SACCOS_Traing_Guide

SACCOS_Traing_Guide SACCOS_Traing_Guide

24.10.2015 Views

78 Mwongozo wa Mafunzo ya SACCOS 15. ELIMU YA UJASIRIAMALI NA STADI ZA BIASHARA 15.1 Ujasiriamali katika sekta ya biashara (Entrepreneurship) Ujasiriamali ni kuanza na kuendesha na kumiliki biashara inayojitegemea. 15.2 Mjasiriamali ni nani? Mtu yeyote anayeamua kuchukua uamuzi hatarishi kwa kuwekeza mtaji katika kuanzisha mradi ili kuingiza kipato na kupata faida. 15.3 Sifa za mjasiriamali Mjasiriamali ana sifa kuu tatu:- ‣ Ni mwenye ufahamu. ‣ Ni mwenye stadi. ‣ Ni mwenye tabia za kijasiriamali. (i) Ni mwenye ufahamu Mjasiriamali lazima awe na ufahamu wa mambo yote yanayohusu kuanzisha na kuendesha miradi ya kuongeza kipato/biashara. Ufahamu wa kujua nini maana ya biashara, kujua kutathmini wazo la mradi, kutengeneza mchanganuo wa mradi na habari zote za masoko. (ii) Ni mwenye stadi Mjasiriamali lazima awe na ujuzi wa mradi anaoamua kuanzisha. (iii) Ni mwenye tabia za kiujasiriamali Ujasiriamali si tu kufanya biashara bali ni ile tabia unayoweza kuionyesha kwenye biashara yako. Mjasiriamali ana tabia zifuatazo:- (a) Ni mbunifu (Innovative) Mjasiriamali ni mbunifu katika biashara kwa kuweka kitu kipya, mambo mapya, taratibu mpya, mipango mipya, kuweka huduma tofauti na wenzake wenye biashara ileile. (b) Ni mwenye kuthubutu (Risk-taking) Kuthubutu kwa mjasiriamali kuna kuja kwa njia nyingi kama vile: ‣ Kufanya uamuzi wa kuwekeza.

Mwongozo wa Mafunzo ya SACCOS 79 ‣ Kufanya uamuzi wa kuanzisha mradi au kufanya Biashara. Mjasiriamali huwa hajutii uamuzi na ushauri alioufanyia kazi pale anapoanguka kibiashara au kupata hasara, hukaa chini na kutafakari na kurekebisha makosa na kuendelea na biashara. (c) Ni mwepesi wa kuona fursa (Opportunistic). Mjasiriamali ni mwepesi wa kuona fursa na kuitumia, anazitafuta fursa, anaziendeleza, na anapata maendeleo. (d) Ni mwenye kuwa na malengo [achievement oriented] Mjasiriamali huweka malengo ya shughuli anazozifanya, huwa haridhiki, anajitahidi kupanua kila wakati biashara yake, anaiendeleza na kuikuza na baadaye malengo yake yanakuwa makubwa.Wafanyabiashara walioridhika siyo wajasiriamali. (e) Ni mwenye bidii (Hard working). Mjasiriamali ni mwenye bidii ya kufanya kazi na hakati tamaa kirahisi. (f) Anayejitegemea (Independent). Ni mwenye kushughulikia matatizo yake kwanza mwenyewe, anatafuta ni jinsi gani ya kujikwamua mwenyewe, anafikiria kwanza mwenyewe kabla ya kutafuta msaada. (g) Ni mwenye kujenga uhusiano (Networking). Mjasiriamali anajitahidi kufahamiana na watu wengine wengi, anapojenga uhusiano na watu mbalimbali inamsaidia kuondoa matatizo mengi ya kibiashara. (h) Ni mwenye kuona mbali (Future oriented). Mjasiriamali anaangalia mbali katika biashara. Hata akifa biashara yake inaendelea kuwepo. (i) Ni mwenye kutunza kumbukumbu. Mjasiriamali ni mtunzaji wa kumbukumbu zinazomsaidia kukumbuka, kuona kama anapata faida au hasara na inamsaidia kujua mambo muhimu yanayohusu biashara zake kwa ajili ya maboresho. 15.4 Changamoto zinazowakabili wajasiriamali (i) (ii) Miradi mingi ya kuongeza kipato inayoendeshwa haina sifa ya kujiendesha kwa faida. Wajasiriamali wengi hufanya biashara zao kwa kubahatisha bila kujua wanatarajia nini na kwa kipindi gani.

78 Mwongozo wa Mafunzo ya SACCOS

15. ELIMU YA UJASIRIAMALI NA STADI ZA BIASHARA

15.1 Ujasiriamali katika sekta ya biashara (Entrepreneurship)

Ujasiriamali ni kuanza na kuendesha na kumiliki biashara inayojitegemea.

15.2 Mjasiriamali ni nani?

Mtu yeyote anayeamua kuchukua uamuzi hatarishi kwa kuwekeza mtaji katika kuanzisha mradi ili

kuingiza kipato na kupata faida.

15.3 Sifa za mjasiriamali

Mjasiriamali ana sifa kuu tatu:-

‣ Ni mwenye ufahamu.

‣ Ni mwenye stadi.

‣ Ni mwenye tabia za kijasiriamali.

(i)

Ni mwenye ufahamu

Mjasiriamali lazima awe na ufahamu wa mambo yote yanayohusu kuanzisha na kuendesha miradi ya

kuongeza kipato/biashara. Ufahamu wa kujua nini maana ya biashara, kujua kutathmini wazo la mradi,

kutengeneza mchanganuo wa mradi na habari zote za masoko.

(ii)

Ni mwenye stadi

Mjasiriamali lazima awe na ujuzi wa mradi anaoamua kuanzisha.

(iii)

Ni mwenye tabia za kiujasiriamali

Ujasiriamali si tu kufanya biashara bali ni ile tabia unayoweza kuionyesha kwenye biashara yako.

Mjasiriamali ana tabia zifuatazo:-

(a)

Ni mbunifu (Innovative)

Mjasiriamali ni mbunifu katika biashara kwa kuweka kitu kipya, mambo mapya, taratibu mpya,

mipango mipya, kuweka huduma tofauti na wenzake wenye biashara ileile.

(b)

Ni mwenye kuthubutu (Risk-taking)

Kuthubutu kwa mjasiriamali kuna kuja kwa njia nyingi kama vile:

‣ Kufanya uamuzi wa kuwekeza.

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!