27.12.2015 Views

MCHANGO WA MOFOLOJIA KATIKA ISIMU

Create successful ePaper yourself

Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.

Chuo Kikuu cha Katoliki Afrika Mashariki

Bewa la Langata

Kitivo cha Sanaa na Sayansi za Kijamii;

Kitivo cha Elimu

Idara ya Kiswahili

Kozi: Kis 300; Mofolojia ya Kiswahili

Kazi ya Muhula: Mchango wa mofolojia katika taaluma nzima ya isimu.

Mwanafunzi wa shahada ya kwanza;

1024584 Chaka Jumaa Ngombeko

@jumaachaka

Chaka Jumaa Nazarety

Agosti-Disemba; 2015

1

UTANGULIZI.

Isimu hushughulikia uchunguzi wa lugha mbalimbali kwa kutumia misingi ya kisayansi.

Matawi ya isimu kama fonetiki, fonolojia, semantiki, mofolojia na sintaksia ndiyo huifanya

isimu kuonekana kuwa sayansi ya lugha kulingana na majukumu mbalimbali yanayofanywa

na matawi haya katika lugha.

Fonetiki huchunguza sauti za lugha ya binadamu; nayo fonolojia huchunguza jinsi sauti hizo

huweza kuunganisha na kuunda maneno yenye maana na baadaye mofolojia huangalia maneno

yaliyoundwa miundo yake na kuzalisha maneno zaidi.

Mofolojia ni taaluma ya isimu ambayo ina jukumu la kuchunguza maneno ili kuelewa maumbo

yake yalivyo (Mgullu, 1999).

MCHANGO WA MOFOLOJIA KATIKA TAALUMA NZIMA YA ISIMU.

Matthews (1991, Uk3) Mofolojia ni tawi la isimu linaloshughulika na ustadi wa maumbo ya

maneno na jinsi maumbo hayo yanavyotumika katika miktadha mbalimbali ya matumizi ya

lugha. Jukumu la neno husika katika sentensi hubainika vyema kulingana na uhusiano baina

ya maneno mengine katiaka tungo. Kwa mfano: Jumaa amefika chuoni. Jumaa ni kiima kwani

ndilo neno linalohusika na utendaji ilhali amefika chuoni ni kiarifu kwani sehemu hii inatoa

maelezo juu ya kiima.

Maneno ni maumbo katika lugha yanayojisimamia. Maneno yenye maumbo sahili huwa na

mofu moja tu; hayawezi kukatwakatwa na kutoa mofu zingine. Mofu hizi ni mofu huru. Kwa

mfano baba, mama. Kwa upande mwingine maneno yenye maumbo changamani huwa na

mofu zaidi ya moja; yaani kiambishi awali, mzizi na kiambishi tamati. Kwa mfano;

Mtangazaji {M+tangaz+a+ji}

{M}-kiambishi awali cha kunominisha;

{-tangaz-} mzizi wa nomino

{-a-} kiambishi tamati endelezi

{-ji} kiambishi tamati cha kunominisha

Bauer Laurie (2003, Uk 91), taaluma ya mofolojia imegawanywa katika matawi mawili;

mofolojia ya minyambuliko ya maneno na mofolojia ya uundaji wa maneno. Mofolojia ya

minyambuliko ya maneno husaidia kupatikana kwa maumbo mbalimbali ya leksimu ilhali

mofolojia ya uundaji wa maneno husaidia kupatikana kwa leksimu mpya. Maneno

yanapoundwa husaidia katika kuboresha mawasiliano baina ya binadamu. Watumiaji wa lugha

2

hutafuta njia mbalimbali ili kupata maneno yanayotosheleza mawasiliano yao. Hivyo basi

mofolojia imejenga isimu-jamii.

Matthews (1991, Uk9) mofolojia ni tawi la kisarufi linalochunguza maumbo ya ndani ya

maneno. Mofolojia hutilia maanani sarufi ambayo ndiyo sehemu muhimu ya kila lugha. Sarufi

ndiyo uti wa mgongo wa kila lugha hapa duniani. Bila sarufi lugha haiwezi kuwa na muundo

sanifu unaokubalika na wenye kueleweka na watumiaji wake. Mofolojia huangalia hijai.

Mofolojia huhakikisha maneno yameendelezwa vizuri. Ni sehemu hii ndiyo inaonyesha jinsi

mofolojia huchunguza muundo wa maneno ambayo yameundwa kwa kutegemea taaluma ya

fonolojia.

Matthews (1991, Uk 63) mofolojia pia huonyesha mifanyiko mbalimbali ya maneno katika

lugha. Kwa mfano nomino huweza kuundwa kutokana na vitenzi, kiwakilishi, vivumishi,

kielezi. Katika lugha ya Kiingereza maumbo ya nomino hutokana na maumbo ya vitenzi

yanapoongezewa mofu –ion-. Kwa mfano:generate-generation.

Katika lugha ya Kiswahili aina ya neno huweza kubadilika linapoambishwa au kunyambuliwa.

Kwa mfano: nomino msomi inaweza kuzalisha maneno kama kisomo, masomo, somea, someka,

kusomeka.

Mofolojia huhusika na utambuzi wa mofu, mofimu, shina, mzizi na alomofu katika neno.

Dhana hizi ambazo zilizalishwa na taaluma ya mofolojia husaidia katika taaluma nzima ya

isimu ambapo dhana hizi huleta maana katika maneno ya lugha. Maana inayopatikana katika

maneno ya lugha ndiyo semantiki.

Mgullu (1999), mofu ni umbo la neno ambalo huwakilisha mofimu na ambalo hudhihirika

kifonolojia. Mofu ni sehemu halisi ya neno ambayo ina maana.

Mtangazaji (M+tangaz+a+ji)

{M} kiambishi awali cha kunominisha;

{-tangaz-} mzizi wa nomino

{-a-} kiambishi tamati endelezi mofimu

{-ji} kiambishi tamati cha kunominisha

Kumekuwa na swala la kuainisha lugha hasa katika karne ya Ishirini. Hapo mwanzo kulikuwa

na haja ya kuelewa lugha ya kilatini na Kigiriki. Uelewa wa lugha zingine uliendelea kukua

pia; ndipo lugha zikaanza kuainishwa kifamilia. Katika taaluma ya mofolojia lugha

zinaainishwa kulingana na muundo wa maneno ya lugha hizo. Kigezo hiki cha kimofolojia

kinatupatia lugha ambishi na tenganishi (Matthews, 1991 uk3-4). Hii husaidia kutofautisha

miundo ya maneno ya lugha mbalimbali. Hivyo basi mofolojia inasaidia kuelewa miundo ya

3

maneno ya lugha. Pia wanaohitaji kujifunza lugha za kigeni huweza kujifunza kwa urahisi

wanapoelewa muundo wa maneno ya lugha hiyo.

Mgullu (1999, Uk 12), lugha ambishi ni ile lugha ambayo maneno yake huambishwa viambishi

mbalimbali ambavyo huwakilisha maana mbalimbali; kwa mfano lugha ya Kiswahili- Neno:

PIGA

Anapiga

Atapiga

Alipigia

Alipigiwa

Matthews (1991, Uk 20) Lugha tenganishi ni ile aina ya lugha ambayo maumbo ya maneno

yake huonekana tu kama mofu moja moja. Mfano ni Kituruki, Kichina na Kiingereza.

Maumbo ya maneno ya lugha tenganishi hayaambishwi wala kunyambuliwa. (Mgullu, 1999

Uk 12). Kwa mfano katika lugha ya Kiingereza;

With,

Rice.

Matthews (1991, Uk 19), mofolojia imeleta mchango mkubwa katika isimu nzima. Mofolojia

ni kiungo muhimu katika isimu. Mofolojia imeweka wazi masuala muhimu kuhusu maumbo

ya maneno katika lugha zote duniani. Mofolojia imeweza kusaidia wanaisimu kutambua mofu,

mofimu, na alomofu katika kuchunguza miundo ya maneno katika lugha.

Kwa mfano; viambishi katika lugha ya Kiingereza hupatikana mwishoni mwa mzizi wa neno

kwa sababu mara nyingi huonyesha dhana ya wingi; kama –s, ies, ren, (child-children). Katika

lugha ya Kiswahili mara nyingi mzizi wa neno hutanguliwa na mofu ambayo ni kiambishi

awali na kisha kufuatiwa na kiambishi tamati. Haya ni yale maneno ambayo yana mofu

tegemezi. Kwa mfano:

-endnaenda

Siendi

Endea

Endeleza

Hivyo basi mofolojia imesaidia kujua maumbo ya maneno ya lugha mbalimbali.

Matthews (1991, Uk 19-20) mofolojia inaeleza jinsi maneno katika lugha yanavyobadilika hasa

kimaendelezo jinsi muda unavyosonga. Hapa mofoloia hujikita kuangalia mabadiliko ya

maneno katika lugha husika kwa kuzingatia vipindi vya kihistoria. Mahitaji ya kimatumizi ya

maneno husika katika lugha ndiyo husukuma wanajamii kubadili dhana za kimatumizi ya

4

maneno fulani kulingana na wakati huo. Kwa mfano; neno girl (gyrle) hapo kale lilikuwa

linamaanisha mtoto wa kiume au wa kike lakini likafinyika kimaana na leo hii linarejelea tu

mtoto wa kike. (http://www.etymonline.com/index.php?term=girl).

Katika lugha ya Kiingereza kipashio –pter- kiliazimwa kutoka lugha ya Kigiriki kikiwa

kinamaanisha unyoya feather au ubawa wing. Kipashio hiki kimetumika kuunda neno

helicopter ambapo kifaa hiki kina tabia sawa na dhana ya kipashio hicho (Katamba na

Stonham, 2006 Uk.22) Hivyo basi mofolojia imesaidia kueleza historia ya maneno katika

lugha.

Matthews (1991, Uk 37) mofolojia husaidia katika kupeana njia mbalimbali za uundaji wa

maneno katika lugha. Hii ni kwa sababu kila lugha inakua kulingana na mahitaji ya jamii yake.

Kila lugha inahitaji maneno mapya yaundwe kila siku kwa sababu jamii mbalimbali

hutagusana kila siku. Ili kurahisisha mawasiliano lazima kuwe na maneno yanayoweza

kusaidia kurahisisha mawasiliano ya watu wa jamii hizo tofauti. Pia maneno yanaweza

kuundwa ili kupeana majina vitu vigeni; yaani vitu vinavyovumbuliwa kila siku kupitia

teknolojia. Kuna njia kama mwambatano, kukopa, kubuni, akronimu. Maumbo ya maneno

yanayoundwa hutegemea mazingira ya jamii na sheria inayothibiti uundaji wa maneno katika

lugha hiyo. Hivyo basi mofolojia husaidia kuchagua njia mwafaka ya uundaji wa maneno

kulingana na mazingira husika.

(Katamba na Stonham, 2006 Uk. 78-79), mofolojia pia inadhihirisha uhusiano uliopo baina ya

lugha moja na nyingine. Lugha nyingi duniani zinategemeana katika mawasiliano. Wenyeji wa

lugha mbalimbali hulazimika kukopa maneno ya lugha za kigeni ili kusaidia katika

mawasiliano. Mofu za kigeni zinapoingizwa katika lugha fulani husahihishwa na kufuata

muundo wa maneno ya lugha husika kulingana na sheria ya uundaji wa maneno wa lugha hiyo.

Hivyo basi mofolojia imesaidia lugha nyingi kuingiza mofu za kigeni na kukuza lugha hizo na

kurahisisha mawasiliano.

Taaluma ya mofolojia hueleza ni kwa nini majina mengine huwa na maumbo yale yale katika

dhana ya umoja na wingi. Majina kama maziwa, mchanga, maji hubaki vivyo hivyo

kimaandishi katika umoja na wingi. Mofolojia imerahisisha kueleweka kwa hali hii kwani

majina mengine huwa tu na dhana ya wingi au umoja katika akili za wazungumzaji. Mofolojia

hutumia mofu kapa kuonyesha umoja au wingi wa majina kama hayo.

5

Kwa mfano:

Wingi

Maziwa

umoja

Ømaziwa

Mofolojia ndiyo chanzo cha kujifunza msamiati. Wanafunzi hutumia elimu ya mofolijia ili

kutambua maana ya maneno yanayoibuka kila wakati. Mofolojia huwa na sharia ambazo

humwongoza msemaji kuongeza umilisi katika lugha.

Mofolojia humhamasisha mwanafunzi kuhusu uandishi na usomaji bora katika lugha.

Mwanafunzi huweza kujua namna ya kuandika maneno na maumbo yake mbalimbali.

Msomaji anapotambua sheria ya uundaji wa maneno katika lugha na jinsi ya kuandika na

kusoma maneno humrahisishia kusoma matini mbalimbali na kuzielewa vizuri. Mofolojia

husaidia kujua maana ya maneno inayonuiwa katika mawasiliano ndani ya lugha. Maana ya

maneno huenda yakabadilika kutegemea mazingira yalimowekwa. Maneno yanapowekwa

pamoja na maneno mengine katika tungo huweza kuwa na maana. Hivyo basi mofolojia

imejenga semantiki na sintaksia na kuifanya isimu nzima ikue (Nagy, Carlisle & Goodwin

(2013).

Maneno huweza kuwekwa katika makundi yaani ngeli. Nomino hugawanywa na kuainishwa

kimakundi kulingana na sarufi; kila kundi likiwa na mabadiliko ya aina moja ya viambishi vya

umoja na wingi (Kihore na wenzake, 2003).Mofolojia ndiyo imechangia kuainisha ngeli

kisintaksia kwani maana ya maneno yanayofafanuliwa na taaluma ya mofolojia ndiyo

huongoza uanishaji wa majina kisintaksia.

6

Marejeleo:

Bauer Laurie (2003), Introducing Linguistic Morphology: 2 nd Edition. Edinburgh. Edinburgh

University Press.

Katamba Francis and Stonham John (2006), Modern Linguistics Morphology: New York.

PALGRAVE MACMILLAN.

Kihore na wenzake (2003), Sarufi Maumbo ya Kiswahili Sanifu. Dar es Salaam: TUKI

Matthews P. H (1991), Morphology (Second Edition): United Kingdom. Cambridge University

Press.

Mgullu R. S. (1999), Mtalaa wa Isimu: Fonetiki, Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili. Nairobi.

Longhorn Kenya Ltd.

Nagy, W. E., Carlisle, J. F, & Goodwin, A. P. (2013). Morphological Knowledge and Literacy

Acquisition. Journal of Learning Disabilities, 47(1) 3–12. DOI: 10.1177/0022219413509967.

7

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!