HISTORIA YA KANISA I DBT 2019 PRINT

21.03.2020 Views

B. USHINDI WA WAKRISTOBaada ya miaka miambili ya mateso kanisa liliishinda dola ya Rumi na kupata amani.Mfalme Deokletiani katika utawala wake aliweka watawala wasaidizi katika majimboyake kutokana na ukubwa wa dola ya Rumi. Baba wa Kostantino alikuwa ni mmoja wawatawala wasaidizi, aliongoza majimbo ya Galia, Uingereza na Hispania, Baada ya kufakwa watawala wasaidizi kulitokea na kugombea madaraka baina ya watoto wao.Baba wa Kostantino alipofariki Kostantino alitangazwa kuwa mtawala badala ya babayake, na hivyo watoto wa watawala wengine waliamua kuanzisha mapigano ili kuuchukuautawala huo. Miongoni mwao hao aliyekuwa na nguvu ni Maksentio, huyu alikuwa ni mtualiyeshabikia mauaji ya wakristo. Walianzisha mapigano huko Italia maili kumi kutokaRumi mnamo 28.10. 312 BKWakiwa katika eneo la mapigano kabla ya vita kuanza Kostantino aliona alama ya msalabaangani ikiwa imeandikwa maneno yafuatayo, “Kwa alama hii utashinda”. Kostantinoaliitikia kwa sala na akaifanya alama ya msalaba kuwa nembo ya Jeshi lake na walipokuwavitani Kostantino aliwashinda kabisa maadui zake, adui yake mkuu Maksentio alikufakatika vita hiyo, hivyo Kostantino akawa mshindi.Kostantino alitambua kwamba msalaba ilikuwa ni alama ya wakristo na hivyo Mungu wawakristo ndio aliyekuwa amemsaidia katika vita hiyo. Mwaka uliofuata Kostantinoalitangaza PATANO LA AMANI na Wakristo, (Edict of Torelant). Patano hilililikomesha mateso juu ya wakristo katika dola yote ya Rumi.Patano hili lililowaletea amani wakristo katika dola ya Rumi lilikuwa na matokeo chanyana hasi katika kanisa.C. MATOKEO YA TAMKO LA AMANIMatokeo ya patano la amani yanaweza kuainishwa katika pande mbili ambazo ni matokeomazuri na matokeo mabaya kama ifuatavyo;I. MATOKEO MAZURI,i. Mateso juu ya wakristo yalikomeshwa.ii. Makanisa yaliyokuwa yamebomolewa wakati wa mateso yalijengwa tena kwa fedha yaserikali.iii. Maaskofu na wachungaji walisamehewa kodi.iv. Watumishi wa kanisa walianza kufadhiliwa na serikali na hawakutakiwa kuhukumiwakwa sheria za kawaida.v. Wakristo waliruhusiwa kujenga makanisa mahali popote katika dola ya Rumi.vi. Dhabihu za kipagani zilikomeshwa.vii. Kostantino alijenga makanisa makubwa katika miji ya Yerusalemu, Bethlehemu nakatika mji wa Kostantinapali ambapo ndio uliokuwa makao makuu mapya ya serikaliyake.viii. Watumwa waliachiwa huru.28

ix. Siku ya jumapili iliwekwa kuwa siku ya mapumziko kwa watumishi wa serikali.x. Mfalme Kostantino Alisaidia kuunda umoja wa kanisa kupitia mikutano mbalimbalialiyoiitisha, mfano mkutano wa Naikea mwaka 325 BK.xi. Mfalme Kostantino alikusudia kuufanya ukristo ukubaliwe na serikali kama dinizingine.II. MATOKEO MABAYA.i. Ilikuwa ni fahari kuwa mkristo, hivyo watu wengi walijiunga na ukristo kwamaslahi binafsi.ii. Watu walijiunga na ukristo ili waweze kupata vyeo katika kanisa na serikali.iii.iv.Maadili ndani ya kanisa yalianza kumomonyoka.Mambo ya kiroho yaliachwa kupewa kipaumbele na badala yake programumbalimbali zikapewa kipaumbele.v. Sherehe na tamaduni za kipagani polepole zilihamia kanisani, kwa kubadilishwajina na malengo na badhi zilibadilishwa kuwa sikukuu za kikanisa, mfanoKrismasi.(Kuabudiwa kwa bikira Maria kuliasiliwa kutoka ibada za kipagani zakuabudu miungu , Zeusi, mungu wa uzuri wa warumi na Diana mungu mwezi).vi.vii.Katika jimbo la mashariki serikali ililitawala kanisa mpaka likapoteza nguvu namaisha ya kiroho.Katika jimbo la magharibi kanisa lilipata nguvu dhidi ya serikali.D. WATAWALA WALIOFUATA BAADA KOSTANTINOKostantino hakutaka kutumia nguvu katika kuwafanya watu kuwa wakristo, alitaka jambohili lifanyike taratibu na kwa uchaguzi wa mtu mwenyewe, jambo hili halikufuatwa nawatawala waliofuata baada yake.Baada ya utawala wa Kostantino watawala waliofuatia walikuwa wakali mno walipigamarufuku ibada za kipagani na waabudu dini hizo walihukumiwa kifo na mali zaozilitaifishwa. Walivunja mahekalu ya kipagani, watawala hawa(wakristo) kwa kutumiajina la ukristo sasa walitumia njia zilezile mbaya zilizokuwa zimetumiwa na serikalikulitesa kanisa.E. AINA MBALIMBALI ZA MATESO.i. Katika kipindi cha Efeso kanisa liliteswa na wayahudi.ii. Katika kipindi cha Smirna kanisa liliteswa na dola ya Rumi.iii. Katika kipindi cha Pergamo ugomvi ulizuka miongoni mwao wenyewe(wakristo).F. UMOJA NA UTAWALA WA KANISA.Kanisa lililazimka kuwa na umoja kamili ili liweze kuwa na nguvu ya kukabiliana namateso yaliyoliandama na uzushi uliokuwa unajitokeza. Hivyo kanisa lilipambana namaadui wakubwa wawili ambao ni mateso na mafundisho potofu.29

B. USHINDI WA WAKRISTO

Baada ya miaka miambili ya mateso kanisa liliishinda dola ya Rumi na kupata amani.

Mfalme Deokletiani katika utawala wake aliweka watawala wasaidizi katika majimbo

yake kutokana na ukubwa wa dola ya Rumi. Baba wa Kostantino alikuwa ni mmoja wa

watawala wasaidizi, aliongoza majimbo ya Galia, Uingereza na Hispania, Baada ya kufa

kwa watawala wasaidizi kulitokea na kugombea madaraka baina ya watoto wao.

Baba wa Kostantino alipofariki Kostantino alitangazwa kuwa mtawala badala ya baba

yake, na hivyo watoto wa watawala wengine waliamua kuanzisha mapigano ili kuuchukua

utawala huo. Miongoni mwao hao aliyekuwa na nguvu ni Maksentio, huyu alikuwa ni mtu

aliyeshabikia mauaji ya wakristo. Walianzisha mapigano huko Italia maili kumi kutoka

Rumi mnamo 28.10. 312 BK

Wakiwa katika eneo la mapigano kabla ya vita kuanza Kostantino aliona alama ya msalaba

angani ikiwa imeandikwa maneno yafuatayo, “Kwa alama hii utashinda”. Kostantino

aliitikia kwa sala na akaifanya alama ya msalaba kuwa nembo ya Jeshi lake na walipokuwa

vitani Kostantino aliwashinda kabisa maadui zake, adui yake mkuu Maksentio alikufa

katika vita hiyo, hivyo Kostantino akawa mshindi.

Kostantino alitambua kwamba msalaba ilikuwa ni alama ya wakristo na hivyo Mungu wa

wakristo ndio aliyekuwa amemsaidia katika vita hiyo. Mwaka uliofuata Kostantino

alitangaza PATANO LA AMANI na Wakristo, (Edict of Torelant). Patano hili

lilikomesha mateso juu ya wakristo katika dola yote ya Rumi.

Patano hili lililowaletea amani wakristo katika dola ya Rumi lilikuwa na matokeo chanya

na hasi katika kanisa.

C. MATOKEO YA TAMKO LA AMANI

Matokeo ya patano la amani yanaweza kuainishwa katika pande mbili ambazo ni matokeo

mazuri na matokeo mabaya kama ifuatavyo;

I. MATOKEO MAZURI,

i. Mateso juu ya wakristo yalikomeshwa.

ii. Makanisa yaliyokuwa yamebomolewa wakati wa mateso yalijengwa tena kwa fedha ya

serikali.

iii. Maaskofu na wachungaji walisamehewa kodi.

iv. Watumishi wa kanisa walianza kufadhiliwa na serikali na hawakutakiwa kuhukumiwa

kwa sheria za kawaida.

v. Wakristo waliruhusiwa kujenga makanisa mahali popote katika dola ya Rumi.

vi. Dhabihu za kipagani zilikomeshwa.

vii. Kostantino alijenga makanisa makubwa katika miji ya Yerusalemu, Bethlehemu na

katika mji wa Kostantinapali ambapo ndio uliokuwa makao makuu mapya ya serikali

yake.

viii. Watumwa waliachiwa huru.

28

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!