21.03.2020 Views

HISTORIA YA KANISA I DBT 2019 PRINT

You also want an ePaper? Increase the reach of your titles

YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.

P.O.BOX 1917 MBEYA TANZANIA

Email: Elamseminary@gmail.com. Tel 0762532121

Kuwaandaa Watendakazi Kwaajili Ya Mavuno Ya Nyakati Za Mwisho

LUKA 10:2

By, Rev.Dr. Erick L, Mponzi (ThD)

Msingi wa Kujenga Watendakazi na Viongozi Watumishi

Wanaojizidisha na wenye Maono ya Kuigusa Dunia Nzima.


©Copyright, ECHASE 20014


MADA YA KWANZA.

UTANGULIZI JUU YA HISTORIA YA KANISA.

A.UTANGULIZI

Somo hili linaanza na kupaa kwa Yesu Mbinguni katika mlima wa mizeituni kama mwaka

wa 30 .AD na linaishia na kurudi kwa Yesu mara ya pili kupitia kwenye mlima wa

mizeituni katika kipindi cha mwisho {ufu 19-16-26, Zek 14:1-9}

Wanahistoria ya kanisa hawakubaliani katika namna ya ugawaji wa vipindi vya historia

ya kanisa .Baadhi hugawa vipindi kulingana na matukio muhimu kuhusu watu Fulani

maarufu, mfano kutawazwa kwa papa wa kwanza mnamo mwaka 590 A.D, au wakati wa

matengenezo ya Martin Luther, alipoandika andiko {Thesis} lake lenye hoja 95 na

kulibandika katika mlango wa kanisa huko Witenberg Ujerumani mwaka 1517 .

Baadhi pia hupenda kugawa vipindi katika historia ya kanisa kulingana na matukio

mbalimbali yaliyoleta athari katika kanisa, mfano kuongoka kwa Kiongozi mkuu wa Dola

ya Rumi Mfalme Kostantino mwaka 313 AD .Au patano la amani la Westphalia mwaka wa

1646.

Pia wataalamu wengine hugawa vipindi vya kanisa kwa kufuata mtindo wa kinabii kwa

kuzingatia orodha ya makanisa saba (7) kama yalivyoainishwa katika kitabu cha Ufunuo

wa Yohana sura ya pili na ya tatu.

Katika somo hili tutagawa vipindi vya historia ya kanisa kwa kufuata mhutasari wa

makanisa saba yanayopatikana katika kitabu cha Ufunuo wa Yohana Sura ya pili na ya tatu

ambapo vipindi mbalimbali vya kanisa vimeorodheshwa kwa njia ya kinabii.

B. DHANA YA HISTORIA.

Historia kama somo inafafanuliwa kwamba ni somo linalohusu matukio mbalimali katika

vipindi mbalimbali vya maendeleo ya mwanadamu.

Baadhi ya wataalamu wanafafanua kwamba historia ni kumbukumbu za shughuli za

binadamu katika vipindi viliyopita mpaka sasa. Kwahiyo historia huhusika na kuainisha

matukio mbalimbali muhimu yaliyotokea katika vipindi mbalimbali katika jamii ya

mwanadamu.

C. MAANA YA HISTORIA YA KANISA

Historia ya Kanisa ni fani inayochunguza historia ya Ukristo na ya miundo yake

mbalimbali tangu Kanisa lilipoanzishwa na Yesu Kristo katika karne ya 1 hadi leo

Ni taaluma inayoelezea vipindi mbalimbali ambavyo kanisa limepitia tangu kuanzishwa

kwake mpaka Yesu kristo atakapokuja kulichukua kwenda mbinguni .

1


D. SABABU ZA KUJIFUNZA HISTORIA YA KANISA

Kuna sababu nyingi ambazo zinatufanya tujifunze historia ya kanisa na kuifanya kuwa

mojawapo ya somo linalotakiwa kufundishwa katika shule za Biblia na vyuo vya thiolojia.

Baadhi ya sababu hizo ni:-

1. Historia ya kanisa inatusaidia kutambua jinsi kanisa lilivyoanza na jinsi

lilivyokabiliana na changamoto mbalimbali.

2. Inatusaidia kujifunza misimamo ya kiimani ya mababa wa kwanza wa kanisa na

kututia moyo sisi kuitetea imani kama wao walivyoitetea.

3. Inatusaidia kujua changamoto mbalimbali kanisa lilizopitia tangu kuanzishwa kwake

mpaka sasa, mfano changamoto ya mateso wakati wa watawala mbalimbali wa Dola

ya Rumi, kama vile kusulubiwa kwa mtume Petro, kukatwa kichwa mtume Paulo,

kuchunwa ngozi na kutumbukizwa kwenye mafuta yanayochemka motoni Mtume

Bathromayo.

4. Inatusaidia kujua jinsi wakristo waliotutangulia walivyoitetea imani kwa kuwa tayari

kufa bila kuisaliti imani mfano John Huss Martini Luther, Porykap, Klement Origen,

Urlich Zwingri. N.k

5. Inatusaidia kujua namna Mungu anavyotimiza Mpango wake wa milele hapa duniani

kupitia kanisa.

D.MAKANISA SABA YA ASIA NDOGO

Mfalme Domitiani alimpeleka mtume Yohana uhamishoni katika kisiwa cha Patmo kwa

sababu ya imani. Akiwa katika kisiwa hiki mtume Yohana alipokea jumbe toka kwa

Bwana Yesu Kristo kwa ajili ya makanisa saba yaliyokuwa katika Asia ndogo. Jumbe hizo

baadae ziliingizwa kwenye orodha ya kanuni ya Maandiko Mtakatifu na sasa ni kitabu

cha Ufunuo wa Yohana. Mtume Yohana alipokea jumbe hizi akiwa na umri wa kama

miaka 90.

Jumbe hizi zilikuwa na matuimizi ya aina nne ambayo ni

1. Zilikuwa ni jumbe maalum kwaaiili ya makanisa katika wakati wa mwandishi.

2. Zilidhihirisha na kufunua hali ya kiroho ya kila kanisa lililoandikiwa jinsi ilivokuwa.

3. Zilikuwa ni jumbe kwa waamini wote wa zama zote za kanisa.

4. Zilikuwa ni muhtasari wa kinabii wa historia ya kanisa.

F. MUHTASARI WA MPANGILIO WA MAKANISA SABA YA ASIA NDOGO.

KANISA KIPINDI MUDA

EFESO KIPINDI CHA MITUME (Kanisa la Mitume)

Tangu kupaa kwa Yesu Kristo Mbinguni mpaka kifo cha

Mtume Yohana.

SMIRNA

KIPINDI CHA MATESO (Kanisa la mateso).

Tangu kuchomwa moto mji wa Rumi mpaka kuongoka kwa

mfalme kostantino.

30 .BK- 100

B.K

64. B.K – 313

B.K

2


PERGAMO

THIATIRA

SARDI

FILADELFIA

LAODEKIA

KIPINDI CHA KIFAHARI (Kanisa la Kifahari)

Tangu kuongoka kwa mfalme Kostantino mpaka kuanguka

kwa dola ya Rumi.

KIPINDI CHA KIPAPA (Kanisa la Kipapa)

Tangu kuanguka kwa dola ya Rumi mpaka kuanguka kwa

Kostantinopali

KIPINDI CHA MATENGENEZO (Kanisa la Matengenezo)

Tangu kuanguka kwa Kostantinopali mpaka patano la

Westphalia

Kipindi cha umisheni au uinjilisti. (KANISA LA

UMISHENARI)

Tangu patano la Westphalia mpaka vita ya kwanza ya Dunia.

KIPINDI CHA UONGO (kanisa la uongo/vuguvugu)

Tangu vita ya kwanza ya dunia mpaka kipindi cha Milenia

mpya.

313 B.K -476.

B.K

476. B.K -

1453 .

1453.- 1648

1648-1914

1914…

3


MADA YA PILI

KIPINDI CHA EFESO.

{Kanisa la Mtume}

A. UTANGULIZI.

Kanisa la Efeso (ufunuo wa Yohana 2:1-7)

MUDA; Tangu kupaa kwa Yesu Kristo kama mwaka 30.AD.Mpaka kifo cha mtume

Yohana kama mwaka wa 100. B.K.

Efeso ulikuwa mji muhimu katika pwani ya Asia ndogo na ulipewa jina la heshima la

Nuru ya Asia. Waefeso waliabudu miungu ya kiasia ambayo ni Artemi, ambae pia aliitwa

Diana. Hekalu la artemi lilihesabiwa kuwa mojawapo ya maajabu ya dunia ya wakati ule.

Mahali pengine walipoabudia paliitwa Augusteum. Mahali hapo walitumia kumwabudu

mfalme . kiwango cha kiburudani za kidunia zilikuwa nyingi na inakadiliwa kuwa ukumbi

wa Efeso ulikuwa na uwezo wa kuchukua watu 25,000.

Kipindi hiki kinaitwa kipindi cha mitume kwa sababu karibia mitume wote12 wa

mwanakondoo {Yesu} waliishi katika kipndi hiki. Kipndi hiki kiliishia na kifo cha Mtume

Yohana ambae alikufa kifo cha kawaida akiwa mzee mwenye umri wa kama miaka 100.

Kuna walimu wa theologia wanaofundisha kwamba mitume na manabii waliishia katika

kipindi hiki. Jambo ambalo si kweli kabisa kwani huduma hizi zimekuwepo katika vipindi

vyote vya kanisa japokuwa katika vipindi fulani zilififia, lakini zimekuwepo katika zama

zote za kanisa.

B.ULIMWENGU WA WAKATI WA MITUME

Kanisa lilikutana na upinzani mara tu lilipoanza.Upinzani huo ulitokana na makundi

mbalimbali

1. Dini ya kiyahudi. Wayahudi walikuwa ni adui namba moja wa kanisa .walilivamia

kanisa wakati lingali changa kwa kushirikiana na mfalme wa kirumi walimsulibisha Yesu

Kristo. Ndani y dini ya kiyahudi kulikuwa na makundi/madhehebu mbalimbali ambayo

yalishiriki katika kulitesa kanisa. Baadhi ya makundi hayo ni:-

a).Mafarisayo. Hawa walianza katika kipindi cha Ezra na Nehemia waliporudi toka

uhamishoni Babeli wakati ukuhani mpya ulipoanzishwa. Mafarisayo Waliamini juu ya

‣ Ufufuo wa wafu

‣ adhabu kwa wenye dhambi

‣ Kutokufa kwa nafsi

‣ Uwepo wa malaika na huduma zao

‣ Kila kitu kinamtegemea Mungu.

‣ Mtazamo wao wa kisiasa ulikuwa ni wa kiyahudi na waliogopa kushirikiana na watu

wasiokuwa mafarisayo. Mfano Wasamaria, na Wamataifa na kwa namna zote

walizishika sheria za Musa na walifanya tohara.

4


b.Masadukayo, Hawa jina lao lilitoka kwa Sadoki kuhani mkuu wa wakati wa Daudi toka

uzao wa Haruni Kuhani Mkuu. Hivyo walikuwa ni uzao wa kikuhani.Wao hawakuamini

ufufuo wa wafu wala uwepo wa malaika.

2. Dola ya Kirumi,. Mwaka 63KK. mfalme wa Rumi Julius Kaizari aliivamia na

kuishinda Palestina na akaanzisha utawala wa kirumi katika nchi ya palestina . Huu

ulikuwa ni ufalme wanne uliokuwa umeishinda na kuitawala Israeli kulingana na unabii wa

Danieli . Israeli ilikuwa chini ya utawala wa dola ya Rumi Yesu Kristo alipozaliwa na

katika kipindi cha maisha yake hapa duniani.

a. Dini ya kipagani(Heathenism), hii ilikuwa ni dini ambayo mianzo yake ni mtawala

Nimrodi katika mnara wa Babeli na dini hii baadae ilisambaa katika maeneo mbalimbali

yaliyoizunguka Babeli mpaka Misri, Ugiriki na Rumi.Waliabudu miungu ya kigeni {Yer

2:25}. Ilikuwa ni miungu ya zamani sana ya Kibabeli, ilikuwa na majina mbalimbali katika

nchi mbalimbali, mfano A=`570rtemi, Diana, Osiris, Jupita Appolo Zeus. N.K

b. Ibada ya mfalme. Hii ilikuwani mojawapo ya tamaduni ya dola ya Rumi. Baadhi ya

wafalme wakirumi walijitangaza kwamba wao ni miungu na wakadai kwamba wananchi

wao wanatakiwa kuwaabudu.hivyo Ibada ya kuwaadudu wafalme {makaisari} ilianzishwa.

Kukataa kumwabudu Kaisari kungepelekea mtu kuhukumiwa adhabu ya kifo. Ibada

ya kumwabudi mfalme ilikuwa imerithiwa toka kipindi cha babeli. Kaisari Domitiani ni

mojawapo wa Makaisari waliosimamisha sanamu zao na kudai ibada zifanywe juu yao.

c. Wanafasalsafa wa Kigiriki. Kulizuka falsafa za kigiriki ambazo zilikuwa zinasisitiza

kwamba lengo la maisha ni furaha na anasa. Walisisitiza kwamba maarifa yanaweza

kupatikana kwa njia ya kufikiri {Logic}.Waliegemea katika vitu vinavyooneka tu

(materialism). Falsafa hizi ndizo ambazo zilikuwa zimeshikiliwa na watu mbalimbali

katika kipindi hiki.

Falsafa hizi zilisisitiza kwamba maisha ni kula na kunywa kwa sababu baada ya kufa

mwanadamu alikuwa anaoza na kwamba hakukuwa na maisha baada ya kufa.

C. KUANZA KWA KANISA.

Kanisa lilianza Yerusalemu siku aliposhuka Roho mtakatifu katika chumba cha juu katika

hekalu la Yerusalem. Baada ya Yesu Kristo kupaa Mbinguni wanafunzi walirudi toka

mlima wa Mizeituni mpaka hekaluni na kukaa katika chumba cha juu. Waliomba na

kusubiri kuvikwa nguvu. Baada ya siku kumi Roho Mtakatifu alishuka na wote

waliokuwemo kwenye chumba cha juu walijazwa Roho Mtakatifu na kuanza

kumwazimisha Mungu kwa Lugha zingine. Kazi ya uinjilisti ilianza papo hapo, mtume

Petro alihubiri na watu 3000 wakaokolewa na kubatizwa. Hii inahesabiwa kwamba ndio

mwanzo wa kanisa la agano jipya.

Matokeo ya kujazwa Roho Mtakaifu

5


1. Kutiwa nuru. Waamini walitiwa nuru katika akili na fahamu zao na wakapata

kuyaelewa maandiko matakatifu.

2. Kutiwa nguvu na ujasiri, wamini hawa walitiwa nguvu na ujasiri na kuwezeshwa

Kulihubiri Neno la Mungu kwa ujasiri.

3. Kutenda ishara na maajabu. Mitume waliwezeshwa kutenda miujiza sawasawa na

ahadi ya Yesu Kristo Mk 16:15-20.

D. WANACHAMA KTIK A KANISA.

Wanachama katika kanisa la mwanzo walikuwa ni wayahudi {proselytes} ambao twaweza

kuwagawanya katika makundi manne. ambayo ni ;

1. Waebrania . hawa walikuwa ni wayahudi ambao baba zao walikaa Palestina na

walikuwa ni uzao wa Kiebrania.

2. Hellenists, (Grecian Jews",) walikuwa ni wayahudi waliokuwa wanakaa katika nchi

zingine wengi wao walikaa Uyunani. Mdo 6:1

3. Proseliti (Proselytes).Walikuwa ni watu wamataifa waliokuwa wamefanyika kuwa raia

wa kiyahudi, walifuata sheria za kiyahudi na walijiunga na dini ya Kiyahudi. Pia

walitahiriwa kama wayahudi. Mfano Nikolasi {Mdo 6:5}

E. UONGOZI NA UTAWALA WA KANISA.

Kanisa la kwanza halikuwa na Mfumo wa uongozi wa kiutawala kama ilivyo sasa. Kila

kanisa la mahali pamoja lilikuwa na uongozi wake uliojitegemea. Hakukuwa uongozi

uliokuwa unasimamia makanisa yote. Mitume walikuwa ni waangalizi wa kanisa na

hawakujiweka kuwa watawala wa kanisa bali watumishi wa kanisa.

F. MAFUNDISHO YA KANISA LA KWANZA. Mafundisho ya kanisa la kwanza

yalikuwa rahisi, Agano jipya lilikua bado halijaandikwa. Ujumbe wao ulikuwa na maeneo

machache ambayo ni ;

i. Uungu wa Yesu Kristo. Yesu kristo wa nazareti ni mwana wa Mungu na ni nafsi

hai. Maelezo haya yalisababisha mateso katika kanisa .

ii. Ufufuo wa Yesu Kristo. Ufufuo wa Yesu kristo ulikuwa ni kiini cha mahubiri au

ujumbe wa kanisa la kwanza.

iii. Toba, Ubatizo wa maji na ubatizo wa Roho Mtakatifu. Waliweka mkazo juu ya

toba inayoleta ondoleo la dhambi na ubatizo wa maji na ujazo wa Roho mtakatifu .

iv. Kurudi kwa Yesu Kristo mara ya pili. Walihubiri kwamba Yesu Kristo atarudi

tena {Mdo 3:20-21, 1The 4;15-17}Hili lilikuwa ni tumaini la Baraka kwa waamini

wote.

G. KUSHINDWA KWA KANISA LA KWANZA.

Kanisa la kwanza lilishindwa kufikia kusudi kwa sababu zifuatazo.

Kukosa maono ya umisheni . Mungu aliliagiza kanisa kwenda kuhubiri Injili

ulimwenguni kote MT20:28, Mk 16:16} lakini kanisa la kwanza hawakufanya hivyo bali

walijihusisha na umisheni katika Yerusalemu.

6


Kujihusisha na shughuli za kijamii, Mitume walianza kujihusisha na mambo ya kijamii

{kiutawala} kwani shughuli zote za kanisa za kila siku zilifanywa na wao.Tunaona Petro

aliyekuwa mhubiri anaanza kujihusiha na mambo ya kiutwala.

Mitume walifika mahali wakagundua tatizo hilo na wakachagua wahudumu saba

waliotakiwa kushughulikia mambo ya kiutawala ili wao wadumu katika kulihubiri Neno

na Kuomba.

Bwana alilionya kanisa lake “Tubu na ukafanye mambo ya kwanza la sivyo nitakiondoa

kinara chako mahli pake. Mungu alitimiza Neno lake kama Tutakavyo ona hapo baadae.

H. KUENEA KWA KANISA LA KWANZA. Kupanuka kwa kanisa tangu mahubiri ya

Stefano {mwaka 35. AD} hadi mkutano wa Yerusalemu {mwka 48. AD}.Mambo ya

msingi katika kipindi hiki yalikuwa ni upandaji wa makanisa. Kipindi hiki kifupi kilikuwa

na umuhimu mkubwa kwa kanisa. Japokuwa kanisa mwanzo lilikuwa Yerusalemu tu sasa

lilipandwa katika maeneo mengine kama vile Siria na Asia ndogo na kuelekea Ulaya.

Waamini wa kwanza walikuwa ni Wayahudi lakini baada ya kipindi hiki kifupi waamini

wengi walikuwa ni wamataifa .

Mwanzoni Injili ilihubiriwa kwa kiebrani na kwa kiaramu lakini baadae iligundulika

kwamba ulimwengu mzima ungefikiwa na Injili kupitia lugha ya Kigiriki kwa sababu

kigiriki wakati huo kilikuwa ni lugha ya mawasiliano ya kimataifa kama ilivyo

kiingereza kwa dunia ya sasa.

I KUTESWA KWA KANISA NA VIONGOZI WA KIYAHUDI.

Yesu aliwaagiza mitume kwenda kuhubiri Injili duniani kote lakini wao walipenda kukaa

Yerusalemu .Mungu alikasirika na akaamua kuruhusu mateso katika kanisa .{Mdo 9}

1. Mahubiri ya Stefano {.Mdo 6:1-4, 7} Kwa sababu ya imani yake kwa Mungu Stefano

alihukumiwa kuuawa na kuwa mfia dini wa kwanza katika imani ya kikristo. Kijana

mmoja mfarisayo wa Tarso Sauli alishuhudia mauaji ya Stefano na Baadae kijana huyo

akawa kiongozi mkuu wa mauaji ya wakristo katika taifa la wayahudi.

Kutokana na tukio hili waamini wote walikimbia Yerusaelimu isipokuwa mitume {Mdo

8:1-4}.Waamini hao walisambaa maeneo mbalimbali na kila mahali walipokwenda

walilihubiri Neno . Kwa njia hii kwa muda mfupi Injili ilipata kuenea kwa haraka katika

maeneo yote yaliyoizunguka Yerusalemu.

2. Kanisa Linakwenda Samaria,{ Mdo 8}.Wasamaria walikuwa ni chotara ambao asili

yao ilikuwa ni Ashuru ambpo walihamishiwa katika eneo la Kaskazini mwa Israeli. Pale

waisraeli walipochukuliwa kwenda utumwani Ashuru {Irani}. Mchanganyiko wa wageni

hao na mabaki ya waisraeli ambao hawakwenda utumwani Ashuru yaliunda jamii ya

Wasamaria kwa njia ya kuzaliana, kutokana na kuoana kati ya wageni na mabaki ya

waisraeli. Watoto waliozaliwa walikuwa chotara na ndio kizazi cha Wasamaria .

Wasamaria Walikuwa na hekalu lao katika mlima Gelzimu na walivitumia vitabu vitano

vya Musa pekee kama Biblia yao. Kwahiyo Wayahudi hawakuchangamana nao.

Roho Mtakatifu alimwambia Shemasi Filipo kwenda kuhubiri Neno Samaria. Mungu

alimtumia kufanya ishara na maajabu kwa jina la Yesu huko Samaria. Uamsho mkuu

7


ulitokea huka Samaria. Watu wa huko Samaria waliokoka na kubatizwa. Mitume

walipopata habari hii walikuja kuwaombea ujazo wa Roho Mtakatifu. Baada ya maombi

hayo Wasamaria walijazwa Roho Mtakatifu.

3. Injili inakwenda Afrika {Mdo 8 }. Roho mtakatifu alimtuma mwinjilisti Filipo kwenda

kumhubiri Neno Toashi wa Kushi {Waziri wa fedha wa Ethiopia}. Filipo alimwongoza

towashi huyu kwa Bwana na kisha akambatiza. Inaaminika kwamba toashi huyu alipeleka

Injili Afrika kwa sabau alikuwa ni mkazi wa Bara la Afrika katika nchi ya Ethiopia

J. MTESI WA KANISA ABADILI UPANGA {Mdo 9 }

Sauli wa Tarso ambae ndiye aliekuwa mtesi mkuu wa kanisa kwa kipindi hiki aliokoka

baada ya kukutana na Yesu Kristo alipokuwa safarini kuelekea Dameski kuwakamata na

kuwaua waamini {Mdo 9:20 }. Mara baada ya kuokoka alianza kuihubiri Injili {Kumhubiri

Kristo Yesu}. Paulo aliweka chini upanga wake wa mauaji na kuchukua upanga wa

Neno la mungu ambao hakuuacha mpaka kifo chake.{ 2Tim 4:7}.

Paulo alikwenda katika jangwa la Arabia kwa miaka Mitatu ambapo alipata mafunuo zaidi

toka kwa Mungu. Baada ya hapo alirudi Yerusalemu kuonana na mitume. Baada ya Sauli

kukutana na Ndugu alirudi tena Tarso. Kanisa lilipata raha baada ya kuokoka kwa Sauli wa

Tarso.{Gal 1:16-18, Mdo 9:20-31}.

5. Injili inakwenda kwa watu wa mataifa{Mdo 10 }. Mtume Petro alitumwa kwenda

kumhubiri Kornelio mtu wa Mataifa. Mtume Petro ndiye aliyefungu mlango wa Injili kwa

wayahudi na kwa Watu wa mataifa. Petro alihubiri Injili kwenye nyumba wote waliokuwa

wamekusanyika wakimsikiliza walishukiwa na Roho Mtakatifu na wakaanza kunena kwa

Lugha mpya, kisha Petro akawabatiza. Huu ulikuwa ni mwanzo wa Injili au kanisa

kuwafikia watu wa mataifa.

6. Injili inakwenda Asia Ndogo {Mdo 13} Katika sura hii tunaona wito wa wamishenari

wawili kwenda kuhubiri katika nchi ya kigeni. Wito huu na kutumwa huku kulifanyika

Antiokia mahali ambapo wanafunzi walipewa jina na kuitwa Wakristo kwa mara ya

kwanza {Mdo 11:26}.

Balnaba alikuwa ni mchungaji wakati Paulo alipokuja kutoka Dameski. Wanafunzi wote

walimwogopa Paulo, Balnaba alimpokea na kumtambulisha kwa kanisa {mitume

Yerusalemu} Mdo 9;26-29.

Japokuwa mitume walimtuma Balnaba Antiokia mahali ambapo kanisa lilikuwa na uamsho

mkubwa aliamua kufunga safari kutembea zaidi ya KM 150 kwa meli ili kwenda

kumtafuta Sauli wa Tarso .Alimpata na kisha akamchukua na kuja nae Antiokia bila kujua

kwamba miaka ya mbele sauti ya Bwana ingemwita kupitia njia ya unabii

‘Nitengeeni Balnaba na Sauli kwa kazi niliowaitia.{Mdo 13:1-5 }.

Balnaba na Paulo waliombewa na kanisa na kisha kwenda kwenye umisheni wao kuelekea

Asia ndogo mahali ambapo walianzisha makanisa mengi. Kama inavyoainishwa katika

Matendo ya Mitume 13 na 14. Baadae walirudi Antiokia mahali ambapo palikuwa ni kituo

chao cha umisheni.

8


K. KUTENGANA KWA WAMISHENARI . Wakati mitume hao {Paulo na Balnaba}

walipokuwa wanajiandaa kwaajili ya safari yao ya pili ya umisheni walipishana. Kulitokea

kutokuelewana katika jambo moja. Balnaba alitaka kumchukua Marko{ ambae aliwaacha

katika safari ya kwanza ya umishenari na kurudi Yerusalemu} ili waende nae katika safari

ya pili ya umisheni, lakini Paulo alikataa kuambatana nae, hivyo kukatokea mgongano kati

yao na kisha wakaamua kutengana.

Hapa tunaona moyo wa kichungaji wa Balnaba, japokuwa Marko alishindwa katika

safari ya kwanza ya umishenari aliamua kumpa nafasi nyingine. tuna mwona Paulo

akiwa mtu wa kushikilia kanuni kuliko kumpendeza mtu yeyote. Mtu ambae yuko tayari

kuvunja mahusiano na Balnaba kuliko kukubaliana nae. Miaka ilipita na Mtume Paulo

akakomaa kiimani. Mtume Paulo ambae alisema katika uchanga wake : mimi si duni

kuliko hao mitume wakubwa {2Kor 11:5}. Baadae alisema ‘Mimi ni wa kwanza kwa

wenye dhambi {1Tim 1:16}. Paulo alifika mahali pakujitambua, kujisifu kulibadilishwa na

kujishusha na upendo ulichukua nafasi mahali pa chuki na kanuni.

Katika waraka wake wa pili kwa Wakorintho alisisitiza sana upendo na msamaha. Baadae

tunamwona Mtume Paulo akiwa katika upweke gerezani akisubiri kunyongwa.

Alimwagiza Timotheo kumleta Marko. Marko huyu huyu ndiye aliyemkataa wakati

wanafanya huduma na Balnaba.

Kutokana na hili tunajifunza ya kwamba tusimkatae mtu kutokana na makosa aliyoyafanya

kwa sababu twaweza kumhitaji tena baadae. Tuwasaidie wakosaji kwa upendo bila

kuwahukumu.

7. Mkutano wa Yerusalemu. {48.B.K}. Tatizo lilitokana na kuokoka kwa watu wa

wamataifa na kujiunga na kanisa. Wakristo wakiyahudi walikuwa na mitazamo tofauti

tofauti juu ya hili .Walikuwa na mitazamo ifuatayo:

1. Kundi lenye msimamo mkali. Kundi hili liliamini ya kwamba hakuna wokovu nje ya

Israeli . Kwa hiyo ingawa wamataifa wamempokea Yesu Kristo kama Masihi wao kwahiyo

walipaswa kutahiriwa na kushika Torati ya Musa {Sheria za Kiyahudi} Ili waweze

kuokolewa Bila kufanya hivyo wokovu wao ungekuwa ni batili.

Kundi la wenye mabadiliko.Hawa waliamini kwamba wokovu ni kwa njia ya imani katika

Yesu Kristo. Bila ya kushika sheria za kiyahudi. Wao waliamini kwamba sheria za

kiyahudi haziwahusu watu wa mataifa. Paulo na Balnaba walikuwa mojawapo wa watu

wenye mtazamo huu. Mkutano uliitishwa Yerusalemu ili kushughulikia jambo hili muhimu

la mafundisho kutokana na watu wa mataifa kumpokea Yesu Kristo kama Bwana na

Mwokozi wao. Baada ya majadiliano marefu Mitume na Wazee walifikia hitimisho ambalo

lilithibitishwa na Roho mtakatifu kwamba Wamataifa hawakuwa chini ya Sheria za

kiyahudi na kwamba walichotakiwa kufanya ni kujiepusha na Ibada ya sanamu, kula

nyama iliyosongolewa na damu, kujiepusha na uasherati na uzinzi.

Mitume waliandika barua na ikapelekwa kwa kanisa la mataifa kwa mikono ya Paulo,

Balnaba, Yuda na Sila. Walipofika Antikoa walilikusanya kanisa na kuwapa ujumbe wa

kikao cha mitume na wazee kilichofanyika Yerusalemu kuhusu tatizo lao. Waamini hawa

walifurahi sana kupata ujumbe wenye kuwatia moyo {Mdo 15:30-31}

9


L. KANISA MIONGONI MWA MATAIFA.

Tangu mauaji ya Stefano (48 B.K) mpaka mauaji ya Paulo mtume mwaka 68 B.K

Katika kipindi hiki chote tunategemea kitabu cha Matendo ya Mitume, nyaraka za Paulo na

waraka wa kwanza wa Petro. Umisheni wa mtume Paulo na Watendakazi wenzake

ulifanyika katika dola yote ya Rumi. Wakati mitume wengine walikwenda nchi za

mbali zaidi. (hii ni kulingana na mapokeo).

Idadi ya waamini wa kimataifa ilikua kwa kasi sana wakati idadi ya waamini wa kiyahudi

iliendelea kushuka.Wayahudi walianza kukasirika na kufanya fitina dhidi ya kanisa na

walikuwa tayari kuanzisha mateso dhidi ya wakristo.

Safari Ya Pili Ya Mtume Paulo

Kwa sababu ya kupishana kwa Balnaba na Paulo, Balnaba alimchukua mpwa wake

Yohana (Marko) na kwenda katika nchi ya kwao Kipro, Paulo alimchukua nabii Sila katika

safari yake ya pili ya umisheni na kwenda kuyatembelea makanisa waliyokuwa

wameyafungua katika safari ya kwanza walipokuwa na Balnaba. Paulo alikusudia kwenda

Bithinia lakini Roho Mtakatifu akamkataza. Kisha walielekea Troa mji wa Kaskazini

Magharibi ya Asia ndogo.

Injili inakwenda Ulaya. (Wito wa Makedonia)

Usiku mmoja wakati Paulo na Sila wakiwa Troa mtu wa Makedonia alimtokea kwenye

maono akisema “Vuka uje Makedonia utusaidie” Mara Paulo na Sila walikwenda

Makedonia katika bara la Ulaya na wakaanzisha kanisa katika mji wa Filipi, Thesolanike,

Beroya, Athene na Korintho.

Tunakumbuka kwamba mwanzoni kila mahali Paulo alipokwenda , aliwaendea Wayahudi

kwanza. Wayahudi toka sehemu mbalimbali za dunia ya wakati ule walikuwepo katika

siku ya Pentekoste na walishuhudia kumiminwa kwa Roho Mtakatifu na ubatizo wa

waamini wapya 3,000. Wengi wao walitoka nchi za mbali kuja kusherehekea sikukuu ya

Pasaka katika mji wa Yesulasalemu na kurudi nchini kwao. Inawezekana baadhi yao

mtume Paulo alikutana nao, kwasababu baadhi yao walionekana kuwa na urafiki zaidi na

Paulo.

Wakati wayahudi wengi walipoikataa Injili ya Kristo kama mfufuka mwana wa Mungu,

Paulo aliwageukia watu wa mataifa.

Kanisa katika Filipi, Mwamini wa kwanza katika Ulaya alikuwa ni mwanamke aliyeitwa

Lidia muuzaji wa rangi za zambarau na mwenyeji wa Tiathira. Yeye na nyumba yake

walibatizwa na alifungua mlango wa nyumba yake kwaajili ya watumishi wa Mungu.

Kanisa katika Thesalonike. Pia katika mji huu mtume Paulo alikwenda kwa Wayahudi

kwanza kama ilvyokuwa desturi yake. Baadhi ya Wayahudi na Wayunani waliamini.

Wayahudi wasioamini walianzisha ghasia dhidi ya watumishi wa Mungu, yaani Paulo na

watendakazi wenzake. Kwa hakika washitaki hawa walijua nini cha kusema. Kama

mitume wangekamatwa kwa kuanzisha dini nyingine hakuna tatizo ambalo lingetokea kwa

watesi kwa sababu Ugiriki ilikuwa ina dini nyingi na walizikubali karibu zote.

Wao walikuja na uvumi mwingine kabisa kwa kusema kwamba

“Watu hawa wanadai kwamba kuna mfalme mwingine”.

10


Inaonekena Wayahudi hao Walianzisha uvumi huo ili serikali iweze kushiriki katika zoezi

la kuwadhibiti mitume.

Kanisa katika Beroya. Injili ilikubaliwa kwa watu wote Wamataifa na Wayahudi. Wakati

Wayahudi wa Thesalonike waliposikia walikuja tena kufanya ghasia dhidi ya mitume

hivyo iliwalazimu Paulo na Sila kuondoka mjini hapo, lakini Neno la Mungu lilikuwa

tayari limehubiriwa.

Hakika mitume hawa waliishi sawasawa na Neno la Kristo “Watakapowafukuza katika mji

mmoja kimbilieni katika mji mwingine. (Mt 10:23)

Kanisa katika Athene. Hapa pia mitume hawa waliwaendea Wayahudi , lakini wayahudi

hao hawakulipokea Neno. Baadae mtume Paulo aligundua ya kwamba Mungu

aliwapofusha macho Waisraeli kwa muda kwa sababu walimsulubisa Kristo Yesu.

Wanafalsafa wa Kigiriki walimpa mtume paaulo changamoto japo kuwa si sana kwa

sababu walitaka kulisikia Neno, hawakutubu bali walivutiwa tu na mdahalo. Walipokuwa

hawajui chakujibu walidhihaki.

Kanisa katika Korintho. Pia mahali hapa kama ilivyokuwa kawaida yake mtume Paulo

alikwenda kwa Wayahudi kwanza. Alikaa na Wayahudi watengeneza mahema (Akila na

Prisila). Inadhaniwa kuwa alitengeneza nao mahema ili kujipatia pesa kwaajili ya kujikimu

ili aweze kuhubiri Injili pasipo kumlemea mtu yeyote.(Mdo 20:34). Japokuwa Paulo

alikuwa ni Rabi aliyeelimika na Mtume hakudharau kazi ndondogo kwaajili ya kueneza

Injili.

Maamuzi Thabiti. Wayahudi waliipinga Injili tena na hii ilileta mtazamo mpya kwa

huduma ya Injili ya Paulo. Mtume Paulo alisema

Damu yenu na iwe juu ya vichwa vyenu mimi ni safi tangu sasa nitakwenda kwa watu wa

mataifa. (Mdo 18:6)

Paulo na Sila walikaa Korintho kwa muda wa miezi kumi na nane (18) wakiwafundisha

waamini. Kutoka Korintho mtume Paulo aliandika nyaraka mbili kwa Wathesalonike

Baada ya shambulio lingine lililofanywa na Wayahudi dhidi yake (Paulo) aliamua

kuondoka Korintho na kurejea Antiokia kwa kupitia Efeso na Kaisaria.

Safari ya tatu ya umisheni ya mtume Paulo (Mdo 18:23-22:17)

Katika awamu hii mtu aliyeambatana na mtume Paulo ni Timotheo aliyejiunga katika timu

yake katika safari ya pili ya umisheni huko Listra. (Mdo 1-3) na kwa muda mfupi idadi

kubwa ya wanatimu walikuwa pamojanae kabla hajamaliza safari hii. Mmojawapo wa

watu hao muhimu alikwa ni Dkt. Luka.

M. PAULO MTUME KATIKA MINYORORO (Mdo 22:23-28: 31)

Paulo alitumia miaka kadhaa akiwa gerezani lakini kamwe hakuacha kufanya kazi ya

umisheni. Mazingira hayakubadili kusudi lake. Baada ya safari ndefu Paulo alifika Rumi

jiji ambalo alitamini sana kuliona. Alikuwa na uhuru wa kuishi katika nyumba aliyokuwa

ameipanga mwenyewe huku akiwa chini ya uangalizi wa askari magereza, japokuwa

11


alikuwa mfungwa bado alileta athari kubwa katika kanisa huko Rumi. Moja ya mambo

makuu aliyofanya ni kuandika nyaraka kwa Waefeso, Wafilipi, Wakolosai na

Filemoni.

Inaaminika kwamba baada ya miaka miwili ya kukaa kifungoni mtume Paulo aliachiwa

huru (Mdo 28:30-31) lakini hakuna kumbukumbu kamili katika kipindi hiki isipokuwa

taarifa chache tu.

Mapokeo yanasema kwamba mtume Paulo alikamatwa Nikroporisi Kaskazini mwa

Ugiriki chini ya mtawala wa Rumi aliyeitwa Nero na akarudishwa Rumi katika kifungo

hiki cha pili aliandika nyaraka zifuatazo:- 1&2Timotheo, na Tito. Barua hizi zilikuwa ni

barua zake za mwisho mnamo mwaka 68. B.K. Mtume Paulo aliuawa kwa amri ya mfalme

Nero. Mtume huyu aliuawa kwa kukatwa kichwa.

N. UANDISHI WA MAANDIKO MATAKATIFU.

Inadhaniwa kwamba mpaka kipindi cha Mkutano Yerusalemu mnamo mwaka 48. B.K

hakuna hata kitabu kimoja cha Agano jipya kilichokuwa kimeandikwa, lakini karibu ya

mwaka 68.B.K idadi kubwa ya Maandiko ya Agano Jipya yalikuwa tayari yameandikwa,

hii ikijumlisha Injili ya Mathayo, marko, Luka, nyaraka za Paulo, Yakobo na 1Petro.

Katika kipindi cha miaka ya 68- 100.B.K vitabu vingine viliandikwa.Waraka kwa

Waebrania, 2Petro, Injili ya Yohana na nyaraka tatu za Yohana, yuda na Ufunuo wa

Yohana.

O. KIPINDI CHA UVULI

Tangu kukatwa kichwa mtume Paulo mwaka 68AD hadi kifo cha mtume Yohana 100 AD.

Kipindi hiki Kinaitwa kipindi cha uvuli kwa sababu wimbi la mateso lilikuwa limetanda

juu ya kanisa na kwamba ni mambo machache tu yanayofahamika kuhusu kipindi hiki.

Kipindi cha miaka 50 cha ukimya kinaelea juu ya kanisa baada ya kuuawa kwa mtume

Paulo. Kutoka mwaka 120AD tunapata maandiko ya mababa wa kwanza wa kanisa, lakini

pia tunakuta kanisa linatofautiana kwa namna nyingi na kanisa la siku za Petro na Paulo.

P. KUANGUKA KWA YERUSALEM

Mnamo mwaka 70AD kulitokea badiliko kubwa la kimahusiano kati ya Wakristo

Wayahudi. Mpaka kufikia kipindi hiki ni Wayahudi pekee waliokuwa wakiishi Israeli ndio

waliokuwa wakimpinga Kaisari. Wayahudi wa sehemu nyingine yote ya dola ya Rumi

walikuwa watii kwa Kaisari na hivyo waliishi kwa amani.

Wayahudi walitafsiri unabii katika Maandiko Matakatifu na kuamini kwamba walitakiwa

kuutawala ulimwengu wote kama ambavyo watafanya katika kipindi cha Milenia.

Mnamo mwaka 66AD wayahudi waliuasi utawala wa Rumi na mnamo mwaka 70AD

mfalme Vespasiani aliamua kuleta maangamizi juu ya taifa la Wayahudi.Alimtuma kijana

wake Tito na jeshi kubwa na imara kwenda kuishambulia Yerusalemu.

12


Kwa msaada wa Josephus (mwanahistoria) Tito ambaye hakutaka kuliangamiza taifa la

Wayahudi aliwasihi wayahudi kujisalimisha na kuweka silaha zao chini. Wayahudi

hawakuwa tayari.Hivyo basi hekalu lilichomwa moto na kubomolewa likiwa na watu

ndani ambao walikuwa wamekimbilia ndani ya hekalu ili kujinusuru na vita hiyo.

Liliongozwa na Tito lilifanikiwa kuiangusha Yerusalemu na kuchukua vitu vyote vya

thamani. Mambo yote yalitimia sawasawa na ilivyotabiliwa na Bwana wetu Yesu Kristo

katika Mathayo 24:1-2

1. Yes akaenda zake, akatoka hekaluni; wanafunzi wake wakamwendea ili

kumwonyesha majengo ya hekalu. 2 Naye akajibu akawaambia, Hamyaoni haya

yote ? Amin, nawaambieni, halitasalia hapa jiwe juu ya jiwe ambalo

halitabomoshwa.

Ingawa wayahudi zaidi ya milioni waliuawa katika vita hiyo lakini ni wakristo

wachache tu waliopoteza maisha yao. Hii ni kwa sababu Bwana Yesu alikuwa amekwisha

kuwaonya tayari kabla ya maangamizi hayo kutokea. Tunajifunza kuwa ni muhimu sana

kufuata maelekezo ya Kimungu ili kuwa salama katika maisha na huduma kwa ujumla.

LUKA 21:20-24

20 Lakini, hapo mtakapoona mji wa Yerusalemu umezungukwa na mejeshi, ndipo jueni ya

kwamba uharibifu wake umekaribia.

21 Ndipo walio katika Uyahudi na wakimbilie milimani, na walio katikati yake wakimbilie

nje, na walio katika mashamba wasiuingie.

22 Kwa kuwa siku hizo ndizo za mapatilizo, ili yatimizwe yote yaliyoandikwa.

Ole wao wenye mimba na wanaonyonyesha katika siku hizo! Kwa kuwa kutakuwa na shida

nyingi katika nchi, na hasira juu ya taifa hili. 24Wataanguka kwa ukali wa upanga, nao

watatekwa nyara na kuchukuliwa katika mataifa yote; na Yerusalemu utakanyagwa na

mataifa, hata majira ya mataifa yatakapotimia.

Mahali lilipokuwepo hekalu umejengwa msikiti mkubwa sana na Wapalestina ambao ndio

mojawapo ya sababu za kutoisha kwa mgogoro wa mashariki ya kati. Israeli walianza

kurudi nchini kwao taratibu na hatimae taifa la Israeli liliundwa kwa upya mnamo mwaka

1948 chini ya Umoja wa mataifa. Umoja wa mataifa ulitangaza kuitambua Israeli kama

jamhuri yenye mamlaka kamili.

Mungu alilionya kanisa Ufunuo wa Yohana 2:4-5

4. Lakini nina neon juu yako, ya kwamba umeuacha upendo wako wa kwanza.

5. Basi, kumbuka ni wapi ulipoanguka; ukatubu, ukayafanye matendo ya kwanza. Lakini

usipofanya hivyo, naja kwako name nitakiondoa kinara chako katika mahali

pake,usipotubu.

Q. VIFO VYA MITUME WA BWANA WETU YESU KRISTO NA MAENEO YAO YA HUDUMA

1. Petro- alikuwa mvuvi wa Samaki kabla ya kuitwa na Yesu na ndiye kiongozi wa

kwanza wa Kanisa. Petro alifanya huduma katika maeneo yafuatayo, Yerusalemu,

13


Yudea, Siria, Rumi na Asia ndogo. Mtume Petro aliuawa kwa kusulubiwa kichwa

chini miguu juu kwa ridhaa yake mwenyewe chini ya utawala wa Klaudi Nero.

2. Yakobo mwana wa Zebedayo- alikuwa mvuvi kabla ya kuitwa na Bwana Yesu.

Baada ya kuitwa na Bwana Yesu aliacha kila kitu na kumfuata Yesu na alikuwa

mmojawapo wa wanafunzi watatu waliokuwa karibu sana na Yesu. Yakobo

alifanya huduma Yudea. Yakabo aliuawa kwa upanga kwa amri ya Herode

Antipa. Yakobo ni mtume pekee kati ya wale mitume waliouawa ambae kifo

chake kimeandikwa katika Biblia.

3. Yohana- alikuwa mvuvi wa samaki kabla ya kuitwa na Yesu. Baada ya kuitwa na

Yesu alikuwa mojawapo ya nguzo katika kanisa la Yerusalemu. Yohana

alifanya huduma Efeso, Patmo na Yudea. Yohana ni mtume pekee aliyekufa kifo

cha kawaida katika uzee mwema akiwa ameshiba siku. Inazaniwa kuwa yohana

alikufa kule efeso mnamo mwaka 100AD.

4. Andrea- Alikuwa mvuvi, alikuwa mwanafunzi wa Yohana mbatizaji na ni mtu wa

kwanza kumfuata Yesu na mwinjilisti wa kwanza. Aliitwa na Yesu kuwa mvuvi

wa watu. Inadhaniwa kwamba Andrea alifanya huduma katika maeneo ya

Ugiriki, Asia ndogo na Urusi. Mtume Andrea aliuawa kwa kusulubiwa katika

msalaba wenye umbo la X huko Ugiriki.

5. Filipo- alikuwa mvuvi kabla ya kuitwa na Yesu. Mtume huyu alifanya huduma

katika maeneo ya alifanya huduma Frigia, Ukraine, Afrika Kaskazini, aliuawa

kwa kusulubiwa huko Hierapolis Uturuki

6. Batholomayo- ambaye anaitwa Nathanaeli, alikuwa mmisionari huko Asia.

Alimshuhudia Kristo katika maeneo ya Uturuki na akauwawa kwa sababu ya

kuhubiri injili huko Armenia, kw alichunwa ngozi akiwa hai mpaka akafa.

7. Thomaso. Mtume huyu kabla ya kuitwa na Yesu alikuwa ni fundi seremala na

fundi uashi. Mapokeo yanatuambia kuwa Thomaso alifanya huduma ya

umishenari katika nchi ya India. Mtume huyu aliuawa kwa kuchomwa

mkuki huko India.

8. Mathayo. Alikuwa ni afisa mapato (mtoza ushuru) katika Serikali ya Rumi katika

mji wa Kapernaum kabla ya kuitwa na Bwana Yesu. Mathayo alifanya huduma

katika nchi za Uajemi na Ethiopia. Mathayo aliuawa kwa kukatwa kichwa kwa

upanga baada ya kukataa kuikana imani.

9. Yakobo mwana wa Alfayo. Alifanya huduma katika nchi za Israeli, Misri na

Siriya. Mtume Yakobo wa Alfayo au Yakobo mdogo Alitupwa kutoka kwenywe

kinara cha hekalu na kisha kupigwa na rungu lenye misumari mpaka kufa huko

Yerusalem

14


10. Yuda/Thadeo- mtume huyu alifanya huduma huko Uturuki, Iraq, Kuwait,

Syria, Iran, na Lebanon. Mtume huyu Aliuawa kwa kupigwa na mshale ubavuni.

11. Simon Mzerote-huyu alikuwa ni mmojawapo wa askari waasi waliokuwa

wanajitayarisha kwaajili ya kuipindua dola ya Rumi. Baada ya kukutana na

Yesu aliacha kazi ya uaskari na kuwa mwanafunzi wa Yesu. Simon mzerote

alifanya huduma katika nchi za Misri, Israel, Siria, Afrika Kaskazini Libya na

Uingereza. Simoni aliuawa kwa kusulubiwa baada ya kukataa kutoa dhabibu

kwa mungu jua.

1 2.Yuda Iskariote- alikuwa ni mtunza Hazina wa Huduma ya Yesu. Yuda

alimsaliti Yesu na kisha kujinyonga.

MADA YA TATU

KANISA LA SMIRNA (KIPINDI CHA MATESO)

KIPINDI CHA SMIRNA

A. UTANGULIZI.

15


Simirna ni mji ambao ulikuwa umbali wa Km 65 Kaskazini mwa Efeso na ulijulikana

kama bandari ya salama kwa wakati ule. Ulikuwa katikati ya njia kuu kutoka Rumi

kwenda India na Persia (Irani)

Katika moja ya mitaa yake kulikuwa na hekalu la mungu wa kigiriki aliyejulikana kwa jina

la Zeus, Mungu mkuu na katika upande mwingine wa mji kulikuwa na hekalu la Cybele

{mama wa mungu}.

Mji wa Smirna pia ulikuwa ni kituo cha ibada ya kumwabudia kaisari. Kulikuwa na hekalu

la mfalme wa Rumi Teberio Kaisari

B. VIPINDI VYA MATESO

Historia ya kipindi cha Smirna. Inaaminika kwamba siku kumi za mateso yaliyotakiwa

kuja juu ya smirna huhusisha vipindi maalum kumi vya mateso chini ya watawala

mbalimbali wa kirumi ambao pia na wao watawala wangekuwa kumi.

Majina ya wafia dini mbalimali katika kipindi hiki cha Smirna chini ya wafalme

mbalimbali wa Rumi yanaorodheshwa hapa.

1. Klaudi Nero (64-68 B.K). Petro alisulubiwa katika kipindi cha utawala wa Nero.

Paulo alikatwa kichwa katika kipindi hiki.

2. Domitiani (90-95 B.K) alijaribu kumuua mtume Yohana kwa kumtumbukiza katika

mafuta yaliyokuwa yakichemka, lakini Yohana alitoka kwa muujiza bila kuungua.

Baada ya hapo akaamua kumpeleka uhamishoni katika kisiwa cha Patmo.Aliwaua

baadhi ya maseneta wa Rumi na kuamuru uzao wa Daudi wote kuuawa.

3. Trajani (104-117 B.K) Simoni ndugu wa Yesu aliuawa katika kipindi hiki

mwaka wa 107 B.K. Askofu Ignatius wa Antiokia aliuawa pia katika utawala wa

mfame huyu mwaka 110.B.K. Watu wengine waliouawa katika kipindi hiki ni

Polikap mwanafunzi wa Mtume Yohana (155 B.K),

4. Marcus Aurelius. (161-180 B.K). Yustini aliuawa katika utawala huu katika mwaka

165 B.K. Pia alifanya mauaji ya wakristo wengine wengi pia.

5. Septimus Severio. (200-211 B.K) alimuua Leonidasi baba wa Origeni,

mwanatheolojia mkuu, Victor askofu wa Rumi aliuawa katika kipindi hiki, pia

aliwaua Perpetua, Felistasi na Ireneusi mwaka 202 B.K

6. Thraker Maximus (235-237 B.K). kiongozi huyu alikuwa katili na asiye na huruma

kabisa. watu wengi sana waliuawa katika kipindi hiki baadhi yao ni, Pontianus

(askofu wa Rumi), Anterose, Maseneta wa Rumi na familia zao, Pamachius, Quirutus,

mwanamwali Martina na Hippolitus.

7. Desiusi. (250-253 B.K. ) katika kipndi cha utawala wake mateso yaliibuka tena juu

ya kanisa na kwa bahati nzuri utawala wake ulidumu kwa muda mfupi sana na baada

ya kuanguka kwa utawala wake kipindi kifupi cha amani kilikuja juu ya kanisa.

16


Baadhi ya watu waliouawa katika kipindi hiki ni Fabiani askofu wa Rumi, Juliani

mwenyeji wa Cicil, (aliwekwa ndani ya ngozi ambayo ndani yake kulikuwa na nyoka

wengi na ng’e na kisha kutupwa baharini). Kijana mmoja aitwae Petro aliuawa baada

ya kukataa kutoa dhabihu kwa mungu wa kipagani Venasi, Nichomachus, binti Denisa.

Epimachus na Alexanda waliuawa kwa kuchomwa kwenye moto.

8. Vareliani (257-260 AD.) Idadi kubwa ya wakristo waliuawa pia katika kipindi hiki,

baadhi ya watu mashujaa walioifia imani yao katika kipindi hiki ni Rufina, Sekunda,

Stefano askofu wa Rumi, (alikatwa kichwa), Saturninus askofu wa Toulouse. Sektasi

askofu wa Rumi na Mashemasi sita waliuawa mnamo mwaka 258AD. Askofu Spriani

wa Kathegi aliuawa pia katika kipindi hiki.

9. Aureliani (270-275 B.K.) Badhi ya watu waliouawa chini ya utawala wa Aureliani ni

Agapetasi kijana aliyeuza shamba lake na kuwapa fedha maskini, Felix askofu wa

Rumi alikatwa kichwa katika kipindi chini ya utawala huu.

10. Deokretiani, Mtawala huyu aliimarisha na kuyakuza mateso katika dola yote ya

Rumi.Mateso yalienea kila eneo la himaya yake. Baadhi ya wafia dini waliouawa

katika kipindi hiki ni;- Sebastian,victor, Romanus,Susanna, Sipriani wa Antiokia,

Dorothea na wengine wengi, Mji wa frigia uliojulikana kama mji wa kikristo

ulichomwa moto na wakazi wake wote wakafa.

C. MATESO YA KITAIFA.

Tabia za msingi katika historia ya kanisa katika karne zote mbili yaani karne ya pili na ya

tatu ni kanisa au wakristo kuteswa na wafalme wa kirumi.

Mateso haya hayakuwa endelevu lakini yalitegemea mtazamo aliokuwa nao mfalme

aliyekuwa akitawala katika kipindi hicho.

Mateso ambayo yalikuwa yakijirudia katika kipindi hiki yalidumu kwa karibu miaka 200

mpaka mfalme Kostantino alipookoka na kutangaza tamko la amani.(Edict of Torelance)

katika mwaka wa 313 B.K

D. SABABU ZA KANISA KUTESWA.

1. Imani juu ya Mungu mmoja. Warumi walikuwa na miungu mbalimbali ambayo

walikuwa wakiiabudu pamoja na sanamu zao. Wakristo walitangaza kwamba kuna Mungu

mmoja tu. Mfalme wa Rumi alijenga hekalu ambalo lilipaswa kutumiwa na watu wote

kuabudu miungu yao.

Wakristo walilazimishwa kushiriki ibada hizo za kuabudu miungu. Kitendo cha Wakristo

kukataa kuabudu miungu hiyo kulisababisha mateso juu yao. Majanga ya aina yoyote

yalipotukia yalitazamwa kama ni matokeo ya muingu kukasirika hivyo basi watu wote

waliogoma kushiriki katika ibada hizo walihesabiwa kuwa ndiyo chanzo cha majanga

hayo hivyo kustahili adhabu.

2. Kukataa kumwabudu kaisari. Kama ilivyokwisha elezwa katika sura iliyopita

kwamba makaisari wa kirumi walijitangaza kwamba wao ni miungu na wakadai

17


waabudiwe na wananchi au raia wao. Makaisari hao walisimamisha sanamu zao na

wananchi wakaziabudu na kutoa sadaka.

Hivyo raia wote wa dola ya Rumi walilazimika kushiriki ibada ya kumwabudu kaisari.

Mahekalu ya ibada za kaisari yalijengwa kila mahali na sanamu za makaisari zikawekwa

na watu wakalazimishwa kumwabudu kaisari na kutoa dhabihu mbele ya sanamu za

kaisari. Hii ilikuwa mojawapo ya ibada za kitaifa katika dola ya Rumi.

Wakristo walipinga vikali ibada hizo na hawakuwa tayari kushiriki ibada hizo wala kutoa

dhabihu mbele ya sanamu za kaisari. Kutokana na sababu hiyo wakristo walihesabiwa

kuwa waasi dhidi ya kaisari na dola kwa ujumla na hivyo walipaswa kuhukumiwa kifo.

Wakristo walianza kuteswa na dola ya Rumi kwa sababu ya kukataa kumwabudu kaisari na

kumwita Yesu Mfalme (Kurious).

3. Kutojihusisha kwenye ibada za sanamu. Ibada hizi za sanamu zilikuwa sehemu ya

maisha ya kila siku katika dola ya Rumi. Sanamu hizo zilisimamishwa katika kila nyumba

na ziliabudiwa katika kila sherehe. Dhabihu za vinywaji zilitolewa kwa sanamu hizo.

Hivyo wakristo walikataa kujihusisha katika shughuli za kila siku za kijamii zilizohusiusha

ibada za sanamu(mfano sherehe mbalimbali). Wakristo walipokataa kujihusisha na hayo

mambo walionekana wako kinyume na jamii nzima.Kwa sababu hiyo jamii iliwahesabu

kama maadui.

4. Kutambuliwa rasmi kwa dini ya kiyahudi: Dini ya kiyahudi ilitambuliwa rasmi na

dola ya Rumi kama dini ya kitaifa. Mwanzoni kanisa wakati linaanza lilitambuliwa kama

kikundi tu ndani ya dini ya kiyahudi chenye msimamo mkali na hivyo kanisa lilipata

upendeleo wa serikali kwa namna fulani. Lakini mara baada ya kuanguka kwa Yerusalemu

na kubomolewa kwa hekalu katika mwaka wa 70 B.K, kanisa au ukristo ulisimama peke

yake na dini ya kiyahudi walikuwa tayari kushirikiana na serikali kulitesa kanisa.

5. Kanisa kufanya mikutano ya faragha. Kutokana na mateso kanisa lilianza kukutana

katika maeneo ya siri na hasa wakati wa usiku. Hii ilipelekea kanisa kuhisiwa vibaya na

serikali kwamba lilikuwa linafanya njama ya kupindua serikali au kufanya maasi kwa

sababu serikali ya Rumi ilipiga marufuku mikutano yote isiyo halali, pia mikutano ya usiku

ilipigwa marufuku kwa kuogopa kwamba mikutano yote iliyokuwa haina kibali cha

serikali na iliyofanyika vifichoni haikuwa na nia njema kwa dola ya Rumi. Kwa sababu

hiyo wakristo walitazamwa na dola kama waasi. Watu wanopanga njama na maadui wenye

kuleta vurugu na maasi ndani ya dola na hivyo dola ilianzisha mateso juu ya kanisa.

6. Usawa katika kanisa. Kanisa liliwaona watu wote kuwa sawa. Hakukuwa na matabaka

katika kanisa. Waliwaona watu wote kuwa sawa na hawakumwogopa mtu yeyote na wala

hawakuogopa cheo cha mtu. Kutokana na sababu hiyo kanisa lilionekana kuwa na dharau,

lisilo na heshima na hivyo kanisa lilifanyika adui wa dola.

7. Kudolola kwa biashara za sanamu.: Kulikuwa na biashara iliyokuwa inafanywa

ndani ya dola ya Rumi. Biashara hiyo ilikuwa ni ya uuzaji wa sanamu. Watu wengi

walijipatia faida kutokana na biashara hiyo. Mitume walipohubiri Injili watu waliokoka

na kuachana na ibada za sanamu .

18


Mitume walifundisha kwamba sanamu si kitu na hazipaswi kuabudiwa anaepaswa

kuabudiwa ni Mungu muumba Mbingu na nchi pekee. Watu wengi waliacha kununua

sanamu hizo. Kitendo hicho kilisababisha biashara hiyo ya uuzaji sanamu kudolola.

Watengenezaji na wauzaji wa sanamu hizo walipata hasara na wakaamua kuja juu na

kuanzisha ghasia dhidi ya kanisa kwani walipoteza wateja wao.

E.HATUA ZA MATESO.

Kuna mwingiliano kati ya kipindi cha Efeso na Smirna. Kipindi cha Efeso kiliishia na kifo

cha mtume Yohana mwaka 100 B.K. Wakati kipindi cha Smirna kilianza wakati wa

mateso ya kitaifa.(dola) wakati mfalme Nero alipouchoma mji wa Rumi mwaka 64 B.K.

F. VIPINDI KUMI VYA MATESO YA KITAIFA.

MATESO YA KWANZA Chini ya Kaisari Nero.(54-68 B.K)

Klaudi Nero alikuwa na umri wa miaka 16 alipoingia katika utawala (ufalme) katika

mwaka 54 AD. Alikuwa mjukuu mkubwa wa Agustus aliyetoa amri ya watu wote

kuhesabiwa sensa (Lk 2). Nero alikuwa mfalme wa kwanza katika wafalme kumi

kuanzisha mateso dhidi ya kanisa.Alichoma mji wa Rumi mwaka 64 B.K .Theruthi mbili

ya mji wa Rumi iliteketea. Mfalme Nero aliwasingizia wakristo kwamba ndiyo

waliohusika na uharibifu huo. Hivyo kanisa lililazimika kuingia kwenye mateso makali.

Katika kipindi hiki mtume Petro alisulibiwa miguu juu kichwa chini mnamo mwaka 67

Pia mtume Paulo alikamatwa na kufungwa Rumi ambapo alihukumiwa kifo na kisha

akauawa kwa kukatwa kichwa mwaka 68 B.K Mjini Rumi.

Mfalme Nero alikuwa katili kuliko makaisari wote wa dola ya Rumi waliomtangulia na

waliomfuata. Kwani hajatokea kaisari katika dola ya Rumi aliyefanya mauaji kama Nero.

Mwaka 59 B.K . Mfalme Nero alimuua mama yake . pia alimuua mke wake wa kwanza

(Octavia)na kisha mkewe wa pili(Pompea) na baadae alimuua kaka yake na rafiki yake

mwalimu Seneka.

Mpaka mwaka wa 64. B.K Rumi ilikuwa katika ghasia kuu. Mfalme Nero alituhumiwa

kwamba yeye ndiye aliyehusika na kuuchoma moto mji wa Rumi. Lakini yeye alikanusha

na kuwashutumu wakristo kuwa ndiyo waliohusika na tukio hilo.

Kutokana na hilo kanisa liliingia katika kipindi cha mateso makali. Maelfu ya wakristo

waliuawa baadhi yao walitupiwa kwenye viwanja vya michezo vya wanyama poli ili

waliwe na wanyama wakali na baadhi yao walichomwa moto na mfalme akaendesha gari

lake juu yao katika bustani yake. Bustani ya mfalme ambako tukio hili lilifanyika leo ni

eneo la la jiji la Vatikani makao makuu ya papa na kania la mtakatifu Petro. Kaisari

Nero alijiua mwenyewe mwaka 68. B.K

KIPINDI CHA PILI CHA MATESO CHINI YA DOMITIAN. (90-96 B.K).

Baada ya Nero kujiua mwaka wa 68 B.K kanisa lilipata amani mpaka alipoinuka mtawala

mwingine ambaye ni Domitiani. Wakristo wengi waliuawa wakati huu .Baada ya juhudi

zote za kumuua mtume Yohana kushindikatiani Domitiani aliamua kumpeleka Mtume

19


Yohana uhamishoni kwenye kisiwa cha Patmo ambapo ndipo mahali alipopokea ufunuo

ambao sasa ni kitabu cha Ufunuo wa Yohana.

KIPINDI CHA TATU CHA MATESO CHINI YA TRAJANI 104-107 AD.

Trajani husemekana kuwa mtu muhimu sana miongoni mwa watawala wa Rumi. Alikuwa

mtawala mzuri kwa nchi yake lakini aliwaua wakristo. Mmoja wa mahakimu wake

aliyeitwa Plin the younger. Gavana wa Bethania alichunguza maisha ya wakristo na

mafundisho yao na kugundua kwamba mafundisho hayo hayakuwa na chochote chenye

kuleta uasi kwa serikali ya Rumi. Alileta ripoti yake mbele ya mfalme Trajani lakini

mfalme alijibu

“ Kama watu hawa walioletwa mbele yako wamepatikana na hatia kwa sababu ya kuwa

wakristo na wauawe lakini ikiwa wataikana imani yao ya kikristo na ikathibitika kwamba

wanaabudu miungu yetu na waachiwe huru. Katika kipindi hiki waliuawa wakristo

mbalimbali kama ifuatavyo.

‣ Simoni mdogo wa Bwana Yesu alisulubiwa katika mwaka wa 107 AD akiwa na

umri wa miaka 110. Alisulubiwa kwa amri ya mfalme wa Rumi {Trajani}.

‣ Askofu Ignatius wa Antiokia ambaye aliandika nyaraka mbalimbali kwa makanisa

mbalimbali ambazo baadhi yake zinapatikana katika kitabu kiitwacho “Mababa wa

Kitume”{Apostolic fathers}. Alikuwa tayari kuuawa kwaajili ya Bwana Yesu.

Aliandika barua za kuwafariji wakristo akiwa njiani kuelekea Rumi ambapo

alitupwa katika hifadhi ya wanyama wakali na akaliwa na wanyama wakali mnamo

mwaka 110.AD

‣ PORIKAP. {69-155 AD} Alikuwa mwanafunzi wa mtume Yohana na rafiki wa

Ignatius na mwalimu wa Ireniusi. Inadhaniwa kuwa Polikap aliteuliwa na mtume

Yohana kuwa askofu wa makanisa saba ya Asia. Alipoamriwa kumkana bwana Yesu

Kristo ili kuepukana na kuuawa yeye alijibu:

“Miaka 86 nimemtumikia Bwana wangu na hajatenda Jambo lolote baya

kwangu, nawezaje kunena vibaya juu ya Bwana wangu aliyeniokoa?

Alichomwa moto na akafa kifo cha kishujaa kwaajili ya Imani yake kwa Yesu Kristo.

Aliuawa chini ya utawala wa mfalme Antonius Pius mwaka 155 A.D.

KIPINDI CHA NNE CHA MATESO CHINI MARCUS

AURELIUS 161-180 A.D.

Marcus alijulikana kam mfalme bora wa nchi yake na mwandishi mwenye maadili.

Japokuwa alikuwa mtu mzuri kwa taifa lake alikuwa mtesi wa kanisa. Alifikiri kurejesha

maisha ya zamani ya kirumi na dini za zamani. Kwa wakati huo ukristo ulikuwa na

mashiko zaidi. Waamini wengi walikuwa tayari kufa kwa ajili ya imani yao na wala

hawakuogopa kifo. Walikikabili kifo kwa shangwe na ushindi mkuu. Katika kipindi hiki

waaminni wengi waliuawa na wengine walitupwa katika viwanja vya michezo vya

wanyama ili waliwe na wanyama wakali.

YUSTINI (JustineMarty) 100-165 A.D alizaliwa na alielimishwa vizuri mpaka kuwa

mwanafalsafa na aliendelea kufundisha hata baada ya kuwa mkristo. Alirejerea kwa

20


manabii wa zamani wa Kiebrania. Aliandika maneno yafuatayo dhidi ya ukatili na mauaji

yaliyokuwa yanaendelea dhidi ya wakristo.

“wanatushitaki, wanatusulubisha kwenye misalaba na kutupa kwenye

viwanja vy wanyama wakali na kwenye moto. Lakini wanapofanya

mabaya zaidi juu yetu ndivyo idadi ya wakristo inaongezeka na kuwa

kubwa zaidi.

Mnamo mwaka 165 A.D alikamatwa na mfalme wa Rumi Marcus Aureliusi na

kuuawa.

KIPINDI CHA TANO CHA MATESO CHINI YA SEPTIMUS. 202-211. A.D.

Baada ya kifo cha Marcus Aurelius kanisa lilipata amani mpaka alipoinuka mtawala

mwingine aliyejulikana kwa jina la Septimus Severus. Mtawala huyu alimuua Leonidasi

baba wa Origeni mwanatheologia mkuu. Katika mji wa kathegi Perpetua na mtumwa wake

Felistas walitupwa katika viwanja vya wanyama poli wakali na wakauawa.

KIPINDI CHA SITA CHA MATESO CHINI YA THRAKA MAXIMUS 235-237

A.D. Baada ya kipindi cha amani Thraka alikalia kiti cha enzi cha Rumi. Alikua

mpiganaji na alikusudia kuonyesha huruma zake kwa dini za kipagani kwa kuwatesa

wakristo. Utawala wake ulikuwa mfupi kwa sababu ya kutawala kwake kwa njia ya

udikteta. Maadui zake walitengeneza kikundi ambacho kilifanikiwa kumuua.

KIPINDI CHA SABA CHA MATESO.CHINI YA DECIUS 250-253 A.D.

Katika kipindi cha utawala wake mateso makali yaliibuka tena na kwa bahati nzuri kipindi

chake cha utawala kilikuwa kifupi na kanisa lilipata raha na amani kwa miaka 40.

KIPINDI CHA NANE CHA MATESO CHINI YA VARELIANI. 257-260. A.D.

Askofu Sipriani wa Kathegi aliuawa pia askofu wa Rumi Sextus aliuawa.

KIPINDI CHA TISA CHA MATESO. CHINI YA AURELIUS. 270-275. A.D

Mfalme Aurelius alikuwa mwabudu jua japokuwa hakulitesa kanisa moja kwa moja

mwanzoni lakini hakuwapa uhuru wakristo. Hatimae aliamuru kwamba wakristo wateswa.

Mateso yalidumu kwa muda mfupi sana chini ya mtawala huyu aana aliuwawa na wafuasi

wake mwenyewe.

KIPINDI CHA KUMI CHA MATESO CHINI YA DEOCLETIAN 303- 3010. A.D

Mfalme Deocletiani na wasaidizi wake waliwafunga wakristo gerezani. Baadae sehemu ya

jengo hili lilibadilishwa na kuwa Kathedro ya Mtakatifu Petro. Deocletiani aliagiza

kuchomwa moto kwa kila nakala Biblia, makanisa kubomolewa na wakristo wenye

msimamo mkali kunyang’anywa uraia.

Akiwa na umri wamiaka 80 Deocletiani aliondoka kwenye kiti cha utawala, lakini wafuasi

wake Galarius na Kostantinusi waliendeleza mateso mpaka mfalme Kostantino mtoto wa

Kostantinus alipotoa tamko la amani kwa kanisa mwaka 313 A. Tamko hili la amani

lilisitisha mateso kwa kanisa kwa kipindi cha karne mbili

21


Siku kumi za kujaribiwa zilizotajwa katika Ufunuo wa Yohana 2:10 zilifikia mwisho.

Baadae mfalme Deocletiani alipotambua kwamba yuko karibu na kufa alitubu dhambi zake

mbele ya askofu wa mji na mnamo mwka 337 A.D alibatizwa. Mtu aliyeamini kwamba

angeweza kuufuta ukristo alijikuta yeye mwenyewe anakuwa mkristo.

G. UONGOZI WA KANISA KATIKA KIPINDI HIKI.

Wakati mitume wakiwa hai uongozi ulionekana ni utumishi yaani kutumikia au

kuwajibika. Wakati Luka alipoandika kitabu cha Matendo na Paulo alipoandika nyaraka

zake tunakuta maneno askofu na wazee yakiwa na maana sawa yaani yakimaanisha ofisi

moja. Lakini katika miaka ya 125 tunakuta maaskofu wamekuwa watawala katika maeneo

yao. Katika baraza la Yerusalemu mwaka 48 A,D {Mdo 15} mitume wote na wazee

walihusika. Lakini katika baraza la mwaka 150 A.D waliohusika ni maaskofu pekee. Hii

inadhihirisha kwamba kanisa liliondoka taratibu kwenye mafundisho halisi ya mitume.

Huduma ya mitume ilizimwa na ikachukuliwa na maaskofu. Maaskofu walijifanya

watawala wa kanisa. Hii ndio sababu inayosababisha baadhi ya wanazuoni wa Kikristo

kuamini kwamba kipindi cha mitume kiliishia na kifo cha mtume Yohan, jambo ambalo si

kweli. Huduma za mitume, manabii, waalimu wachungaji na wainjilisti kama

zinavyoelezwa katika waefeso 4:11 ziliendelea kuwapo katika kipindi cha mitume na

vipindi vingine vyote vya kanisa, japokuwa zimekuwa zikikataliwa na katika vipindi

fulani ilionekana kama zimetoweka lakini kwa uhakika zimekuwapo na bado zimekuwa

zikifanya kazi katika kanisa hata sasa.

H. SHULE ZA THEOLOGIA.

Shule ya Alexandria. Ilianzishwa mwaka 180. A.D na Pantaenusi ambaye alikuwa ni

mwanafalsafa wa kigiriki na baadae akwa mkristo. Kisha alikwenda India, Irani na Saudi

Arabia katika huduma kama mmishenari. Alikufa mwaka 200 AD .

Klementi wa Alexandria alikuwa mwanafunzi wa Pantaenusi na alimsaidia katika

uendeshaji wa shule. Alikuwa ni mkuu wa shule hadi alipoondolewa kwenye wadhifa huo

katika kipindi cha mateso cha Septimus Severusi mwaka 2002AD, Baadhi ya vitabu vyake

mpaka sasa vipo.

Origeni (185-254 A.D). Alikuwa ni mwanatheologia mkuu. Alikuwa ni mtoto wa

Leonidasi. Baba yake aliuawa kutokana na imani yake katika Kristo chini ya utawala wa

mfalme Severus katika mwaka wa 2002 AD. Wakati huo Origeni alikuwa na umri wa

miaka 17. Origeni aliisaidia familia yake kwa kufundisha falsafa ya kigiriki pamoja na

fasihi. Aliianzisha shule ya Biblia kwa upya iliyokuwa imefungwa kutokana na kuondoka

kwa Klementi. Baadae alikuwa ni mwandishi wa vitabu vya Dogma na Thiologia. Baadae

alikwenda Kaisaria na alianzisha shule nyingine ya Biblia ambapo alikuwa ni kiongozi wa

shule hiyo kwa karibu zaidi ya miaka 20. Alifungwa jela chini ya mateso ya Deciani na

alikufa kutokana na kutendewa kinyama akiwa gerezani. alikufa akiwa na umri wa miaka

69 mnamo mwaka 254 AD.

Shule ya Asia ndogo. Shule hii haikuwa katika mji wowote ilikuwa ni shule ya masafa

(mobile Bible School). Ilihusisha waalimu wa thiolojia na waandishi. Baadhi yao ni

22


Ireneusi (130-202A.D) aliyezaliwa Smirna. Alipata elimu yake ya awali ya Biblia chini ya

Porikap. Kanisa la Asia ndogo lilimpeleka Ufaransa kama mmisionari. Aliuawa wakati wa

mateso ya Severusi mwaka wa 202 AD

Shule ya kathegi: Shule hii ilikuwa kaskazini mwa Afrika na ilifanya vizuri kuliko shule

zingine kubadili imani ya Kithiologia katika Ulaya. Watu wakuu katika shule hii

walikuwa ni Tetuliani na Sipriani. Tetuliani (160-200 A.D) Alikuwa ni mteteaji shujaa

wa imani ya kikristo dhidi ya dini ya kiyahudi na mafundisho potofu. Alijiunga na

umontano na alitumia kalamu na mahubiri kuthibitisha kile alichofikiri ni mambo ya

kidunia na mabishano katika kanisa.

Sipriani Askofu wa Kathegi (195-258 A.D) Alikuwa ni mtoto wa afisa wa ngazi ya juu

wa dola ya Kirumi. Alikuwa mkristo wakati wa ujana wake. Mambo matatu yaliyomvutia

mpaka kuwa mkristo ni Maandiko ya tetuliani, mafundisho ya Cellius toka Rumi na

Maandiko matakatifu (Biblia).

Mwaka mmoja baada ya kuwa mkristo alikuwa askofu na kiongozi mkuu wa makanisa ya

Afrika Kaskazini mwaka 248AD. Mnamo Mwaka 257AD Mfalme Valentine alimfungia

kufanya huduma na mwaka 258AD aliuawa.

Kanisa la karne ya pili lilipambana na mambo makuu mawili ambayo ni Mateso na

uzushi(Heresy) yaani mafundisho potofu. Mtume Paulo alitabiri ya kwamba:

“ Najua mimi ya kuwa baada ya kuondoka kwangu mbwa mwitu wakali wataingia kwenu

wasilihurumie kundi. Tena katika ninyi wenyewe watainuka watu wakisema mapotovu,

wawavute hao wanafunzi wawaandamie wao”Mdo20:29-30

I. UZUSHI NA MAFUNDISHO YA UONGO.

Mafundisho yasiyokubaliana na mafundisho rasmi ya kanisa yaliitwa uzushi na waamini

waliamriwa na kanisa kuyapinga na kutokuyapokea mafundisho hayo.

Kanisa katika historia yake lilitangaza kuwa baadhi ya mafundisho yaliyokuwa

yanaibuliwa na baadhi ya viongozi na waamini wa kanisa yalikuwa ni mafundisho potofu

na yakapewa jina UZUSHI (heresy) kutokana na kutokukubaliwa rasmi kwa mafundisho

hayo na uongozi wa kanisa kwa ujumla wake.

Si kila mafundisho waliyoyaita uzushi yalikuwa mabaya, kwani kile kilichoitwa

uzushi kilikubaliwa baadae na kanisa na kile ambacho kilionekana chema

kilikataliwa na kuitwa uzushi baadae. Hoja au mawazo yale waliyoyaita uzushi baadhi

yalikuwa na mambo mema ndani yake kama tutakavyotazama hapo baadae

Kanisa halikupambana na mateso tu bali pia na mafundisho ya uongo, sawsawa na unabii

uliotolewa

J. MAKUNDI YA UZUSHI.

1. UYAHUDISHAJI.

Hili lilikuwa ni kundi la wakristo wa kiyahudi lililojitokeza wakati kanisa linapanuka

katika miji ya wamataifa. Wayahudishaji hawa walifundisha kwamba wakristo wote

walitakiwa kuzifuata sheria za Musa na mapokeo ya dini ya kiyahudi. Waliyakataa

23


maandiko ya mtume Paulo kwa sababu yalipinga mafundisho yao. Kundi hili lilitoweka

katika karne ya pili BK.

2. UNOSTIKI

Unostiki ilikuwa ni falsafa iliyojaribu kutumia imani ya ukristo katika kuthibitisha

ukweli wake. Kundi hili waliamini kwamba Baada ya ngazi ya Mungu mkuu kulikuwa na

miungu wengine wengi ambao baadhi wakiwa wema na wengine waovu. Unosti ulikuwa

na elementi za falsafa za kiyunani na dini za kipagani. Hivyo kanisa lilipinga vikali mno

unosti likikana kwamba imani yake si falsafa na wokovu hautegemei falsafa na mafumbo

bali ufunuo wa Yesu kristo.

Wanostiki walipunguza thamani ya maisha na huduma ya Yesu Kristo. Habari nzima juu

ya maisha na huduma ya Yesu ilielezwa kwa njia ya mafumbo (allegory). Unostiki ulizuka

katika karne ya pili baada ya Kristo na ulishamiri katika karne ya tatu na ya nne.

Unostiki hata sasa unajidhihirisha katika karne hii ya ishirini na moja katika dini

mbalimbali hapa ulimwenguni. Hususani kupitia falsafa ya mpango mpya wa dunia (New

World order Philosophy)

MAFUNDISHO YA UNOSTIKI.

i. Maarifa ya pekee hufunuliwa kwa watu wachache tu.

ii. Wokovu si kwa watu wote, ni kwa watu wachache tu wenye kuyaelewa maarifa

yanayofunuliwa.

iii. Ulimwengu huu na vitu vilivyomo ndani yake vimeumbwa kwa nguvu isiyokamili na

hii ndio asili ya maovu yote katika ulimwengu.

iv. Yesu si mwanadamu, alikuwa na roho tu. Yesu alikuwa ni roho aliyejifanya aonekane

katika umbile la binadamu.

v. Waliamini kwamba mmoja wa miungu wadogo alikuwa ndani ya Yesu na ndio

aliyekuwa asili ya uungu wake.

3. MARSION

Huyu alikuwa ni mtoto wa askofu wa Pontus. Alikuja Rumi yapata mnamo mwaka

138AD. Alipofika Rumi alijulikana kwa haraka sana kutokana na jinsi alivyojitolea sana

katika kanisa kwa mali zake. Pia mafundisho yake yalimpa umaarufu na kumfanya

ajulikane sana. Kutokana na umaarufu huo Marsion alipata wafuasi wengi. Mafundisho

yake hayakukubaliwa na kanisa hivyo alitangazwa kuwa mzushi na alitengwa na kanisa

mnamo mwaka 144 BK.

Marsioni aliunda kikundi chake ambacho kiliwaunganisha wafuasi wake wote. Kikundi

chake hakikuongezeka kwa njia ya kuzaliana kwa sababu ya kukataa mambo ya ndoa.

Waliongezeka kwa njia ya wanachama wapya kujiunga. Marsion alikuwa ni mtu wa

kwanza kutunga kanuni ya maandiko. Alipogoapogoa baadhi ya vitabu na kutunga orodha

ya maandiko matakatifu aliyoakuwa anaiamini yeye.

MAFUNDISHO YA MARSION

24


Kwa kiasi kikubwa mafundisho yake yalifanana na mafundisho ya wanostiki.

i. Aliweka sharti la wafuasi wake (wanandoa) kutokutana kimwili na kwamba

walitakiwa kuachana na kuishi maisha ya upweke.

ii. Alikaza kwamba wokovu ni kwa watu wote. Wokovu hutegemea Injili ya Yesu

Kristo na si kwa kufunuliwa mafumbo kifalsafa.

iii. Injili ya upendo wa Mungu inahitaji kusikika zaidi katika kanisa.

iv. Kanisa limeichafua Injili kwa kuichanganya na mambo ya dini ya kiyahudi.

v. Mungu wa Agano la kale ni tofauti na baba wa Bwana wetu Yesu Kristo. Kwa

sababu Mungu wa agano la kale alifurahia dhabihu za damu.

vi. Mungu aliyeumba ulimwengu na watu wake ni Mungu mwovu, Mungu mwingine

mwema alijificha hadi wakati wa Yesu Kristo.

4. UMONTANO.

Kilikuwa ni kikundi kilichoanzishwa na mtu mmoja aliyeitwa Montano mwenyeji wa

Frigia. Wafuasi wa kikundi hiki waliitwa wamontano. Kikundi hiki kilienea sana kuanzia

mwishoni mwa karne ya pili na kuendelea kwa karne mbili zaidi.

Wakati wa ubatizo wake Montano alinena kwa lugha nyingine na kutabiri na hivyo akajiita

kuwa ni kinywa cha Roho Mtakatifu aliyetabiriwa na Yohana. Alikuwa na wasaidizi

wawaili wanawake ambao nao pia walijitambulisha kuwa ni vyombo pekee vya Roho

Mtakatifu. Karama za kinabii zilijidhihirisha katika mlengo wa umontano. Kutokana na

mikazo yao wamontano walihukumiwa uzushi na kutengwa na kanisa.

MAMBO MUHIMU YA MONTANO.

i. Walikaza kwamba wamefunuliwa juu ya mwisho wa dunia uliokuwa karibu sana

kutokea.

ii. Baadhi ya wafuasi wa umontano walikataa kulima kwa sababu Yesu angekuja kabla

ya msimu wa mavuno.

iii.

iv.

Baadhi ya wamontano walikataa ndoa kwa kuwa mwisho wa dunia ulikuwa karibu.

Kiongozi wao mmoja wa huko Pontusi aliwapeleka washirika wake porini kwenda

kumlaki Bwana Yesu wakati anarudi duniani kwa mara ya pili.

v. Kiongozi mwingine wa huko Shamu aliwakataza washirika wake wasilime kwa

sababu Yesu angerudi kabla ya msimu wa mavuno.

vi.

vii.

viii.

Montano alikataa hali ya kanisa kumezwa na ulimwengu.

Alidai kuwa kanisa lilikuwa limepoa na hivyo lisitarajie kurudi kwa Yesu.

Walipinga suala la uaskofu kuchukua mamlaka katika kanisa. Waliweka mkazo

katika huduma ya unabii na ukuhani wa waamini wote.

5. KUMEGEKA KWA KANISA CHINI YA UONGOZI WA NOVATIANO NA DONATO.

Katika karne ya tatu na ya nne kulitokea na kumegeka kwa kanisa. Mmeguko huo

uliongozwa na Novatiano katika karne ya tatu na Donato karne ya nne. Kugawanyika

huko kulitokana na kurejeshwa kwa viongozi na wamini waliokuwa wameikana imani

25


katika kipindi cha mateso. Pia makundi haya yalijitenga baada ya kuona kwamba wakristo

wengi walikuwa wanaishi maisha machafu kama wapagani waliokuwa wanawazunguka.

I. UASI WA NOVATIANI.

Katika karne y tatu askofu wa Rumi aliyeitwa Kalisto alitangaza kwamba dhambi yoyote

inaweza kusamehewa ikiwa mkosaji anaonesha toba ya kweli. Fundisho hili lilienea

sana. Wakristo waliokuwa wameikana imani yao wakati wa mateso walitaka kurudi

kanisani na askofu Kalisto alikubali kuwapokea watu hao.

Kiongozi mmoja wa kanisa aliyeitwa Novatiani, hakukubaliana na jambo hilo na alilipinga

vikali na akaungwa mkono na wachungaji wengine ambao nao walikuwa kinyume na

maamuzi hayo ya askofu. Walijitenga na kanisa na kuanzisha ushirika wao. Novatiani

alichaguliwa kuwa kiongozi wao.

II. UASI WA DONATO.

Mmeguko wa kanisa chini ya uongozi wa Donato ulitokea Afrika ya kaskazini karne ya

nne baada ya utawala wa mfalme Deokletiani. Mfalme huyu katika kipindi cha utawala

wake alikuwa na mpango wa kufuta ukristo na kuchoma moto Biblia zote. Wakati

wakipindi cha mateso makali baadhi ya viongozi wa kanisa waliasi imani wakaamua kutoa

maandiko matakatifu (Biblia) yateketezwe ili kujinusuru na kifo.

Baada ya kipindi cha mateso kumalizika viongozi hao yaani wachungaji na maaskofu

walioasi walitaka kurudi kanisani. Kanisa katoliki lilikuwa limekubali kuwapokea. Kanisa

lilikubali kuwarudishaviongozi hao katika sharika zao. Katika mji wa Karthegi waamini

wengi sana walikataa kuongozwa na mtu aliyemkana Yesu na kutoa Biblia kwa

serikali ili ziteketezwe.

Donatuno alikuwa kiongozi wa mgomo huo na alipata wafuasi wengi. Watu hao

walijitenga na kanisa na kuanzisha huduma yao. Kulikuwa na ugomvi kati ya wakatoliki na

wadonato kwa kwa muda mrefu.

K. HALI YA KANISA KATIKA KIPINDI CHA MWISHO WA KARNE YA PILI:

i. Kanisa lililotakasika. Mateso yaliwaondolea mbali wale ambao hawakuwa

waaminifu katika imani yao. Wale ambao hawakuwa na imani kamilifu na

waliojiunga na kanisa kwa masilahi yao binafsi mateso yaliwatupa nje yya kanisa.

ii.

iii.

Mafundisho yenye mfumo mmoja. Japokuwa kanisa lilihusisha watu wa

tamaduni , rangi na jamii mbalimbali bado lilikuwa na umoja wa imani katika

kanisa lote. Walifuata mafundisho ya mtume Paulo, Petro na mitume wengine.

Mdo 2:42.

Kanisa lenye muundo: kazi iliyofanywa na Paulo ya kuweka viongozi wa Kanisa

katika kila mji ilileta ufanisi. Viongozi hao walikutana katika mikutano na

kujadili mambo mbalimbali muhimu kuhusu kanisa. Hii ilisababisha kutokea kwa

ushirikiano imara wa kimataifa. (International Fellowship) ambao umekuwepo

mpaka sasa.

26


iv.

Kanisa lenye kusitawi {kukua}. Licha ya mateso yaliyolikumba kanisa, kanisa

liliendelea kukua kwa kasi. Kanisa lilikumbana na mateso makali chini ya

watawala mbalimbali wa Kirumi, lakini kanisa liliendelea kukabiliana na mateso

hayo na likawa tayari kuwapelekea watesi hao Injili ya uzima. Mateso

yalisababisha kanisa kukua na kuongezeka.

L. KUANDIKWA KWA AGANO JIPYA.

Hatuwezi kueleza kwa udhahiri au kikamilifu kwamba ni lini hili lilifanyika. Baadhi ya

vitabu kama vile nyaraka za Paulo zilikubaliwa kila mahali, wakati vingine kama vile

Waebrania, Yakobo na Ufunuo wa Yohana vilikubaliwa Mashariki peke yake na

kukataliwa Magharibi.

Kanisa la mashariki lilikubali baadhi ya vitabu ambavyo havipo katika Biblia. Baadhi ya

vitabu hivyo ni Waraka wa Balnaba, Mafundisho ya mitume kumi na wawali na Ufunuo

wa mtume Petro. Mabaraza yalikutana mara kwa mara ili kutambua ni vitabu gani

vilivyokuwa vimevuviwa na vipi havikuvuviwa. Inadhaniwa kwambaAgano jipya

halikutambuliwa rasmi mpaka baada ya mwaka 300AD.

MADA YA NNE

KIPINDI CHA PERGAMO

KANISA LA KIFAHARI/ KITAIFA.

A. UTANGULIZI.

KIPINDI: Toka tamko la amani la mfalme Kostantino (313 BK) hadi kuanguka kwa dola

ya Rumi mnamo mwaka 476 BK.

27


B. USHINDI WA WAKRISTO

Baada ya miaka miambili ya mateso kanisa liliishinda dola ya Rumi na kupata amani.

Mfalme Deokletiani katika utawala wake aliweka watawala wasaidizi katika majimbo

yake kutokana na ukubwa wa dola ya Rumi. Baba wa Kostantino alikuwa ni mmoja wa

watawala wasaidizi, aliongoza majimbo ya Galia, Uingereza na Hispania, Baada ya kufa

kwa watawala wasaidizi kulitokea na kugombea madaraka baina ya watoto wao.

Baba wa Kostantino alipofariki Kostantino alitangazwa kuwa mtawala badala ya baba

yake, na hivyo watoto wa watawala wengine waliamua kuanzisha mapigano ili kuuchukua

utawala huo. Miongoni mwao hao aliyekuwa na nguvu ni Maksentio, huyu alikuwa ni mtu

aliyeshabikia mauaji ya wakristo. Walianzisha mapigano huko Italia maili kumi kutoka

Rumi mnamo 28.10. 312 BK

Wakiwa katika eneo la mapigano kabla ya vita kuanza Kostantino aliona alama ya msalaba

angani ikiwa imeandikwa maneno yafuatayo, “Kwa alama hii utashinda”. Kostantino

aliitikia kwa sala na akaifanya alama ya msalaba kuwa nembo ya Jeshi lake na walipokuwa

vitani Kostantino aliwashinda kabisa maadui zake, adui yake mkuu Maksentio alikufa

katika vita hiyo, hivyo Kostantino akawa mshindi.

Kostantino alitambua kwamba msalaba ilikuwa ni alama ya wakristo na hivyo Mungu wa

wakristo ndio aliyekuwa amemsaidia katika vita hiyo. Mwaka uliofuata Kostantino

alitangaza PATANO LA AMANI na Wakristo, (Edict of Torelant). Patano hili

lilikomesha mateso juu ya wakristo katika dola yote ya Rumi.

Patano hili lililowaletea amani wakristo katika dola ya Rumi lilikuwa na matokeo chanya

na hasi katika kanisa.

C. MATOKEO YA TAMKO LA AMANI

Matokeo ya patano la amani yanaweza kuainishwa katika pande mbili ambazo ni matokeo

mazuri na matokeo mabaya kama ifuatavyo;

I. MATOKEO MAZURI,

i. Mateso juu ya wakristo yalikomeshwa.

ii. Makanisa yaliyokuwa yamebomolewa wakati wa mateso yalijengwa tena kwa fedha ya

serikali.

iii. Maaskofu na wachungaji walisamehewa kodi.

iv. Watumishi wa kanisa walianza kufadhiliwa na serikali na hawakutakiwa kuhukumiwa

kwa sheria za kawaida.

v. Wakristo waliruhusiwa kujenga makanisa mahali popote katika dola ya Rumi.

vi. Dhabihu za kipagani zilikomeshwa.

vii. Kostantino alijenga makanisa makubwa katika miji ya Yerusalemu, Bethlehemu na

katika mji wa Kostantinapali ambapo ndio uliokuwa makao makuu mapya ya serikali

yake.

viii. Watumwa waliachiwa huru.

28


ix. Siku ya jumapili iliwekwa kuwa siku ya mapumziko kwa watumishi wa serikali.

x. Mfalme Kostantino Alisaidia kuunda umoja wa kanisa kupitia mikutano mbalimbali

aliyoiitisha, mfano mkutano wa Naikea mwaka 325 BK.

xi. Mfalme Kostantino alikusudia kuufanya ukristo ukubaliwe na serikali kama dini

zingine.

II. MATOKEO MABAYA.

i. Ilikuwa ni fahari kuwa mkristo, hivyo watu wengi walijiunga na ukristo kwa

maslahi binafsi.

ii. Watu walijiunga na ukristo ili waweze kupata vyeo katika kanisa na serikali.

iii.

iv.

Maadili ndani ya kanisa yalianza kumomonyoka.

Mambo ya kiroho yaliachwa kupewa kipaumbele na badala yake programu

mbalimbali zikapewa kipaumbele.

v. Sherehe na tamaduni za kipagani polepole zilihamia kanisani, kwa kubadilishwa

jina na malengo na badhi zilibadilishwa kuwa sikukuu za kikanisa, mfano

Krismasi.(Kuabudiwa kwa bikira Maria kuliasiliwa kutoka ibada za kipagani za

kuabudu miungu , Zeusi, mungu wa uzuri wa warumi na Diana mungu mwezi).

vi.

vii.

Katika jimbo la mashariki serikali ililitawala kanisa mpaka likapoteza nguvu na

maisha ya kiroho.

Katika jimbo la magharibi kanisa lilipata nguvu dhidi ya serikali.

D. WATAWALA WALIOFUATA BAADA KOSTANTINO

Kostantino hakutaka kutumia nguvu katika kuwafanya watu kuwa wakristo, alitaka jambo

hili lifanyike taratibu na kwa uchaguzi wa mtu mwenyewe, jambo hili halikufuatwa na

watawala waliofuata baada yake.

Baada ya utawala wa Kostantino watawala waliofuatia walikuwa wakali mno walipiga

marufuku ibada za kipagani na waabudu dini hizo walihukumiwa kifo na mali zao

zilitaifishwa. Walivunja mahekalu ya kipagani, watawala hawa(wakristo) kwa kutumia

jina la ukristo sasa walitumia njia zilezile mbaya zilizokuwa zimetumiwa na serikali

kulitesa kanisa.

E. AINA MBALIMBALI ZA MATESO.

i. Katika kipindi cha Efeso kanisa liliteswa na wayahudi.

ii. Katika kipindi cha Smirna kanisa liliteswa na dola ya Rumi.

iii. Katika kipindi cha Pergamo ugomvi ulizuka miongoni mwao wenyewe

(wakristo).

F. UMOJA NA UTAWALA WA KANISA.

Kanisa lililazimka kuwa na umoja kamili ili liweze kuwa na nguvu ya kukabiliana na

mateso yaliyoliandama na uzushi uliokuwa unajitokeza. Hivyo kanisa lilipambana na

maadui wakubwa wawili ambao ni mateso na mafundisho potofu.

29


Kutokana na uzushi kutokea, kanisa ilibidi liwe na utambulisho au jina ambalo lingeli

tofautisha na makundi ya uzushi, hivyo kanisa lilianza kujiita Katoliki. Jina katoliki

linatokana na neno la kiingereza universal, lenye maana “ya popote au ya mahali

popote” Kanisa lilianza kutumia jina Katoliki kwa maana mbili, ambazo ni:

i. Kanisa lisilo na mipaka ya majimbo au ya nchi. Kanisa moja lililo katika nchi zote

ulimwenguni.

ii. Kanisa leye mafundisho sahihi.

G. SABABU ZA KANISA KUHITAJI UTAWALA WENYE NGUVU.

i. Kutokea kwa ukiri wa imani.(kanuni ya imani)

ii. Kutokea kwa Kanuni Ya Maandiko Matakatifu.

iii. Kutokea kwa maaskofu waliopewa mamlaka ya kutunza mafundisho yaliyotokana na

mitume wa kwanza.

i. Ukiri Wa Imani.

Huu ulikuwa ni ushuhuda mfupi uliotumiwa katika kazi za kawaida sharikani kama vile

ubatizo. Ukiri wa imani ulieleza kwa kifupi kile kanisa linachoamini na ulitumika kama

kiapo kuwa mtu anakubaliana na taratibu za kanisa hilo hivyo anastaili kubatizwa na

kupokelewa katika kanisa.

ii. Kanuni Ya Maandiko Matakatifu.

Kanuni ni kawaida inayotumiwa kupima usawa na usahihi wa kitu. Kanuni huelezea

vitabu vilivyokubaliwa na kupokelewa na kanisa kama maandiko Matakatifu. Kanisa

liliweka kanuni ili kubainisha kati ya vitabu vilivyokuwa ni neno la Mungu na vile

visivyokuwa Neno la Mungu. Mfano wa vitabu visivyokuwa neno la Mungu ni vile

vilivyoandikwa na wanosti. Makundi ya uzushi kama vile wanostika na Marsion

waliharakisha kutungwa kwa kanuni hii.

Mababa wa kanisa walitumia kanuni mbalimbali katika kuvibaini vitabu hivyo. Baadhi ya

njia hizo ni kumtambua mwandishi kama alikuwa ni mtume au la, Kupokelewa kwa kitabu

na watu walionadikwa kwa mara ya kwanza na matumizi ya kitabu hicho katika makanisa

mbalimbali na mamlaka ya kitabu chenyewe N.k

iii. Haja Ya Kutokea Kwa Viongozi Wenye Mamlaka.

Maaskofu walitokea kama watu wenye mamlaka ya kutafsili maandiko na kufundisha

wazi mafundisho ya mitume. Neno askofu maana yake ni mwangalizi/msimamizi. Neno

hili hapo awali lilitumiwa na watu wote na kulikuwa na maaskofu katika idara mbalimbali

za serikali, baadae matumizi ya istilahi hii yalibakia katika Kanisa tu.

Uaskofu ulisaidia kuleta utawala wenye nguvu na umoja katika kanisa kupitia mambo

mawili ambayo ni mafuatano ya mitume na ibada.

Mafuatano Ya Mitume

30


Ilidaiwa kwamba maaskofu walikuwa badala ya mitume. Kwa namna fulani uaskofu

ulitokana na mitume, yaani maaskofu waliwekwa na mitume kuwa watawala katika kanisa

na mamlaka ya utawala wao ilihusisha kuhubiri na kuitetea Injili.

Umoja Wa Ibada

Ibada mbalimbali zilizokuwa zikifanywa na kanisa kwa pamoja zilisaidia kukuza umoja wa

kanisa na kutokea kwa viongozi wenye mamlaka. Kulikuwa na ibada mbalimbali ambazo

zilifanywa na kanisa, baadhi ya ibada hizo ni ibada ya ubatizo na ibada ya meza ya

Bwana. Pia kanisa liliadhimisha sikukuu mbalimbali ambazo pia kwa namna fulani

zilichangia kukuza umoja wa kanisa.

H. MABISHANO YA KITHIOLOJIA.

Mabishano ya kitheolojia yalikuwa ni majadiliano ya mafundisho na mitazamo mbalimbali

ya kitheolojia na kiuongozi iliyokuwa ikiibuliwa na baadhi ya viongozi wa kanisa.

Kutokana na kutofautiana mitazamo juu ya hoja Fulani za kitheolojia mababa wa kanisa

walibishana na kuitisha mikutano ili kuweza kutoa suluhu juu ya tofauti hizo za

kimafundisho na kitheolojia. Kundi la walioshindwa katika mikutano hiyo lilihukumiwa na

kuitwa wazushi na kisha kutengwa na kanisa.

Mabishano ya kithiolojia yalisababishwa na mitazamo mbalimbali ambayo wakristo

walikuwa nayo juu ya Yesu Kristo. Baadhi ya mitazamo hiyo ni .

Uungu wa Yesu Kristo.

Wakristo wa awali walimpa Yesu heshima kwa kumwita majina mbalimbali kama vile

Masihi, Kurios, Kritos na Logos.

Jina la Logosi lilitokana na falsafa za kigiriki, Kutokana na falsafa hizo Logos ilikuwa ni

njia ya Mungu kufanyika mwili na kukaa na watu hapa duniani. Hivyo wakristo wa awali

walimtambua Yesu kama Mungu.

Kristo kama Logosi.

Katika kipindi cha karne ya pili na ya tatu karibu wanazuoni wote wa kikiristo

walifundisha kwamba Kristo alikuwa ni Logos. Kulikuwa na mwanazuoni moja aliyeitwa

Yustini Shahidi ambae aliweka mkazo kuwa Logos alikuwa ni Mungu wa pili.

Wanazuoni wengine waliweka mkazo katika umoja wa Yesu.Walikubali kwamba Logos

amefanyika kuwa mwili katika Yesu Kristo lakini alikuwa ni Mungu halisi, Mungu

mwana ndiye aliyefanyika mwili, si Mungu wa pili. Kulingana na mtazamo waYustini ni

dhahiri kwamba alikana ubinadamu wa Yesu. Yesu kama Logos alikuwa Kweli Mungu

na mwanadamu kweli.

Monarchianism. Dhana ya Mungu mmoja.

Kulikuwa na wanazuoni wengine waliopinga mafundisho ya kumhusisha Yesu na Logos

kwa sababu jambo hili lilielekea kupinga imani yakuwa Mungu ni mmoja. Wanazuoni

31


hao waliona kwamba dhana ya utatu wa Mungu ilielekea kuwa ni uzushi wa kuwa na

miumngu mingi.

Wamonarchianism waligawanyika katika makundi mawili ambayo ni;

1. Wamonarchianism wa kimabadiliko, hawa walikuwa na mtazamo wenye kumwona

Yesu kama mwanadamu pekee tu, ambae hakuwa Mungu aliyefanyika mwili. Kundi hili

liliongozwa na Askofu Paulo Samosota wa Antiokia.

2. Wamonarchianism wa kimfano. Hawa waliona kuwa hakuna tofauti kati ya baba na

mwana. Baba ndiye aliyevaa mwili. Kwa hiyo majina haya baba, mwana na Roho

mtakatifu yalitumika kuonesha kwetu njia au hali tatu Mungu alizotumia

kujidhihirisha. Hivyo hakuna nafsi tatu bali ni nafsi moja. Kundi hili liliongozwa na

Sabelio.

Baada ya mateso kukoma katika kanisa kulitokea mgogoro mwingine ndani ya kanisa

uliohusisha mgongano wa kimafundisho (doctrinal controversals).

Baadhi ya viongozi wa kanisa walianza kuibuka na mafundisho yaliyoonekana kuwa

mageni katika kanisa na hivyo walihukumiwa uzushi na kutengwa na kanisa.

Wakristo walitumia muda mwingi kujadiliana wao kwa wao badala ya kuipeleka

Injili mbele. Katika moduli hii tutajadili badhi tu ya mabishano ya kithiolojia yaliyotokea

ndani ya kanisa.

1. Mabishano Baina Ya Mchungaji Ario Na Askofu Alexander.

Ario alimshutumu askofu wake kuwa alikuwa anaweka mkazo sana juu ya uungu wa Yesu

katika mafundisho yake. Alexander alifundisha kwamba mwana ni wa milele sawa na

baba. Ario alipinga fundisho hilo yeye alidai kwamba baba ni wa milele lakini mwana

alikuwa na mwanzo wake. Kuna kipindi ambapo mwana hakuwapo. Askofu Alexander

aliitisha mkutano wa sinodi huko Iskanderia ili kujadili suala hilo na hatimae Ario

alitangazwa kuwa mzushi na alitengwa na kanisa.

Ario aliungana na Askofu Euzebio wa Nikomedia na wakaandika nyaraka mbalimbli

ambazo zilitetea fundisho lao na wakazisambaza maeneo mbalimbali ili ziendelee

kusomwa na wakristo mbalimbali.

Mkutano Wa Naikea.

Baada ya nyaraka hizo kusomwa majadiliano miongoni wa viongozi wa kanisa yalipamba

moto na kuleta mgawanyiko ndani ya kanisa. Mfalme Kostantino hakupendezwa na

mgogoro huo ulioleta mgawanyiko miongoni mwa wakristo hivyo aliwaomba viongozi hao

wapatane na iliposhindikana kupatana kwa viongozi hao, mfalme akitumia nguvu ya dola

aliamua kuitisha mkutano wa viongozi wote wa kanisa toka sehemu mbalimbali ili aweze

kuwapatanisha. Mkutano huo ulifanyika mwaka 325BK katika mji wa Naikea na

kutambulikana kama mkutano wa kwanza wa kanisa zima, kwa sababu ulihusisha viongozi

mbalimbali toka sehehemu mbalimbali.

Katika mkutano huo Askofu alexender alishinda kwa hoja na hatimae Ario alitangazwa

kuwa mzushi na akatengwa na kanisa. Katika kipindi hiki kanisa lilitunga ukiri wa imani

32


ambao ulipaswa kutumiwa na makanisa yote. Ukiri huo uliweka mkazo katika uungu wa

Yesu kuwa Yesu ni sawa na baba.

Mkutano wa Naikea haukuweza kumaliza majadiliano na badala yake uliyachochea

kwani majadiliano hayo yaliendelea kwa muda wa miaka 35 baada ya mkutano wa Naikea.

Baadhi ya viongozi wa kanisa walitilia mashaka ukiri wa Naikea kwasababu hawakuuzoea.

Mkutano Wa Kostantinopali

Kutokana na majadiliano hayo ya muda mrefu na makali kulikuwepo na haja ya kuitisha

mkutano mwingine wa kanisa zima. Mkutano hu uliitishwa katika mji wa Kostantinopali

mnamo mwaka wa 381 BK. Katika mkutano huu walifanya marekebisho kidogo ya

ukiri wa imani wa Naikea.

Mkutano Wa Efeso. (Mabishano kati ya Sirilo na Nestori)

Baada ya Apolinari kuhukumiwa uzushi, kuliendelea mabishano makali katika kanisa.

Baadhi ya mabishano hayo yalikuwa baina ya askofu Sirilo wa Iskandelia na askofu

Nestori wa Kostantinopali.

Sirio alipinga fundisho la Apolinari. Aliona kwamba uungu na ubinadamu wa Yesu

kuwa ni hali mbili zisizoweza kutenganishwa . Alipokuwa anataka kueleza uungu wa

Yesu alianza kwa kumwita bikira Maria ‘Theotokos’ yaani mama wa Mungu.

Askofu Nestori alibaini uzushi katika maelezo ya Sirilo, yeye alipendekeza Mariamu aitwe

mama wa Kristo. Maaskofu hao walishambuliana vikali sana kwa maandishi. Shauli hilo

lilipelekwa kwa askofu wa Rumi ili aweze kutoa uamuzi. Askofu wa Rumi alimpa ushindi

Sirilo na kumtangaza Nestori kuwa mzushi.Hayo yalifanyika katika mkutano wa tatu wa

kanisa uliofanyika katika mji wa Efeso mnamo mwaka 433 BK.

2. Majadiliano Ya Apolinari.

Apolinari alikuwa ni askofu wa Laodikia. Askofu huyu alijaribu kueleza uhusiano uliopo

baina ya hali mbili tofauti alizo nazo Yesu. Yaani hali ya uungu na hali ya ubinadamu.

Yeye alikuwa na mtazamo wa kwamba mwili wa Yesu ni ubinadamu na akili na roho

yake ni Logosi aliyefanyika mwili. Katika kueleza fundisho hilo askofu huyu alikaza

uugu wa Yesu uliokana ubinadamu wake. Kutokana na fundisho hili Apolinari

alitangazwa kuwa mzushi katika mkutano wa Kostantinopali mnamo mwaka 381BK.

3. Mabishano Ya Pelegio.

Pelegio alikuwa ni mmonaki, mwingereza aliyekuja Afrika Kaskazini kwajili ya kuhubiri

Neno la Mungu katika kanisa la Afrika ya Kaskazini.

Peregio alifundisha kwamba mtu harithi dhambi toka kwa Adamu, lakini kila mtu ni

lazima afanye uchaguzi yeye mwenyewe.

Pelegio alipingwa vikali na Agustino mkuu kwa mafundisho yake. Agustino alifundisha

kwamba Adamu alipotenda dhambi alikiwakilisha kizazi chote cha binadamu na

33


kwamba mtu hawezi kuokolewa kwa uchaguzi wake mwenyewe, bali ni kwa mapenzi ya

Mungu na kwamba neema ya Mungu haiwezi kukataliwa na wanadamu.

Mafundisho ya pelegio yalipingwa vikali na kanisa na kuonekana ni uzushi. Kanisa

lilikubali mafundisho ya Agustino mkuu ambayo pia yalijengewa hoja na

wanamatengenzo ya kanisa katika kipindi cha matengenezo katika karne ya 16 1

I. KUZUKA KWA UMONAKI.

Utawa au umonaki ulianza katika karne ya tatu BK. Kabla ya kipindi hicho wakristo

waliishi katika jamii na familia. Mara baada ya ukristo kushamiri mambo ya dunia yalianza

kuingia kanisani, baadhi ya wacha Mungu hawakuridhika na hali hiyo hivyo waliamua

kujitenga na kukaa peke yao nje ya mji katika mapango au katika nyumba walizokuwa

wamejenga. Nyumba hizo zilijulikana kama nyumba za watawa maarufu kama Monastery.

Baadhi ya mambo yaliyochochea kuanzishwa kwa utawa ni

i. Mvuto wa Injili, Injili ya Yesu alipomwambia Yule kijana tajiri kuuza kila kitu na

kuwapa maskini kasha kumfuata Yesu.

ii. Maovu kukithirikatika kanisa. Kutokana na mmonyoko wa maadili na kuhalalishwa

kwa dhambi ndani ya kanisa.s

iii. Falsafa ya uovu wa mwili. Imani ya kuwa mwili ni muovu na hivyo unapaswa

kuteswa vikali ili kuudhibiti.

Kutokana na mikazo juu ya mambo yaliyotajwa hapo juu, kulikuwa na watu ambao

waliuza kila kitu walichokuwanacho wakawagawia maskini na kisha wakajitenga na

kuamua kuishi maisha ya kimasikini mbali na jamii yao. Baadhi ya watu hao ni;

Antoni Mtawa Wa Kwanza.

Mtu huyu alikuwa ni mwenyeji wa Misri na ndiye mwanzilishi wa utawa. Antoni aliuza

kila kitu alichokuwa nacho na kuwagawia maskini mali zake na kisha akaishi nje ya mji

akilima na kuwapatia maskini chakula alicholima. Baada ya muda alijitenga na kuishi

peke yake pangoni mlimani. Watu mbalimbali walimwendea huko pangoni ili kujifunza na

kisha alifanikiwa kupata wafuasi ambao nao waliamua kuungana nae kuishi maisha ya

utawa. Alipat wafuasi karibuni 2000

Pokomeo Mwanzilishi Wa Nyumba Za Utawa.

Huyu alikuwa mdogo wa Antoni na ndie aliyeanzisha nyumba za utawa. Yeye alijenga

boma kubwa ambalo wafuasi wake waliishi ndani wakijitenga na mambo ya ulimwengu.

Watawa hawa walijishughulisha na ibada na kazi, utawa huu ulikaza ushirika na

ulipendwa na watu wengi.

Jerome (Hironimo)

34


Utawa ulienea sana sehemu ya magharibi kwa njia ya Jerome. Mtu huyu alikuwa na uwezo

mkubwa wa kufasiri Maandiko na alifanywa kuwa katibu wa Papa wa Rumi kwa kipindi

kirefu. Aliishi maisha ya kujikana. Alisema “ Mtu asieoa hujipatia sifa ya pekee mbele ya

Mungu. Alikiri kwa wazi kabisa kwamba “ Maisha ya utawa hayawezi kuondoa majaribu

yote” Alidai kwamba alipokaa katika boma la utawa huko mlimani bado aliwaza juu ya

wasichana wa Rumi.

Jerome alikuwa fundi wa Maandiko na elimu. Alitafsiri Biblia kwa lugha ya Kilatini

iliyojulikana kwa jina la Vulgate. Tafsiri inayopendwa sana na wakatoliki wa Rumi mpaka

sasa.

Yeye alishirikiana na wanawake watawa kutunza yatima Huko Bethrehemu na Palestina.

Walikuwa na nyumba mbili za watawa, moja ikiwa ya watawa wa kiume na nyingine ya

watawa wa kike.

Benedikto Mwanzilishi wa Kanuni Za Utawa.

Benedikto wa Nusia alianzisha shirika la utawa huko Monte Kasino Italia. Yeye aliweka

mkazo katika umoja. Aliweka uongozi uliosimamia nyumba zote za utawa. Aliona kuwa

kila nyumba ya utawa ni jeshi la Yesu waliotayari kumtumikia wakati wowote.

Kiongozi wa kila nyumba ya utawa aliitwa Aboot, na watawa wote walipaswa kumtii.

Aliweka mpangilio mzuri wa saa za ibada, sala na kusoma. Nyumba za kanuni za

Benedikto zilikuwa mahali pakuu pa elimu na kilimo.

Umonaki katika nchi za Ulaya

Umonaki uienea taratibu katika nchi za Ulaya ikilinganishwa na Afrika na Asia. Badala ya

kila mtu kuishi peke yake, umonaki wa ulaya ulipangiliwa na kusimamiwa vizuri. Kazi na

sala ziliunganishwa pamoja.

Faida Za Utawa.

1. Ulifanyika kuwa vituo vya wakimbizi.

2. Walitoa msaada kwa watu wenye mahitaji , mfano kusaidia maskini na wasiojiweza.

3. Walileta mchango mkubwa katika kuinua kilimo.

4. Walikuza elimu kwani watawa walitumia muda mwingi katika kusoma na kuandika

maandiko mbalimbali.

5. Walipeleka wamishenari katika mataifa mbalimbali kueneza Injili.

6. Walitoa viongozi bora katika jamii na katika kanisa.

7. Walitafsiri Maandiko katika lugha mbalimbali.

Madhaifu Ya Utawa.

1. Mkazo wa juu ya kuishi maisha ya useja.waliwakataza wafuasi wao wasioe wala

kuolewa.

2. Walikuwa omba omba kwa watu waliowatembelea

35


3. Upendeleo na anasa. Baada ya utawa kupata umaarufu, walianza kuishi maisha ya

anasa na kukwepa kulipa kodi.

4. Utawa haukuwa na msingi ki-Biblia

5. Watawa waliielewa visivyo Injili ya Yesu kristo waliyoitumia kuhalalisha utawa.

J. KUANGUKA KWA DOLA YA RUMI

Mfalme Kostantino mara baada ya kuingia katika utawala alihamishia makao makuu ya

dola ya Rumi katika mji wa Kostantinopali. Tutatazama namna Rumi ilivyokuwa makao

makuu ya kanisa. Wakati kanisa la Orthodox la mashariki lilikuwa likitawaliwa na serikali,

Patriaki wa Rumi alidai kuwa na mamlaka katika kanisa lote la ulimwengu wa magharibi,

ambao ulikuwa kupitia kanisa la Katoliki la Rumi. Hii iliwezekana kwa sababu kadhaa,

badhi zikiwa ni;

Kufanana kiutawala. Kulikuwa na mazoea kuongoza kanisa kwa mfumo wa kiserikali

ambapo kunakuwa na kiongozi mkuu mmoja anaetakiwa kusikilizwa . wakati huu

kulikuwa na maaskofu karibu kila mji, ambao katika miji mikubwa waliitwa Patriaki

(patriarch) yaani baba mkubwa. Kulikuwa na mapatriaki katika miji ya Yerusalemu,

Antiokia, Iskanderia, Rumi na Kostantinopali.

Kulikuwa na mashindano ya kugombea ukuu miongoni mwa mapatriaki. Swali lilikuwa

nani angekuwa kiongozi mkuu wa kanisa lote ulimwenguni. Rumi ikiwa imetengeneza njia

ya kuwa makao makuu ya kanisa ilikuwa na viongozi bora.

Kwa muda mrefu kanisa la Rumi lilikuwa imara. Lilisimama kidete kupinga mafundisho

potofu. Kanisa la Rumi liliihudumia Jamii kiroho na kimwili kwa kuanzisha kazi za kijamii

dunia nzima. Nyumba za utawa, shule na hospitali zilianzishwa katika maeneo

mbalimbali, jambo hili lililipa umaarufu kanisa la Rumi. Wamishenari walitumwa katika

ulimwengu mzima wa wakati ule kueneza Neno la Mungu.

Wakati nguvu ya kanisa ilikuwa inakua, nguvu ya dola iliendelea kuzorota, nguvu ya

kisiasa ya Rumi ilizidi kuporomoka.

Kwa muda mrefu wa utawala wake dola ya Rumi ilikuwa imetajirika sana. Maadui zake

waliokuwa wanaishi jirani nae waliutamani utajiri wake. Maadui hao waliivamia Rumi

ambayo sasa haikuwa na uzoefu wa kivita. Baadhi ya maadui walioivamia Rumi na

kuishambulia ni wavisigothi, wasaksoni, wavandali, , wahuni, wabarigandiana na

wafranka. Uvamizi wa mataifa haya ulipunguza nguvu ya dola ya Rumi.

Janga lingine lilikuwa ni vita ya wenyewe kwa wenyewe, baina ya wanachama wa seneti

kugombania kiti cha utawala. Kabila la kijerumani lililojulikana kama Herulisi liliivamia

na kuishinda dola ya Rumi mnamo mwaka 476 BK.

36


MADA YA TANO

KIPINDI CHA THIATIRA; KANISA LA NYAKATI ZA GIZA.

KIPINDI. Tangu kuanguka kwa dola ya Rumi hadi kuanguka kwa Kostantinopali.

A. UTANGULIZI

37


Katika kipindi cha Pergamo tuliona jinsi Patriaki wa Rumi alivyochukua mamlaka ya

uongozi wa kanisa na kuinuka kwa Rumi kuwa makao makuu ya kanisa. Tuliona jinsi

mafundisho potofu pamoja mambo ya kipagani yalivyoingia kanisani

Haikutosha kwa Patriaki wa Rumi kuwa Askofu mkuu wa kanisa lote duniani na kuwa na

mji wa Rumi kama makao makuu ya kanisa lote duniani, baada ya hapo alijitangaza kuwa

kiongozi wa mataifa kwa njia ya kukuza upapa katika karne kumi za kipindi cha giza.

Kipindi cha giza kilikuwa na hatua tatu ambazo ni, kukua, kusitawi na kuanguka.

1. Kukua.

Gregori I alipokuwa kijana aliteuliwa kuwa msimamizi wa majengo na vyakula katika Mji

wa Rumi. Baada ya kifo cha baba yake aliamua kutoa kwa kanisa mirathi ya babaye.

Mnamo mwaka 578 BK Gregori I aliteuliwa na papa kuwa balozi wake katika mji wa

Kostantinopali. Mwaka 585 hadi 590 BK alikuwa msaidizi wa papa huko Rumi na

kiongozi mkuu wa Monastery(nyumba za utawa). Baada ya papa Pelegio II kufariki dunia

kwa ugonjwa wa tauni mwaka 590 BK, Grogori I aliteuliwa na umati wa watu huko Rumi

kuwa Askofu badala ya Peregio II.

Kukua kwa nguvu ya upapa kulianza baada ya Gregori I kushika wadhifa wa upapa

katika mwaka wa 590 BK. Mfumo wa kubadilisha majina mtu alipokuwa anaingia

katika nafasi ya upapa ulianza katika kipindi hiki. Gregori aliitwa mkuu kwa sababu ya

mafanikio yake ambayo baadhi ni,

i. Alitumia uwezo wa kikanisa katika kuwasaidia watu, (kuwapa chakula na nguo).

ii. Serikali ilipolega aliimarisha ulinzi katika mji wa Rumi.

iii. Alimtambua papa wa Rumi kuwa na mamlaka juu ya viongozi wengine wote wa

kanisa.

iv. Alilipatia kanisa nguvu ya kisiasa na kidini.

v. Alitengeneza dogma ya kanisa.

vi. Kutokana na misaada ya kijamii iliyokuwa ikitolewa na papa Gregori I wananchi wa

Rumi walianza kumheshimu na kumhesabu kama kiongozi wao. Hivyo basi Gregori

Mkuu aliimarisha nguvu ya upapa katika mambo ya kidini na kisiasa pia.

Sababu za kukua kwa upapa

Mbali na mchango wa Gregori Mkuu katika kukuza nguvu ya upapa kulikuwa mambo

mengine kadhaa yaliyopelekea kukua kwa upapa katika kipindi hiki. Baadhi ya sababu

hizo ni:

1. Nguvu ya haki, kanisa liliwatetea raia dhidi ya watawala dhalimu hivyo likapendwa na

watu wengi.

Kuzolota kwa serikali, Wakati serikali inazolota kanisa lilizidi kujiimarisha, kiuchumi na

kijeshi hivyo viongozi dhaifu walihitaji msaada wa kanisa katika kupambana na adui zao

hivyo kanisa likazidi kuwa na mamlaka na nguvu ya ushawishi.

2. Ulaghai, Kanisa lilitumia kigezo cha ujinga wa watu kujipatia mamlaka. Kanisa

lilitengeneza nyaraka mbalimbali zenye kulipa mamlaka ya kiutawala na kudai kwamba

38


nyaraka hizo ziliandikwa na wahusika walioandikwa kumbe sivyo. Zifuatazo ni baadhi ya

nyaraka hizo

Waraka wa mfalme Kostantino kwa askofu Silvesta (314-335 BK). Huu ulikuwa ni waraka

uliogushiwa na viongozi wa kanisa kwamba uliandikwa na Kostantino kumpa askofu wa

Rumi (Silvesta) mamlaka ya kiutawala juu ya wafalme wote wa Ulaya na Ulaya nzima.

Tamko la uongo la Isodore(850 BK). Kulikuwa na maandiko yaliyokuwa yanadai

kwamba askofu wa Rumi alikuwa amepokea waraka toka kwa mitume uliokuwa

unamtangaza askofu wa Rumi kuwa askofu wa kanisa dunia nzima na kwamba kanisa

lilitangazwa kuwa huru (yaani kanisa kutokuwa chini ya serikali).

2 KUSITAWI KWA UPAPA (1073- 1216 )

Nguvu ya upapa ilifikia kilele chake katika utawala wa Gegori VII ambaye pia alijulikana

kama Hildebrand. Katika kipindi hiki upapa ulikuwa na nguvu kamili kikanisa na

kiserikali katika mataifa yote ya kule Ulaya.

i. Papa Gregori VII alifanya matengenezo ya ukreli na kukataza ndoa kwa wakreli.

ii. Aliliondoa kanisa chini ya utawala wa serikali, kanisa likaanza kujitawala, alifuta suala

la maaskofu kuteuliwa na watawala wa serikali (wafalme).

iii. Alilifanya kanisa kuwa juu ya selikali.

Papa Innocent III (1198 -1216).

Huyu alikuwa ni papa mwingine mwenye nguvu kubwa. Katika siku yake ya kutawazwa

kuwa papa alitoa usemi wenye maneno yafuatayo.

“ Mahalifa wa mtakatifu Petro wako katikati ya Mungu na watu; wadogo kuliko

Mungu lakini wakubwa kuliko watu, wenye uwezo wa kuwahukumu watu wote lakini

wasioweza kuhukumiwa na yeyote”

Katika barua yake ya kiofisi aliandika

“ papa hajapewa mamlaka kwa kanisa pekee bali kwa ulimwengu mzima. Akiwa na

haki ya kuwaondoa na kuwaweka watawala katika uongozi”

Papa innocent III alijitwalia mamlaka ya serikali ya mji wa Rumi akijifanya yeye

mwenyewe kuwa bwana kwa kuanzisha nchi ndani ya nchi ijulikanayo kama nchi ya

Vatikani. Hivyo papa akawa kiongozi wa kidini na kiserikali.

3 KUANGUKA KWA UPAPA.

Kuanguka kwa upapa kulianza wakati wa papa Bonifasi VIII katika mwaka 1303. Jambo

hili lilisababishwa na kuanza kuibuka kwa roho ya utaifa miongoni mwa nchi mbalimbali.

Jambo hili lilileta mtikisiko dhidi ya Bonifasi VIII. Watu walianza kuwaheshimu viongozi

wa nchi zao kuliko kumheshimu papa. Amri na maagizo mbalimbali ya papa yalipuuzwa

na viongozi wa nchi. Baada ya mfalme wa ufaransa kukata kutii maagizo ya papa, papa

39


Alianzisha vita na mfalme wa ufaransa na hatimae Bonifasi VII akashindwa vita hiyo na

kuwekwa kizuizini mpaka mauti ilipomfika.

B. KUINUKA KWA UISLAMU

Kanisa lilipata mashambulizi makuu katika karne ya saba kutoka kwa waislamu. Dini ya

Uislamu ilianzishwa na kijana mmoja aliyeitwa Mohamed. Kijana huyo alizaliwa mnamo

mwaka 570 BK katika mji wa Maka. Alianza kazi yake kama nabii na mwana

matengenezo kwa kuanzisha dini yake mnamo mwak 610 BK katika mji aliozaliwa.

Kutokana na kutokukubaliwa na watu wa mji huo aliamua kuhamia katika mji wa Madina

katika mwaka wa 622 BK. Kipindi hicho kinaitwa Hajira. Kalenda ya Waislamu inaanza

wakati huo wa kuhama kwa Mohamed toka Maka kwenda Madina.

Ndani ya kipndi cha miaka miambili waislamu walikuwa wameisha zishinda sehemu

mbalimbali za dunia na kuanzisha dini yao ya uislamu, Uanzishaji wa dini hiyo ulienda

sambamba na uanzishaji wa dola ya Kiislamu katika maeneo yoyote waliyoyashinda.

Baadhi ya maeneo waliyokuwa wameyashinda na kuanzisha utawala wao ni nchi za

Mashariki ya kati, Afrika ya Kaskazini na Asia ndogo. Mohamedi na wafuasi wake

walieneza dini yao kwa kutumia upanga, mahali popote watu walipokataa kuipokea dini

hiyo walilazimika kutumia vita na nguvu ya kijeshi.

Maeneo yoyote waliyofanikiwa kuyateka hatua ya kwanza ilikuwa ni kufuta dini zingine

zote zilizokuwa maeneo hayo na kuwalazimisha raia wote kujiunga na dini hiyo.

Kuinuka kwa dini ya Uislamu kulichangia katika kuanguka kwa upapa na kuzoofisha

nguvu ya kanisa kwa ujumla. Kwa mfano Afrika kaskazini kanisa lilidhoofika na hatimae

likafifia kabisa.

C. KUTENGANA KWA KANISA KATOLIKI.

Kanisa la katoliki la mashariki na lile la magharibi yalitengana rasmi mwaka 1054 BK,

japokuwa kihuduma yalitengana tangu zamani. Daima kulikuwa na kushindania madaraka

ya kwamba ni nani aliyekuwa mkuu kati ya papa wa Rumi na Patriaki wa Kostantinopali.

Hatimae katika mwaka 1054 BK makanisa haya yalitengana ramsi.

SABABU ZA KUTENGANA

Kutofautiana kimafundisho, Kuhusu asili ya Roho mtakatifu. Kanisa la magharibi lilidai

kwamba Roho mtakatifu alitoka kwa baba na kwa mwana wakati lile la mashariki lilidai

kwamba Roho mtkatifu alitoka kwa baba pekee.

Ndoa kwa makuhani. Kanisa la magharibi lilikataza makuhani kuoa wakati kanisa la

mashariki liliruhusu makuhani kuoa.

Sababu ya kisiasa, Baada ya kuanguka kwa dola ya Rumi mataifa ya magharibi yalitaka

kuwa chini ya Kostantinopali.

Kuabudu sanamu. Kanisa la magharibi lilianzisha matumizi ya sanamu katika ibada

wakati kanisa la mashariki lilipinga matumizi ya sanamu.

40


Kugombea ukuu, Madai ya kanisa la mashariki ya kuwa ni kanisa la kitawala.

D. KUSITAWI KWA UTAWA.

Mashirika mbalimbali ya kitawa yalisitawi katika kipindi hiki na yakajitolea kusaidia jamii

katika maeneo mbalimbali. Baadhi ya mashrika hayo ni :

Wabenedectino walianza mwaka 529 BK

Wasisteri mwaka 1098.

Wafransiska mwaka 1209.

Wadomenica mwaka 1215.

Kipindi cha karne za katikati kilichangia sana katika ustaarabu wa ulimwengu, hasa katika

mambo ya elimu, maandiko, na mambo ya ufundi, katika kipindi hiki zilijengwa kathedro

kubwa . kuna baadhi ya vyuo vikuu vikubwa vilivyojengwa wakati huu, mfano wa vyuo

vikuu hivyo ni Chuo kikuu cha Parisi huko Ufarasnsa, Chuo Kikuu cha Kambridge,

Chuo Kikuu cha Oxford, na vyote viwili vikiwa huko Uingereza. Kuanzishwa kwa vyuo

vikuu hivi kulipelekea elimu kukua na kuleta mtazamo mpya katika jamii kama

tutakavyoangalia baadae katika kipindi kitakachofuata.

E. WATANGULIZI WA MATENGENEZO YA KANISA.

Katika mwaka wa 1229 kanisa la Rumi lilikataza waumini wa kawaida wasisiome Biblia

isipokuwa makuhani tu. Lugha ya kilatini iliteuliwa kuwa lugha takatifu na hivyo mtu

yeyote asiyejua kilatini alizuiliwa kuhubiri.

1. PITA WALDO.

Katika miaka ya 1170 alitokea mfanya biashara mmoja aliyeitwa Pita waldo mwenyeji

wa Loyona Ufaransa. Mtu huyu alipenda kujua mambo yaliyo katka Biblia lakini

hakuweza kwa sababu hakufahamu kilatini hivyo aliwaajiri mapadri wawili wamtafsirie

Biblia katika lugha ya kifaransa. Baada ya kusoma neno la Mungu alivutiwa nalo sana

hivyo akauza kila kitu alichokuwa nacho na akala kiapo cha umaskini, akajitoa kikamilifu

kuhubiri neno la Mungu.

Pita Waldo Alianzisha timu iliyoitwa watu maskini. walianza kuhubiri, lakni walipingwa

na papa. Mwaka 1184 walijitenga na kanisa kwa sababu hawakukubali kitendo cha wao

kuzuiwa kuhubiri,

Waldo alipinga baadhi ya mafundisho ya kanisa Katoliki. Baadhi ya mambo aliyoyapinga

ni

Mafundisho kuhusu toharani,

Misa kwaajili ya wafu

Kumwabudu Mariamu mama wa Yesu.

Kanisa kuwa na mamlaka juu ya Biblia

Kuifanya lugha ya kilatini kuwa lugha takatifu

41


Watu hawa waliamini kwamba kila mtu alitakiwa kuwa na Biblia katika lugha yake ya asili

na ya kwamba Biblia ilitakiwa kuwa mamlaka ya mwisho na iliyokuu katika mambo

ya imani na maisha. Kanisa lilianzisha mateso dhidi ya wawadeni yaani wafuasi wa

Waldo.Watu hawa Kadili walivyoteswa ndivyo walivyokuwa wakiongozeka. Mnamo

mwaka 1211 wawadeni 80 walichomwa moto huko Ujerumani. Pita waldo alisaidia kuleta

matengenezo ya kanisa kwani alisaidia kupatikana kwa Biblia katika Lugha zingine na

kuhamasisha kila mtu kusoma Biblia. Waldo anajulikan kama mmoja wa wanamatengezo

ya kanisa watangulizi.

2. JOHN WIKRIF

Huyu alikuwa mwalimu wa Chuo kikuu cha Oxford. Mnamo mwaka 1378 Wikrif alitaka

kuleta matengenezo katika kanisa kwa kuwaondoa watumishi wa kanisa waliokuwa

dhalimu,na kuwanyang’anya mali ambazo aliamini kwamba ndizo zilizokuwa chanzo cha

watumishi hao kuwa dhalimu. Alichapisha andiko lililoeleza maadili wanayotakiwa

kuwa nayo watumishi wa kanisa.

Alifundisha kwamba wakati viongozi wa kanisa wanapokuwa mafisadi serikali ilitakiwa

kuchukua mali zao na kuwapa watu wengine wenye nia ya kumtumikia Mungu. Katika

mwaka wa 1379 alianza kupinga dogma ya kanisa kwa kutoa madai yafuatayo;

Yesu pekee ndiye aliyekuwa kiongozi mkuu wa kanisa na si papa.

Biblia pekee ndio yenye mamlaka kuu na ya mwisho kwa waamini na si kanisa wala

papa.

Kanisa lilitakiwa kuiga mfano wa kanisa la agano jipya.

Kwa msaada wa tajiri Lord Cobham John Wikrif alitafsiri Biblia katika lugha ya

kiingereza na kuisambaza katika maeneo mbalimbali . Alianzisha chama cha Wahubiri

maskini na wakaanza kuzunguka katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo wakihubiri neno

la Mungu watu

Mwaka 1382 alipinga fundisho la mageuzo ya maumbo ya mwili na damu ya Yesu

linalojulikana kama transubstan-tiation. Mawazo yake yalipingwa vikali na kanisa na

serikali na akafukuzwa ukufunzi. Mwaka 1402 Bunge La Uingereza lilipitisha sheria ya

hukumu ya kifo kwa watu wanohubiri mafundisho kinyume na yale yaliyokubaliwa na

kanisa. Wahubiri maskini waliteswa vikali sana, baadhi walifungwa na kuchomwa moto

na kufukuzwa nchini. Viongozi wa kanisa walijaribu kuchoma moto Biblia zote za

Kiingereza. Wikrif alifariki mnamo mwaka 1384.

Shujaa huyu anakumbukwa sana katika historia ya kanisa kwa mchango wake wa kutafsiri

Biblia katika Lugha ya kiingereza. Wikrif ndiye mtu wa kwanza kutafsiri Biblia kwa lugha

ya kingereza.

3. JOHN HUS

Huyu alikuwa ni mkuu wa chuo kikuu cha Plague huko Bohemia, mtawa na padre wa

kanisa katoliki. Mwaka 1401 John Hus alipata upadrisho. Padre huyu alipendezwa na

42


maandiko ya John Wikrif na hivyo alianza kuhubiri mafundisho ya mtangulizi wake

Wikrif.

Alipinga mafundisho mbalimbali yasiyo ya ki-Biblia ya kanisa la Romani katoliki na

akasisitiza watu kuishi maisha matakatifu. Alisisitiza kwamba Biblia ndiyo mamlaka ya

mwisho kwa mwamini na katika huduma za kanisa.

Katika kitabu chake alichoandika juu ya kanisa, alifasili kwamba kanisa ni mwili wa

Kristo, na Yesu Kristo pekee akiwa kiongozi wake mkuu. Alitetea nafasi ya ukuhani na

kudai kwamba Mungu pekee ndiye aliyekuwa na uwezo wa kusamehe dhambi. Alieleza

kwamba hakuna mamlaka ya kanisa inayoruhusiwa kuanzisha mafundisho (doctrine)

yaliyo kinyume na Biblia na kwamba Waamini hawatakiwi kutii maagizo yasiyo ya

kimaandiko.

John Hus Alipinga baadhi ya mambo yafuatayo,

Udhalimu wa mapadre

kuuzwa kwa vyeti vya msamaha,

kuondolewa kikombe cha divai kwa walei.

Kanisa kuwa na mamlaka juu ya Biblia

Uwezo wa Makuhani kusamehe dhambi

Ukuhani wa wachache (crerism)

Baada ya mashambulizi hayo mazito dhidi ya mafundisho ya kanisa Hus alifukuzwa

upadre na akaambiwa abadilishe msimamo wake kwa kufuta kauli, jambo ambalo Hus

hakukubaliana nalo. Hatimae Hus alihukumiwa kifo na akachomwa moto. Hus akiwa

anachomwa moto alitoa unabii kwa kusema “leo mnaniua mimi lakini miaka miamoja

ijayo Mungu atamwinua mtu mwingine ambaye matengenezo yake hayataweza

kuzimwa” Kweli baada ya kipindi hicho Mungu alimwinua Martin Luther mwana

matengenezo mkuu kama tutakavyoona hapo baadae.

4. JEROME SAVANAROLA.

Alizaliwa Ferrara Italia mnamo mwaka 1452, alikuwa ni mtawa wa shiriki la wadominico.

Mtu huyu alijaribu kuleta matengenezo katika kanisa na serikali. Alipinga uovu uliokuwa

unafanywa na mapapa. Alisomea mambo ya ubinadamu na utabibu. Kufikia mwaka 1491

alikuwa mhubiri maarufu kule Frolence.

Alitabiri kwamba papa na mfalme wa Naples wangekufa siku moja, jambo ambalo

lilitokea kama alivyotabiri. Katika mahubiri yake alitabiri hukumu kubwa ambayo

ingekuja juu ya mji ikifuatiwa na kipindi chema ambapo Frolence ingewaunganisha watu

wote wa Itali. Utimilizo wa unabii huu ulionekana kuwa ni kuvamiwa kwa Itali na mfalme

Charles VIII. Ambaye mwaka 1494 aliuondoa utawala dhalimu wa Frolence.

Baada ya kuanzishwa kwa serikali mpya Saravano alipata umaarufu sana pale Frolence

kupitia mahubiri yake na alileta mabadiliko mengi katika jamii. Alianzisha matengenezo

ya kodi, Kusaidia maskini na matengenezo katika mahakama. Aliubadilisha mji kutoka

katika maisha ya kimwili na kuishi maisha ya kiroho.

Kutokana na mabadiliko hayo kila mtu katika mji alikwenda kanisani na matajiri waliwapa

misaada masikini.Wafanya biashara walirudisha vitu walivyokuwa wamewatapeli wateja

wao. Waimbaji waliacha kuimba nyimbo za kidunia na kuanza kuimba nyimbo za kumsifu

Mungu. Waliachana na maisha maovu, walichoma moto mawigi, vinyago, vitabu vya

43


kipagani, picha za ngono na kila kitu walichodhani kuwa ni kiovu. Hakika uamsho mkuu

ulitokea kama alivyokuwa ametabiri.

Jerome alitabiri kwamba angehubiri kwa miaka nane tu pale Florence na kisha angeuawa.

Katika mwaka 1498 Jerome alimshutumu papa Alexander VI kwa kutangaza hadharani

maovu aliyokuwa anayafanya yeye na wasaidizi wake. Baada ya mkasa huo Alexander VI

aliamua kumwekea vikwazo na kisha baadaye akamnyonga na kuuchoma moto mwili

wake mnamo mwaka huohuo wa 1498. Maneno yake ya mwisho akiwa anauawa alisema

“ Bwana Aliteseka sana kwaajili yangu”. Mapambano yake dhidi ya papa yalimfanya

kuwa shujaa na kuwa mtangulizi wa matengenezo ya kanisa. Alikuwa tayari kuitetea

imani kwa gharama yoyote.

Wanamatengenzo watangulizi walionyesha ushujaa katika kuitetea imani. Hawakukubali

kusalimu amri kwa uongozi wa kanisa au serikali na hawakuwa tayari kunyamaza kimya

na kuacha hali mbaya kuendelea kulitafuna kanisa, walikubali kulipa gharama katika

kuitetea imani na kupinga uovu. Walitengeneza njia ambayo ilifuatwa na

wanamatengenezo wakuu baadae kidogo katika kipindi cha kanisa la Sardi yaani kanisa la

matengezo.

Kuna mengi ambayo twaweza kujifunza kwa watu hao kutokana na vile kila mmoja

alivyosimamia kusudi lake kwa ujasiri na imani kuu. Kama tutajifunza na kutetea imani kama

wao tunaweza kuleta matengenezo katika kanisa vuguvugu la wakati huu wa mwisho

F. KUANGUKA KWA KOSTANTINOPALI.

Wanahistoria wengi wana tazama kuanguka kwa Kostantinopali kama mpaka wa kipindi

cha karne za katikati na nyakati hizi zetu. Waislamu toka Uturuki waliivamia

Kostantinopali na kuishinda mnamo mwaka 1453. Hekalu zuri liliojengwa na mfalme

Kostantino lililojulikana kama Saint Sophia liligeuzwa na kuwa msikiti. Huu ndio

uliokuwa mwisho wa kipindi cha giza au mediaval Period.

MADA YA SITA

KIPINDI CHA SARDI KANISA LA MATENGENEZO

KIPINDI : Tangu kuanguka kwa Kostantinopali hadi Patano la Amani la Westpharia.

A. SABABU ZA KUZUKA KWA MATENGENEZO YA KANISA.

Kitendo cha Kanisa la Rumi kutokuwa tayari kupokea mabadiliko yaliyokuwa

yanapendekezwa na watu wema kama vile, Wikrif na Hus, viongozi wa baraza la

44


matengenezo na mengine mengi kulipeleka kuanza kwa nguvu wimbi kubwa la

matengenezo.

Hadi kufikia miaka 1500 misingi ya jamii ya kipindi cha giza ilikuwa inabadilika

kutokana na mabadiliko ya kielimu, kisiasa, kidini na kiuchumi. Kanisa la ulimwengu

lilianza kupoteza nguvu na kanisa la kitaifa likaanza kuchukua nafasi

Kupanuka kijiografia kulileta mabadiliko mengi katika kufikiri. Kwa kifupi kulikuwa na

sababu mbalimbali zilizopelekea wimbi la matengenezo ya kanisa kutokea, baadhi ya

sababu hizo ni;

1. Kukua kwa utaifa(nationalism).

Kila nchi ilianza kuweka mkazo kujijenga yenyewe, hivyo nchi mbalimbali zilianza

kujitenga na ushirikiano wa kimataifa, Hii ilipelekea kanisa la ulimwengu kokosa nguvu

kwani utaifa ulisababisha kuanza kwa kanisa la kitaifa kila mahali.

Mgogoro wa kanisa katika karne ya 14 na 15.(Utumwa wa Babeli. Kugombania madaraka

yaupapa.)(Great Schism)

2. Kuvumbuliwa kwa mashine za uchapishaji.

Johann Guthenberg alivumbua mashine ya uchapaji mwaka 1456. Mpaka wakati huu

vitabu vyote viliandkwa na kunakiliwa kwa mkono. Kuvumbuliwa kwa mashine hii

kulisababisha Biblia na maandiko mengine kuchapwa na kusambazwa katika maeneo

mbalimbali. Kusambazwa kwa maandiko hayo kulipelekea kuamsha akili za watu na

kutambua hitaji la kuwepo kwa mabadiliko katika maeneo mbalimbali ikiwemo Kanisa.

3. Kuzuka kwa mwamko wa kujifunza. (Renaissence)

Hiki kilikuwa ni kipindi ambacho ulizuka mwamko mkubwa

wa kujifunza . Kipindi hiki kilianza huko Ulaya Italia karne ya 14 na kuendelea hadi

karne ya 17. Wasomi wengi waliibuka katika kipindi hiki. Watu walianza kufikiri mambo

kwa upya kutokana na elimu waliyokuwa wamepata. Kutokana na elimu hiyo watu

walihitaji mabadiliko katika maeneo mbalimbali ili kuweza kuleta maendeleo. Hivyo

kanisa nalo likajikuta linahitaji mabadiliko japo kuwa halikuwa tayari kwaajili ya

mabadiliko hayo. Tunaweza kufupisha sababu zilizopelekea matengenezo ya kanisa kwa

kuziorodhesha hapa chini kama ifuatavyo:-

Mgogoro wa kanisa katika karne ya 14 na 15.( Great Schism)

Rushwa.

Kanisa kutojali maisha ya kiroho ya watu na kujikita katika mambo ya kiuchumi.

Kuuzwa kwa vyeti vya msamaha

Upendeleo. (Mtu mmoja kuwa na vyeo vingi kwa wakati mmoja)

Mapapa kukosa maadili.

Mapadri kuwa na elimu duni.

Kuzuka kwa falsafa ya Mantiki.

45


B. VIONGOZI WA MATENGENEZO YA KANISA.

Katika kipengele hiki tutawatalii baadhi ya wanamatengenezo ya kanisa, yaani

tutawachunguza watu ambao Mungu aliwatumia kuleta kweli ya neno la Mungu katika

kanisa lililokuwa limepotoka na lisilokubali matengenezo kwa hiali. Tutawatalii

wanamatengenezo wafuatao, Martn Luther, John Calvin, Ulrich Zwingli na John

Knox.

1. ULRICH ZWINGLY

Alikuwa ni mwanamatengenezo wa kanisa wa kiswisi asiyejulikana sana kama Martn

Luther na John Calvin lakini aliye na mchango mkubwa katika mategenezo ya kanisa.

Alizaliwa mwaka 1484, na kuelimishwa katika Chuo kikuu cha Basel na Vienna

akisomea fani ya ubinadamu (humanism). Alifanya kazi kama Padre wa Parish Huko

Glarus Uswisi mwaka 1512. Katika mwaka wa 1515 Ulrich alianza kuyatilia shaka

mafundisho ya Kanisa Katoliki na alianzisha kile kilichoitwa matengenezo ya Zurich.

Alihubiri jumbe za ki-Biblia na kufanikiwa kulibadilisha baraza la mji kuwa na mtazamo

kama wa kwake.

Baraza hili liliufanya mji kuwa ngome ya Uprotestant. Hoja 67 za Zwingli

ziliasiliwa(adopted) na kufanywa Mafundisho rasmi ya mji na mji uliweza kubadilika kwa

haraka sana. Mahubiri na mafundisho yalifanywa mara kwa mara, sanamu ziliondolewa ,

mapadre waliruhusiwa kuoa, Watawa walihamasishwa kutoka katika makao yao

yaliyowatenga na jamii na kuja kuishi na jamii. Nyumba za kitawa zilivunjika na

wakatumia mali zao katika kufadhili elimu na misaada kwa maskini.

Mwaka 1525 Zwingly alijitenga na kanisa katoliki, na akaanzisha mlengo wake. Mnamo

mwaka 1450 baada ya kuongoka Zwingly alianza kuwakusanya wanafunzi waliopenda

kujifunza kigiriki, baadhi ya wanafunzi hawa waliongoka na wakavutiwa sana na Biblia.

Katika mdahalo wa mji uliofanyika katika ukumbi wa mji, Zwingly aliwasilisha hoja 67

Mnamo Februari1523 ambamo aliambatisha mamlaka ya Kanisa la Romani Katoliki.

Mamlaka ya papa, kuwabudu watakatifu, wokovu kwa matendo mema, mifungo, sikukuu,

hija, vikundi (order) vya watawa, useja kwa mapadre, Uuuzaji wa vyeti vya msamaha,

adhabu na toharani. Viongozi wa mji walivutiwa sana na hoja za Zwingli.

Katika mdahalo mwingine wa Oktoba 1523 Zwingli alishambulia matumizi ya sanamu na

akataka kuiondoa Krismas. Viongozi wa mji hawakukubaliana na jambo hili na hivyo

zwingly alikaa kimya. Zwingry aliwaogopa watawala. Kulitokea kutoridhishwa kwa

wanafunzi wake Zwinngry

Baadhi ya wanafunzi wake waliokuwa wamemsaidia katika kuhitimisha hoja zake zote

mbili walijisikia kwamba wamesalitiwa na Zwingli. Kwa kuacha kushughulikia swala la

Sakramenti, kwa kuwapendeza watawala. Walikuwa wamefundishwa na yeye mwenyewe

kufuata mafundisho ya Biblia hivyo wakatambua kwamba Zwingly hakuwa anawaongoza

katika mwelekeo sahihi. Hivyo wakaamua kuanza kujisimamia wenyewe.

Vijana hawa walikuwa ni Conrad Grebel na Felix Manz. Conrad alikuwa ni mwanazuoni

wa kigiriki na Felix alikuwa ni mwanazuoni wa kiebrania. Kwa pamoja vijana hawa

46


waliongoza kikundi cha watu katika kujifunza kikamilifu mafundisho ya Biblia juu ya

ubatizo.

Mwaka 1524 walihitimisha kwamba ubatizo usifanywe kwa watoto wadogo. Walifundisha

kwamba watu waliompokea Yesu kama Bwana na mwokozi wao ndio wanaostahili

kubatizwa. Pia walitengeneza mawazo mapya kuhusu kanisa wakiamini kwamba kanisa la

kweli lilikuwa linahusisha watu wale walibatizwa baada ya kukiri.

Vijana hawa walijaribu kumshawishi mlezi wao wa zamani akubaliane na mawazo haya,

kwa kiasi fulani Zwingli alikubaliana na mawazo haya, japo shauku yake ya kuwapendeza

watawala ilisababisha kuwakataa na kupinga mawazo ya hawa wanafunzi wake wa

zamani.

Katika mdahalo wa Januari 18-19 – 1525 vijana hawa walibishana na Zwingli kuhusu

suala la ubatizo wa watoto, Kiongozi wa mji alimtangaza Zwingly kuwa mshindi wa

mdahalo huo na akatangaza ya kwamba yeyote ambaye hangefanya ubatizo wa watoto

wadogo au angebatiza ubatizo wa waamini alitakiwa ama kutubu au kuondoka Zurich

ndani ya siku nane.

Kuanzishwa kwa kanisa huru la kwanza.

Katika nyumba ya Conrad Grebel walikusanyika watu wachache ili kujadili nini

walitakiwa kufanya. Baada ya majadiliano hayo walifikia uamuzi wa kwamba wanatakiwa

kubatizwa upya kwa kwa sababu wote walibatizwa wakiwa watoto katika kanisa Katoliki.

Conrad alimbatiza George Blaurock kwa sababu mtu huyu alikuwa ni padre. Hivyo baada

ya kubatizwa kwake alipewa jukumu la kuwabatiza wengine. Kwa sababu hii walianza

kuitwa wanabatisti, maana yake ikiwa ni wabatizwa upya.

Hii ilikuwa ni moja ya mapinduzi ya matengenezo. Mapinduzi haya yalianzisha kanisa

jipya. Watu hawa walianza kukutana kwaajili ya ibada na wakaanza kueneza kanisa lao

katika maeneo mbalimbali.Kikundi hiki pia kiliitwa undugu wa uswisi.

Baada ya mlengo huu kukua na kuenea, ulishambuliwa na kupingwa sana karibu katika

Ulaya nzima. Kanisa la Romani Katoliki, pamoja na wanamatengenezo yaani Martin

Luther pamoja na John Calvin walihusika katika kuwaua Wanabatisti. Zaidi ya wanabatisti

4000 walinyongwa.

Mnamo mwaka 1529 wanamatengenezo walikutana katika mji wa Marbag ili kuweza

kuimarisha umoja wao. Wanamatengezo hao walikubaliana katika mambo kadhaa, lakini

kulitokea kutokukubaliana katika jambo moja ambalo ni meza ya Bwana. Zwingli alisema

kwamba mkate na divai ni kielelezo tu cha ukumbusho wa mauti ya Yesu, wakati Luther

alikaza kwamba kwa namna fulani Yesu alikuwa katika mkate na divai kwa njia ya fumbo.

Jambo hili lilileta utengano mkubwa baina ya wanamatengenezo hawa.

Kulizuka vita baina ya Kanisa la Romani katoliki na Waprotestant, katika vita hiyo

Zwingly aliuawa, hii ilikuwa mwaka 1531.

2. MARTIN LUTHER.

Martin Luther alizaliwa mnamo mwaka 1483. Baba yake aliitwa Hans na mama yake

aliitwa magareth. Alizaliwa katika familia ya kimsikini, baba yake alikuwa mfanyakazi

katika mgodi wa madini. Martin Luther alisoma Theolojia katika vyuo vikuu vya Erfurt

na Edburg. Mnamo mwaka 1505 alitunukiwa shahada ya kwanza katika falsafa na katika

47


mwaka 15012 alipata shahada ya pili ya udaktari katika Theolojia. Baada ya masomo yake

alianza kufundisha Biblia katika Vyuo Vikuu vya Erfurt na Witternberg Mnamo mwaka

1507 alipata ubarikio na kuwa padre.

Mnamo mwaka 1510, Martin Luther na mmonaki mwingine mmoja walisafiri kwenda

Rumi kwaajili ya shughuli za Chama chao cha umonaki. Akiwa Rumi alishangaa kuona

udhalimu uliokuwa ukifanywa na mapdre huko Rumi. Martin akiwa mmonaki alipata

mabishano makubwa moyoni mwake, na alijiuliza namna gani ambavyo angeweza

kupata rehema za Mungu. Alijipiga, Alifunga na kujitesa kwa muda mrefu ili aweze

kusamehewa dhambi zake. Alipata majibu ya maswali yake yote baada ya kusoma Waraka

kwa Warumi 1:16-17. Ukiwa na maneno mwenye haki ataishi kwa imani.

Wakati huo huo papa Leo X aliwatuma wawakilishi wake katika nchi mbalimbali

kukusanya fedha kwajili ya ujenzi wa kanisa la Mt Petro. Walikusanya fedha hivyo kwa

njia ya kuuza vyeti vya msamaha. Wakristo waliweza kununua vyeti kwajili yao wenyewe

na kwaajili ya ndugu zao waliokwisha kufariki ili waweze kupata msamaha.

Luther alipinga vikali jambo hili pamoja na mambo mengine ambayo yalikuwa kinyume

na Maandiko matakatifu kwa kuandika hoja 95 na kuzibandika katika mlango wa kanisa

Huko Wittenberg. Rafiki zake Luther walipiga kopi hoja hizo na kuzisambaza katika

maeneo mbalimbali ya nchi ya ujerumani ili ziweze kusomwa na watu wote. Kwa muda

mfupi nakala hizo ziliweza kuenea na mafundisho ya Luther yakaenea katika maeneo

mbalimbali.

Baada ya hoja hizo kuenea Luther aliitwa na Kardinali, Cajetan katika mji wa Dusgbarg (

1518). Kardinari huyo alimtaka Luther kukiri makosa yake lakini Luther alipinga swala

hilo.

Papa Leo X alimwandikia Luther barua ya kumtishia kumtenga na kanisa iwapo hangekiri

makosa yake. Baada ya Luther kuipata barua hii aliichoma moto hadharani mbele ya

kadamnasi

Mnamo mwaka 1521. Luther alitengwa rasmi na kanisa Katoliki. Luther aliitwa katika

mkutano uliofanyika katika mji wa worms ulioitishwa na kaisari Charles V, ili aweze

kusikilizwa na kumaliza mgogoro. Katika mkutano huo Luther alitakwa kukiri makosa

yake kuhusu vitabu alivyokuwa ameviandika na kuvisambaza. Luther alikataa kubadili

msimamo wake, kuyakana maandishi yake, na hatimaye kaisari na wafalme wake

walitangaza hukumu ya kifo dhidi ya Luther. Katika mkutano huo kulitokea fujo na

hatimae Luther alitoroka na kuokolewa na mfalme Fredrick wa Saksoni na kupelekwa

katika boma lake la Wartburg. Akiwa huko alijificha kama mfungwa na alibadilishwa jina

na kuitwa Jorg na kupelekewa nguo zingine. Alibadili sura yake kwa kufuga ndevu.

Akiwa katika boma hilo alianza kazi ya kutafsiri Biblia katika lugha ya kijerumani.

Katika muda huu wa kukaa mafichoni Luther alifanya kazi kubwa ya matengenzo kuliko

wakati mwingine wote kwake.

Mnamo mwaka 1529 Wafalme walibadili msimamo wao wakaamua kupigana dhidi ya

wanamatengenezo. Wafalme 19 walipinga uamuzi huu, na hivyo wakaitwa waprotestanti.

48


Hivyo neno hilo wakapewa watu wale waliokubali matengenezo ya kanisa. Martin Luther

alifariki dunia mnamo mwaka 17, Februari, 1546.

3. JOHN CALVIN

John Calvin Kwa kifarnsa Jean Cauvin alizaliwa mnamo Julai 10, 1509 katika mji wa

Nayoni jimbo la Picard Ufaransa. Baba yake aliitwa Gerard Cauvin, Mama yake aliitwa

Jeahn Lefrenc. Katika familia yao walizaliwa watoto watano, wakiume watatu na wakike

wawili ambapo mtoto wa kiume wa tatu alifariki angali mchanga siku chache tu baada ya

kuzaliwa. John Calvin alikuwa mtoto wa pili kuzaliwa katika familia ya baba yake. Gerard

Cauvin alikuwa Mwanasheria na msajiri katika ofisi ya Askofu wa Nayon.Gerard Cauvini

alitaka watoto wake wapate elimu bora kulingana na nafasi yake aliyokuwa nayo katika

kanisa. John alikuwa mtoto mwenye akili sana, akiwa na umri wa miaka 12 alipata kazi

katika ofisi ya askofu wa mji. Baba yake alipenda mtoto wake awe kuhani (padre) hivyo

basi John alijiunga na chuo kikuu cha Paris kusomea clasics.

Kabla ya kendelea na masomo zaidi kulitokea mgongano kati ya baba yake na askofu wa

Nayon, jambo ambalo lilimfanya baba yake kumsitisha John kuendelea na masomo katika

chuo kikuu cha Parisi ili asiendelee na matayarisho ya upadri badala yake John Calvin

alijiunga na chuo cha Orleans kusomea sheria.

Katika mwaka wa 1531 Gerard Cauvin alifariki dunia na hapo John Calvin akawa huru

kuchagua kusomea taaluma aliyoihitaji mwenyewe. John Calvin alirudi Paris tena

japokuwa baadae kidogo tena alirejea katika chuo ch Orleans kumalizia masomo yake ya

sheria.

Akiwa Paris alichapisha kitabu chake kimoja alichokiita Ufafanuzi wa kitabu na Seneka

(A commentary of a book by Seneca) mwandishi aliyeishi wakati wa dola ya zamani ya

Rumi.

Kwa wakati huu John Calvin alivutiwa sana na mafundisho ya wanamatenegenzo wa

Ujerumani. Moyo wake ulijazwa na upendo kwa Mungu na kwa watu wake. Inaamininka

kuwa kati ya wanamatengenezo wote wa Kanisa hakuna aliyetoa mchango mkubwa

katika kanisa kama John Calvin. Kwa kuwa hakuna kati yao aliyechunguza Neno la

Mungu kwa kina zaidi na kwa maombi zaidi kama John Calvin.

Wakati Waprotestanti wakiwindwa na kuteswa, john Calvin kwa wazi kabisa aliamua

kuwa upande wao. Aliwatembelea na kuwa tia moyo kwa kadli alivyoweza. Rafiki yake

aliyeitwa Nicholas Cop aliteuliwa kuwa mkuu wa chuo (rector ) chuo kikuu cha mji na

ilionekana kuwa john Calvin alimsaidia kuandaa hotuba yake ya Ufunguzi ambayo katika

hotuba hiyo Nicholas alilishambulia sana kanisa la Roman katoliki na kusisitiza

kufanyika kwa matengenezo. Baada ya hotuba hiyo Nicholas alishambuliwa na wanazuoni

wenzake na viongozi wengine na kuitwa mzushi na akalazimika kukimbia na kwenda

kuishi na wakimbizi kule Uswis Basel ili kuokoa uhai wake.

Baadae john Calvin alihusishwa kwamba alishirikiana na Nicholas Cop hivyo mwaka

uliofuta nayeye alilazimika kukimbia kwaajili ya usalama wake na kwenda Basel Uswisi

Mji wa Basel ulielezwa kuwa mji wa Uhuru na wa makimbilio kwa miaka mingi.

49


Baada ya kukaa Basel kwa mwaka mmoja john Calvin alimaua kwenda Straburg. Lakini

ilikuwa vigumu kwa yeye kuendelea kuwepo kule kutokana na vita ilyokuwepo kati ya

mfalme Francis I na Mfalme Charles V. hivyo basi John Calvin aliamua kuelekea kusini

na akaamua kutumia usiku mmoja pale Jiniva. Baada ya taarifa za ujio wa John Calvin

kumfikia William ferali mwanamatengenezo ya kanisa wa ufaransa pale Jiniva

alimkaribisha john Calvin na kumuomba kukaa pamoja nae na kuendeleza kazi ya

matengenzo ya kanisa pamoja. Hivi ndivyo john Calvin alivyoingia rasmi katika kazi ya

matengenezo ya Kanisa. Inasadikiwa kuwa john Calvin aliokoka mnamo mwaka 1530.

Ferali aliandika rasimu ya ukiri wa Imani na Calvin aliandika andiko lake la Uhuisho wa

Muundo wa Kanisa jiniva (Reorganization). Mnamo Januari, 16, 1537 Waliwasilisha

Rasimu yao mbele ya baraza la mji. Mwaka huohuo baraza lilikubali na kupitisha rasimu

hiyo.

Kadli miaka ivyozidi kwenda uhusiano baina ya baraza na wanamatengenzo hao ulianza

kuteteleka.Baraza lilisita kusimamia mapendekezo ya rasimu yao kwasababu wananchi

wengi walionekana kutokukubaliana na mapendekezo ya rasimu hiyo. Novemba 26

mwaka hu huo wanamatengenezo hao walifanya mdahalo na baraza kuhusu rasimu yao.

Kulitokea kutokuelewana katika mdahalo huo.

Mgongano mkubwa ulitokea pale ambapo viongozi wa mji wa Bern uliokuwa umeungana

na Jiniva katika matengenezo ya makanisa ya Uswisi ulipotoa mapendekezo ya

kuanzishwa kwa mfumo mmoja unaofanana (unifoymity) wa uendeshaji wa misa. Moja

ya mapendekezo hayo ilikuwa ni kutumika kwa mkate usiotiwa chachu katika sakramenti

ya Ekaristi Takatifu. Wanamatengenezo hao hawakuwa tayari kufuata wala kutekeleza.

Hawakuendesha misa ya sakramenti ya ekaristi wakisubiri mkutano wa sinodi kule Zurich

ambao ndio ungepaswa kutoa maamuzi ya mwisho Baraza liliwaamuru wanamatengenezo

hao kuendesha misa ya sakramenti ya ekaristi wakati wa pasaka. Wanamatengenezo hao

walikataa kuongoza misa wakati wa ibada ya pasaka. Jambo hili lilisababisha vurugu

katika ibada na siku iliyofuata baraza liliwaamuru Wanamatengenezo hao kuondoka mjini

hapo.

Wanamatengenezo hao wawili walipeleka kesi yao kule Zurich na Bern. Sinodi ilipoketi

iliwalaumu sana wanamatengenezo kwa kutokuwa watii kwaajili ya watu wa jiniva. Sinodi

iliwaomba Bern kufanya suruhu kwa lengo la kuwarudisha wanamatengenezo hao.

Baraza la Jiniva lilikataa kuwarudisha wanamatengenezo.

Ferali alipata mwaliko wa kwenda kuongoza kanisa Neuchâtel, John Calvin alipata

mwaliko wa kwenda Strasburg kuongoza kanisa la wakimbizi (refugees) John Calvin

alikutana na wanamatengenezo wa kanisa katika mji huu ambao ni Martin Bucer,

Wolfgang Capito. Miezi michache baadae John Calvin alipewa uraia katika mji huu.

Katika kipindi hiki John Calvin hakuambatana na kanisa moja tu bali bali alifanya kazi

katika makanisa kadhaa yakiwemo St. Nicholas na Kanisa la Dominika. Aliwahudumua

waamini 400-500 katika ibada moja.

50


Rafiki zake walimshauri John Calvin kuoa lakini yeye alikataa lakini baada ya muda kupita

alikubali na akamuoa mjane mmoja wa watoto wawili aliyeitwa Idelete Burry Walizaa

mtoto mmoja wa kiume aliefariki siku chache tu baada ya kuzaliwa kwake. Mkewe John

Calvin alifariki baada ya miaka tisa tu tangu kuoana kwao.

John Calvin alikaa kwa muda wa miaka mitatu hivi Strasburgy, wakati huu kanisa Katoliki

lilitaka kuurudisha mji wa Jiniva mikononi mwao. Kwa bahati rafiki zake Calvin

walifanikiwa kuchukua nafasi za uongozi katika baraza la mji wa Jiniva na wakaamua

kumwita John Calvin kurejea tena Jiniva. Mwanzoni Calvin hakuwa tayari kurejea Jiniva

kwa sababu hakuwa na uhakika kama alikuwa mtu sahihi kwa kazi ile. Hatimae mwaka

1541 aliamua kurudi Jiniva.

John Calvin alipokelewa kwa furaha mno pale jiniva na akapewa jukumu la kurejesha

mfumo wa maisha ya kijamii na kidini kulingana na neno la Mungu. Calvin alianza kazi

ya kuhuburi Neno la Mungu kwa mara ya pili pale Jiniva. Kutokana na kanuni

zilizowekwa watu wote kwa pamoja walikuja kusikiliza neno la Mungu. Jiniva

iligawanywa katika sharika (parish) tano zikiwa na wahudumu watatu na wahudumu

wasaidizi wawili. Ilikuwa ni lazima kuhudhuria ibada, faini iliwekwa kwa yeyote

asiyehudhuria

Kufikia katikati ya karne ya 16 John Calvin alikuwa kiongozi maarufu sana wa

matengenezo ya kanisa. Baada ya kifo cha Martin Luther mwaka 1546 watu wengi

waliotilia mashaka mafundisho ya Kanisa Katoliki walimwendea John Calvin kwaajili ya

ushauri na maelekezo.

Afya ya John Calvin ilianza kuzorota, mwili wake ulianza kuwa dhaifu kutokana na

kusoma na mifungo (Fasting). Calvin aliweza kupitisha siku kadhaa bila kula wala kupata

usingizi. Miaka mitatu kabla ya kifo chake afya yake ilizidi kuwa mbaya zaidi. Rafiki zake

walimshauri kupunguza kazi lakini yeye alikataa akawajibu mnataka Bwana anikute

sijamaliza kazi yake ?

Watu wengi waliokimbia mateso kutoka maeneo mbalimbali walipokelewa Jiniva. Mmoja

wa wakimbizi hao alikuwa ni John Knox wa Skotilandi. Vijana wengi walikwenda Jiniva

kuandaliwa kwaajili ya kazi ya huduma ya Injili Ulaya ya kati na ulaya Magharibi.

Mvuto mkubwa wa Calvin ulitokana na mafundisho na mihadhara yake. Vijana wengi

waliokuja kuandaliwa kwaajili ya huduma waliporudi kwao walibeba Kweli ya Neno la

Mungu katika mioyo na akili zao. Walieneza Nuru ya Injili katika maeneo yote.

John Calvin alikuwa anabebwa na kupelekwa kwenye mikutano aliyokuwa anahitaji

kuhudhuria. Mwaka 1564 alipelekwa kwenye ukumbi wa mji kuhudhuria mkutano wa

baraza na aliwashukuru sana kwa yote waliyofanya kwaajili yake. Siku chache viongozi

wa kanisa walimtenbelea akiwa kitandani, Calvin alisalimiana nao na kuwaaga.

Mwanamatengenezo huyu alifariki mnamo Mei 27, 1564 na alizikwa katika kaburi la

51


Cemetri ambalo halikuwekwa alama yoyote. Hadi sasa kaburi la John Calvin halijulikani

lilipo.

4. JOHN KNOX

John Knox alizaliwa katika miaka ya 1513 katika Haddington, mji mdogo kaskazini mwa

Edinburg, Scotland. Maisha yake ya awali yalimwezesha kukutana na watu wengi, na

elimu yake ya juu ilimwezesha kuwafikia watu wa hali ya juu katika jamii. Alipoteza

wazazi wake akiwa bado mtoto. Knox alijifunza kilatini shuleni Haddington. Mwaka 1529,

alianza masomo ya Theolojia katika chuo cha mtakatifu Andrews. Aliwekewa mikono ya

ukuhani mwaka 1536 ila hakuajiriwa katika nafasi hiyo kutokana na Scotland kuwa na

makuhani wengi.

Mwaka 1540, utawala wa Scotland ulianza kuwatesa wahubiri wa Neno la Mungu. George

Wishart hakuogopa muda wa majaribu na akasafiri kutoka kijiji kimoja hadi kijiji kingine

kuhubiri ukweli wa Biblia. Knox, kwa kushawishika na ujumbe wa Wishart, aliamua

kumsindikiza kama mlinzi wake, akiwa na mapanga mawili kumkinga mhubiri huyu dhidi

ya vitisho vya watesi. Kwa wiki tano, alimsindikiza Wishart katika kuhubiri kwake mpaka

mamlaka yaliamua kunyamazisha sauti ya mheshimiwa huyu kwa kumfunga gerezani.

John Knox Aliamua kujiunga nae na kumuunga mkono, lakini Wishart alimsihi arudi

nyumbani, akisema: “Hapana, rudi kwa watoto wako, na Mungu akubariki. Mmoja

anatosha kuwa kafara. Knox alirudi.

Henry Balnaves, mmoja ya waheshimiwa, alifurahishwa na kipaji chaa ufundishaji wa

wanamatengenezo na kuungana na mhubiri John Rough kwa kumwalika Knox kuwa mkuu

wa kanisa na mchungaji wa kanisa la nyumba ya mtakatifu Andrews. Knox alikataa

mwaliko huo, nakusema hawakuwa na mamlaka ya kutoa wito huo na kurudi chumbani

mwake

. Wiki chache baade, alihudhuria ibada ambayo mhudumu alitetea kanisa la kikatoliki

kuwa mke wa Kristo. Knox alishindwa kunyamaza na kuzungumza kwamba kanisa la

kikatoliki sio mke wa Kristo bali ni kahaba. Kanisa waliomba maneno yake yachunguzwe

jumapili iliyofuata. Baada ya siku saba, alihubiri Danieli 7, akilinganisha upapa na mpinga

Kristo, Knox alitambua maandiko kuwa mamlaka pekee kwa kutunga mafundisho ya dini

na kuthibitisha umhimu wa haki kwa imani pekee, mambo yaliounda msingi wa mahubiri

yake hadi mwisho wa uhai wake.

Siku kadhaa baadae, John Knox alitoa maandishi ya mafundisho yanayopinga utaratibu wa

misa, pugatori, na maombi kwa wafu. Ndipo palianza kazi ya John Knox, aliyetokea kuwa

mmoja wa wahubiri wa kupinga mafundisho potofu ya kanisa.

Kutoka utumwani kuwa mkuu wa Kanisa katika huduma kwa mfalme

Kundi la waheshimiwa kumi na sita, wafuasi wa mfia dini Wishart, waliokuwa

wamekasirishwa na padre David Beaton kwa kuuwa mhubiri huyo, waliuwa padre huo

52


nyumbani kwake miezi miwili baadae na kuhamia kwenye nyumba ya mfalme ya

Mtakatifu Andrews, ambako Knox alikuja kuisha mwaka mmoja baadae.

Kutokana na uasi huo, malkia wa kikatoliki Maria wa Gise aliamua kutafuta msaada

wa mfalme Henry II, mfalme wa Ufaransa, alietuma jeshi la meli na kushambulia nyumba

ya kifalme ya mtakatifu Andrews. Mweli Julai, 1547, wanamatengezo waliokuwa ndani ya

ngome hiyo walijisalimisha kwa jeshi la majini la Ufaransa wakachukuliwa mateka. Kati

yao alikuwepo pia na John Knox, ambae alifungwa pingu kwenye viti vya meli akiwa hana

nafasi ya kubadirisha mkao wake. Pamoja na wafungwa wengine wa vita na waharibifu

wengine , Knox alilazimishwa kusaidia kusukuma meli, afisa mmoja akiwa upande mmoja

kusubiri kuwapiga wafungwa ambao hawakuwa tayari kufuata maagizo katika kufanya

kazi ngumu.

Ndani ya meli, wafungwa walilazimishwa kushiriki misa na kutoa ishara ya kumheshimu

bikira Maria, au wateswe. Knox alikataa. Pale picha ya bikira Maria iliposukumizwa usoni

mwake ili aibusu, aliichukua nakuitupia baharini akisema, “Acha mama yetu ajiokoe; yeye

ni mwepesi sana; acha ajifunze kuogelea.”

Baada ya miezi kadhaa na kwa kuwa katika kipindi kikali cha msimu wa baridi kwenye

meli, afya ya Knox ilidhoofu sana. Pamoja nakuumwa bado alifariji wenzake katika

mateso, akiwa na uhakika ya kwamba wataachiwa huru na kuendeleza kazi yake ya

kutangaza ukweli wa Biblia. Miezi kumi na tisa ya mateso makali, majaribu na maumivu

makali. Inadhaniwa kuwa kwa ombi la mfalme wa Uingereza Edward VI John Knox

aliachiwa huru mwezi Februari 1549.

April 7, 1549, Knox aliitwa kutumika kama mhubiri katika mji wa Berwick-upon-Tweed,

chini ya Kanisa la Uingereza. Mwishoni mwa 1550, alihamishwa kama mhubiri wa kanisa

la Mtakatifu Nikolasi, mji wa Newcastle sehemu ya Taini; na 1551, aliwekwa kuwa

msimamizi mkuu wa dini wa Mfalme pamoja na wengine watano, ikimpa nafasi ya

kuhubiria ufalme. Kwa kipindi hiki, alipinga taratibu ya kupokea meza ya bwana kwa

kupiga magoti na pia mafundisho ya kwamba mwili halisi wa Kristo upo kwenye

Sakramenti

Knox alikutana na Elizabeth Bowes, mahiri na msomi wa maandiko, ambae alikuja

kumtambua kama mwelekezaji wake kwa mambo ya kiroho, na Margery Bowes, mmoja

wa binti zake Elizabeth, ambae alimchumbia mwaka 1553 na kuoa muda mfupi baadae.

Mwaka mmoja baadae alikuwa Geneva, Uswisi, akiwa ametoroka Uingereza alipoingia

Mary Tudor kwenye utawala na kurudisha uKatoliki nchini Uingereza. Knox alichapisha

kipeperushi akimshambulia malkia huyo kwa msimamo wake wa kikatoliki pamoja na

maaskofu waliomsaidia kuingia kwenye utawala, na pia kiongozi wa kirumi, Charles V,

akimtaja kuwa “Adui wa Kristo kama Nero

Kuhubiri Frankfurt

Muda mfupi baada ya kufika Uswisi, Knox alipokea barua ya mwaliko kuwa mchungaji

wa kanisa la wakimbizi wa Uingereza wanaoishi mji wa Frankfurt, Ujerumani na

53


akakubali. Kule Frankfurt tatizo lingine liliibuka: Taratibu za ibada. Mawazo

yaligawanyika na ujio wa wakimbizi wapya. Wengine waliunga utaratibu mpya uliokuwa

ukipendekezwa na Knox na wengine kuzitingatia kwa umakini sana kama ilivyo kwenye

kitabu cha taratibu za ibada za kanisa la katoliki. Kupitia ushauri wa Calvin, Knox

alifanikiwa kufikia makubaliano; ila na ujio wa wakimbizi wengi zaidi, msukumo ulizidi

kiasi ya kwamba waliokuwa wakipinga walishitaki kwa utawala wa Frankfurt, na

akaombwa aondoke. Hata hivo Knox alirudi Geneva.

Jaribio Jipya Scotland

Ndani ya Scotland, pamoja na nguvu ya kirumi, baadhi ya waheshimiwa waliamua

kusimamisha neno la Mungu kama msingi wa makanisa yao, walipinga mafundisho potofu

yaliyokuwa yakitolewa na kanisa. Baadhi yao walimwalika Knox kurudi Scotland ili

kusimamia maengenezo ya Kanisa. Kwa miezi tisa Knox alijitoa sana kuhubiri

mafundisho ya matengenezo na taratibu mpya za ibada katika makanisa mbali mbali ya

Scotland.

Kurudi kwake Scotland na umarufu wake kulishangaza makuhani wa Katoliki, waliomuita

ajitokeze mjini Ediburg mwezi Mei 15, 1556, wakimchukulia kuwa tishio kwa mamlaka ya

kanisa. Alisindikizwa kwenye hicho kikao na waheshimiwa wengi wenye ushawishi, na

maaskofu waliomshitaki waliamua kufuta mashtaka. Knox alikuwa huru kuhubiri wazi

misingi ya uprotestanti.

Kazi ya tatu Geneva

Gafla Knox aliamua kurudi Uswisi, na alifika Uswisi mwezi Septemba 13, 1556, pamoja

na mke wake, Margery Bowes, na mama mkwe wake, Elizabeth Bowes. Hii ilikuwa miaka

ya Knox ya furaha zaidi, licha ya kazi yake ngumu kama mchunganji katika kanisa la

kiingereza la Geneva, ambalo lilikusanyika kwenye Eglise de Notre Dame la Neuve,

ambalo kwa sasa linajulikana kama Ukumbi wa Calvin. Akiwa Geneva, watoto wake

wawili wakiume walizaliwa, Nathaniel na Eleazar.

Knox alishauri Geneva kwa marafiki zake wote Uingereza kuwa sehemu bora zaidi ya

kimbilio. Katika moja wa barua zake aliandika: “Sina hofu wala aibu kusema, (Geneva) ni

shule ya kristo iliyokamilika zaidi kutokea duniani tangu siku za mitume. Katika baadhi ya

sehemu na shuhudia Kristo kuhubiriwa kiukweli; ila tabia na dini yenye matengenezo ya

dhati sijawahi kuona katika sehemu nyingine.

Mwaka 1558 Knox aliandika akiwa Geneva mmoja wa vipeperushi vyake maarufu

kiitwacho “Sauti ya kwanza ya tarumbeta dhidi ya utawala wa kinyama wa wanawake.”

Knox alimaanisha Maria I wa Uingereza na Maria wa Gise wa Scotland kwa kutesa wa

protestanti na kusema wanapaswa kuondolewa katika utawala. Jarida hilo lilichapishwa

kisiri bila ushauri wa Calvin. Lilipigwa marufuku nchini Uingereza na hata Geneva na

Calvin, alilikataa kabisa. Knox mwenyewe alikubali kwamba jarida hili lilikamilisha

kufarakana kwake na marafiki zake wa Uingereza. Elizabeth Tudour, aliyekuja kuwa

malkia miezi michache baadae, alikwazika sana na jarida hilo na hakumsamehe Knox.

54


Kufunguka kwa matengenezo ya kiprotestanti Scotland

Pale malkia aliependelea uprotestanti, Elizabeth Tudor, alipoingia madarakani Uingereza,

wakambizi waliokuwa Ujerimani waliamua kurudi nchini kwao. Knox aliamua kurudi

Scotland. Kabla hajaondoka, utawala wa Geneva ulimtaja kwa heshima kwa mchango

wake kwa uprotestanti. Nchini Scotland, hali ilikuwa tete kati ya malkia Maria wa Gise na

kuandamana kwa waprotestanti.

Baada ya siku chache kufika Scotland, Knox alihubiri mahubiri ya kuvutia katika mji wa

Perth kupinga kuabudu sanamu kwa wa katoliki. Mara baada ya kumaliza tu, maandamano

yaliibuka dhidi ya kanisa la Katoliki, na kusababisha kuharibiwa kwa sanamu,

madhabahu, na hekalu na mji wa Perth uliozungushwa na ukuta kuchimbwa chimbwa.

Maria wa Gise alituma jeshi kuzingira huo mji. Mazungumzo yalifikia makubaliano na

jeshi la waprotestanti ili kusitokee vita na jeshi la Ufaransa waliounganika na Malkia Maria

wa Gise. Lakini baada ya kuingia kwenye huo mji, malkia aliujaza na jeshi la wa Scot kwa

kudhaminiwa na Ufaransa. Jambo hili lilichukuliwa kama usaliti kwa upande wa baadhi ya

waheshimiwa waliounga mkono makubaliano kati ya waprotestanti na wanaomuunga

mkono Mary wa Gise, hivo waliamua kubadili msimamo wao na kuunga mkono

matengenezo ya uprotestanti

Kutokana na matatizo ya Perth, Knox alienda katika kanisa la mtakatifu Andrews, huko

alihubiri ujumbe wa moto uliosababisha athari kama kule Perth - maandamano na

kuvunjwa kwa mali ya kanisa. Jeshi la waprotestanti waliweza kuvamia miji kadhaa

Scotland, wakiungwa mkono na mahubiri ya Knox yenye nguvu. Waheshimiwa wa

kiprotestant, wakisaidiwa na jeshi, pia walivamia Edinburgh, mji mkuu wa Scotland.

Mwezi Julai 25, 1559, baada ya viongozi wa kiprotestant, waitwao mabwana wa

kusanyiko, kujitoa katika mji Edinburgh, na malkia waScotland, Maria wa Gise, kuahidi

uhuru wa dhamira.

Ila malkia alikuwa na mpango mwingine. Aliomba msaada kutoka jeshi la ufaransa.

Walipotua Leith, waprotestanti waliuvamia na kuuchukua tena mji Edinburgh na kumvua

cheo Maria wa Gise kwenye kuongoza Scotland. Baadhi ya waheshimiwa waliweza

kushawishi Uingereza kutuma wanajeshi kusaidia waprotestanti.

Kifo cha malkia kiongozi Maria wa Gise mwezi Juni 10, 1560, kilitengeneza njia ya

muafaka wenye amani. Julai 6 mwaka huo, makubaliano ya Edinburgh yalitiwa sahihi,

ambapo jeshi la majini la Ufaransa na jeshi la Uingereza walipaswa kuondoka Scotland,

hivyo kuimarisha mwendelezo wa kiprotestant. Julai 19, Knox aliongoza ibada ya shukrani

kwa ngazi ya taifa kwenye kanisa la mtakatifu Gilles mjini Edinburgh. Kuanzia Agosti, 1,

1560, bunge lilikutana kutoa mwongozo mpya juu ya dini inayotambulika kitaifa. Knox,

pamoja na wachungaji wengine, waliandaa mwongozo mpya wa imani ambao bunge

lilipitisha na rasmi kuanzisha matengenezo ya kiprotestant nchini humo. Baadhi ya mambo

yaliyokataliwa na waprotestanti ni:-

‣ Mamlaka ya papa nchini Scotland yaliondolewa

‣ Mafundisho na matendo yote yalio kinyume na uprotestanti yalikataliwa

‣ Kuabudu Maria kulikataliwa

55


‣ Misa kwa lugha ya kilatini kuliondolewa

‣ Siku kuu za kikatoliki zilifutwa

‣ Maombi ya wafu yalipigwa marufuku

‣ Imani ya kwamba wafu wapo toharani ilikataliwa

‣ Misalaba ilikataliwa

‣ Sherehe za misa zilikataliwa

‣ Ilidhibitishwa kwamba mkate kuwa mwili wa Yesu ni mfano tu na sio kwamba mkate ni

mwili wake halisi.

Pamoja na hayo, bunge liliwaagiza Knox na wachungaji wengine kuandaa kuundwa upya

kwa kanisa la matengenezo nchini Scotland na taratibu mpya za ibada zilihamisha

msisitizo kutoka kweye kutazama makuhani na kuuweka kwenye kushirikiana kwa

waumini wote, na masomo ya Biblia, mahubiri, maombi, kusoma Zaburi na kuimba kwa

kusanyiko lote.

Magumu mapya

Disemba 1560, Knox alipokea pigo kubwa pale mke wake Margery alipofariki, akiachwa

na watoto wawili wadogo wakuwatunza, Muda usio mrefu sana baada ya hapo, Agosti 19,

1561, sauti ya mabomu ilisikika kwenye bandari ya Leith, ikitambulisha ujio wa Malkia

mdogo Maria, mtoto wa Maria Gise, aliyekuwa amekimbilia Ufaransa. Ilitangazwa

kwamba hakutakuwa na mabadiriko yoyote juu ya maswala ya dini na hakuna

kinachopaswa kusumbua wafanyakazi wake wakikatoliki.

Baadhi ya waheshimiwa, waliopendelea siasa, waliamua kumuunga mkono malkia mpya,

na si John Knox. Knox alipaza suti, akihubiri kupinga msimamo wa malkia kuhusu

mambo ya dini. Malkia Mary alimuita Knox wiki mbili baada ya kufika Scotland,

akimtuhumu kwa uasi wake na kuandika kupinga mamlaka yake.

"Baada yakuletwa uso kwa uso na malkia wa Scotland, mahali ambapo udhahiri wa

viongozi wakiprotestanti ulikosa nguvu, John knox alisimama bila kutikisika kushuhudia

ukweli. Hakukubali kununuliwa na maneno matamu, hakuwa na hofu kwa kutishwa.

Malkia alimshtaki kwa mafundisho potofu. Alikuwa amefundisha watu kupokea dini

iliokataliwa na taifa, alisema, hiyo ni kuvunja amri ya Mungu kwamba watu watii walio

juu yao.

Knox aliitwa Mara kadhaa na malkia kujibu mashtaka, lakini mwanamatengenezo huyu

alijibu kila wakati kwa msimamo na kuweza kubaki huru kutokana na ushawishi wake

mkubwa na kuungwa mkono na waheshimiwa wakiprotestanti. Malkia alimkumbusha

kwamba anapaswa kuishi kulingana na sheria za Scotland na kwamba misa ilikatazwa.

Mwezi Machi 26, 1564, Knox, akiwa hana mke, akiwa na miaka 50, aliamua kuoa tena, na

alimuoa Margaret wa Stewart, ambae alizaa nae watoto wakike watatu ambao ni Martha,

Margaret, na Elizabeth.

Knox hakunyamaza, Mwaka 1565, alihubiri, kama siku zote, kwa ujasiri, akipinga ndoa ya

malkia na Henry Stuart. Ndoa hiyo haikudumu, Stuart aliuwawa. Malkia Maria aliolewa

tena, . Kutokana na hayo, mamlaka ya Scotland ilimlazimisha Malkia Maria ajiuzuru

56


wadhifa wake, alifungwa jela kwenye nyumba ya kifalme ya Loch Leven lakini alifanikiwa

kutoroka Mei 2, 1568.

Miaka ya mwisho ya John Knox

Scotland ilijikuta ikiwa kwenye vita ya wenyewe kwa wenyewe kati ya wale waliomuunga

mkono malkia aliyeondolewa na waprotestanti.1571, msimamizi wa nyumba ya kifalme ya

Edinburgh, nae alimuunga mkono malkia, alifukuza waprotestanti wote kwenye jiji hilo.

Knox alistaafu kwenye nyumba ya kifalme ya mtakatifu Andrew lakini akarudi tena

mwaka 1572, tayari akiwa dhaifu kimwili kutokana na umri wake lakini, kama siku zote,

akiwa imara katika misingi yake ya kusambaza neno kwenye kanisa la mtakatifu Gilles,

akimtambulisha mrithi wake, mchungaji Lawson Aberdeen. Knox alirudi nyumbani kwake

kwa mara ya mwisho na kufariki Novemba 24, 1572, mke wake akimfariji na akiwa

amezungukwa na waprotestanti wenye vyeo vya heshima. Ombi lake la mwisho

lilikuwa kusomewa neno la Mungu. Mwili wake ulizikwa ndani ya kanisa la mtakatifu

Gilles

Mwanamatengenezo huyu hakuogopa sura ya mwanadamu. Moto wa Injili ya kweli

uliwaka ndani yake daima na alikuwa tayari kuitetea kweli ya Neno kwa gharama yoyote

ile.

Knox aliishi kwa imani. Alibaki kuwa mkweli kwa kazi yake na kwa ukweli wa Mungu,

akipigania vita ya Bwana hadi Scotland ilipata wa uhuru. Kanisa la Presbyterian lina

mtambua Knox kuwa mmoja wa waanzilishi wake.

Hitimisho

" Tunapaswa kuwa na shauku kama aliyokuwa nayo John Knox alipoomba mbele ya

Mungu kwa ajili ya Scotland. Alilia, "Nipe Scotland, Bwana, au nitakufa. Hakika shujaa

huyu alipewa Scotland kama alivyoomba na akawa tayari kufa kupona kuhakikisha nuru ya

matengenezo inang’aa Scotland.

Kwa hakika Wanamatengenezo walisimama kidete kuitetea kweli ya Mungu. Bado leo

Mungu anahitaji na anainua wanamatengezo katika kanisa la sasa. Kazi ya matengenezo

ya kanisa haijamalizika. Mungu analiandaa kanisa lake kwaajili ya unyakuo . Kazi ya

matengenezo ya kanisa itakwisha pale kanisa litakapokuwa limenyakuliwa kwenda

mbinguni.

Kanisa la leo limekengeuka. Ulimwengu umeingia kanisani na karibu kila mtu katika

dunia ya sasa anajiita ameokoka. Wanahitajika wanamatengenezo wa kizazi hiki

watakaosimama na kupaza sauti zao ili kulirudisha kanisa katika nafasi yake.

Kama mtumishi wa Mungu unapaswa kusimama katika zamu yako. Usimezwe na dunia

na anasa zake. Hubiri kweli ya neno la Mungu. Usikubali kuhalalisha baadhi ya mambo ili

kujipatia kundi kubwa au kujijengea umaarufu. Simama na Bwana katika utumishi

aliokwitia bila kuyumbishwa na mtu yeyote.

57


Ni matumaini yangu kuwa mambo yote uliyojifunza katika kozi hii yatakuwa chachu ya

kukufanya usimame katika nafasi yako ya kiutumishi na kumtumikia Bwana Yesu sawa

sawa na agizo lake.

Mungu anamtaka kila kiongozi asimame kwa miguu yake mwenyewe katika utumishi

Bwana aliomuitia.

Ezekieli 2:1 Akaniambia, mwanadamu simama kwa miguu yako, name nitasema nawe.

Kumbuka kuwa utumishi huu hatuufanyi kwa nguvu zetu wenyewe bali kwa kuwezeshwa

na Mungu mwenyewe.

(Zekaria 4:6) “Si kwa uwezo, wala si kwa nguvu, bali ni kwa roho yangu, asema Bwana

wa majeshi.”

1Wakoritho 2:4 Na neno langu na kuhubiri kwangu hakukuwa kwa maneno ya hekima

yenye kushawishi akili za watu, bali kwa dalili za Roho na nguvu, ili imani yenu

isiwe katika hekima ya wanadamu, bali katika nguvu ya Mungu.

Simama katika kweli ya Mungu na acha Mungu akutumie mwenyewe kama apendavyo.

PICHA ZA BAADHI YA WANAMATENGENEZO MAARUFU WA KANISA

Ulrich Zwingli Dr. Martin Luther John Carvin John Knox

58

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!