SACCOS_Traing_Guide

SACCOS_Traing_Guide SACCOS_Traing_Guide

24.10.2015 Views

10 Mwongozo wa Mafunzo ya SACCOS Aidha, wanapenda kuona kuna taratibu rahisi za kuweka na kuchukua Akiba na Amana pia kuona Ofisi ya SACCOS inayokuwa wazi saa zote za kazi. (iv) Wanachama kuwapatia faida. Wawekaji Akiba hutarajia kupata faida ya Akiba au Amana walizoweka. Pia, wanachama hutarajia kupata gawio kutokana na hisa zao. 2.3 Kukuza mtaji kwa kuwekeza upya Faida Ukwasishaji(Upatikana wa fedha) wa aina hii ni pale wanachama wa SACCOS wanapoamua kutogawana faida ya mwaka iliyopatikana na badala yake kuelekeza fedha hiyo kutumika kwenye shughuli za SACCOS ili kuiongezea uwezo wa kifedha. 2.4 Kukuza mtaji kwa kukopa nje SACCOS inaweza kukuza mtaji kwa kukopa kutoka kwenye asasi nyingine za fedha (Ukwasishaji [Upatikana wa fedha]wa nje). Ili SACCOS iweze kukopa nje ni lazima Ajenda ya kuomba ukomo wa madeni iwasilishwe kwenye mkutano mkuu kwa ajili ya kujadiliwa na kupitishwa. Ajenda hii itaelezea madhumuni ya mkopo na asasi inayotarajiwa kutoa mkopo huo. Mkutano ukiridhia Ajenda hiyo, maombi ya ukomo wa madeni yatawasilishwa kwa Mrajisi kwa ajili ya kujadiliwa na kuidhinishwa baada ya kukidhi vigezo vinavyotakiwa. ‣ Ni busara kufanya mlinganisho wa mikopo inayotolewa na Asasi za fedha zisizopungua nne kabla ya kufanya uamuzi wa kuchukua mkopo, ili kupata na kufahamu masharti ya mikopo wanayoitoana na kuifanyia uchambuzi wa kina. ‣ Fanya utafiti wa machapisho ya mkopeshaji mbali ya riba ya mikopo, tathmini vigezo vya kupata mkopo kama vile masharti ya mkopo unaotaka kuomba. 2.5 Hali halisi ikoje katika SACCOS (a) Wanachama wengi wamekuwa hawakamilishi kulipia Hisa zao kwa wakati. (b) Wanachama wamekuwa wagumu kununua Hisa za Ziada. (c) Thamani ya hisa moja inaendelea kuwa ndogo. (d) Wanachama wamekuwa wagumu kuweka Akiba kwenye SACCOS na hivyo kuzifanya SACCOS kutegemea zaidi mikopo ya benki kwa ajili ya kupata fedha za kuwakopesha wanachama wao. (e) Kuna hatari ya SACCOS kugeuka kuwa wakala wa benki. (f ) SACCOS zimekosa mvuto na ushawishi kwa wanachama wake kwa jamii. Hakuna faida ya akiba au amana, Akiba zinatumika tu kama kigezo cha wanachama kukopea, hakuna gawio la hisa. (g) Baadhi ya wanachama wamekuwa hawazingatii sera na Utaratibu za uwekaji Akiba hivyo kutoa fedha za akiba bila kufuata utaratibu uliowekwa na hivyo kuathiri mfuko wa kukopshana wa SACCOS.

Mwongozo wa Mafunzo ya SACCOS 11 2. 6 Manufaa ya ukuzaji mtaji [i] [ii] [iii] [iv] Huwezesha upatikanaji wa mtaji na kusababisha kukua kwa SACCOS. Huzijengea SACCOS mazingira mazuri ya kutoa huduma zake kwa wanachama na hivyo kuhimili ushindani kutoka Asasi nyingine za fedha. Huwawezesha wawekaji kupata kipato cha kudumu kwa njia ya gawio la faida. Huwezesha wawekezaji kujenga utajiri. 2.7 Athari za kutokukuza mtaji wa SACCOS [i] [ii] [iii] Kudumaa kwa huduma za SACCOS pamoja na ukuaji wa SACCOS yenyewe. SACCOS kushindwa kuhimili ushindani wa soko na hivyo kuwa na uwezekano wa kutowavutia wanachama wapya na kupoteza wanachama waliopo. Wanachama kupata gawio dogo au kutopata kabisa. 2.8 UBAKIZAJI NA UONGEZAJI WA WANACHAMA KATIKA SACCOS SACCOS inapokuwa na juhudi za kuwabakiza wanachama wasiondoke na juhudi za kuongeza wanachama wapya husababisha mtaji katika SACCOS kuongezeka pia. A. Juhudi za kubakiza wanachama wasiondoke Wanachama huacha uanachama kwa sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na:- ‣ Huduma zisizoridhisha. ‣ Uhusiano mbaya kati ya viongozi na wanachama. ‣ Kukosa mikopo. Ukosefu wa aina za huduma wanazotaka Juhudi za kubakiza wanachama huanza na utafiti wa kufahamu hali ya kuridhika kwa wanachama waliopo. ‣ Kuwa na sanduku la maoni katika sehemu zinazofikiwa kwa wingi na wanachama. ‣ Zungusha fomu yenye maswali yanayolenga kujua ni kwa kiasi gani wanachama wa sasa wanatosheka au hawatosheki na huduma za sasa. Katika kufanya utafiti huu ni lazima kutumia sampuli ndogo lakini inayowakilisha makundi muhimu yafuatayo ya wanachama wa SACCOS:- i. Wanachama walio mstari wa mbele katika shughuli za chama, ni waaminifu kwa chama na wako tayari kushawishi wengine kujiunga na chama. Hii itakuwezesha kubaini ni mikakati gani inatakiwa kuendeleza utoshelevu wa kundi hili. ii. Wanachama baridi(wanachama vigeugeu) ambao wanatosheka na huduma za SACCOS lakini uaminifu wao niwa shaka, hawaizungumzii SACCOS mazuri mbele ya wasio wanachama na mara nyingi hutafuta huduma katika vyombo vingine vya fedha. Hii itakuwezesha kubaini ni mikakati gani inatakiwa kuendeleza utoshelevu wa kundi hili. iii. Wakashifishaji(wanachama wanaokashifu SACCOS) ni wanachama ambao hawafurahii

10 Mwongozo wa Mafunzo ya SACCOS

Aidha, wanapenda kuona kuna taratibu rahisi za kuweka na kuchukua Akiba na Amana pia kuona Ofisi

ya SACCOS inayokuwa wazi saa zote za kazi.

(iv)

Wanachama kuwapatia faida.

Wawekaji Akiba hutarajia kupata faida ya Akiba au Amana walizoweka. Pia, wanachama hutarajia

kupata gawio kutokana na hisa zao.

2.3 Kukuza mtaji kwa kuwekeza upya Faida

Ukwasishaji(Upatikana wa fedha) wa aina hii ni pale wanachama wa SACCOS wanapoamua kutogawana

faida ya mwaka iliyopatikana na badala yake kuelekeza fedha hiyo kutumika kwenye shughuli za

SACCOS ili kuiongezea uwezo wa kifedha.

2.4 Kukuza mtaji kwa kukopa nje

SACCOS inaweza kukuza mtaji kwa kukopa kutoka kwenye asasi nyingine za fedha (Ukwasishaji

[Upatikana wa fedha]wa nje).

Ili SACCOS iweze kukopa nje ni lazima Ajenda ya kuomba ukomo wa madeni iwasilishwe kwenye

mkutano mkuu kwa ajili ya kujadiliwa na kupitishwa.

Ajenda hii itaelezea madhumuni ya mkopo na asasi inayotarajiwa kutoa mkopo huo. Mkutano

ukiridhia Ajenda hiyo, maombi ya ukomo wa madeni yatawasilishwa kwa Mrajisi kwa ajili ya kujadiliwa

na kuidhinishwa baada ya kukidhi vigezo vinavyotakiwa.

‣ Ni busara kufanya mlinganisho wa mikopo inayotolewa na Asasi za fedha zisizopungua nne

kabla ya kufanya uamuzi wa kuchukua mkopo, ili kupata na kufahamu masharti ya mikopo

wanayoitoana na kuifanyia uchambuzi wa kina.

‣ Fanya utafiti wa machapisho ya mkopeshaji mbali ya riba ya mikopo, tathmini vigezo vya

kupata mkopo kama vile masharti ya mkopo unaotaka kuomba.

2.5 Hali halisi ikoje katika SACCOS

(a) Wanachama wengi wamekuwa hawakamilishi kulipia Hisa zao kwa wakati.

(b) Wanachama wamekuwa wagumu kununua Hisa za Ziada.

(c) Thamani ya hisa moja inaendelea kuwa ndogo.

(d) Wanachama wamekuwa wagumu kuweka Akiba kwenye SACCOS na hivyo kuzifanya SACCOS

kutegemea zaidi mikopo ya benki kwa ajili ya kupata fedha za kuwakopesha wanachama wao.

(e) Kuna hatari ya SACCOS kugeuka kuwa wakala wa benki.

(f ) SACCOS zimekosa mvuto na ushawishi kwa wanachama wake kwa jamii. Hakuna faida ya akiba

au amana, Akiba zinatumika tu kama kigezo cha wanachama kukopea, hakuna gawio la hisa.

(g) Baadhi ya wanachama wamekuwa hawazingatii sera na Utaratibu za uwekaji Akiba hivyo

kutoa fedha za akiba bila kufuata utaratibu uliowekwa na hivyo kuathiri mfuko wa kukopshana

wa SACCOS.

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!