HISTORIA YA KANISA I DBT 2019 PRINT
Cemetri ambalo halikuwekwa alama yoyote. Hadi sasa kaburi la John Calvin halijulikanililipo.4. JOHN KNOXJohn Knox alizaliwa katika miaka ya 1513 katika Haddington, mji mdogo kaskazini mwaEdinburg, Scotland. Maisha yake ya awali yalimwezesha kukutana na watu wengi, naelimu yake ya juu ilimwezesha kuwafikia watu wa hali ya juu katika jamii. Alipotezawazazi wake akiwa bado mtoto. Knox alijifunza kilatini shuleni Haddington. Mwaka 1529,alianza masomo ya Theolojia katika chuo cha mtakatifu Andrews. Aliwekewa mikono yaukuhani mwaka 1536 ila hakuajiriwa katika nafasi hiyo kutokana na Scotland kuwa namakuhani wengi.Mwaka 1540, utawala wa Scotland ulianza kuwatesa wahubiri wa Neno la Mungu. GeorgeWishart hakuogopa muda wa majaribu na akasafiri kutoka kijiji kimoja hadi kijiji kinginekuhubiri ukweli wa Biblia. Knox, kwa kushawishika na ujumbe wa Wishart, aliamuakumsindikiza kama mlinzi wake, akiwa na mapanga mawili kumkinga mhubiri huyu dhidiya vitisho vya watesi. Kwa wiki tano, alimsindikiza Wishart katika kuhubiri kwake mpakamamlaka yaliamua kunyamazisha sauti ya mheshimiwa huyu kwa kumfunga gerezani.John Knox Aliamua kujiunga nae na kumuunga mkono, lakini Wishart alimsihi arudinyumbani, akisema: “Hapana, rudi kwa watoto wako, na Mungu akubariki. Mmojaanatosha kuwa kafara. Knox alirudi.Henry Balnaves, mmoja ya waheshimiwa, alifurahishwa na kipaji chaa ufundishaji wawanamatengenezo na kuungana na mhubiri John Rough kwa kumwalika Knox kuwa mkuuwa kanisa na mchungaji wa kanisa la nyumba ya mtakatifu Andrews. Knox alikataamwaliko huo, nakusema hawakuwa na mamlaka ya kutoa wito huo na kurudi chumbanimwake. Wiki chache baade, alihudhuria ibada ambayo mhudumu alitetea kanisa la kikatolikikuwa mke wa Kristo. Knox alishindwa kunyamaza na kuzungumza kwamba kanisa lakikatoliki sio mke wa Kristo bali ni kahaba. Kanisa waliomba maneno yake yachunguzwejumapili iliyofuata. Baada ya siku saba, alihubiri Danieli 7, akilinganisha upapa na mpingaKristo, Knox alitambua maandiko kuwa mamlaka pekee kwa kutunga mafundisho ya dinina kuthibitisha umhimu wa haki kwa imani pekee, mambo yaliounda msingi wa mahubiriyake hadi mwisho wa uhai wake.Siku kadhaa baadae, John Knox alitoa maandishi ya mafundisho yanayopinga utaratibu wamisa, pugatori, na maombi kwa wafu. Ndipo palianza kazi ya John Knox, aliyetokea kuwammoja wa wahubiri wa kupinga mafundisho potofu ya kanisa.Kutoka utumwani kuwa mkuu wa Kanisa katika huduma kwa mfalmeKundi la waheshimiwa kumi na sita, wafuasi wa mfia dini Wishart, waliokuwawamekasirishwa na padre David Beaton kwa kuuwa mhubiri huyo, waliuwa padre huo52
nyumbani kwake miezi miwili baadae na kuhamia kwenye nyumba ya mfalme yaMtakatifu Andrews, ambako Knox alikuja kuisha mwaka mmoja baadae.Kutokana na uasi huo, malkia wa kikatoliki Maria wa Gise aliamua kutafuta msaadawa mfalme Henry II, mfalme wa Ufaransa, alietuma jeshi la meli na kushambulia nyumbaya kifalme ya mtakatifu Andrews. Mweli Julai, 1547, wanamatengezo waliokuwa ndani yangome hiyo walijisalimisha kwa jeshi la majini la Ufaransa wakachukuliwa mateka. Katiyao alikuwepo pia na John Knox, ambae alifungwa pingu kwenye viti vya meli akiwa hananafasi ya kubadirisha mkao wake. Pamoja na wafungwa wengine wa vita na waharibifuwengine , Knox alilazimishwa kusaidia kusukuma meli, afisa mmoja akiwa upande mmojakusubiri kuwapiga wafungwa ambao hawakuwa tayari kufuata maagizo katika kufanyakazi ngumu.Ndani ya meli, wafungwa walilazimishwa kushiriki misa na kutoa ishara ya kumheshimubikira Maria, au wateswe. Knox alikataa. Pale picha ya bikira Maria iliposukumizwa usonimwake ili aibusu, aliichukua nakuitupia baharini akisema, “Acha mama yetu ajiokoe; yeyeni mwepesi sana; acha ajifunze kuogelea.”Baada ya miezi kadhaa na kwa kuwa katika kipindi kikali cha msimu wa baridi kwenyemeli, afya ya Knox ilidhoofu sana. Pamoja nakuumwa bado alifariji wenzake katikamateso, akiwa na uhakika ya kwamba wataachiwa huru na kuendeleza kazi yake yakutangaza ukweli wa Biblia. Miezi kumi na tisa ya mateso makali, majaribu na maumivumakali. Inadhaniwa kuwa kwa ombi la mfalme wa Uingereza Edward VI John Knoxaliachiwa huru mwezi Februari 1549.April 7, 1549, Knox aliitwa kutumika kama mhubiri katika mji wa Berwick-upon-Tweed,chini ya Kanisa la Uingereza. Mwishoni mwa 1550, alihamishwa kama mhubiri wa kanisala Mtakatifu Nikolasi, mji wa Newcastle sehemu ya Taini; na 1551, aliwekwa kuwamsimamizi mkuu wa dini wa Mfalme pamoja na wengine watano, ikimpa nafasi yakuhubiria ufalme. Kwa kipindi hiki, alipinga taratibu ya kupokea meza ya bwana kwakupiga magoti na pia mafundisho ya kwamba mwili halisi wa Kristo upo kwenyeSakramentiKnox alikutana na Elizabeth Bowes, mahiri na msomi wa maandiko, ambae alikujakumtambua kama mwelekezaji wake kwa mambo ya kiroho, na Margery Bowes, mmojawa binti zake Elizabeth, ambae alimchumbia mwaka 1553 na kuoa muda mfupi baadae.Mwaka mmoja baadae alikuwa Geneva, Uswisi, akiwa ametoroka Uingereza alipoingiaMary Tudor kwenye utawala na kurudisha uKatoliki nchini Uingereza. Knox alichapishakipeperushi akimshambulia malkia huyo kwa msimamo wake wa kikatoliki pamoja namaaskofu waliomsaidia kuingia kwenye utawala, na pia kiongozi wa kirumi, Charles V,akimtaja kuwa “Adui wa Kristo kama NeroKuhubiri FrankfurtMuda mfupi baada ya kufika Uswisi, Knox alipokea barua ya mwaliko kuwa mchungajiwa kanisa la wakimbizi wa Uingereza wanaoishi mji wa Frankfurt, Ujerumani na53
- Page 3 and 4: MADA YA KWANZA.UTANGULIZI JUU YA HI
- Page 5 and 6: PERGAMOTHIATIRASARDIFILADELFIALAODE
- Page 7 and 8: b.Masadukayo, Hawa jina lao lilitok
- Page 9 and 10: Kujihusisha na shughuli za kijamii,
- Page 11 and 12: K. KUTENGANA KWA WAMISHENARI . Waka
- Page 13 and 14: Inaonekena Wayahudi hao Walianzisha
- Page 15 and 16: Kwa msaada wa Josephus (mwanahistor
- Page 17 and 18: 10. Yuda/Thadeo- mtume huyu alifany
- Page 19 and 20: Baadhi ya watu waliouawa katika kip
- Page 21 and 22: Mitume walifundisha kwamba sanamu s
- Page 23 and 24: manabii wa zamani wa Kiebrania. Ali
- Page 25 and 26: Ireneusi (130-202A.D) aliyezaliwa S
- Page 27 and 28: Kwa kiasi kikubwa mafundisho yake y
- Page 29 and 30: iv.Kanisa lenye kusitawi {kukua}. L
- Page 31 and 32: ix. Siku ya jumapili iliwekwa kuwa
- Page 33 and 34: Ilidaiwa kwamba maaskofu walikuwa b
- Page 35 and 36: ambao ulipaswa kutumiwa na makanisa
- Page 37 and 38: Utawa ulienea sana sehemu ya maghar
- Page 39 and 40: MADA YA TANOKIPINDI CHA THIATIRA; K
- Page 41 and 42: nyaraka hizo ziliandikwa na wahusik
- Page 43 and 44: Kugombea ukuu, Madai ya kanisa la m
- Page 45 and 46: maandiko ya John Wikrif na hivyo al
- Page 47 and 48: matengenezo na mengine mengi kulipe
- Page 49 and 50: waliongoza kikundi cha watu katika
- Page 51 and 52: Hivyo neno hilo wakapewa watu wale
- Page 53: Rafiki zake walimshauri John Calvin
- Page 57 and 58: Kufunguka kwa matengenezo ya kiprot
- Page 59 and 60: wadhifa wake, alifungwa jela kwenye
nyumbani kwake miezi miwili baadae na kuhamia kwenye nyumba ya mfalme ya
Mtakatifu Andrews, ambako Knox alikuja kuisha mwaka mmoja baadae.
Kutokana na uasi huo, malkia wa kikatoliki Maria wa Gise aliamua kutafuta msaada
wa mfalme Henry II, mfalme wa Ufaransa, alietuma jeshi la meli na kushambulia nyumba
ya kifalme ya mtakatifu Andrews. Mweli Julai, 1547, wanamatengezo waliokuwa ndani ya
ngome hiyo walijisalimisha kwa jeshi la majini la Ufaransa wakachukuliwa mateka. Kati
yao alikuwepo pia na John Knox, ambae alifungwa pingu kwenye viti vya meli akiwa hana
nafasi ya kubadirisha mkao wake. Pamoja na wafungwa wengine wa vita na waharibifu
wengine , Knox alilazimishwa kusaidia kusukuma meli, afisa mmoja akiwa upande mmoja
kusubiri kuwapiga wafungwa ambao hawakuwa tayari kufuata maagizo katika kufanya
kazi ngumu.
Ndani ya meli, wafungwa walilazimishwa kushiriki misa na kutoa ishara ya kumheshimu
bikira Maria, au wateswe. Knox alikataa. Pale picha ya bikira Maria iliposukumizwa usoni
mwake ili aibusu, aliichukua nakuitupia baharini akisema, “Acha mama yetu ajiokoe; yeye
ni mwepesi sana; acha ajifunze kuogelea.”
Baada ya miezi kadhaa na kwa kuwa katika kipindi kikali cha msimu wa baridi kwenye
meli, afya ya Knox ilidhoofu sana. Pamoja nakuumwa bado alifariji wenzake katika
mateso, akiwa na uhakika ya kwamba wataachiwa huru na kuendeleza kazi yake ya
kutangaza ukweli wa Biblia. Miezi kumi na tisa ya mateso makali, majaribu na maumivu
makali. Inadhaniwa kuwa kwa ombi la mfalme wa Uingereza Edward VI John Knox
aliachiwa huru mwezi Februari 1549.
April 7, 1549, Knox aliitwa kutumika kama mhubiri katika mji wa Berwick-upon-Tweed,
chini ya Kanisa la Uingereza. Mwishoni mwa 1550, alihamishwa kama mhubiri wa kanisa
la Mtakatifu Nikolasi, mji wa Newcastle sehemu ya Taini; na 1551, aliwekwa kuwa
msimamizi mkuu wa dini wa Mfalme pamoja na wengine watano, ikimpa nafasi ya
kuhubiria ufalme. Kwa kipindi hiki, alipinga taratibu ya kupokea meza ya bwana kwa
kupiga magoti na pia mafundisho ya kwamba mwili halisi wa Kristo upo kwenye
Sakramenti
Knox alikutana na Elizabeth Bowes, mahiri na msomi wa maandiko, ambae alikuja
kumtambua kama mwelekezaji wake kwa mambo ya kiroho, na Margery Bowes, mmoja
wa binti zake Elizabeth, ambae alimchumbia mwaka 1553 na kuoa muda mfupi baadae.
Mwaka mmoja baadae alikuwa Geneva, Uswisi, akiwa ametoroka Uingereza alipoingia
Mary Tudor kwenye utawala na kurudisha uKatoliki nchini Uingereza. Knox alichapisha
kipeperushi akimshambulia malkia huyo kwa msimamo wake wa kikatoliki pamoja na
maaskofu waliomsaidia kuingia kwenye utawala, na pia kiongozi wa kirumi, Charles V,
akimtaja kuwa “Adui wa Kristo kama Nero
Kuhubiri Frankfurt
Muda mfupi baada ya kufika Uswisi, Knox alipokea barua ya mwaliko kuwa mchungaji
wa kanisa la wakimbizi wa Uingereza wanaoishi mji wa Frankfurt, Ujerumani na
53