilimo, eneo la makazi, mifugo,
huduma za jamii na kadhalika.
Yaani wananchi kupitia mkutano
wao wa kujiji wanajipangia
namna ya kutumia ardhi yao
iliyopimwa kwa faida yao.
Matumizi bora ya ardhi ndio
chanzo cha mradi wa hewa ya ukaa
kwa maana ya kutenga maeneo ya
hifadhi ya misitu na kuilida sawia.
Mradi wa Ntakata Mountains
Redd Plus Project unalenga kuhifadhi
misitu ya asili na kulinda
bayoanuai zote muhimu hasa zilizo
hatarini kutoweka ikiwemo sokwe.
Mradi pia umejikita katika
kukabiliana na mabadiliko ya
tabianchi, kutunza vyanzo vya
maji, kutunza wanyamapori na kuwawezesha
wananchi walio katika
vijiji venye uhifadhi wa misitu asili
kunufaika na mauzo ya hewa ukaa.
Mashuleni wanafuzi hufundishwa
kwamba sisi binadamu
hupumua hewa ya ukaa na baadaye
hewa hiyo hufyonzwa na miti
na kuhifadhiwa kwenye miti na
ardhini lakini sisi binadamu huvuta
hewa ya oksijeni inayotolewa na
mimea.
Mbali na hewa tunayopumua,
anga letu limejaa hewa ukaa zinazozalishwa
na shughuli mbalimbali
za mwanadamu hususani viwanda.
Uchomaji wa mimea pia husababisha
hewa ukaa kwenda angani kwa
njia ya moshi.
Uzalishaji mkubwa wa hewa
ukaa (kaboni) angani huchochea
athari ya jotogesi na kusababisha
mabadiliko ya tabianchi.
Ongezeko la viwango vya hewa
ya ukaa na gesi nyingine angani
zinazotokana na shughuli za binadamu
husababisha pia kiwango cha
joto duniani kuongezeka.
Mabadiliko haya yana maana
gani? Mabadiliko haya yana maana
ya kuongezeka kwa joto duniani,
kuwa na misimu ya mvua isiyoaminika,
kupata mvua chache au
nyingi zinazosababisha mafuriko,
utabiri wa majira kuwa mgumu
na mvua kunyesha nje ya misimu
iliyozoeleka.
Hali hii huleta athari katika
kilimo, uzalishaji wa chakula
kupungua kwa sababu ya uhaba
wa mvua au mafuriko yanayozoa
mazao na ongezeko kubwa la joto,
milipuko ya magonjwa ya mimea
na wadudu waharibifu wa mazao
wanaweza kusambaa hata maeneo
ambayo awali hawakuwepo.
Ongezeko la joto duniani limesababisha
kuyeyuka kwa theluji katika
ncha za dunia na kusababisha
ongezeko la kima cha maji baharini.
Kimsingi, kasi ya mwanadamu
kuongeza hewa ukaa angani ni
kubwa kuliko uwezo wa dunia
kufyonza gesi hiyo.
Ukataji wa misitu kwa sababu
mbalimbali hupunguza uwezo wa
ardhi kuhifadhi hewa ya ukaa, tunapochoma
mafuta kwa kuendesha
magari yetu na wakati mwingie kuzalisha
umeme kwa njia ya mafuta
pia tunaongeza hewa ukaa angani.
Kwa kuwa kasi ya ongezeko la
hewa ukaa angani ni kubwa, kitu
ambacho ni hatari kwa maisha ya
mwanadamu mintarafu suala la
mabadiliko ya tabianchi, wataalamu
wamefanya tafiti na kubaini
kuwa njia moja wapo katika kukabiliana
na mabadiliko ya tabianchi
ni uhifadhi wa misitu ya asili.
Misitu ya asili ina uwezo
mkubwa wa kutumia hewa ya ukaa
na hewa sumu kama chakula chake.
Misitu ya asili iliyopo katika
Halmashauri ya Tanganyika ni
miongoni mwa misiti iliyo na
uwezo wa kuchangia katika suala
la kabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Wananchi mkoani Katavi,
watanzania na Waafrika kwa ujumla
hatuna budi kuhifadhi misitu
na kutunza mazingira yetu kwa
manufaa yetu na vizazi vilivyo.
Tuendelee kutunza mazingira yetu
kwa kupanda miti mbali ikiwemo
ya matunda kwa ajili matumizi
mbambali sambamba na kufyonza
hewa ukaa kwa manufaa yetu.
Mwandishi wa makala haya ni
Ofisa Habari Mkuu, Ofisi ya Mkuu
wa Mkoa wa Katavi.