SACCOS_Traing_Guide

SACCOS_Traing_Guide SACCOS_Traing_Guide

24.10.2015 Views

12 Mwongozo wa Mafunzo ya SACCOS huduma za SACCOS yao na wako mstari wa mbele kuwaeleza wengine juu ya ubaya wa SACCOS hiyo. Hawa watakuwezesha kutambua uwezekano wa kunusuru baadhi ya wanachama na kuwaongezea utoshelevu wa huduma za SACCOS. Katika juhudi za kubakiza wanachama, Imarisha thamani ya uanachama kwa kufanya yafuatayo:- i. Kuzungumzia manufaa ya kuwa ndani ya SACCOS kila fursa zinapojitokeza. ii. Wahamasishe wanachama walionufaika na huduma za SACCOS kueleza mbele ya wenzao kila fursa zinapojitokeza. iii. Wahudumie wanachama haraka ili waokoe muda. iv. Wawezeshe wanachama kuokoa gharama. v. Wasaidie wanachama kufanya uamuzi wenye tija. vi. SACCOS iviwezeshe vikundi vilivyo wanachama wa SACCOS vitoe huduma bora kwa wanavikundi wake. vii. Wasaidie wanachama kutumia fursa ili kujipatia mafanikio katika biashara zao. viii. Zingatia utoaji wa huduma bora. ix. Hakikisha unachangia mahitaji ya wanachama wako mara kwa mara ukitumia njia mbalimbali kama vile uchunguzi wa kutumia maswali ili kupata majibu kwa sampuli ya watu wachache, majadiliano katika makundi na mazungumuzo ya ana kwa ana kubaini nini hasa wanachama wanatarajia kutokana na uanachama wao katika SACCOS. Kila utakapopata majibu basi jitahidi kuwa na huduma zile wanazotaka. x. Viongozi wabadilike katika mawazo yao, kufikiria kuwa mtu akisha kuwa mwanachama atabakia kuwa mwanachama wa kutumainiwa na hakuna juhudi inayotakiwa kumbakiza .Juhudi zinatakiwa kuwabakiza wanachama waliopo hasa ukizingatia kwamba gharama ya kumpata mwanachama mpya ni kubwa zaidi ya mara nne ya kumbakiza yule aliyetayari mwanachama. B. Juhudi za kuongeza wanachama wa SACCOS Ili kuhakikisha SACCOS inapata biashara ya kutosha kulingana na hali ya uchumi katika eneo lake, SACCOS ina jukumu la kutoa huduma kwa watu wengi iwezekanavyo. Kwa hiyo, kuongeza wanachama linatakiwa kuwa lengo kubwa la SACCOS. Hata hivyo unapoongeza wanachama, inabidi kuhakikisha kuwa unawabakiza waliotayari wanachama. Uongozi wa SACCOS unatakiwa kutumia njia mbalimbali kuongeza wanachama wapya kama ifuatavyo:- (i) (ii) (iii) (iv) Unda kamati ya kutayarisha mikakati ya kuongeza wanachama. Washirikishe wanachama wale hodari ili watoe majina ya watu wanaotarajia kujiunga na SACCOS iwapo wataendewa. Waombe wanachama hao wajihusishe na kuwashawishi watu hao kuwa wanachama. Panga kufanya tamasha ambalo litatoa maelezo ya mafanikio ya SACCOS, zawadi kwa waliofanya vizuri sana kikazi au kuweka Akiba au kurudisha mikopo. Katika tamasha la namna hiyo wasio wanachama watavutwa kuwa wanachama. Wajumbe wa bodi watembelee shule na kueleza faida na fursa za kuwa mwanachama wa SACCOS. Hakika vijana wengi wanaomaliza shule watajiunga na SACCOS.

Mwongozo wa Mafunzo ya SACCOS 13 (v) (vi) (vii) (viii) (ix) (x) (xi) Wajumbe wa bodi wazungumze na watu baada ya ibada makanisani na misikitini ili waumini wapate habari za SACCOS moja kwa moja. Tengeneza vipeperushi na weka mabango yanayoelezea shughuli za SACCOS sehemu zote za mbao za matangazo. Wajumbe wa bodi wajipange kwa kutumia simu wawasiliane na wanachama watarajiwa ambao watakuwa katika orodha iliyoandaliwa na kamati ya kuongeza wanachama. Wajumbe wanatakiwa kuwa wamejiandaa vema kwa maswali kutoka kwa wanachama watarajiwa, kama vile faida ya uanachama wa SACCOS, upatikanaji wa mikopo, riba, gawio n.k. matumizi ya simu ya moja kwa moja kwa mwanachama mtarajiwa yanamguso wa pekee tofauti na matumizi ya barua au mkutano wa watu wengi. Wajumbe wa bodi wasaidiane na wanachama wa kawaida watembelee mlango kwa mlango wakiwashawishi watu kujiunga na SACCOS. SACCOS inaweza kuwazawadia wanachama watakaoingiza wanachama wengi zaidi. SACCOS iweke kumbukumbu ya majibu yaliyotolewa na kila mtu aliyeendewa kumshawishi awe mwanachama wake. Kumbukumbu hizo zitunzwe kwa marejeo ya baadaye kwa wale wanaokataa au kushindwa kujiunga na SACCOS kwa wakati huo. Tengeneza na tunza orodha ya watu wanaotarajiwa kujiunga na SACCOS na ipitie mara kwa mara orodha hiyo.

Mwongozo wa Mafunzo ya SACCOS

13

(v)

(vi)

(vii)

(viii)

(ix)

(x)

(xi)

Wajumbe wa bodi wazungumze na watu baada ya ibada makanisani na misikitini ili waumini

wapate habari za SACCOS moja kwa moja.

Tengeneza vipeperushi na weka mabango yanayoelezea shughuli za SACCOS sehemu zote za

mbao za matangazo.

Wajumbe wa bodi wajipange kwa kutumia simu wawasiliane na wanachama watarajiwa

ambao watakuwa katika orodha iliyoandaliwa na kamati ya kuongeza wanachama. Wajumbe

wanatakiwa kuwa wamejiandaa vema kwa maswali kutoka kwa wanachama watarajiwa, kama

vile faida ya uanachama wa SACCOS, upatikanaji wa mikopo, riba, gawio n.k. matumizi ya simu

ya moja kwa moja kwa mwanachama mtarajiwa yanamguso wa pekee tofauti na matumizi ya

barua au mkutano wa watu wengi.

Wajumbe wa bodi wasaidiane na wanachama wa kawaida watembelee mlango kwa mlango

wakiwashawishi watu kujiunga na SACCOS.

SACCOS inaweza kuwazawadia wanachama watakaoingiza wanachama wengi zaidi.

SACCOS iweke kumbukumbu ya majibu yaliyotolewa na kila mtu aliyeendewa kumshawishi

awe mwanachama wake. Kumbukumbu hizo zitunzwe kwa marejeo ya baadaye kwa wale

wanaokataa au kushindwa kujiunga na SACCOS kwa wakati huo.

Tengeneza na tunza orodha ya watu wanaotarajiwa kujiunga na SACCOS na ipitie mara kwa

mara orodha hiyo.

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!