SHUJAAZ TANZANIA TOLEO 54

26.07.2019 Views

Mambo vipi? Tumepokea meseji nyingi sana kutoka kwenu na kama kawaida mimi na Jay tutajibu baadhi. #VEE mimi nina ndoto ya uchoraji wa ramani za nyumba. Nifanye nini ili ndoto yangu ikamilike? - Malugu Sijajua una kiwango gani cha elimu lakini nakushauri usomee masomo ya Usanifu majengo (Architecture) ya kiwango cha chuo kwa kuwa kipaji pekee hakitoshi kufanikisha ndoto zako. Ujenzi ni jambo linalohusisha sanaa na sayansi hivyo uelewa wa yote mawili unahusika sana. Isitoshe, ili kazi zako ikubalike, unahitaji vibali kutoka serikalini na vibali hivi hupewa watu waliokidhi vigezo. #Vee mimi ni mvulana nina miaka 27, nina mpenzi ambaye nipo naye kwenye uchumba kwa miaka mitatu sasa. Kila nikimwambia tuanze maisha anakataa, nifanyaje kwa sasa? Ndoa ni maamuzi makubwa na hufanywa mara moja hivyo mtu kupatwa na wasiwasi wa kuingia kwenye ndoa ni jambo la kawaida. Jaribu kuongea naye kuhusu sababu zinazompelekea kukataa, labda anaweza akawa na mipango ya kimaisha ambayo angependa kuikamilisha kabla hajaingia kwenye ndoa kama masomo,kazi au biashara au labda bado hajajiridhisha kwamba wewe ni mtu sahihi kwake. Muondoe wasiwasi na mhakikishie kuwa utamsapoti kwenye masomo au mishe zake hata baada ya ndoa na kuwa wewe ndiye mtu sahihi kwake. #VEE, kuna umuhimu wowote wa kuwa na boyfriend ukiwa shule? Sijawahi kusikia mtu amefaulu kwa kuwa na mpenzi bora shuleni kwa kuwa ulichokifuata pale ni elimu na si kingine. Hakuna ulazima wa kuwa na mpenzi ukiwa shuleni kwa kuwa wanafunzi wengi hujiingiza kwenye mahusiano si kwa mapenzi ila ni kwa kufuata mkumbo na mihemko inayotokana na ukuaji. Huna haja ya kufuata wengine, kuwa wewe kwa kuwa dunia nzima ina wewe mmoja na imejaa watu wengine. 1 2 Vee, mimi ni msichana wa miaka 20 na kuna kaka ananipenda sana na mimi nampenda lakini nasikia kuwa ni mume wa mtu. Nikimuuliza anakataa na nikimwambia tuachane hataki, nifanyeje? Kuna mambo matatu muhimu ya kuzingatia: Wanaume wako wengi sana, huna haja ya kuwa na mume wa mtu na kuvunja ndoa za watu. Bado una umri mdogo, una nafasi ya kupata mtu mwingine atakayekufaa hapo mbeleni hivyo usiogope kuachana naye. Huna haja ya kumuomba kuachana naye, ni kitendo cha kumpa taarifa tu na kuendelea na maisha yako. Hakuna mtu anayemiliki maisha ya mwingine hivyo chukua umiliki wa maisha yako.

Vee mimi ni kijana wa miaka 24, nina mchumba ananipenda nami nampenda, tatizo anapenda hela! Nikimwambia sina ananiambia mimi mwanaume gani sina hela? Naomba ushauri - Fadhili Wanaume huvutiwa na uzuri wa wanamke na wanawake huvutiwa na wanaume wazuri na wenye mafanikio hivyo ni muhimu kuhakikisha unafanikiwa au unaonesha jitihada na una mipango ya kuleta mafanikio ili kuendeleza mahusiano yako. Lakini kama huyo msichana anakupenda kipindi una pesa na kukudharau kipindi huna basi kuna uwezekano mkubwa kuwa anapenda pesa zako zaidi ya kukupenda wewe. Endelea naye lakini akiendelea kukudharau haina haja ya kuendelea naye. #Vee je, ukitumia njia za uzazi wa mpango unaweza kupata madhara? - Asha Njia za uzazi wa mpango zipo nyingi, kuna vidonge, kitanzi, sindano, kijiti, mipira ya kike na ya kiume, pachi na kadhalika. Zote hizi hufanya kazi tofauti tofauti na kutokea kwa madhara kutategemea na mwili wako uta-react vipi na njia hizo hivyo, ni muhimu kupata ushauri wa daktari kuhusu njia sahihi na itakayokufaa kabla ya kuanza kutumia. Kama ikishindikana kupata daktari basi tumia mipira ya kike au ya kiume. #Vee nataka kufuga kuku lakini sijui nitatoa wapi mkopo wa kuanzisha biashara hii, naomba ushauri. Kuna mifumo rasmi na isiyo rasmi ya kupata mikopo. Njia rasmi ni pamoja benki, vikoba, SACCOSS, serikali za mitaa kupitia mifuko ya maendeleo ya vijana, mitandao ya simu na kadhalika, huku njia zisizo rasmi ni pamoja na vikundi vya kuwezeshana (mchezo), mikopo kutoka kwa ndugu, jamaa na marafiki, taasisi za kidini na kadhalika. Kwa njia zilizo rasmi, kuna mahitaji utatakiwa kuwasilisha kulingana na ukubwa wa mkopo au mifumo wanayotumia kwa mfano dhamana, rekodi zako za kibenki na kadhalika wakati njia zisizo rasmi mara nyingi huwa na masharti machache na kiwango kidogo cha pesa. Unaweza kujaribu njia yoyote kati ya hizi kulingana na mahitaji yako. Nakushauri uanze kidogo kidogo, usichukue mkopo mkubwa halafu biashara ikafanya vibaya na ukashindwa kurudisha pesa za watu. # Vee, kuna msichana nampenda sana ila ana V.V.U, nifanyaje? Kumpenda mtu mwenye V.V.U hakuna ubaya wowote kwa kuwa siku hizi V.V.U ni ugonjwa unaoweza kuudhibiti kama umeupata na unaweza kujizuia kuupata kama bado. Cha muhimu ni kwenda kwa muelimisha rika ili kupata ushauri zaidi na kujua jinsi gani ya kuishi pamoja bila ya mmoja kumuambukiza mwenzake, mtoto na kadhalika. Tuma maswali kwenda 0784551616 nasi tutayajibu. Kumbuka, anza na #Vee. Kwa maswali yanayohusiana na unyanyasaji unaweza kupiga 116 ili kuongea na mtaalam. Kwa maswali ya elimu ya afya ya uzazi piga 0800753333.

Vee mimi ni kijana wa miaka 24, nina mchumba ananipenda nami nampenda, tatizo

anapenda hela! Nikimwambia sina ananiambia mimi mwanaume gani sina hela?

Naomba ushauri - Fadhili

Wanaume huvutiwa na uzuri wa wanamke na wanawake huvutiwa na wanaume wazuri na

wenye mafanikio hivyo ni muhimu kuhakikisha unafanikiwa au unaonesha jitihada na una

mipango ya kuleta mafanikio ili kuendeleza mahusiano yako. Lakini kama huyo msichana

anakupenda kipindi una pesa na kukudharau kipindi huna basi kuna uwezekano mkubwa

kuwa anapenda pesa zako zaidi ya kukupenda wewe. Endelea naye lakini akiendelea

kukudharau haina haja ya kuendelea naye.

#Vee je, ukitumia njia za uzazi wa mpango unaweza kupata madhara? - Asha

Njia za uzazi wa mpango zipo nyingi, kuna vidonge, kitanzi, sindano,

kijiti, mipira ya kike na ya kiume, pachi na kadhalika. Zote hizi hufanya

kazi tofauti tofauti na kutokea kwa madhara kutategemea na mwili

wako uta-react vipi na njia hizo hivyo, ni muhimu kupata ushauri wa

daktari kuhusu njia sahihi na itakayokufaa kabla ya kuanza kutumia.

Kama ikishindikana kupata daktari basi tumia mipira ya kike au ya kiume.

#Vee nataka kufuga kuku lakini sijui nitatoa wapi

mkopo wa kuanzisha biashara hii, naomba ushauri.

Kuna mifumo rasmi na isiyo rasmi ya kupata mikopo. Njia

rasmi ni pamoja benki, vikoba, SACCOSS, serikali za mitaa

kupitia mifuko ya maendeleo ya vijana, mitandao ya simu

na kadhalika, huku njia zisizo rasmi ni pamoja na vikundi vya

kuwezeshana (mchezo), mikopo kutoka kwa ndugu, jamaa na

marafiki, taasisi za kidini na kadhalika. Kwa njia zilizo rasmi,

kuna mahitaji utatakiwa kuwasilisha kulingana na ukubwa wa

mkopo au mifumo wanayotumia kwa mfano dhamana, rekodi

zako za kibenki na kadhalika wakati njia zisizo rasmi mara nyingi

huwa na masharti machache na kiwango kidogo cha pesa.

Unaweza kujaribu njia yoyote kati ya hizi kulingana na mahitaji

yako. Nakushauri uanze kidogo kidogo, usichukue mkopo

mkubwa halafu biashara ikafanya vibaya na ukashindwa

kurudisha pesa za watu.

# Vee, kuna msichana nampenda sana ila ana V.V.U, nifanyaje?

Kumpenda mtu mwenye V.V.U hakuna ubaya wowote kwa kuwa

siku hizi V.V.U ni ugonjwa unaoweza kuudhibiti kama umeupata

na unaweza kujizuia kuupata kama bado. Cha muhimu ni kwenda

kwa muelimisha rika ili kupata ushauri zaidi na kujua jinsi gani ya

kuishi pamoja bila ya mmoja kumuambukiza mwenzake, mtoto na

kadhalika.

Tuma maswali kwenda 0784551616 nasi tutayajibu. Kumbuka, anza na #Vee.

Kwa maswali yanayohusiana na unyanyasaji unaweza kupiga 116 ili kuongea na

mtaalam. Kwa maswali ya elimu ya afya ya uzazi piga 0800753333.

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!