HISTORIA YA KANISA I DBT 2019 PRINT

21.03.2020 Views

Watu hawa waliamini kwamba kila mtu alitakiwa kuwa na Biblia katika lugha yake ya asilina ya kwamba Biblia ilitakiwa kuwa mamlaka ya mwisho na iliyokuu katika mamboya imani na maisha. Kanisa lilianzisha mateso dhidi ya wawadeni yaani wafuasi waWaldo.Watu hawa Kadili walivyoteswa ndivyo walivyokuwa wakiongozeka. Mnamomwaka 1211 wawadeni 80 walichomwa moto huko Ujerumani. Pita waldo alisaidia kuletamatengenezo ya kanisa kwani alisaidia kupatikana kwa Biblia katika Lugha zingine nakuhamasisha kila mtu kusoma Biblia. Waldo anajulikan kama mmoja wa wanamatengezoya kanisa watangulizi.2. JOHN WIKRIFHuyu alikuwa mwalimu wa Chuo kikuu cha Oxford. Mnamo mwaka 1378 Wikrif alitakakuleta matengenezo katika kanisa kwa kuwaondoa watumishi wa kanisa waliokuwadhalimu,na kuwanyang’anya mali ambazo aliamini kwamba ndizo zilizokuwa chanzo chawatumishi hao kuwa dhalimu. Alichapisha andiko lililoeleza maadili wanayotakiwakuwa nayo watumishi wa kanisa.Alifundisha kwamba wakati viongozi wa kanisa wanapokuwa mafisadi serikali ilitakiwakuchukua mali zao na kuwapa watu wengine wenye nia ya kumtumikia Mungu. Katikamwaka wa 1379 alianza kupinga dogma ya kanisa kwa kutoa madai yafuatayo; Yesu pekee ndiye aliyekuwa kiongozi mkuu wa kanisa na si papa. Biblia pekee ndio yenye mamlaka kuu na ya mwisho kwa waamini na si kanisa walapapa. Kanisa lilitakiwa kuiga mfano wa kanisa la agano jipya.Kwa msaada wa tajiri Lord Cobham John Wikrif alitafsiri Biblia katika lugha yakiingereza na kuisambaza katika maeneo mbalimbali . Alianzisha chama cha Wahubirimaskini na wakaanza kuzunguka katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo wakihubiri nenola Mungu watuMwaka 1382 alipinga fundisho la mageuzo ya maumbo ya mwili na damu ya Yesulinalojulikana kama transubstan-tiation. Mawazo yake yalipingwa vikali na kanisa naserikali na akafukuzwa ukufunzi. Mwaka 1402 Bunge La Uingereza lilipitisha sheria yahukumu ya kifo kwa watu wanohubiri mafundisho kinyume na yale yaliyokubaliwa nakanisa. Wahubiri maskini waliteswa vikali sana, baadhi walifungwa na kuchomwa motona kufukuzwa nchini. Viongozi wa kanisa walijaribu kuchoma moto Biblia zote zaKiingereza. Wikrif alifariki mnamo mwaka 1384.Shujaa huyu anakumbukwa sana katika historia ya kanisa kwa mchango wake wa kutafsiriBiblia katika Lugha ya kiingereza. Wikrif ndiye mtu wa kwanza kutafsiri Biblia kwa lughaya kingereza.3. JOHN HUSHuyu alikuwa ni mkuu wa chuo kikuu cha Plague huko Bohemia, mtawa na padre wakanisa katoliki. Mwaka 1401 John Hus alipata upadrisho. Padre huyu alipendezwa na42

maandiko ya John Wikrif na hivyo alianza kuhubiri mafundisho ya mtangulizi wakeWikrif.Alipinga mafundisho mbalimbali yasiyo ya ki-Biblia ya kanisa la Romani katoliki naakasisitiza watu kuishi maisha matakatifu. Alisisitiza kwamba Biblia ndiyo mamlaka yamwisho kwa mwamini na katika huduma za kanisa.Katika kitabu chake alichoandika juu ya kanisa, alifasili kwamba kanisa ni mwili waKristo, na Yesu Kristo pekee akiwa kiongozi wake mkuu. Alitetea nafasi ya ukuhani nakudai kwamba Mungu pekee ndiye aliyekuwa na uwezo wa kusamehe dhambi. Alielezakwamba hakuna mamlaka ya kanisa inayoruhusiwa kuanzisha mafundisho (doctrine)yaliyo kinyume na Biblia na kwamba Waamini hawatakiwi kutii maagizo yasiyo yakimaandiko.John Hus Alipinga baadhi ya mambo yafuatayo, Udhalimu wa mapadre kuuzwa kwa vyeti vya msamaha, kuondolewa kikombe cha divai kwa walei. Kanisa kuwa na mamlaka juu ya Biblia Uwezo wa Makuhani kusamehe dhambi Ukuhani wa wachache (crerism)Baada ya mashambulizi hayo mazito dhidi ya mafundisho ya kanisa Hus alifukuzwaupadre na akaambiwa abadilishe msimamo wake kwa kufuta kauli, jambo ambalo Hushakukubaliana nalo. Hatimae Hus alihukumiwa kifo na akachomwa moto. Hus akiwaanachomwa moto alitoa unabii kwa kusema “leo mnaniua mimi lakini miaka miamojaijayo Mungu atamwinua mtu mwingine ambaye matengenezo yake hayatawezakuzimwa” Kweli baada ya kipindi hicho Mungu alimwinua Martin Luther mwanamatengenezo mkuu kama tutakavyoona hapo baadae.4. JEROME SAVANAROLA.Alizaliwa Ferrara Italia mnamo mwaka 1452, alikuwa ni mtawa wa shiriki la wadominico.Mtu huyu alijaribu kuleta matengenezo katika kanisa na serikali. Alipinga uovu uliokuwaunafanywa na mapapa. Alisomea mambo ya ubinadamu na utabibu. Kufikia mwaka 1491alikuwa mhubiri maarufu kule Frolence.Alitabiri kwamba papa na mfalme wa Naples wangekufa siku moja, jambo ambalolilitokea kama alivyotabiri. Katika mahubiri yake alitabiri hukumu kubwa ambayoingekuja juu ya mji ikifuatiwa na kipindi chema ambapo Frolence ingewaunganisha watuwote wa Itali. Utimilizo wa unabii huu ulionekana kuwa ni kuvamiwa kwa Itali na mfalmeCharles VIII. Ambaye mwaka 1494 aliuondoa utawala dhalimu wa Frolence.Baada ya kuanzishwa kwa serikali mpya Saravano alipata umaarufu sana pale Frolencekupitia mahubiri yake na alileta mabadiliko mengi katika jamii. Alianzisha matengenezoya kodi, Kusaidia maskini na matengenezo katika mahakama. Aliubadilisha mji kutokakatika maisha ya kimwili na kuishi maisha ya kiroho.Kutokana na mabadiliko hayo kila mtu katika mji alikwenda kanisani na matajiri waliwapamisaada masikini.Wafanya biashara walirudisha vitu walivyokuwa wamewatapeli watejawao. Waimbaji waliacha kuimba nyimbo za kidunia na kuanza kuimba nyimbo za kumsifuMungu. Waliachana na maisha maovu, walichoma moto mawigi, vinyago, vitabu vya43

Watu hawa waliamini kwamba kila mtu alitakiwa kuwa na Biblia katika lugha yake ya asili

na ya kwamba Biblia ilitakiwa kuwa mamlaka ya mwisho na iliyokuu katika mambo

ya imani na maisha. Kanisa lilianzisha mateso dhidi ya wawadeni yaani wafuasi wa

Waldo.Watu hawa Kadili walivyoteswa ndivyo walivyokuwa wakiongozeka. Mnamo

mwaka 1211 wawadeni 80 walichomwa moto huko Ujerumani. Pita waldo alisaidia kuleta

matengenezo ya kanisa kwani alisaidia kupatikana kwa Biblia katika Lugha zingine na

kuhamasisha kila mtu kusoma Biblia. Waldo anajulikan kama mmoja wa wanamatengezo

ya kanisa watangulizi.

2. JOHN WIKRIF

Huyu alikuwa mwalimu wa Chuo kikuu cha Oxford. Mnamo mwaka 1378 Wikrif alitaka

kuleta matengenezo katika kanisa kwa kuwaondoa watumishi wa kanisa waliokuwa

dhalimu,na kuwanyang’anya mali ambazo aliamini kwamba ndizo zilizokuwa chanzo cha

watumishi hao kuwa dhalimu. Alichapisha andiko lililoeleza maadili wanayotakiwa

kuwa nayo watumishi wa kanisa.

Alifundisha kwamba wakati viongozi wa kanisa wanapokuwa mafisadi serikali ilitakiwa

kuchukua mali zao na kuwapa watu wengine wenye nia ya kumtumikia Mungu. Katika

mwaka wa 1379 alianza kupinga dogma ya kanisa kwa kutoa madai yafuatayo;

Yesu pekee ndiye aliyekuwa kiongozi mkuu wa kanisa na si papa.

Biblia pekee ndio yenye mamlaka kuu na ya mwisho kwa waamini na si kanisa wala

papa.

Kanisa lilitakiwa kuiga mfano wa kanisa la agano jipya.

Kwa msaada wa tajiri Lord Cobham John Wikrif alitafsiri Biblia katika lugha ya

kiingereza na kuisambaza katika maeneo mbalimbali . Alianzisha chama cha Wahubiri

maskini na wakaanza kuzunguka katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo wakihubiri neno

la Mungu watu

Mwaka 1382 alipinga fundisho la mageuzo ya maumbo ya mwili na damu ya Yesu

linalojulikana kama transubstan-tiation. Mawazo yake yalipingwa vikali na kanisa na

serikali na akafukuzwa ukufunzi. Mwaka 1402 Bunge La Uingereza lilipitisha sheria ya

hukumu ya kifo kwa watu wanohubiri mafundisho kinyume na yale yaliyokubaliwa na

kanisa. Wahubiri maskini waliteswa vikali sana, baadhi walifungwa na kuchomwa moto

na kufukuzwa nchini. Viongozi wa kanisa walijaribu kuchoma moto Biblia zote za

Kiingereza. Wikrif alifariki mnamo mwaka 1384.

Shujaa huyu anakumbukwa sana katika historia ya kanisa kwa mchango wake wa kutafsiri

Biblia katika Lugha ya kiingereza. Wikrif ndiye mtu wa kwanza kutafsiri Biblia kwa lugha

ya kingereza.

3. JOHN HUS

Huyu alikuwa ni mkuu wa chuo kikuu cha Plague huko Bohemia, mtawa na padre wa

kanisa katoliki. Mwaka 1401 John Hus alipata upadrisho. Padre huyu alipendezwa na

42

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!