SACCOS_Traing_Guide

SACCOS_Traing_Guide SACCOS_Traing_Guide

24.10.2015 Views

66 Mwongozo wa Mafunzo ya SACCOS 11. RIBA ZA AKIBA NA AMANA 11.1 Riba za akiba Riba za akiba inalipwa kwa wanachama na wateja wanaoweka fedha zao ili kuwavutia kwa sababu SACCOS hutumia fedha hizo katika biashara yake ya mikopo. 11.2 Kukokotoa Riba Za Akiba. Riba za akiba hukokotolewa ili:- (i) Kutambua kiasi cha riba kitakacholipwa na SACCOS kwa wenye akiba. (ii) Riba inayolipwa na SACCOS kwa wenye akiba ni mapato kwao, ambapo kwa SACCOS ni gharama ya fedha. 11.3 Kanuni ya kukokotoa riba ya akiba. Riba = Kiasi cha akiba × (kiwango cha Riba ÷ 100) × Muda. ‣ Kiasi cha Akiba:- Ni fedha aliyojiwekea mwanachama au mteja kwenye SACCOS. ‣ Kiwango cha Riba:- Huainishwa katika asilimia kwa mwaka au kwa mwezi. ‣ Muda:- Huainishwa katika siku,mwezi au mwaka ambapo fedha za akiba zimekua chini ya mamlaka yaSACCOS. Wakati wa Kukokotoa Riba lazima kuzingatia kwamba, kama muda umeainishwa kwa siku basi kiwango cha Riba nacho kiainishwe kwa siku. Mfano: Riba ya asilimia 60 kwa mwaka wenye siku 365, Basi kiwango cha Riba kwa siku = 60% ÷ Siku 365 = 0.164% 11.4 Kukokotoa gharama za riba kwenye akiba. Mabenki hukokotoa Riba kwenye akiba kila siku kwa kuzingatia salio la akaunti linalostahili kupata Riba. Mfano, Kama kiasi cha chini kinachostahili kupata riba ni shilingi 20,000/=, mteja mwenye akaunti yenye salio la shilingi 18,000/= hastahili kupata riba hata kama fedha hizo zitakaa benki kwa mwaka mzima. Ni vyema SACCOS zifuate utaratibu huu wakati zinapoamua kulipa riba kwenye akaunti za Akiba. MAJADILIANO. SACCOS ya Tusaidiane imeamua kulipa Riba ya asilimia tatu (3%) kwa mwaka kwa wanachama na wateja wote wenye akiba isiyopungua shilingi 20,000/=, Devota ambaye ni mwanachama alikua na akiba ya shilingi 150,000/= ambazo zimekaa kwa siku 90, baada ya hapo Devota aliongeza akiba na kufikisha shilingi 250,000/= ambazo zimekaa kwenye SACCOS kwa muda wa siku 30. Tafuta jumla ya riba atakayolipwa Devota.

Mwongozo wa Mafunzo ya SACCOS 67 Kanuni: Mwaka una siku 365 Riba = kiasi cha riba × (kiwango cha riba÷100) × Muda. (a) Salio la shilingi 150,000 ‣ Kiasi cha akiba(siku 90) = shs 150,000/= ‣ Kiwango cha Riba kwa siku = 3% ÷ 365 = 0.00822% ‣ Muda wa akiba kwenye SACCOS ni siku 90. (b) Salio la shilingi 250,000/= ‣ Kiasi cha Akiba (siku 30) = shs 250,000/= ‣ Kiwango cha riba kwa siku = 3% ÷ 365 = 0.00822% ‣ Muda wa akiba kwenye SACCOS ni siku 30, Kokotoa riba kwa kuzingatia salio lililopo kwenye akaunti kila siku. Kipindi Salio kwenye akaunti Kanuni Kiasi cha akiba × (3% ÷ 365) × idadi ya siku Kiasi cha riba Siku 90 150,000/= 150,000 × 0.0000822 × 90 1,109.70 Siku 30 250,000/= 250,000 × 0.0000822 × 30 616.50 JUMLA 1,726.20

Mwongozo wa Mafunzo ya SACCOS

67

Kanuni:

Mwaka una siku 365

Riba = kiasi cha riba × (kiwango cha riba÷100) × Muda.

(a) Salio la shilingi 150,000

‣ Kiasi cha akiba(siku 90) = shs 150,000/=

‣ Kiwango cha Riba kwa siku = 3% ÷ 365 = 0.00822%

‣ Muda wa akiba kwenye SACCOS ni siku 90.

(b) Salio la shilingi 250,000/=

‣ Kiasi cha Akiba (siku 30) = shs 250,000/=

‣ Kiwango cha riba kwa siku = 3% ÷ 365 = 0.00822%

‣ Muda wa akiba kwenye SACCOS ni siku 30,

Kokotoa riba kwa kuzingatia salio lililopo kwenye akaunti kila siku.

Kipindi Salio kwenye akaunti

Kanuni

Kiasi cha akiba × (3% ÷ 365) × idadi ya siku

Kiasi cha riba

Siku 90 150,000/= 150,000 × 0.0000822 × 90 1,109.70

Siku 30 250,000/= 250,000 × 0.0000822 × 30 616.50

JUMLA 1,726.20

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!