SACCOS_Traing_Guide

SACCOS_Traing_Guide SACCOS_Traing_Guide

24.10.2015 Views

46 Mwongozo wa Mafunzo ya SACCOS wa udhibiti wa hesabu za ushirika maana utaelezea kwa ufasaha mali zilizopo katika himaya ya ushirika, zimetokana na nini na zimefika vipi, katika chama na wenyewe ni akina nani na zinaangaliwa vipi. 8.4.3 USHIRIKIANO WA MPE NA MTOE (Kanuni za MPE na MTOE) Katika masuala ya miamala ya kifedha ni lazima pawepo matukio mawili:- ‣ Tukio la kutoa na lile la kupokea. ‣ Ni lazima awepo anayetoa na anayepokea. ‣ Ni lazima iwepo akaunti inayotoa na inayopokea. Matukio haya mawili ni pacha, moja likitokea na lingine linatendeka muda huohuo na kuwa hitimisho la tukio lililotangulia. Kutendeka kwa tukio la pili ni kuthibitisha kuwa tukio la kwanza limefika salama mahali panapostahili. MPE (+) VS MTOE (-) MPE- anayepokea VS MTOE- anayetoa MPE-Kinachoingia VS MTOE-kinachotoka MPE-Viingiavyo VS Mtoe-vitokavyo Ili kuhitimisha matendo ya mpe na mtoe ni lazima kila chama cha ushirika kiwe na akaunti za kuingiza miamala hii, akaunti hizi zitatunzwa ndani ya kitabu kinachoitwa Leja kuu. Kila akaunti ndani ya kitabu cha leja kuu ni lazima iwe na pande mbili yaani upande wa MPE na upande wa MTOE ili kuonyesha ni thamani gani imeingizwa au kutolewa kwenye akaunti hiyo. 8.5 KUANDAA TAARIFA SAHIHI NA KWA WAKATI UNAOSTAHILI Bodi inatakiwa kuhakikisha kwamba taarifa zote za mahesabu ya SACCOS ziko sahihi wakati wote. Taarifa sahihi zinaweza kupatikana endapo kama bodi:- a) Itaanzisha mfumo mzuri wa utawala na uhasibu. b) Kuajiri wafanyakazi wenye ujuzi na uzoefu katika uhasibu. c) Kuajiri meneja ambaye ataendesha na kusimamia shughuli za kila siku. d) Kuweka mazingira mazuri ya kufanya kazi kama vile kuwa na ofisi, ulinzi n.k. e) Kuwapatia wafanyakazi wake vitendea kazi bora kama vile vikokotozi, samani, kasiki, ofisi nzuri na imara.

Mwongozo wa Mafunzo ya SACCOS 47 8.6 KUANDAA TAARIFA ZA KILA MWEZI Taarifa za kila mwezi zinatokana na taarifa sahihi za kila siku ambazo nazo hutokana na kukamilika kwa kazi za kila siku. Taarifa za kila siku ni pamoja na makusanyo ya kila siku, malipo ya kila siku na ulinganisho wa fedha taslimu kila siku n.k. Taarifa za kila mwezi ni lazima zipatikane kila mwisho wa mwezi ni lazima zipatikane kila mwisho wa mwezi ili ziweze kujadiliwa na kuona kama mipango ya SACCOS inaenda kama ilivyokusudiwa na kuangalia sehemu zinazohitaji marekebisho na ufuatiliaji. Taarifa za kila mwezi ni pamoja na:- ‣ Mapato na matumizi. ‣ Ulinganisho wa fedha taslimu. ‣ Ulinganisho wa fedha benki. ‣ Taarifa za mikopo (kiasi kilichotolewa, kilichorejeshwa, kiasi ambacho hakijarejeshwa na orodha ya wadaiwa na kiasi wanachodaiwa). Taarifa hizi ni muhimu sana na bodi inatakiwa kuwa nazo na zinapokosekana ni wajibu wa bodi kupata sababu za kukosekana na hali hiyo lazima irekebishwe mapema ili ziweze kupatikana na kutumika. Kama ni uzembe basi aliyepewa jukumu la kutayarisha achukuliwe hatua zinazostahili na bodi. 8.7 UPATIKANAJI WA TAARIFA ZA MWAKA Uwezo wa kusimamia shughuli za SACCOS umekasimiwa na wanachama kwenye bodi, kwa hiyo ni wajibu wa bodi kuhakikisha kwamba taarifa za fedha, kisheria zinapatikana kwa wakati unaostahiki na kuwasilishwa kwenye vyombo husika kama vile wakaguzi wa hesabu ili wazikague na kuthibitisha kama ni sahihi. Taarifa hizi ni:- ‣ Taarifa ya bodi (inayohusu shughuli zilizofanyika kipindi husika). ‣ Mizania. ‣ Taarifa ya mapato na matumizi. ‣ Mtiririko wa fedha. Endapo bodi itashindwa kuandaa taarifa hizi katika kipindi cha miezi mitatu baada ya kumalizika kwa mwaka wa fedha husika, kila mjumbe wa bodi kwa kipindi hicho atavuliwa madaraka ya ujumbe na hataruhusiwa kuchaguliwa kwenye ujumbe mpaka ipite miaka sita na kama hakutakuwa na hasara iliyotokana na uongozi wao watatozwa adhabu ya kila mmoja Sh. 100,000 na kuchukuliwa hatua ya kufidia hasara waliyosababisha. 8.8 WATUMIAJI WA TAARIFA ZA SACCOS Mwisho wa mzunguko wa uhasibu ni kuandaa taarifa mbalimbali kwa walengwa kwa wakati mwafaka ili waweze kufanya uamuzi sahihi wanapotakiwa.

Mwongozo wa Mafunzo ya SACCOS

47

8.6 KUANDAA TAARIFA ZA KILA MWEZI

Taarifa za kila mwezi zinatokana na taarifa sahihi za kila siku ambazo nazo hutokana na kukamilika

kwa kazi za kila siku. Taarifa za kila siku ni pamoja na makusanyo ya kila siku, malipo ya kila siku na

ulinganisho wa fedha taslimu kila siku n.k.

Taarifa za kila mwezi ni lazima zipatikane kila mwisho wa mwezi ni lazima zipatikane kila mwisho wa

mwezi ili ziweze kujadiliwa na kuona kama mipango ya SACCOS inaenda kama ilivyokusudiwa na

kuangalia sehemu zinazohitaji marekebisho na ufuatiliaji. Taarifa za kila mwezi ni pamoja na:-

‣ Mapato na matumizi.

‣ Ulinganisho wa fedha taslimu.

‣ Ulinganisho wa fedha benki.

‣ Taarifa za mikopo (kiasi kilichotolewa, kilichorejeshwa, kiasi ambacho hakijarejeshwa na

orodha ya wadaiwa na kiasi wanachodaiwa). Taarifa hizi ni muhimu sana na bodi inatakiwa

kuwa nazo na zinapokosekana ni wajibu wa bodi kupata sababu za kukosekana na hali

hiyo lazima irekebishwe mapema ili ziweze kupatikana na kutumika. Kama ni uzembe basi

aliyepewa jukumu la kutayarisha achukuliwe hatua zinazostahili na bodi.

8.7 UPATIKANAJI WA TAARIFA ZA MWAKA

Uwezo wa kusimamia shughuli za SACCOS umekasimiwa na wanachama kwenye bodi, kwa hiyo ni

wajibu wa bodi kuhakikisha kwamba taarifa za fedha, kisheria zinapatikana kwa wakati unaostahiki

na kuwasilishwa kwenye vyombo husika kama vile wakaguzi wa hesabu ili wazikague na kuthibitisha

kama ni sahihi. Taarifa hizi ni:-

‣ Taarifa ya bodi (inayohusu shughuli zilizofanyika kipindi husika).

‣ Mizania.

‣ Taarifa ya mapato na matumizi.

‣ Mtiririko wa fedha.

Endapo bodi itashindwa kuandaa taarifa hizi katika kipindi cha miezi mitatu baada ya kumalizika kwa

mwaka wa fedha husika, kila mjumbe wa bodi kwa kipindi hicho atavuliwa madaraka ya ujumbe na

hataruhusiwa kuchaguliwa kwenye ujumbe mpaka ipite miaka sita na kama hakutakuwa na hasara

iliyotokana na uongozi wao watatozwa adhabu ya kila mmoja Sh. 100,000 na kuchukuliwa hatua ya

kufidia hasara waliyosababisha.

8.8 WATUMIAJI WA TAARIFA ZA SACCOS

Mwisho wa mzunguko wa uhasibu ni kuandaa taarifa mbalimbali kwa walengwa kwa wakati mwafaka

ili waweze kufanya uamuzi sahihi wanapotakiwa.

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!