13.09.2015 Views

Je Watoto Wetu Wanajifunza?

Isome hapa. - Twaweza.org

Isome hapa. - Twaweza.org

SHOW MORE
SHOW LESS

You also want an ePaper? Increase the reach of your titles

YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.

Je, Watoto Wetu Wanajifunza?

Kuhesabu na Kusoma katika Afrika Mashariki

Juni 2011

Je, Watoto Wetu Wanajifunza?

Kuhesabu na Kusoma katika Afrika Mashariki

Uwezo ni juhudi katika Afrika Mashariki inayofanya kazi yake kupitia TEN/MET

nchini Tanzania; WERK nchini Kenya na UNNGOF nchini Uganda, na hupata msaada

wa kudhibiti ubora na usimamizi kutoka Twaweza/Hivos. Ripoti hii imeandaliwa

na kitengo cha Uwazi kilichopo Twaweza. Waandishi wakuu ni Hans Hoogeveen na

Dorica Andrew. Shukrani nyingi kwa Fenohasina Mareth kwa msaada wake katika

kutayarisha seti za data na kutengeneza seti ya kwanza ya majedwali na michoro.

Sara Ruto na Rakesh Rajani walitoa ushauri wa jumla na kusimamia ubora. Uhariri

ulifanywa na Stephanie McDonald na Maggie Bangser.

Data zote zilizotumiwa katika ripoti hii zimetolewa na Uwezo na zinapatikana kutoka

www.uwezo.net.

Picha kwenye ukurasa wa nje: Hisani ya Uwezo

Uwezo Uwezo Afrika East Africa Mashariki (managed (ikisimamiwa by Twaweza) na Twaweza)

S.L.P. P.O Box 19875, 19875, 00200 00200 Nairobi, Nairobi, Kenya Kenya

Simu: Tel: +254 20 3861372

Baruapepe: Email: info@uwezo.net. Web: Tovuti: www.uwezo.net

Twaweza Afrika East Africa Mashariki

127 Mtaa Mafinga wa Mafinga, Rd, Off Kando Kinondoni ya barabara Rd ya Kinondoni

S.L.P. P.O Box 38342, 38342, Dar es Dar Salaam, es Salaam, Tanzania. Tanzania

Simu: Tel: +255 22 266 4301. Nukushi: Fax +255 +255 22 266 22 266 43084308.

Barua Email: pepe: info@twaweza.org. Web: Tovuti: www.twaweza.org

Barua Email: pepe: info@uwazi.org. Web: Tovuti: www.uwazi.org

Je Watoto Wetu Wanajifunza?

ii

Dibaji

Kazi hii inatupatia matokeo yaliyotafitiwa vema kuhusu mafanikio ya mfumo wa elimu hususan katika kusoma na kuhesabu.

Uwezo na Twaweza zimeonesha umadhubuti mkubwa na viwango vya juu vya ubora katika kukusanya, kuchambua na

kufasiri takwimu za msingi katika elimu na uwezo wa jumla wa watoto katika kusoma na kuhesabu. Matokeo ya msingi

yanaonesha ukubwa wa changamoto iliyo mbele yetu sote, na hasa kama ukanda wa Afrika Mashariki unahitaji kuongeza

kasi ya maendeleo kuendana na ulimwengu wa sasa ambao umejengwa katika maarifa na ushindani mkali.

Katika ngazi ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (EAC), ushirikiano katika maendeleo ya rasilimali watu, sayansi na teknolojia

ni moja ya mihimili muhimu katika kufikia malengo ya Jumuiya. Kifungu cha 102 cha Mkataba wa Kuanzishwa kwa

Jumuiya ya Afrika Mashariki kinaeleza bayana jinsi Nchi Wanachama walivyokubali kuchukua hatua madhubuti za pamoja

kuendeleza ushirikiano katika elimu na mafunzo ndani ya Jumuiya. Ili kuchukua hatua hizo katika ngazi za kanda na nchi,

taarifa nyingi zinahitajika ili kuandaa na kutekeleza sera na mikakati inayofaa.

Kwa hiyo, umuhimu wa taarifa zilizokusanywa katika taftishi hii kuhusiana na kusoma na kuhesabu katika nchi tatu za

Afrika Mashariki utasaidia sana Nchi Wanachama katika juhudi zao za kuwa na mfumo wa elimu ulioandaliwa vema na

kurandanishwa; hasa katika kurandanisha mitaala, mitihani, utoaji vyeti na uthibitishaji wa kitaaluma wa taasisi za elimu

na mafunzo. Miongoni mwa vipengele muhimu katika ripoti hii ni jinsi inavyoshughulikia suala la jinsia, ukuzaji mitaala,

kuhusika kwa sekta binafsi na viwango vya uhamasishaji kuelekea ngazi inayofuata. Maeneo yote haya ni muhimu kwa

Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambazo zimejikita katika kutekeleza sera muhimu za elimu na mafunzo

ya msingi, zaidi sana sera ya elimu kwa wote ambayo inahitaji taarifa za kina kuwasaidia watoa maamuzi kufanya uamuzi

makini wakijua bayana nini wanachokifanya.

Ripoti hii inachambua zaidi uhusiano kati ya kipato cha kaya na vigezo vya elimu kama vile mafanikio, uwezekano wa

kuacha masomo, uandikishaji kwa kutazama jinsia, umri n.k. Kwa miongo mingi tumetumia viwango vya uandikishaji

watoto shuleni kama vigezo muhimu vya maendeleo ya elimu. Ripoti ya Uwezo inaonesha kwamba uandikishaji pekee

hautoshi kwa sababu watoto walio shuleni bado hawawezi kusoma na kuhesabu, ambazo ni stadi za msingi katika kujifunza

na kuendelea (kukua kimaarifa). Hata hivyo, matokeo ya ripoti hii yatakuwa muhimu katika mchakato unaoendelea

wa kurandanisha sera za elimu na mafunzo katika Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kwa mfano, baada ya kudhibitishwa na

kupimwa ufaaji wake, taarifa zilizokusanywa katika taftishi zinaweza kutumiwa katika kufanya mapitio ya sheria na kufanya

marekebisho yanayostahili katika ngazi ya kanda na kitaifa.

Ni matarajio yangu kwamba kazi hii inayostahili pongezi itatumiwa kwa mapana na marefu na pande zinazohusika na

kwamba Uwezo na Twaweza kama taasisi zitaendelea kujibainisha kama wanaharakati muhimu katika eneo hili. Jambo

hili pia linahusisha changamoto ya kuhakikisha ubora wa matokeo. Wakati kuongeza idadi ya watoto walio mashuleni ni

muhimu, kipengele cha muhimu zaidi cha kupima mafanikio ni kuthibitisha kama watoto wanaokwenda shule kwa hakika

wanajifunza au la. Hili ni eneo lingine ambalo linastahili kuchunguzwa na Uwezo na Twaweza. Vilevile, ni matumaini yangu

kwamba utafiti kama huu utakaofuata utahusisha Nchi Wanachama tano za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Dkt Richard Sezibera

Katibu Mkuu

Jumuiya ya Afrika Mashariki

Juni 2011

Kuhesabu na Kusoma Katika Afika Mashariki

iii

1. Utangulizi

Ni wachache wanaohoji umuhimu wa kujifunza, kama haki ya msingi na umuhimu wake katika kuandaa vizazi vijavyo

kwa kuwajengea uwezo wa kuishi maisha yenye ustawi. Serikali za Tanzania, Uganda na Kenya zinaunga mkono

mtazamo huu. Nchi zote tatu zinatekeleza sera ya Elimu ya Msingi bure kwa matarajio kwamba itawezesha watoto

kupata elimu, ili walau wawe raia wenye uwezo wa kuhesabu na kusoma. Ili kufanikisha lengo hili kiasi kikubwa cha

fedha kimewekezwa na kinaendelea kuwekezwa katika elimu ya msingi. Mathalan, katika mwaka 2009/10, Serikali

ya Tanzania ilitenga asilimia 14 ya bajeti yake (sawa na asilimia 4 ya Pato la Taifa) kwa ajili ya elimu ya msingi pekee 1 .

Kenya na Uganda nazo zinatumia kiasi kikubwa cha fedha, na katika muongo uliopita takwimu zinaonesha kwamba

bajeti ya elimu imeongezeka kwa kiwango kikubwa katika nchi hizi.

Katika nchi hizi kufutwa kwa ada ya elimu ya msingi kulifuatiwa na ongezeko kubwa la idadi ya watoto wanaokwenda

shule. Ukweli huu unaoneshwa na wiano za idadi ya uandikishaji watoto katika shule kama inavyoonekana katika

Kielelezo cha 1 (uwiano wa jumla wa uandikishaji ni jumla ya idadi ya watoto wanaosoma katika shule za msingi

ikilinganishwa na watoto wenye umri wa kwenda shule). Nchini Uganda, ambako elimu ya msingi bure ilianza

kutolewa kwa mara ya kwanza mwaka 1997, idadi ya jumla ya watoto walioandikishwa ilipanda kutoka pungufu

kidogo ya asilimia 70 mwaka 1997 hadi kufikia zaidi ya asilimia 120 mwaka 2000. Nchini Tanzania, baada ya ada

za shule kufutwa mwaka 2001, uandikishaji uliongezeka kutoka karibu asilimia 70 hadi karibu asilimia 110. Nchini

Kenya, ongezeko halikuwa kubwa sana hasa kwa sababu tayari uandikishaji ulikuwa juu, lakini hata katika nchi hii,

kuanzishwa upya kwa elimu ya msingi bure katika mwaka 2003 kulifanikisha uandikishaji kuongezeka hadi kufikia

karibu asilimia 105.

Kielelezo cha 1: jumla ya uandikishaji katika shule za msingi 1990-2008 (katika %)

Chanzo cha data: Taasisi ya Takwimu ya UNESCO 2

Mafanikio ya kuvutia yaliyopatikana katika uandikishaji watoto shuleni yalitoa fursa kwa jitihada kuelekezwa katika

kusimamia kujifunza. Je, watoto wote hawa ambao sasa wanakwenda shule kweli wanafanikiwa kujenga uwezo wa

kuhesabu na kusoma? Je, uwekezaji huu mkubwa unaofanywa na serikali hizi katika elimu ya msingi unazaa matunda

yanayotarajiwa na watunga sera na wazazi?

Ili kutathmini kiwango cha uwezo wa kusoma na kuhesabu walichonacho watoto wa umri wa kwenda shule, Uwezo

ilifanya tafiti katika nchi za Kenya, Tanzania na Uganda. Tafiti zilihusisha kuwapima maelfu ya watoto katika mazingira

ya nyumbani. Majaribio yaliyotumika yalikuwa ya ngazi ya Darasa la 2 kwa Kiingereza, Kiswahili na Kuhesabu.

Majaribio haya yalitayarishwa kwa kuzingatia mitaala ya kila nchi inayohusika. Ripoti hii inatumia data hizi ili

kutathmini ustadi wa watoto wa umri wa kwenda shule kutokana na majaribio ya Uwezo yaliyofanywa katika nchi hizi

tatu.

1 Basic Education Statistics in Tanzania 2010

2 http://stats.uis.unesco.org

Kuhesabu na Kusoma Katika Afika Mashariki 1

Jambo muhimu ambalo upimaji huu umebaini ni kwamba uwezo wa watoto katika nchi hizi tatu ulikuwa katika

kiwango cha chini sana. Wanafunzi wengi waliokuwa katika Darasa la 3, ambao wote walitarajiwa wangekuwa

wamepata stadi za kusoma na kuhesabu za ngazi ya Darasa la 2, hawakufaulu majaribio ya Uwezo. Kwa kulinganisha

nchi hizi tatu tunaona kwamba watoto nchini Kenya walifanya vizuri zaidi na wale wa Tanzania walifanya vibaya zaidi.

Vilevile uchambuzi unaonesha kwamba karibu wanafunzi wote wa Darasa la 7 nchini Kenya na Uganda walionesha

kuwa wanamudu stadi za ngazi ya Darasa la 2. Hali ni tofauti nchiniTanzania ambako ni kati ya asilimia 50 hadi 80 tu

ya wanafunzi wa Darasa la 7 ndiyo walioweza kukamilisha vizuri majaribio ya ngazi ya Darasa la 2 ya Uwezo.

Ripoti hii inazingatia pia vipengele vingine. Inalinganisha fursa za upatikanaji wa elimu ya msingi katika nchi hizi tatu,

inachambua na kulinganisha uwezo wa wanafunzi katika shule za serikali na zile za binafsi, na inazingatia tofauti za

kijinsia, upatikanaji wa nyenzo shuleni na uwezo wa kiuchumi wa kaya.

Ripoti hii imepangwa kwa sehemu. Sehemu ya 2 ya ripoti inaeleza zaidi kuhusu mbinu ya utafiti iliyotumiwa na

Uwezo, wakati na namna ulivyotekelezwa na kiwango ambacho majaribio yanalingana katika nchi hizi tatu. Sehemu

ya 3 inazungumzia upatikanaji wa elimu ya msingi; na sehemu ya 4 inajadili matokeo ya ujifunzaji. Sehemu ya 5

inaangalia upatikanaji wa vifaa/nyenzo katika shule. Sehemu ya 6 na ile ya 7 zinajadili shule binafsi na tofauti za

kijinsia. Wakati ambapo sehemu za 4 hadi 7 zinazingatia uhusiano baina ya vipengele mbalimbali (jinsia, madaraja ya

utajiri wa kaya, kiwango cha ubora wa shule) na uwezo wa wanafunzi kwa upekee, sehemu ya 8 inawasilisha matokeo

ya uchambuzi wa vipengele vilivyojadiliwa mapema katika ripoti kupitia matokeo ya ukokotozi wa kihesabu. Sehemu

hii inawasilisha uchambuzi wa athari za vipengele mbalimbali katika ujumla wake. Hitimisho linawasilishwa katika

sehemu ya 9.

2. Taftishi na majaribio ya Uwezo

Uwezo ilifanya tafiti kubwa za kaya na kupima uwezo wa kusoma na kufanya hesabu kwa watoto wenye umri wa kati

ya miaka 6-16 (5-16 nchini Tanzania) katika mazingira ya nyumbani. Tafiti za Uwezo ndizo zilizotumia sampuli kubwa

sana kuliko tafiti nyingine zozote zilizowahi kufanywa katika kanda hii. Vilevile, timu za utafiti zilikusanya data kutoka

katika shule moja katika kila kijiji.

Nchini Kenya, utafiti wa awali ulifanywa mwaka 2009. Taarifa za wilaya 70 kati ya 158 (zilizojumuishwa katika sensa)

za Kenya zilikusanywa na jumla ya watoto 68,945 wenye umri wa miaka 6-16 kutoka kaya 40,286 walipimwa. Taarifa

za shule zilikusanywa kutoka shule za msingi za serikali 2,030 343 Nchini Uganda, utafiti wa kwanza wa Uwezo ulifanyika

mwaka 2010. Utafiti ulikusanya taarifa za wilaya 27 (kati ya wilaya 80 za Uganda wakati huo). Jumla ya vijiji 810 na

kaya 16,200 zilitembelewa na watoto 34,752 wenye umri wa miaka 6-16 walipimwa.

Nchini Tanzania, utafiti ulifanyika mwaka 2010. Ulihusisha wilaya 38 kati ya 133, vjijiji 1,140 na kaya 22,800

zilitembelewa. Jumla ya watoto 42,033 wenye umri wa miaka 5-16 walipimwa.

Majaribio yaliyotumiwa naUwezo katika upimaji yalikuwa ya ngazi ya Darasa la 2 na yalizingatia mitaala ya kila nchi.

Nchini Kenya na Tanzania, watoto walipimwa katika kuhesabu na kusoma Kiswahili na Kiingereza. Nchini Uganda

watoto walipimwa katika kuhesabu na kusoma Kiingereza. Ngazi ya Darasa la 2 imechaguliwa kwa sababu kwa

mujibu wa viwango vya kimataifa baada ya ngazi hiyo ya kujifunza mwanafunzi anatarajiwa kuwa amepata stadi za

msingi katika kuhesabu na kusoma, stadi ambazo ni muhimu katika kujifunza masomo mengine yote katika miaka ya

baadaye.

3 Kwa sasa kuna wilaya zaidi nchini Kenya, lakini wakati wa utafiti, wilaya 158 zilikuwa zimeorodheshwa katika gazeti la Serikali na kushirikishwa katika sensa ya

watu ya mwaka 2009.

Je Watoto Wetu Wanajifunza? 2

Jedwali la 1: Utafiti wa Uwezo nchini Kenya, Tanzania na Uganda—muhtasari wa taarifa muhimu

Kenya Tanzania Uganda

Tarehe ya utafiti Sept/Okt 2009 Mei 2010 Aprili 2010

Idadi ya wilaya 70 (kati ya 158) 38 (kati ya 133) 27 (kati ya 80)

Idadi ya kaya 40,386 22,800 16,200

Idadi ya watoto waliopimwa 68,945 43,033 34,752

Idadi ya shule zilizotembelewa 2,030 1,140 810

Ngazi za umri 6-16 5-16 6-16

Jaribio la kuhesabu Ndiyo Ndiyo Ndiyo

Jaribio la Kiswahili Ndiyo Ndiyo Hapana

Jaribio la Kiingereza Ndiyo Ndiyo Ndiyo

Chanzo cha data: Ripoti za kitaifa za Uwezo 54

Majaribio yote yalitayarishwa kwa namna ambayo wanafunzi wangeweza kupimwa katika ngazi mbalimbali.

Mathalani, jaribio la kusoma lililenga kubaini uwezo wa kusoma herufi mojamoja, kisha maneno, sentensi na/au aya,

na mwisho hadithi iliyofuatiwa na maswali ya ufahamu. Vivyo hivyo, jaribio la hesabu lilianza na utambuzi wa namba,

kujumlisha, kutoa, kuzidisha na kugawanya. Watoto walipewa alama za ziada iwapo walifanya fumbo la hesabu

lililojumuisha shughuli na/au vitendo vya nyumbani vya kila siku, fumbo hilo lilitolewa katika lugha aliyoipendelea

mtoto.

Kwa kuwa majaribio yaliakisi mitaala ya kitaifa, hayakuweza kulinganishwa moja kwa moja. Badala yake, ulinganishaji

alama za majaribio unaonesha iwapo watoto katika kila nchi wamepata stadi za ngazi ya Darasa la 2 za mtaala wa

elimu wa taifa lao. Katika kila nchi, iwapo mfumo wa elimu ungekuwa mzuri, watoto wote (asilimia 100) walio katika

Darasa la 3 wangekuwa wamepata stadi za ngazi ya Darasa la 2.

Japo haiwezi kulinganishwa sawasawa, matarajio ya ufahamu wa wanafunzi katika Darasa la 2 si tofauti sana katika

nchi hizi tatu. Hali hii inaonekana katika Jedwali la 3 ambalo linawasilisha majaribio yaliyotumika katika upimaji

kwenye kila nchi. Jaribio la Kiswahili lingeweza kulinganishwa katika nchi za Kenya na Tanzania, huku ikionekana

kwamba maswali ya ufahamu kwa Tanzania yalikuwa magumu zaidi kuliko yale ya Kenya. Jaribio la Kiingereza lilikuwa

sawa katika nchi zote tatu, japo hadithi ya Tanzania ilikuwa fupi na rahisi kuliko zile za Kenya na Uganda. Vilevile

majaribio ya kuhesabu yalikuwa sawa, isipokuwa tu kwamba jaribio la Tanzania lilikuwa na maswali ya kujumlisha kwa

kuhamisha, na maswali ya kutoa kwa kuhamisha ambayo hata hivyo hayakuulizwa Kenya na Uganda. Kwa upande

mwingine, nchini Uganda na Kenya wanafunzi walifanya hesabu za kugawanya, maswali ambayo watoto wa Tanzania

hawakuulizwa.

Inaweza kusemwa kwamba majaribio haya yalipima uwezo wa watoto katika kuhesabu na kusoma, na si kujifunza.

Ili kupima kujifunza, ambacho ni kipimo cha kuonesha mabadiliko, mtafiti angepaswa kuchunguza tofauti katika

viwango vya kufikiri tangu wakati wanafunzi wanapoanza shule katika nchi hizi zinazohusika. Kwa ujumla, inaelezwa

kwamba katika nchi za Uganda na Kenya, Kiingereza kinazungumzwa kwa upana zaidi kuliko ilivyo nchini Tanzania.

Kwa hiyo, kama ubora wa viwango vya ufundishaji vitabaki kuwa sawa katika nchi zote tatu, na jaribio kuwa na

kiwango cha ugumu kilicho sawa, inatarajiwa kuwa watoto nchini Kenya na Uganda wangefanya vizuri zaidi katika

jaribio la Kiingereza kuliko wale wa Tanzania. Kwa mantiki hiyo, hali kama hiyo inaweza kujitokeza kwa lugha ya

Kiswahili ambayo inazungumzwa kwa upana zaidi nchini Tanzania kuliko Kenya na kwa kawaida haizungumzwi nchini

Uganda. Pia, kiwango cha elimu ya wazazi kinaweza kusababisha tofauti wakati watoto wanapoingia shule.

Mathalan, kwa mujibu wa tafiti za idadi ya watu na afya (Demographic and Health Surveys), nchini Kenya asilimia

19 ya akina mama hawana elimu; takwimu kama hizo nchini Tanzania ni asilimia 33 na Uganda asilimia 23. Iwapo

mazingira ya nyumbani yanaathiri uwezo wa watoto wakati wanapoanza shule, basi tofauti katika matokeo ya

majaribio ya kuhesabu na kusoma hayamaanishi moja kwa moja uwepo wa tofauti katika kujifunza. Wakati huo huo

uhusiano wa karibu unatarajiwa baina ya matokeo ya majaribio ya kuhesabu na kusoma na ujifunzaji katika shule.

4

Uwezo 2010, Are our children learning? Annual Learning Assessment Report. Kenya 2009; Uganda 2010; Tanzania 2010. Zote zinapatikana kutoka www.uwezo.

net

Kuhesabu na Kusoma Katika Afika Mashariki 3

Ripoti hii, kwa kiasi kikubwa, inawasilisha takwimu za kitaifa. Hii ni kwa kuzingatia kwamba utaratibu wa kupata

sampuli za wilaya ulikuwa wa kinasibu. Ndani ya wilaya, vijiji vilichaguliwa kinasibu, na pia ndani ya vijiji taratibu za

kinasibu zilitumika (japo taratibu zilizotumika Tanzania ziliwaruhusu watafiti kwa kiasi fulani kufanya uchaguzi huru

ambao huenda ulisababisha upendeleo). Ili kuthibitisha kiwango ambacho matokeo ya kitaifa ya Uwezo yanafanana

na yale yaliyopatikana katika tafiti nyingine za kitaifa zilizohusisha kaya, Jedwali la 2 linawasilisha idadi ndogo ya

sifa za kaya, zilizopatikana kutoka tafiti za Uwezo na nyinginezo. Ulinganishaji wa data za Uganda (ambao ulifuata

kanuni kali za kinasibu) unaonesha kufanana kwa karibu kwa matokeo ya Uwezo na yale ya Taftishi za Kaya katika

Mambo ya Binadamu (Demographic Household Survey (DHS)). Kumekuwa na tofauti ndogo katika umiliki wa redio

na runinga lakini tofauti hizi huenda zinaakisi kipindi cha miaka minne kilichopita katikati ya tafiti hizi mbili. Vilevile

kwa Kenya, matokeo ya Uwezo yanafanana na yale ya DHS. Kuna tofauti ndogo, kama ambavyo ingetarajiwa, pale

zinapolinganishwa sampuli za tafiti mbili, hata hivyo tofauti hizo si kubwa.

Inaweza kusemwa, hata hivyo, kwamba sampuli ya Uwezo kwa upande wa Kenya inaonekana kuelemea zaidi

kwa kaya masikini na zenye elimu ya chini. Nchini Tanzania kwa upande mwingine, tofauti kubwa zaidi zinaweza

kuonekana. Katika nchi hii sampuli ya Uwezo inaonekana kuegemea zaidi kwenye kaya zenye elimu nzuri kidogo na

zilizojaliwa kiuchumi. Tofauti katika kipengele cha akina mama wasio na elimu (asilimia 30 katika HBS; asilimia 14

katika utafiti wa Uwezo) inastusha zaidi. Pia ukweli kwamba Uwezo inaripoti asilimia 19 ya kaya zenye umeme dhidi

ya asilimia 12 katika utafiti wa HBS ni tofauti kubwa.

Katika sehemu zinazofuata za ripoti hii masuala haya yanajadiliwa, lakini msomaji anatahadharishwa kwamba sampuli

ya Tanzania inaweza kuwa imeegemea zaidi katika kaya zenye hali nzuri, na sampuli ya Kenya kuegemea zaidi kwenye

kaya zenye hali duni.

Jedwali la 2: Mlinganisho wa matokeo ya kitaifa ya Uwezo na tafiti nyingine za kitaifa za kaya

Tanzania Kenya Uganda

Uwezo HBS Uwezo

2009

DHS

Uwezo 2010

DHS

Elimu ya mama

2010 2007

2009

2006

Hana elimu 14 30 24 19 Hakuna taarifa kuhusu elimu ya mama

Elimu ya msingi 1-4 8 9 53 60

katika utafiti wa Uwezo

Elimu ya msingi 5-7/8 66 52

Elimu ya sekondari 1-4 6 6 23 20

Zaidi ya sekondari 2 2

Mali &Umeme

Umeme 19 12 11 23 8 9

Redio 70 66 73 74 74 61

Runinga 18 8 22 28 13 6

Chanzo cha data: Uwezo, DHS (Uganda naKenya) na HBS (Tanzania) 65

5

www.measuredhs.com; Idara ya takwimu 2009; Utafiti wa Bajeti za Kaya 2007.

Je Watoto Wetu Wanajifunza? 4

Jedwali la 3: Sampuli za majaribio ya Kuhesabu, Kiingereza na Kiswahili yaliyotumiwa na Uwezo

3a: Jaribio la Kuhesabu

Utambuzi wa

Namba 1-9

Utambuzi wa

Namba

Kujumlisha bila kubeba Kujumlisha na

kubeba

Kutoa bila kukopa Kutoa na kukopa

Kuzidisha Kugawanya Hesabu zenye uhusiano na utamaduni

10-99

TZ 2 8

87 31

55 49

77 45 89 76 33 62 12 15

Shilingi 300 + Shilingi 200 = Shilingi

+23 +30

+25 +48 -42 -33 -15 -25 x 4 x 4

6 0

51 60

24 33

23 12 66 48 70 97 11 9

7 5

28 99 +71 +42

+68 +64 - 55 - 4 -34 -48 x 5 x24

KE 3 6

16 34

32 60

+24 +15

46 59

-24 -38

3 x 4 =

5 ÷1 =

Una shilingi 80. Utabaki na shilingi ngapi

baada ya kununua mfuko mmoja wa

unga unaouzwa kwa shilingi 60?

2 7 33 78

5 x 2 =

15 ÷3 =

24 43

53 74

4 5 50 99 +71 +51

-41 -21

3 x 2 =

8 ÷2 =

UG 9 5

1 3

11 91

91 47

14 88

+12 +11

71 46

-60 -14

7 x 3 =

3 x 4 =

6 ÷2 =

2 ÷2 =

Jane anataka kamba ambayo inauzwa

shilingi 250. John anampa Jane shilingi

300. Je, Jane atabaki na shilingi ngapi

baada ya kununua kamba?

15 13

66 89

8 6

72 69 +13 +14

- 15 -14

5 x 1 =

8 ÷2 =

3b Jaribio la Kiingereza

Herufi Maneno Sentensi/Aya Hadithi

TZ e n

d u

w f

boy tall

good best

come sing

This is my cat.

That dog is big.

I like my school.

My home is small.

Juma is living in a small village. He gets a letter once a month. The letter is from his son Musa. Musa lives in Dodoma. Juma cannot

read the letters. He asks Sara to read the letters for him.

Questions: 1. Where does Juma live?

2. What does Sara read?

3. What is the name of Juma’s son?

Kuhesabu na Kusoma Katika Afika Mashariki 5

KE e x

d w

k c

Room face

table dog

desk pen

My mother works in Lamu.

Lamu is the busy town.

The people there are good.

They are very kind.

Juma reads to us a story from his book every day. He reads the story aloud in class. We enjoy listening to the stories. Yesterday, he

read about the sun and the wind. Both of them lived in the same sky. The wind did not like the sun .It wanted to be the head of

the sky. One day, the wind chased the sun away. It told sun to go to another sky. The sun did not go. The next morning, the wind

ran after the sun. The sun fell down and started crying. That is how it began to rain. We clapped for Juma.

Questions: 1. What does Juma do every day?

2. How did rain begin?

UG i o

w y

cow mat

car sing

This is our goat.

She has two kids.

Tom is our best football player. He stays far away from school. One day we had a big match. Tom had not come to school that day.

The teacher went to look for Tom. The teacher found Tom weeding cassava. The teacher called Tom from the garden. All pupils

were happy when Tom came. Our school won the match. We danced the whole day.

s h bus leg She likes her kids.

Questions: 1. Where was Tom?

She feeds them well.

2. Why were the children dancing?

3c Majaribio ya Kiswahili

Silabi Maneno Aya Hadithi

TZ fa ki Chai sherehe Baba amejenga nyumba nzuri.

mwa njo

le chi

vuta maziwa

mama kaka

Nyumba yetu imezungukwa na

miti.

Miti huzuia upepo mkali.

Hapo zamani za kale samaki waliishi nchi kavu. Waliishi kwa kula wadudu kama vile panzi, mende na sisimizi. Siku moja wadudu

hawa walikaa kikao na kupanga namna ya kuwaondoa samaki. Kikao chao wengi walichangia. Ikafika zamu ya sisimizi. Sisimizi

alisimama na kusema, “Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu”. Wote walisimama na kupiga kelele “samaki wauaweee”. Samaki

waliposikia hivi walikimbia na kujificha majini. Hadi hivi leo samaki wanaishi majini.

Maswali: 1. Hapo zamani samaki waliishi wapi?

Miti hutupatia hewa safi.

2. Zamani samaki walikuwa wanakula wadudu gani?

3. Hadithi hii inatufundisha nini?

KE be di

na tu

ho le

kiti taa

soko uso

mali choo

Mama anapika uji.

Juma anasoma kitabu.

Maria anacheza mpira.

Naye baba analima shambani.

Jina langu ni Fatuma Abdi. Ninaishi Nakuru na familia yetu kwenye nyumba kubwa. Baba yangu ni mwalimu katika shule ya upili.

Wanafunzi wanampenda mama yangu kwakuwa ni mwalimu mzuri. Nao nyanya na babu wanaishi kule kijijini. Wao wana mbuzi

na kondoo wengi. Mimi huwatembelea siku za likizo. Nyanya hunipa hadithi nzuri za kuchekesha. Mimi hucheka hadi mbavu zikaniuma.

Likizo ikiisha, nyanya hunipa maziwa nimletee mama yangu.

Maswali: 1. Mama ya Fatuma hufanya kazi gani?

2. Fatuma huwatembelea Nyanya na Babu wakati gani?

(*) Angalizo: Wilaya za Kenya zina rangi ya buluu, wilaya za Ugandani kijani, wilaya za Tanzania ni nyekundu.

Chanzo cha data: Ripoti za kitaifa za Uwezo

Je Watoto Wetu Wanajifunza? 6

3. Upatikanaji wa Elimu

3.1 Uandikishaji katika shule za msingi uko juu lakini si kila mahali

Kielelezo cha 2 kinaonesha uandikishaji katika shule za msingi kulingana na umri wa watoto katika nchi

zinazohusika. 76 Mihimili katika kilelelezo inaonesha tofauti katika mifumo ya elimu miongoni mwa nchi hizi. Nchini

Kenya elimu ya msingi hutolewa kwa miaka nane na watoto wanatarajiwa kwenda shule tangu wakiwa na umri wa

miaka 6 hadi 13. Katika nchi za Tanzania na Uganda, elimu ya msingi huchukua miaka saba. Nchini Uganda watoto

wanaanza shule wanapokuwa na miaka 6 na kumaliza wanapokuwa na umri wa miaka 12, wakati nchini Tanzania

wanaanza shule wanapokuwa na miaka 7 na kumaliza wakiwa na miaka 13. Kielelezo kinaonesha pia watoto walio nje

ya viwango hivi vya umri.

Mihimili katika kielelezo inaonesha jinsi uandikishaji ulivyo wa chini sana nchini Tanzania. Bila kujali umri, idadi ya

watoto waliojiunga na shule nchini Tanzania bado ni ndogo kuliko katika nchi nyingine. Vilevile kielelezo kinaonesha

jinsi nchini Uganda, ikilinganishwa na Kenya, watoto wengi zaidi walivyoandikishwa katika shule za msingi walipokuwa

na umri wa miaka sita. Nchini Kenya, kwa kiasi fulani kutokana na kuwa na mtaala wenye nyongeza ya mwaka mmoja

zaidi, sehemu kubwa ya watoto wenye umri mkubwa (wale waliokuwa na miaka 14-16) walikwenda shule.

Kielelezo cha 2: Uandikishaji katika shule za msingi kwa umri

Chanzo cha data: Uwezo

3.2 Fursa za kujiandikisha zinabaki kuwa si sawa na hutegemea utajiri wa kaya

Kielelezo cha 3 kinaonesha jinsi uandikishaji ndani ya nchi unavyotofautiana kulingana na uwezo wa kimapato wa

kaya ya mtoto. Madaraja matano ya viwango vya utajiri yaliainishwa: masikini zaidi, masikini, hali ya kati (kipimo cha

kati), tajiri na tajiri sana na kila daraja lilikuwa na kaya asilimia 20. Madaraja ya utajiri yaliundwa kwa kutumia data

zilizokusanywa toka katika nchi husika, ikimaanisha kwamba inawezekana kaya masikini katika Kenya ni bora zaidi

kuliko zile zilizo katika kiwango cha kati nchini Tanzania. Kielelezo hiki kinajikita katika uandikishaji wa watoto ndani

ya umri rasmi wa kwenda shule katika kila nchi. Viwango vya uandikishaji vilikuwa vya chini sana katika Kenya (karibu

asilimia 84) na juu sana katika Uganda (karibu asilimia 90). Kielelezo kinaonesha vilevile kwamba watoto kutoka

katika kaya masikini walikuwa na uwezekano mkubwa wa kutoandikishwa shule. Tofauti hizi zimeonekana zaidi katika

Kenya na kwa kiwango kidogo katika Uganda na Tanzania.

6

Kipengele hiki kinatokana na maswali kwa wazazi kuhusu uandikishaji mashuleni. Matokeo yake tunatumia maneno “uandikishwaji shuleni”, japokuwa inawezekana

wazazi walielewa swali waliloulizwa kama swali kuhusu mahudhurio. Dhana ya uwezekano wa wazazi kuongelea mahudhurio wakati wameulizwa kuhusu

uandikishaji inatokana na ukweli kwamba viwango vya uandikishwaji vilivyoonekana kutoka kwenye data za Uwezo vinakaribiana sana na viwango vya mahudhurio

kama ilivyooneshwa na tafiti za DHS (angalia mathalan takwimu katika www.measuredhs.com)

Kuhesabu na Kusoma Katika Afika Mashariki 7

kwendashulekatikakilanchi.ViwangovyauandikishajivilikuwavyachinisanakatikaKenya(karibu

asilimia84)najuusanakatikaUganda(karibuasilimia90).Kielelezokinaoneshavilevilekwamba

watotokutokakatikakayamasikiniwalikuwanauwezekanomkubwawakutoandikishwashule.

TofautihizizimeonekanazaidikatikaKenyanakwakiwangokidogokatikaUgandanaTanzania.

Kielelezo cha 3: Uandikishaji wa watoto walio katika umri wa lazima kwenda shule (*) kwa madaraja matano ya

Kielelezocha3:Uandikishajiwawatotowaliokatikaumriwalazimakwendashule utajiri

(*) kwa

madarajamatanoyautajiri

100

82

86 88 90

92

87

82

86 87 86

90 91 92 93

90

80

74

70

60

50

40

30

20

10

0

Asilimiayawatotowaumriwa

kwendashulewalioandikishwa

Maskinizaidi

Maskini

Kipimochakak

Tajiri

Tajirisana

Maskinizaidi

Maskini

(*) Nchini Kenya umri wa lazima kwenda shule ni miaka 6-13; Tanzania ni 7-13 na Uganda ni 6-12.

(*)NchiniKenyaumriwalazimakwendashulenimiaka6‐13;Tanzaniani7‐13naUgandani6‐12.

Chanzo cha data: Uwezo

Chanzochadata:Uwezo

Namna nyingine ya kuonesha taabu za watoto kutoka kaya masikini sana ni kwa kuangalia watoto ambao kamwe

hawakwenda Namnanyingineyakuoneshataabuzawatotokutokakayamasikinisananikwakuangaliawatoto

shule ya msingi. Kama inavyoonekana wazi katika Kielelezo cha 4, watoto kutoka kaya masikini sana

ndiyo ambaokamwehawakwendashuleyamsingi.KamainavyoonekanawazikatikaKielelezocha4,

walioathirika zaidi. Nchini Kenya asilimia 64 watoto wa umri wa miaka 5-16 hawakwenda

shule watotokutokakayamasikinisanandiyowalioathirikazaidi.NchiniKenyaasilimia64yawatotowa

walitoka kaya sana katika madaraja umasikini ambapo nchini Uganda idadi hiyo ilikuwa asilimia 45

na umriwamiaka5‐16ambaokamwehawakwendashulewalikuwakutokakayamasikinisanakatika

nchini Tanzania asilimia 45 87 .

madarajayaumasikiniambaponchiniUgandaidadihiyoilikuwaasilimia45nanchiniTanzania

asilimia45 7 .

Kielelezo cha 4: Asilimia ya watoto wenye umri wa miaka 5-16 ambao hawakuwahi kwenda shule ya msingi, kwa

madaraja matano ya utajiri

Kipimochakak

Tajiri

Tajirisana

Maskinizaidi

Maskini

Kipimochakak

Tajiri

Tajirisana

7 KwaTanzaniaumriulikuwakatiyamiaka5‐16.

Chanzo cha data: Uwezo

13

Kama ilivyo idadi ya watoto ambao hawakuandikishwa, idadi ya wale walioacha shule ilikuwa juu miongoni mwa kaya

masikini zaidi, ingawa tofauti zilikuwa ndogo ikilinganishwa na ile ya wasioandikishwa. Miongoni mwa wale walioacha

shule, nchini Kenya asilimia 61 walitoka katika kaya masikini au masikini zaidi ikilinganishwa na asilimia 50 kutoka

Uganda na 41 kutoka Tanzania.

7

Kwa Tanzania umri ulikuwa kati ya miaka 5-16.

Je Watoto Wetu Wanajifunza? 8

Kielelezo cha 5: Watoto wa miaka 5 hadi 16 walioacha shule, kwa vipimo vya utajiri wa kaya

Chanzo cha data: Uwezo

Hitimisho: Licha ya ongezeko kubwa la uandikishaji kufuatia kuanzishwa kwa sera ya elimu ya msingi bure, data za

utafiti wa Uwezo zinaonesha kwamba uandikishaji haukuwa umejumuisha watoto wote wenye umri wa kwenda

shule. Kutegemeana na kiwango cha utajiri, kati ya asilimia 7 na 26 ya watoto wa umri wa kwenda shule walikuwa

hawaendi shuleni . Viwango hivi vinalingana na viwango vya mahudhurio vilivyopatikana katika tafiti nyingine. Tafiti

za DHS zinaonesha viwango vya mahudhurio vya asilimia 73 kwa Tanzania (2004/5), 79 kwa Kenya (2008/9), na 82

kwa Uganda (2006).

Watoto kutoka makundi ya kaya masikini na masikini zaidi walikuwa na uwezekano mdogo wa kuhudhuria wote

shuleni ikilinganishwa na watoto wanaotoka kwenye kaya zenye kipato bora zaidi. Hivyo si tu kwamba mpango

wa kufikisha elimu kwa watoto wote haukufanikiwa kikamilifu, lakini pia fursa za kwenda shule hazikuwa sawa, na

zilitegemea kiwango cha kipato cha kaya.

4. Ujifunzaji

4.1 Uwezo (umahiri) katika majaribio ya Kiingereza, Kuhesabu na Kiswahili

Lengo kuu la jaribio la Uwezo lilikuwa kupima uwezo wa watoto katika stadi za kusoma na kuhesabu. Kwa kuwa

majaribio yanaonesha ufahamu ambao wanafunzi walipaswa kuwa nao baada ya kukamilisha masomo ya ngazi

ya Darasa la 2, watoto wote katika madarasa ya juu walipaswa kufaulu vizuri katika jaribio la Darasa la 2. Kama

itakavyooneshwa katika sehemu hii, matokeo yalikuwa kinyume cha matarajio hayo. Jambo hili lilijidhihirika hata

miongoni mwa watoto wa ngazi ya Darasa la 7, wengi hawakuwa na stadi za kuhesabu na kusoma za ngazi ya Darasa

la 2.

Kiingereza: Kielelezo cha 6 kinawasilisha jinsi watoto walivyofanya katika jaribio la Kiingereza huku kikionesha tofauti

baina ya madarasa tofauti. Kielelezo kinaonesha jinsi ambavyo katika kila nchi watoto wachache wa Darasa la 3 ndiyo

waliokuwa na stadi za kiwango cha Darasa la 2 katika jaribio la kusoma. Nchini Kenya ni asilimia 28 tu ya watoto

wa Darasa la 3 ndiyo waliokamilisha jaribio kwa mafanikio, yaani waliweza kusoma hadithi bila shida. Katika nchi za

Uganda na Tanzania viwango vya ufaulu vilikuwa vya chini zaidi, asilimia 4 kwa asilimia 8 kwa mpangilio wa nchi hizo.

Watoto katika madarasa ya juu walionekana kufanya vizuri katika majaribio ya Uwezo kama ilivyotarajiwa. Nchini

Kenya asilimia 94 ya watoto wa ngazi ya Darasa la 7 walionesha kumudu stadi za Darasa la 2 katika kusoma kifungu

cha maneno cha Kiingereza. Umahiri ulionekana kuimarika kulingana na ngazi ya darasa katika nchi za Uganda na

Tanzania vilevile. Bila kuangalia darasa, asilimia ya watoto wa Kenya waliokuwa katika kiwango cha juu cha uelewa

ilikuwa kubwa kuliko ile ya wenzao katika nchi za Uganda na Tanzania. Nchini Tanzania matokeo yanakatisha tamaa; ni

asilimia 51 tu ya watoto katika Darasa la 7 ndiyo waliofaulu jaribio la Kiingereza lililokuwa katika kiwango cha Darasa

la 2.

Kuhesabu na Kusoma Katika Afika Mashariki 9

Kadri muda wa kuwa shule unayoongezeka ndivyo tofauti kati ya Kenya na Uganda katika asilimia ya watoto ambao

wamepata stadi za kiwango cha Darasa la 2 polepole inavyopungua. Wakati katika Darasa la 4 tofauti katika viwango

vya ufaulu kati ya nchi hizi mbili ilikuwa ni asilimia 39, ilipofika Darasa la 7 tofauti ilikuwa imepungua hadi asilimia

14. Kwa Kenya na Tanzania hali hii haikujitokeza na karibu mara mbili ya watoto katika Kenya walifaulu jaribio la

Kiingereza katika Darasa la 7 ikilinganishwa na ilivyokuwa katika Tanzania.

Kielelezo cha 6: Umahiri wa wanafunzi katika jaribio la Kiingereza la Uwezo,kwa darasa

Chanzo cha data: Uwezo

Kuhesabu: Matokeo katika jaribio la kuhesabu yalifanana na yale ya Kiingereza, watoto wa Kenya wakiwa wamefanya

vizuri (japokuwa ‘vizuri’ ni kwa kiwango cha wastani tu) wakilinganishwa na watoto wa Uganda na Tanzania. Kama

ilivyokuwa katika jaribio lililotangulia watoto wa Tanzania ndiyo waliofanya vibaya zaidi. Kama ilivyokuwa katika

jaribio la Kiingereza, uwezo wa watoto uliimarika kulingana na wakati na walipofika Darasa la 7 wengi wao walikuwa

wamepata stadi za msingi katika kuhesabu na walikuwa na stadi zilizotarajiwa katika ngazi ya Darasa la 2. Lakini hata

katika Kenya, nchi yenye ufaulu wa juu, asilimia 12 ya watoto katika Darasa la 7 walishindwa kufanya vizuri katika

mazoezi ya kuhesabu yaliyotarajiwa katika kiwango cha Darasa la 2.

Ikilinganishwa na kusoma Kiingereza, tofauti kiuwezo katika jaribio la kuhesabu kati ya Tanzania kwa upande

mmoja na Kenya na Uganda kwa upande mwingine, ni dogo. Inawezekana, ingawa hii ni kwa kukisia, pengo kubwa

kwa Kiingereza kuliko kuhesabu linaakisi kuwa watoto katika Kenya na Uganda wanaishi katika mazingira ambapo

Kiingereza kinasikika na kinazungumzwa kwa upana zaidi. Matokeo yake watoto hao wananufaika zaidi kuliko watoto

wa Tanzania ambao nje ya shule hawapati fursa hiyo na walimu wao wana uzoefu mdogo katika Kiingereza. Tofauti

katika alama za kuhesabu inaonesha kwamba haya si maelezo pekee kuhusu udhaifu wa stadi walizo nazo watoto

wa Tanzania. Kwa kuwa kiwango cha ufaulu katika majaribio yote mawili (Kiingereza na Kuhesabu) ni wa chini zaidi

chini Tanzania, inaonekana kwamba huenda kwa kiasi kikubwa watoto wa Tanzania wanajifunza kwa kiasi kidogo

wanapokuwa shuleni kuliko watoto wenzao katika nchi za Kenya na Uganda.

Kielelezo cha 7: Umahiri wa wanafunzi katika jaribio la kuhesabu la Uwezo, kwa darasa

Je Watoto Wetu Wanajifunza? 10

Chanzo cha data: Uwezo

Kiswahili: Hitimisho hili linaungwa mkono na matokeo yaliyoonekana katika jaribio la Kiswahili. Jaribio hili

liliendeshwa katika nchi ya Kenya na Tanzania pekee (kwa sababu Kiswahili hakitumiwi kwa upana nchini Uganda).

Ruwaza iliyoonekana awali ya matokeo mabaya kwa wanafunzi wa Darasa la 3 na hali ya uwezo kuimarika polepole

jinsi watoto wanavyopanda katika madarasa ya juu ilijirudia. Watoto wa Kenya walifanya vizuri zaidi kuliko watoto

wa Tanzania. Tofauti inayoonekana katika uwezo wa watoto kati ya Tanzania na Kenya katika Kiswahili ilikuwa

ndogo kuliko ile iliyopo katika Kiingereza na kuhesabu (huenda matokeo haya yanaakisi ukweli kwamba Kiswahili

kinazungumzwa kwa upana zaidi katika Tanzania ikilinganishwa na Kenya), lakini bado tofauti ilikuwepo. Hivyo hata

katika jaribio ambalo watoto wa Tanzania wangepaswa kuwa na nafasi nzuri zaidi ya kufaulu kuliko wale wa Kenya,

watoto wa Tanzania walifanya vibaya. Kielelezo cha 8 kinaonesha zaidi uwezo wa watoto katika Kiswahili, kwa darasa,

katika Kenya na Tanzania.

Kielelezo cha 8: Umahiri wa wanafunzi katika jaribio la Kiswahili la Uwezo, kwa darasa

Chanzo cha data: Uwezo

4.2 Tofauti katika uwezo wa watoto ki-wilaya

Licha ya tofauti katika uwezo wa watoto miongoni mwa nchi hizi tatu, kuna tofauti nyingine kubwa zilizokuwepo

miongoni mwa wilaya ndani ya kila nchi. Jedwali la 5 linaonesha asilimia ya watoto katika Darasa la 3 wenye stadi za

kuhesabu na kusoma za Darasa la 2. Nchini Tanzania asilimia 33 ya watoto katika wilaya ya Moshi Mjini, iliyofanya

vizuri zaidi, walifaulu jaribio la Kiingereza lakini hakuna mtoto hata mmoja (asilimia 0) katika wilaya ya Liwale

aliyefaulu jaribio hilo. Nchini Kenya, asilimia 66 ya watoto katika wilaya ya Kikuyu walifaulu jaribio la kuhesabu, lakini

ni asilimia 5 tu ya watoto walifaulu katika wilaya ya Lagdera. Na nchini Uganda, asilimia 40 ya watoto katika wilaya

ya Bushenyi walifaulu jaribio la kuhesabu, lakini ni asilimia 7 tu walifaulu katika wilaya ya Nakapiripirit. Tofauti hizo

zinaweza kuonekana katika kila jaribio katika majaribio matatu, na katika kila nchi. Tofauti hizi zinaleta wasiwasi.

Hakuna sababu kwa nini watoto wa Nakapiripirit, Lagdera au Liwale wafanye vibaya kuliko watoto wenzao wa

Bushenyi, Kikuyu au Moshi Mjini. Mahali anapozaliwa mtoto na kwenda shule pasiathiri uwezekano wa yeye kupata

stadi za msingi na uwezo wa kufanya vizuri katika kusoma na kuhesabu. Ukweli kwamba matokeo yako hivyo ni

kiashiria cha kutosha kuonesha kwamba hakuna usawa katika mifumo ya elimu katika kila nchi.

Jedwali la 4 linawasilisha wilaya kumi zilizofanya vizuri na zilizofanya vibaya nchini Kenya, Uganda na Tanzania. Katika

majaribio ya Kiingereza na Kuhesabu , wilaya zote 10 bora za mwanzo zilikuwa za Kenya. Katika zile za chini, kulikuwa

pia na wilaya chache za Kenya lakini nyingi kati ya hizo zilikuwa za Uganda na Tanzania. Ruwaza ya jumla ilionesha

kwamba wilaya kutoka Kenya zilikuwa juu katika chati, wilaya za Tanzania zilikuwa chini, na za Uganda zilikuwa

k a ti k a ti .

Kuhesabu na Kusoma Katika Afika Mashariki 11

Jedwali la 4: Wilaya zilizofanya vizuri sana na vibaya sana, wanafunzi wa Darasa la 3 katika majaribio ya Kiingereza

na Kuhesabu

Jaribio la Kiingereza

Jaribio la Kuhesabu

Zilizofanya vizuri sana Zilizofanya

Zilizofanya vizuri

Zilizofanya vibaya sana

vibaya sana

sana

1 Kikuyu Adjumani Kikuyu Kasulu

2 Naivasha Liwale Kaloleni Lagdera

3 Pokot Kaskazini Katakwi Naivasha Bukoba Vijijini

4 Taita Bundibugyo Meru Kusini Nakapiripirit

5 Nandi Mashariki Shinyanga Vijijini Nandi Kaskazini Gulu

6 Imenti Kaskazini Gulu Mbeere Kotido

7 Nyeri Kusini Kamuli Kibwezi Mwanga

8 Ruiru Mayuge Gatanga Singida Vijijini

9 Nakuru Kaskazini Yumbe Keiyo Mayuge

10 Gatanga Amuru Imenti Kaskazini Shinyanga Vijijini

(*) Angalizo: Wilaya za Kenya ni buluu, wilaya za Uganda ni kijani, wilaya za Tanzania ni nyekundu.

Chanzo cha data: Uwezo

Jedwali la 5 linaonesha kwamba wilaya zilizofanya vizuri katika jaribio moja, ziliweza pia kufanya vizuri katika

majaribio mengine. Katika Tanzania, wilaya za Moshi Vijijini na Rombo zilikuwa miongoni mwa wilaya tatu bora

katika kila jaribio katika majaribio matatu. Nchini Kenya, wilaya za Kikuyu na Naivasha ndizo zilizofanya vizuri katika

kila jaribio, na kule Uganda wilaya za Wakiso na Masaka zimejitokeza. Je, wilaya hizi zinafanana kwa namna gani?

Miongoni mwa wilaya zilizofanya vibaya kulikuwa na tofauti nyingi japo wilaya za Muleba na Kasulu katika Tanzania,

na Lagdera na Wajir Mashariki katika Kenya zinaonekana zaidi ya mara moja katika orodha ya wilaya zinazofanya

vibaya zaidi. Kwa ufupi inaonekana kwamba wilaya zinazofanya vizuri zote zinafanana, wilaya zinazofanya vibaya

zinafanya vibaya kwa namna yao.

Jedwali la 5: Wilaya zilizofanya vizuri sana na vibaya sana kwa Darasa la 3, kwa wilaya na nchi

Tanzania Kenya Uganda

Kiingereza Waliofanya vizuri

sana

Waliofanya Waliofanya vizuri

sana

Waliofanya vibaya

sana

Waliofanya vizuri

sana

Waliofanya

vibaya sana

vibaya sana

1 Moshi Mjini 33% Liwale 0% Kikuyu 64% Lagdera 4% Wakiso 12% Adjumani 0%

2 Rombo 23% Shinyanga

Vijijini

1% Naivasha 53% Trans Mara 9% Masaka 8% Katakwi 0%

3 Moshi

Vijijini

23% Muleba 2% Pokot

North

52% Rachuonyo 10% Nakasongola

8% Bundibugyo

1%

Kuhesabu

1 Moshi Mjini 40% Kasulu 5% Kikuyu 66% Lagdera 5% Busheni 40% Nakapiripirit

7%

North

2 Rombo 39% Bukoba Vijijini 7% Kaloleni 65% Samburu 14% Masaka 38% Gulu 7%

3 Moshi 35% Mwanga 8% Naivasha 57% Wajir 17% Wakiso 38% Kotido

Vijijini

Mashariki

8%

1

Kiswahili

Rombo 63% Muleba 9% Naivasha 68% Lagdera 4% Hawakufanya

2 Moshi Mjini 58% Mwanga 16% Taita 64% Wajir 12%

Mashariki

3 Kisarawe 57% Kasulu 17% Kikuyu 62% Trans Mara 14%

(*) Angalizo: Wilaya za Kenya ni buluu, wilaya za Ugandani kijani, wilaya za Tanzania ni nyekundu

Chanzo cha data: Uwezo

4.3 Tofauti katika umahiri wa wanafunzi kwa mujibu wa utajiri wa kaya

Sifa za kaya vilevile zilionesha kuathiri umahiri wa watoto katika majaribio. Kielelezo cha 9 na 10 hapa chini

vinaonesha jinsi utajiri wa kaya unavyohusiana na uwezo wa wanafunzi. Watoto kutoka kaya tajiri sana walifanya

vizuri zaidi katika majaribio ya Uwezo kuliko watoto kutoka kaya zenye hali ya chini. Mathalan, nchini Kenya karibu

nusu (asilimia 47) ya watoto wa Darasa la 3 kutoka kaya tajiri sana walionesha kuwa na stadi za kusoma za Darasa

la 2, kinyume na asilimia 19 tu ya watoto kutoka katika kaya maskini zaidi. Vivyo hivyo, asilimia 48 ya watoto kutoka

kaya tajiri sana katika Kenya walifaulu jaribio la kuhesabu, kinyume na asilimia 28 tu ya watoto kutoka kaya maskini

zaidi.

Je Watoto Wetu Wanajifunza? 12

Kielelezo cha 9: Ufaulu wa wanafunzi wa Darasa la 3 katika jaribio la Kiingereza la Uwezo, kwa madaraja ya utajiri

na nchi

Chanzo cha data: Uwezo

Kielelezo cha 10: Umahiri wa wanafunzi wa Darasa la 3 katika jaribio la kuhesabu, kwa madaraja ya utajiri na nchi

Chanzo cha data: Uwezo

Kulikuwa na uwezekano mdogo kwa watoto kutoka kaya masikini zaidi nchini Kenya kufaulu majaribio ya Kuhesabu

na Kiingereza kuliko watoto kutoka kaya tajiri. Hata hivyo, uwezekano wa kufanikiwa ulikuwa bado juu kwa mtoto

kutoka kaya masikini zaidi nchini humo kuliko mtoto kutoka kaya tajiri sana katika Uganda au Tanzania. Mathalani,

asilimia 19 ya watoto kutoka kaya masikini zaidi nchini Kenya walifaulu jaribio la Kiingereza, ikilinganishwa na asilimia

16 ya watoto kutoka kaya tajiri sana za Uganda na asilimia 11 ya watoto kutoka Tanzania. Kwa jaribio la Kuhesabu,

matokeo yanafanana, isipokuwa watoto wa Kenya kutoka kaya masikini zaidi walifaulu kwa kiwango kinachokaribiana

na watoto wenzao kutoka kaya tajiri zaidi za Uganda na Tanzania.

Hitimisho: Matokeo ya utafiti wa Uwezo yanaonesha kwamba stadi za kuhesabu na kusoma zilikuwa dhaifu katika

nchi zote tatu na watoto walio wengi katika Darasa la 3 hawakufikia stadi za kiwango cha Darasa la 2 katika kuhesabu

na kusoma. Kati ya waliofanya vibaya, Kenya ilifanya vizuri zaidi kuliko Uganda na Tanzania. Tanzania inaonesha

udhaifu mkubwa zaidi katika majaribio ya Uwezo. Tofauti kubwa katika umahiri wa watoto zimeonekana katika

wilaya ndani na kati ya nchi na kwa watoto kutoka kaya zenye viwango tofauti vya kipato. Inawezakana kukawa na

matumaini kutokana na tofauti za msingi katika ufaulu zilizojitokeza ndani ya kila nchi. Kuwepo kwa tofauti hizo

kunaashiria kwamba umahiri wa watoto unaweza kuimarika katika mifumo ya elimu iliyopo sasa na inatoa fursa ya

kutafuta sababu zilizopelekea kuwepo kwa tofauti hizi.

Kuhesabu na Kusoma Katika Afika Mashariki 13

5. Upatikanaji wa nyenzo shuleni

Inawezekana tofauti zilizobainika katika umahiri wa watoto ki-wilaya ni kutokana na tofauti ya upatikanaji wa nyenzo

shuleni au tofauti katika ufundishaji. Japokuwa utafiti wa Uwezo haukujumuisha taarifa kuhusu ubora wa ufundishaji,

taarifa katika dodoso la shule ziliruhusu kwa namna fulani kuangalia mahitaji yaliyokuwa yanapatikana katika shule.

Kwa kila moja ya nchi hizi tatu dodoso la shule la Uwezo lilikusanya taarifa ambazo zingeweza kukokotolewa kuhusu

idadi ya wanafunzi kwa mwalimu, wanafunzi kwa darasa, na wanafunzi kwa choo.

Ulinganishi kwa mujibu wa nchi unaonesha kwamba shule za Kenya zilikuwa na uwiano mdogo wa

wanafunzi:mwalimu, wanafunzi:darasa, na wanafunzi wachache kwa vyoo kuliko shule za Uganda na Tanzania.

Tofauti kati ya Kenya na Tanzania na Uganda ilikuwa kubwa. Mathalan, nchini Tanzania kulikuwa na wanafunzi 60

kwa mwalimu mmoja, nchini Kenya ni wanafunzi 38. Uganda kulikuwa na wanafunzi 83 kwa darasa, wakati Kenya

ni 48. Kwa ujumla viashiria vya upatikanaji wa mahitaji ya elimu nchini Kenya vinakaribiana sana na viwango rasmi

vinavyotakiwa kufikiwa kuliko hali ilivyo katika nchi za Uganda na Tanzania.

Kielelezo cha 11: Viashiria vya upatikanaji wa mahitaji shuleni kwa Kenya, Uganda na Tanzania

Chanzo cha data: Uwezo

Ndani ya nchi hizi tofauti kubwa zilionekana. Tofauti hizi zinaweza kuonekana katika Jedwali la 6 linaloonesha nafasi

za wilaya kulingana na upatikanaji wa mahitaji ya shule kwa kuzingatia wiano hizi tatu. Nafasi ya jumla ya wilaya

ilipatikana baada ya kukokotoa nafasi ya wilaya katika kila kiashiria kwa viashiria vyote vitatu na kuzipa wilaya namba

kulingana na nafasi iliyopata. Jumla ya namba zinazoambatana na nafasi zilizopata wilaya kwa viashiria vyote vitatu

ndizo zinazotoa nafasi za jumla ambazo wilaya zilipewa kutoka wilaya ya juu kabisa hadi ya chini kabisa katika Jedwali

la 6.

Jedwali linaonesha kwamba wastani ulitofautiana sana: kutoka wanafunzi 25 kwa mwalimu (chini kabisa) kama

iliyokuwa katika wilaya ya Imenti Kusini, Kenya, hadi wanafunzi 91 kwa mwalimu (juu kabisa) katika wilaya ya Muleba,

Tanzania. Vilevile wiano za mwanafunzi: darasa zilitofautiana kutoka wanafunzi 23 (chini kabisa pia) katika wilaya

ya Imenti Kusini, hadi kufikia 173 (juu kabisa) katika wilaya ya Buliisa, Uganda. Uwiano wa wanafunzi kwa choo pia

ulitofautiana, kutoka uwiano wa chini kabisa wa wanafunzi 14 kwa choo katika wilaya ya Nyeri Kusini, Kenya hadi

kufikia kiwango cha juu kabisa, kiasi cha wanafunzi 110 kwa choo kimoja katika wilaya ya Kamuli, Uganda. Hizi wiano

ni wastani katika ngazi ya wilaya, ikimaanisha kuwa zinaficha tofauti kubwa zaidi zilizopo baina ya shule. Kwa shule

moja moja na madarasa, tofauti zilikuwa za juu zaidi. Mathalan, nchini Kenya data za Uwezo zinaonesha kwamba

wiano za mwanafunzi:mwalimu zinaanzia 10:1, chini kabisa hadi kufikia zaidi ya 200:1.

Jambo jingine lililoonekana ni kwamba wilaya za Kenya zilikuwa katika nafasi za juu, ambapo za Tanzania na Uganda,

na chache za Kenya zilionekana katika nafasi za chini ya orodha. Katika upangaji wa nafasi uliofanywa na Uwezo katika

Afrika Mashariki, wilaya za Kenya zilionekana kuwa katika nafasi 24 za juu. Wilaya ya kwanza isiyo ya Kenya ilikuwa

ya Tanzania katika nafasi ya 25, ambapo wilaya ya kwanza ya Uganda ilionekana katika nafasi ya 44. Hakuna wilaya za

Kenya zilizokuwa miongoni mwa zile zilizoshika nafasi 10 za chini.

Je Watoto Wetu Wanajifunza? 14

Jedwali la 6: Wilaya zilizofanya vizuri na vibaya sana katika kipimo kinachojumuisha uwiano wa

mwanafunzi:mwalimu, mwanafunzi: darasa na mwanafunzi: choo

Wanafunzi kwa

Nafasi Jina la wilaya Wanafunzi kwa mwalimu darasa

Wanafunzi kwa choo

Wilaya 10 za juu

1 ImentiKusini 25 23 14

2 Mbeere 27 28 17

3 Meru Kusini 28 25 17

4 Imenti Kaskazini 28 29 23

5 Nyeri Kusini 33 28 14

6 Kericho 28 35 30

7 Nyandarua Kaskazini 35 33 17

8 Kikuyu 35 31 25

9 Tharaka 29 29 39

10 Wareng 31 35 31

Wilaya 10 za chini

126 Muleba 91 83 79

127 Kamuli 66 86 110

128 Mayuge 64 99 100

129 Urambo 86 110 69

130 Amuru 70 117 76

131 Amuria 69 100 89

132 Budaka 69 101 87

133 Geita 83 108 92

134 Buliisa 67 173 112

135 Ilemela 87 140 107

(*) Angalizo: wilaya za Kenya ni buluu, wilaya za Uganda ni kijani, wilaya za Tanzaniani nyekundu

Chanzo cha data: Uwezo

Kielelezo cha hali ya upatikanaji mahitaji shuleni kinaweza kuundwa kwa kutumia utaratibu uleule uliotumika kuunda

kielelezo cha utajiri wa kaya 98 . Madaraja matano ya upatikanaji wa mahitaji, kila moja likiwa na asilimia 20 ya shule

zilizotembelewa, yaliainishwa kwa kila nchi. Madaraja hayo matano hayakuweza kulinganishwa moja kwa moja

miongoni mwa nchi zote tatu kwa kuwa viashiria tofauti vilitumika kuunda kielelezo cha kila nchi. Ndani ya nchi, kwa

kiasi kikubwa ufaulu wa wanafunzi wa Darasa la 3 katika majaribio ya Uwezo haukutofautiana sana kulingana na

daraja la hali ya mahitaji katika shule. Tofauti moja iliyojitokeza ni kwamba katika nchi za Kenya na Tanzania umahiri

wa wanafunzi katika jaribio la Kiingereza ulikuwa mkubwa zaidi kwa watoto waliosoma katika shule iliyokuwa katika

daraja la juu la upatikanaji wa mahitaji.

Kielelezo cha 12: Watoto wa Darasa la 3 wenye stadi za kusoma Kiingereza za Darasa la 2, kwa madaraja ya

upatikanaji wa nyenzo shuleni

Chanzo cha data: Uwezo

8

Angalia, mathalani Filmer D na Pritchett LH. Estimating wealth effect without expenditure data-or tears: an application to educational enrollments in states of

India. Demography 2001; 38:115-32.

Kuhesabu na Kusoma Katika Afika Mashariki 15

Kielelezo cha 13: Watoto wa Darasa la 3 wenye stadi za kuhesabu za Darasa la 2, kwa madaraja ya upatikanaji wa

nyenzo shuleni

Chanzo cha data: Uwezo

Kielelezo cha 14 na kile cha 15 vinawasilisha ubora wa shule kwa kuzingatia hali ya upatikanaji nyenzo katika shule

walizohudhuria watoto kutoka daraja la chini na la juu la utajiri. Inaonekana kwamba, kwa ujumla, watoto kutoka

kaya masikini walihudhuria shule duni, ambapo watoto kutoka familia bora walihudhuria shule bora. Nchini Kenya,

tofauti zilionekana zaidi na watoto asilimia 37 kutoka asilimia 20 ya kaya masikini zaidi walihudhuria shule duni zaidi,

ambapo ni asilimia 9 tu kutoka kaya masikini zaidi ndiyo walihudhuria shule bora zaidi. Nchini Uganda, mgawanyo

ulionekana kuwa wa usawa zaidi, wakati Tanzania ikichukua nafasi ya katikati.

Kielelezo cha 14: Hali ya nyenzo katika shule walizosoma watoto kutoka kaya masikini zaidi

Chanzo cha data: Uwezo

Kielelezo cha 15: Hali ya nyenzo katika shule walizosoma watoto kutoka kaya tajiri zaidi

Je Watoto Wetu Wanajifunza? 16

Chanzo cha data: Uwezo

Hitimisho: Kuna tofauti kubwa katika hali ya upatikanaji wa mahitaji baina ya shule. Ubora wa shule ukitafsiriwa kwa

kutumia seti ya viashiria sahili vya mahitaji (wanafunzi kwa mwalimu, wanafunzi kwa darasa, na wanafunzi kwa choo)

ulionesha kuwepo kwa tofauti kubwa miongoni mwa nchi hizi tatu, kati ya wilaya ndani ya nchi, na kati ya shule zilizo

katika wilaya moja. Kwa jumla shule nchini Kenya zilikuwa zina hali nzuri zaidi kuliko shule za Uganda na Tanzania;

shule za Uganda ndizo zilizokuwa na hali duni zaidi.

Uhusiano kati ya hali ya upatikanaji mahitaji shuleni na umahiri wa watoto katika majaribio ya Uwezo ulionekana

kuwa hafifu. Hali hii inapaswa kuwatahadharisha wale wanaoamini kuwa utendaji katika shule utakuwa bora zaidi

kwa kupunguza uwiano wa mwanafunzi:mwalimu au uwiano wa mwanafunzi:darasa. Data za Uwezo zinaashiria kuwa

vipengele hivi ni muhimu ila vipengele ambavyo havikuangaliwa katika utafiti vinaweza kuwa ni muhimu zaidi. Namna

ya ufundishaji, uwajibikaji wa mwalimu na motisha ni baadhi ya vipengele vingine muhimu vinavyoathiri ufaulu wa

shule. Kwa bahati mbaya hakuna taarifa zilizokusanywa kuhusu vipengele hivi.

Mwisho, watoto kutoka kaya masikini walikuwa na mazingira magumu zaidi kwa maana si tu kwamba kulikuwa na

uwezekano mkubwa wa wao kutokwenda shule au kuacha shule, wao vilevile walikuwa na uwezekano mkubwa zaidi

wa kusoma katika shule zilizo na hali duni ya mahitaji.

6. Shule binafsi

Mpaka sasa ripoti hii imejikita katika stadi za kuhesabu na kusoma katika shule za msingi za serikali. Lakini kuna idadi

kubwa ya watoto wanaosoma katika shule binafsi katika nchi za Afrika Mashariki. Nchini Kenya asilimia 9 ya watoto

wenye umri wa kwenda shule wanasoma katika shule binafsi na nchini Uganda watoto wanaofikia asilimia 28 ya

watoto wote walioandikishwa shule wanahudhuria shule binafsi. Tanzania ndiyo nchi ambayo ina watoto wachache

zaidi wanaosoma katika shule binafsi (asilimia 2).

Kuhesabu na Kusoma Katika Afika Mashariki 17

Kielelezo cha 16: Mgawanyo wa wanafunzi wa elimu ya msingi katika shule za serikali na binafsi

Chanzo cha data: Uwezo

Haishangazi, bila shaka, kwamba watoto walio wengi waliosoma katika shule binafsi walitoka katika kaya tajiri sana;

wachache walitoka katika kaya masikini. Ruwaza hii ilijitokeza zaidi katika Tanzania, ambako watoto waliosoma katika

shule binafsi kwa kawaida walitoka katika kaya zilizo katika madaraja mawili ya juu ya kipimo cha utajiri. Nchini

Uganda, elimu katika shule za binafsi ilipatikana pia kwa watoto kutoka kaya masikini, ingawa watoto kutoka kaya

tajiri bado ndiyo waliokuwa na nafasi kubwa zaidi ya kusoma katika shule hizo. Kenya inashika nafasi ya katikati.

Kielelezo cha 17: Uandikishaji watoto katika shule za binafsi kwa mujibu wa madaraja ya utajiri

Je Watoto Wetu Wanajifunza? 18

Chanzo cha data: Uwezo

Wanafunzi wanaosoma katika shule binafsi walifanya vizuri katika majaribio ya Uwezo kuliko wale wanaosoma katika

shule za serikali. Matokeo haya yamejidhihirisha katika nchi zote tatu. Nchini Kenya asilimia 60 ya watoto katika shule

binafsi Darasa la 3 walifaulu majaribio ya Kiingereza na Kuhesabu. Matokeo haya yalikuwa pungufu ya asilimia 100

yaliyoyatarajiwa lakini mazuri mara mbili zaidi ikilinganishwa na matokeo katika shule za serikali. Nchini Tanzania

tofauti katika uwezo wa watoto wa Darasa la 3 kati ya shule za serikali na binafsi ilikuwa dhahiri zaidi. Wakati watoto

chini ya asilimia 10 katika shule za serikali walifaulu jaribio la Kiingereza, karibu nusu ya wale waliokuwa katika

shule binafsi walifaulu. Tofauti kama hiyo, japo ndogo ilionekana pia katika jaribio la kuhesabu. Pengine matokeo

yanayostusha zaidi yalikuwa kutoka Uganda ambako shule binafsi zilifanya vizuri kuliko shule za serikali lakini ni

asilimia 10 tu ya watoto katika Darasa la 3 wanaohudhuria shule binafsi ndio waliofaulu jaribio la Kiingereza. Hii ni

licha ya kuwa lugha ya Kiingereza inatumiwa kwa kiasi kikubwa katika baadhi ya shule za Uganda. Matokeo haya

ndiyo yaliyokuwa mabaya zaidi katika Afrika Mashariki. Miongoni mwa wanafunzi wanaosoma katika shule binafsi

wanafunzi katika shule binafsi za Uganda pia walifanya vibaya sana katika jaribio la kuhesabu.

Wakati watoto wanapokuwa wamefika Darasa la 7, tofauti katika ufulu haionekani kati ya wale wanaosoma katika

shule za serikali na wanaosoma katika shule binafsi, isipokuwa kwa Tanzania ambako wanafunzi wa Darasa la 7

katika shule za serikali wameonekana kufanya vibaya zaidi kuliko wanafunzi wanaosoma katika shule binafsi. Wakati

huohuo, nchini Uganda na Tanzania idadi kubwa ya wanafunzi katika shule binafsi katika Darasa la 7 waliendelea

kushindwa katika majaribio ya Uwezo. Mathalan, mwanafunzi mmoja kati ya watano wa Darasa la 7 wa shule binafsi

nchini Uganda walishindwa jaribio la hesabu la Uwezo. Nchini Tanzania, mwanafunzi mmoja kati ya watatu wa darasa

la saba toka shule binafsi walishindwa jaribio la hesabu la Uwezo.

Kielelezo cha 18: Umahiri katika majaribio ya Uwezo ya Kiingereza na Hesabu kwa mujibu wa

aina ya shule na darasa

Chanzo cha data: Uwezo

Hitimisho: Mahudhurio ya wanafunzi katika shule binafsi yametofautiana sana katika nchi za Afrika Mashariki, kukiwa

na mtoto mmoja kati ya watoto wanne anayesoma katika shule za binafsi nchini Uganda, na mtoto mmoja kati ya

watoto 50 nchini Tanzania. Kama ilivyotarajiwa, ni watoto kutoka kaya tajiri sana ndiyo wanaosoma katika shule

binafsi, ingawa nchini Uganda upatikanaji wa shule ulionesha mgawanyo wenye usawa zaidi miongoni mwa matabaka

ya utajiri.

Umahiri wa wanafunzi wanaosoma katika shule binafsi katika majaribio ya Uwezo ulikuwa mzuri zaidi kuliko ya wale

wanaosoma katika shule za serikali, lakini bado hayaridhishi. Wanafunzi wanaosoma katika shule binafsi kwa kiasi

fulani walifanya vibaya hasa katika nchi za Tanzania na Uganda. Hata Kenya, ambako watoto kutoka shule zake za

binafsi walifanya vizuri zaidi, mtoto mmoja katika watoto watatu wa Darasa la 3 alishindwa katika majaribio ya Uwezo

ya kuhesabu na Kiingereza.

Matokeo mazuri ya shule binafsi yanatoa fursa ya kuchunguza ni nini hasa chanzo cha matokeo hayo mazuri. Je, shule

za binafsi zina vitendea kazi bora kama vile vitabu, walimu wenye sifa bora kitaaluma, uwajibikaji, mishahara mizuri

ya walimu, au vichocheo vingine? Wakati huo huo ni wazi kwamba shule binafsi zenyewe si ufumbuzi, kwa kuwa

matokeo ya wanafunzi wao bado hayaridhishi sana.

Kuhesabu na Kusoma Katika Afika Mashariki 19

7. Usawa wa Kijinsia

Sehemu hii inajadili usawa wa kijinsia kwenye shule. Kama ilivyojadiliwa katika Sehemu ya 3, zilionekana tofauti

katika viwango vya uandikishaji katika nchi hizi tatu. Hata hivyo, kama Kielelezo cha 19 kinavyoonesha, nchi zote

zimefanikiwa kukuza usawa wa kijinsia katika uandikishaji. Katika nchi za Uganda na Kenya uandikishaji ulikuwa juu

kidogo kwa wanafunzi wavulana ukilinganishwa na ule wa wasichana, wakati Tanzania kiwango cha uandikishaji

kilikuwa juu kidogo kwa wasichana.

Kielelezo cha 19: Uandikishaji kwa mujibu wa jinsia kwa watoto wenye umri wa kwenda shule

Chanzo cha data: Uwezo

Wakati ambapo tofauti za kijinsia katika uandikishaji wanafunzi zimepungua sana, majaribio ya Uwezo yameonesha

kuwepo kwa tofauti kidogo katika viwango vya ufaulu baina ya wanafunzi wa kike na wa kiume kama inavyoonekana

katika Jedwali la 20. Nchini Kenya, wanafunzi wa kike walifanya vibaya kidogo katika majaribio matatu ya Uwezo,

wakati katika nchi za Uganda na Tanzania ushahidi ulichanganyika. Nchini Uganda, wanafunzi wa kike walifanya

vizuri kidogo katika jaribio la Kiingereza tofauti na wavulana na vibaya katika jaribio la kuhesabu. Nchini Tanzania,

wanafunzi wa kike pia walifanya vibaya kidogo katika jaribio la kuhesabu, vizuri katika jaribio la Kiingereza, na vizuri

zaidi katika jaribio la Kiswahili.

Je Watoto Wetu Wanajifunza? 20

Kielelezo cha 20: Ufaulu wa wanafunzi wa Darasa la 3 katika majaribio ya Uwezo, kwa mujibu wa jinsia

Chanzo cha data: Uwezo

Hitimisho: Ubaguzi wa kijinsia mara nyingi huonekana katika nyanja za siasa-jamii. Hali hii haikuonekana katika

elimu ya msingi, angalau katika uandikishaji au umahiri wa wanafunzi katika stadi za msingi za kusoma na kuhesabu:

wanafunzi wa kike na wa kiume walikuwa na ufaulu usiotofautiana sana. Nchini Kenya, wanafunzi wa kike waliachwa

nyuma kidogo katika uandikishaji na pia hawakufanya vizuri katika majaribio ya Uwezo ukilinganisha na wenzao wa

kiume. Kwa upande wa Uganda na Tanzania matokeo yalichanganyika, na inaweza kuwa haki kuhitimisha kuwa kwa

ujumla wasichana na wavulana walionesha umahiri sawa.

8. Ni vipengele vipi vinaathiri zaidi ufaulu wa watoto?

Hadi hapa ripoti hii inaonesha kwamba stadi za msingi za kuhesabu na kusoma zilihusiana kwa karibu zaidi na

darasa analosoma mtoto, iwapo alitoka katika kaya tajiri, na kama alisoma katika shule ya binafsi. Stadi za msingi za

kuhesabu na kusoma hazina uhusiano wa karibu na upatikanaji wa nyenzo au mahitaji shuleni, na jinsia ya mtoto.

Kwa kuwa wanafunzi waliosoma katika shule duni pia walitarajiwa kukabiliwa na changamoto nyingine kama vile

kipato kidogo katika kaya, ni vigumu kuchanganua athari za hali ya upatikanaji wa nyenzo shuleni kwa mafanikio ya

watoto. Katika sehemu hii tunachunguza uhusiano wa vipengele tulivyojadili kwa ujumla na umahiri wa wanafunzi

shuleni. Tunaangalia pia vipengele vingine vinavyoweza kuwa na uhusiano na ufaulu wa wanafunzi kama vile

kiwango cha elimu ya mama au umri wa mtoto. Kwa kufanya ukokotozi wa kimahesabu tunajaribu kukadiria athari ya

vipengele hivi kila kimoja, kikiwa peke yake, bila kuwepo kwa athari ya kipengele kingine katika ufaulu wa mtoto.

Tunawasilisha matokeo kwa nchi moja moja kwa kuwa data za Uwezo zinaruhusu kuingiza vigezo tofauti tofauti katika

kila nchi. Mathalan, katika utafiti wa Uwezo nchini Uganda maswali kuhusu elimu ya mama hayakuulizwa, wakati

yaliulizwa katika Tanzania na Kenya.

Kuhesabu na Kusoma Katika Afika Mashariki 21

Katika nchi zote tatu na kwa majaribio matatu tofauti, ruwaza ya kufanana inajitokeza. Darasa alilokuwa anasoma

mwanafunzi ni kipengele kilichoonekana kuwa na uhusiano wa karibu zaidi na uwezekano wa mtoto kuwa na stadi

za msingi za kuhesabu na kusoma. Elimu ya mama nayo vilevile ilikuwa na athari kubwa kwa uwezekano wa mtoto

kumudu stadi hizi za msingi lakini, na hii ilionekana dhahiri zaidi, hasa kwa kinamama wenye elimu ya sekondari na

kuendelea. Ilipotokea kuwa mama ana elimu ya shule ya msingi au chini ya hapo, athari chanya kwenye umahiri wa

mtoto katika kumudu stadi za msingi shuleni haikuonekana. Vipengele vya utajiri wa kaya na mtoto kusoma katika

shule za binafsi vilikuwa na athari chanya kubwa katika ufaulu shuleni. Vipengele vya jinsia na upatikanaji wa nyenzo/

mahitaji ya shule vilikuwa na athari kidogo sana.

Kielelezo cha 21: Athari za ziada kutokana na vipengele mbalimbali kwa umahiri wa wanafunzi katika jaribio la

Uwezo: Kenya

Chanzo cha data: Uwezo

Kielelezo cha 22: Athari za ziada kutokana na vipengele mbalimbali katika uwezo wa wanafunzi katika jaribio la

Uwezo:Tanzania

Chanzo cha data: Uwezo

Je Watoto Wetu Wanajifunza? 22

Figure 23: Athari za ziada kutokana na vipengele mbalimbali kwa umahiri wa wanafunzi katika jaribio la Uwezo:

Uganda

9. Hitimisho

Chanzo cha data: Uwezo

Muhtasari wa matokeo makuu

Ripoti hii imechunguza uwezo wa kuhesabu na kusoma kwa maelfu ya wanafunzi wenye umri wa kati ya miaka 6 na

16 katika nchi za Kenya, Tanzania na Uganda kwa kutumia majaribio ya Uwezo yaliyofanywa mwaka 2009/10. Kwa

mujibu wa matokeo haya, watoto katika nchi zote tatu walifanya vibaya ikilinganishwa na viwango vya mitaala ya

nchi zao. Wanafunzi wa shule za msingi za Kenya ndiyo walioonekana kuwa wanajifunza zaidi. Katika majaribio yote

matatu–Kiswahili, Kiingereza na kuhesabu–wanafunzi wa Kenya walikuwa juu, wakifuatiwa na wanafunzi wa Uganda.

Wanafunzi wa Tanzania ndiyo waliofanya vibaya zaidi hata katika jaribio la Kiswahili, lugha ambayo watoto wa

Tanzania wanaitumia zaidi kuliko watoto wa Kenya.

Wakati watoto wa Kenya wameonesha kuwa na stadi bora zaidi katika kuhesabu na kusoma, nao pia hawakufanya

vizuri sana. Katika Darasa la 3, watoto kama wawili kati ya watatu hawakuweza kufaulu majaribio ya Uwezo ya

Kiingereza, Kiswahili na kuhesabu. Matokeo haya yanatia wasiwasi, kwa kuwa matarajio yalikuwa asilimia 100 au

watoto wote katika Darasa la 3 wangeweza kufaulu jaribio la Darasa la 2. Ni pale wanafunzi walipofika Darasa la 7

ndipo karibu wote walionesha kuwa wamepata stadi za msingi za kuhesabu na kusoma za Darasa la 2, japo katika

Tanzania nusu ya wanafunzi wa Darasa la 7 bado hawakuweza kufanya jaribio la Kiingereza la Darasa la 2.

Shule nchini Kenya zilionekana kuwa na hali nzuri zaidi ya upatikanaji wa mahitaji ya shule (kwa kuangalia uwiano

wa wanafunzi kwa mwalimu; uwiano wa wanafunzi kwa darasa, na vilevile wa wanafunzi kwa choo) zikilinganishwa

na shule katika nchi za Uganda na Tanzania. Hata hivyo, jambo muhimu tuliloliona, ukizingatia rasilimali nyingi

zimewekezwa katika miaka ya karibuni ili kuongeza ubora wa miundo mbinu ya shule, ni kwamba upatikanaji

wa nyenzo hizi ulikuwa na uhusiano mdogo sana na viwango vya ustadi wa watoto katika kusoma na kuhesabu.

Wanafunzi katika maeneo yenye shule zenye miundombinu bora hawakufanya vizuri kuliko wale wanaosoma katika

shule zenye miundombinu isiyotosheleza au katika madarasa yenye msongamano mkubwa.

Kuhesabu na Kusoma Katika Afika Mashariki 23

Kenya ilikuwa nchi pekee ambako tofauti za kiusawa zilionekana wazi zaidi. Miongoni wa kaya masikini zaidi, watoto

wachache zaidi waliofikia umri wa lazima kwenda shule waliandikishwa katika shule za msingi za Kenya (asilimia 74)

ikilinganishwa na Tanzania (asilimia 82) na Uganda (asilimia 86). Watoto masikini wa Kenya walikuwa na uwezekano

mkubwa wa kusoma katika shule zenye hali ya chini kuliko watoto masikini katika nchi za Uganda au Tanzania. Watoto

masikini Kenya walikuwa na uwezekano mkubwa zaidi wa kutokwenda shule ya msingi na kuacha shule kuliko watoto

wenzao wa Tanzania.

Licha ya hali hii, kwa upande wa matokeo ya kujifunza, watoto masikini nchini Kenya walikuwa na uwezekano

mkubwa wa kufanya vizuri katika majaribio ya Uwezo kuliko watoto kutoka kaya tajiri zaidi katika nchi ya Tanzania

na Uganda.Nchini Kenya asilimia ya watoto kutoka kaya masikini katika Darasa la 3 waliofaulu jaribio la kuhesabu

walikuwa asilimia 31, ikilinganishwa na asilimia 28 ya watoto kutoka kaya tajiri zaidi Uganda waliofaulu jaribio hili.

Asilimia ya watoto wa Kenya kutoka kaya masikini zaidi waliofaulu jaribio la Kiingereza ilikuwa 19, ikilinganishwa na

asilimia 16 ya watoto kutoka kaya tajiri sana katika Tanzania waliofaulu jaribio hili.

Nchini Uganda, watoto walifanya vibaya sana katika madarasa ya chini lakini walipofika katika madarasa ya juu

waliimarika na kuweza kuonesha ustadi wa kumudu majaribio ya viwango vya Darasa la 2. Walipofika Darasa la 7,

kiwango cha ufaulu cha watoto wa Uganda kilikuwa karibu sawa na cha watoto wa Kenya. Matokeo kwa upande

wa watoto wa Tanzania yalikuwa tofauti: kiwango cha ufaulu wa watoto kilibadilika kwa kiasi kidogo sana kadri

walivyoendelea kupanda madarasa. Matokeo yake ni kwamba, ni asilimia 51 tu ya watoto wa Tanzania katika Darasa

la 7 walifaulu jaribio la Kiingereza la Uwezo na ni asilimia 68 tu katika Darasa la 7 walifaulu jaribio la kuhesabu la

Darasa la 2.

Watoto wanaosoma katika shule za binafsi walifanya vizuri kiasi wakilinganishwa na wale wanaosoma katika shule

za serikali. Utafiti unathibitisha kwamba elimu ya mama ilikuwa na athari kubwa katika uwezo wa mtoto shuleni

iwapo mama alikuwa angalau na elimu ya sekondari. Tofauti za kijinsia katika uandikishaji au ufaulu shuleni hazikuwa

kubwa.

Nini kifanyike

Ukiangalia matokeo haya bila shaka utagundua kuna changamoto kubwa zinazokabili serikali za Afrika Mashariki,

walimu na wazazi katika kuhakikisha kwamba watoto wanapata stadi za msingi za kuhesabu na kusoma. Tofauti katika

ujifunzaji vilevile zinapunguza matumaini ya ushirikiano mkubwa na maendeleo kati ya nchi za ukanda wa Afrika

Mashariki. Hali katika Tanzania ni mbaya zaidi, lakini matokeo ya Kenya na Uganda yanatoa faraja kidogo. Jitihada

zaidi zinahitajika sana kushughulikia viwango vya watoto kutokwenda shule na kuacha shule. Vile vile kuna haja ya

kuhakikisha kwamba watoto si tu waende shuleni lakini pia wajifunze wakiwa shuleni. Kimataifa inazidi kutambuliwa

kuwa watoto wanahitaji kuwa shuleni na kujifunza pia.

Matokeo mabaya lazima huibua swali, nini kifanyike? Matokeo katika ripoti hii yanaashiria kwamba watunga sera

wangefanya vizuri iwapo wangehoji ufanisi wa mbinu zilizotumika hadi kufikia sasa, badala ya kuendelea kutekeleza

mbinu zile zile zilizozoeleka. Japo uwekezaji wa aina tofauti tofauti unaweza kuleta matokeo chanya, viwango vya

ufanisi wa uwekezaji vinatofautina. Uwekezaji wa aina fulani unaweza kuleta mabadiliko bora na ya haraka zaidi

kuliko mwingine, au kuonesha kuwa na manufaa zaidi kwa thamani ya matumizi ya fedha. Katika muktadha ambapo

rasilimali hazitoshelezi, ni muhimu kupima ushahidi uliopo kwa uangalifu zaidi ili kutambua kile kinachoweza

kuchangia zaidi katika kuleta mafanikio.

Matokeo ya Uwezo yanatoa uelekezi kidogo kuhusu mambo yanayoweza kufanyika ili kusukuma mbele maendeleo.

Kwanza, kuwepo kwa uhusiano mdogo kati ya wiano za mwanafunzi:mwalimu na mwanafunzi:darasa na kujifunza

ni taarifa muhimu, kwa kuwa inauliza swali iwapo vitendea kazi na fedha katika maeneo haya vitakuwa suluhisho

katika kukabili hali ya hatari iliyopo. Huu ni wakati muafaka wa kushughulikia ubora wa ufundishaji na vichocheo na

motisha kwa walimu. Licha ya yote, inawezekana kabisa kwamba sababu mojawapo ya watoto wanaokwenda shule

kujifunza kidogo inatokana na motisha zisizowaridhisha walimu, mahudhurio ya walimu shuleni yakiwa hafifu pia.

Kwa mfano, ushahidi kutoka Tanzania unaonesha kwamba asilimia 23 ya walimu hawahudhurii shuleni kila siku na

hata wanapokuwa shuleni, walimu wanatumia karibu nusu ya muda wao nje ya madarasa. Matokeo yake watoto

wanafundishwa kwa masaa mawili tu na dakika nne kwa siku, badala ya masaa matano yanayotarajiwa. 109 Tafiti katika

nchi za Uganda na Kenya zinabaini kuwepo kwa hali inayofanana na ya Tanzania.

9

Worldbank Service Delivery Indicators:Education and Health Care in Africa,iliyowasilishwa REPOA, Machi 4,2011

Je Watoto Wetu Wanajifunza? 24

Tofauti zilizoonekana katika kiwango cha ufaulu wa wanafunzi miongoni mwa wilaya ndani ya kila nchi hizi tatu,

na baina ya shule za serikali na zile za binafsi, zinaashiria kwamba baadhi ya shule ‘zimetafuta’ namna ya kupata

matokeo mazuri katikati ya vikwazo vilivyopo. Tukichunguza kwa nini baadhi ya wilaya, na ndani ya wilaya baadhi ya

shule zinafanya vizuri kuliko nyingine huenda tukapata dokezo kuhusu mambo ya msingi zaidi yanayotakiwa kufanywa

ili kuboresha ujifunzaji.

Mbinu rahisi na isiyo na gharama kubwa ingekuwa kuanza kwa kubainisha ni shule zipi zinafanya vizuri (au vibaya)

kuliko inavyotarajiwa ikilinganishwa na rasilimali zilizopo, kuzitembelea shule hizi na kubainisha mambo yale

yanayoweza kueleza matokeo yao, na kutokana na ziara hizi, kuweza kujifunza yale mambo ya msingi yanayofanana.

Mbinu nyingine zinaweza kutumika. Kuna ushahidi mwingi kutoka Kenya unaotokana na tafiti za kimajaribio,

unaoonesha kwamba programu zilizoongeza vitendea kazi vya shule kwa kiasi kikubwa hazikuleta matokeo

yaliyotarajiwa katika ufanisi. Kwa mfano kuongeza vitabu na vifaa vya walimu kuandikia, havikusaidia kuongeza ubora

wa uwezo wa wanafunzi, na kupunguza ukubwa wa darasa kwa kuongeza walimu vilevile hakukubadilisha matokeo.

1110

Hatua zilizoongeza viwango vya ufaulu wa wanafunzi shuleni ni zile zilizobadili vichocheo kwa walimu kwa namna

inayoridhisha. Hatua ya kuwalipa walimu kwa kuhudhuria kazini au kwa maksi za mitihani walizopata wanafunzi wao

zilionesha matokeo mchanganyiko, na utaratibu wa kuwapa wazazi taarifa kuhusu hali ya shule vilevile haikuwa na

manufaa. Lakini, programu zilizowezesha shule kuajiri walimu zaidi kwa mikataba ya muda mfupi na zile zilizozipa

kamati za shule mamlaka juu ya walimu zilifanikiwa kuongeza viwango vya ufaulu wa wanafunzi. Kujaribu mbinu hizi

mpya, kwa kutumia utaratibu wa majaribio yanayosimamiwa vizuri, kunaweza kuwa njia mojawapo ya kuhamasisha

kuimarisha ujifunzaji katika shule.

Mbinu mojawapo kama hiyo, ambayo bado haijathibitishwa lakini mpango wake umeundwa kutokana na ushahidi

kuhusu mbinu zinazoweza kuwa na matokeo yenye ufanisi, unaitwa malipo baada ya matokeo (Cash on Delivery) 1211 .

Wazo kuu hapa ni kwamba badala ya kugharimia vitendea kazi, kuundwe mfumo ambao malipo yatatolewa

kwa kufuata ufanisi katika viashiria vya matokeo vilivyoanishwa na kuthibitishwa, kwa mfano, dola 50 kwa kila

mwanafunzi atakayemaliza Darasa la 2 akiwa amefaulu kwa asilimia 80 katika stadi za kusoma na kuhesabu. Mbinu hii

awali ilibuniwa ili kuboresha ufanisi katika misaada iliyotolewa kwa serikali za kitaifa, lakini huenda mbinu hii ikawa

na manufaa zaidi katika namna serikali za kitaifa zinavyounda vichocheo vyake ili kuboresha ufaulu katika ngazi za

wilaya na shule.

Kuna hali ya hatari katika ujifunzaji Kenya, Tanzania na Uganda. Serikali zinajivunia mafanikio yake katika kupanua

uandikishaji wa wanafunzi. Lakini vilevile sasa zisijifiche nyuma ya mafanikio haya, ila badala yake ziweke malengo

yake katika kuhakikisha kwamba watoto wanapokwenda shule wanajifunza. Ushahidi kutoka mapitio mbalimbali

na tafiti za kimajaribio zilizofanywa kwa umakini, pamoja na data za Uwezo zilizowasilishwa katika ripoti hii

zinabaini kwa kiasi kikubwa kwamba kuwekeza katika vitendea kazi pekee hakutoshi, na kwamba fikra mpya

zinahitajika kuhusu suala la vichocheo 1312 . Mabilioni ya shilingi na masaa yanayotumiwa katika elimu ya msingi kila

mwaka na wazazi, serikali na wafadhili yatakuwa yametumika vizuri iwapo watoto watajifunza, na kupata stadi

katika kusoma na kuhesabu. Huu ni wakati wa kulikabili sakata hili ipasavyo, na kufikiri kuhusu suluhisho linalofaa

ambalo si tu lina lengo jema, bali linaweza pia kuleta mabadiliko chanya.

10

“Improving Education in the Developing World: What have we Learned from Randomized Evaluations?” Michael Kremer na Alaka Holla,Novemba 10,2008.

Inapatikana

http://www.economics.harvard.edu/faculty/kremer/files/Annual_Review_081110%20-%20NO%20TRACK%20CHANGES.pdf.

11

Wazo hili lilibuniwa na Centre for Global Development, angalia katika

http://www.cgdev.org/section/initiative/_active/codaid. For a comment on its strength and value in local application

Angalia :http://blogs.cgdev.org/globaldevelopment/2011/04/guest-post-five-reason-i-am-a-fan-of-cash-on-delivery-and-five-ways-to-make-it-sharper.php

12

Mathalan, angalia http://siteresources.worldbank.org/EDUCATION/Resources/278200-1298568319076/makingschoolwork.pdf na thamani ya mbinu za kitafiti

angalia Banerjee, A and Duflo, E, Poor Economics:A radical rethinking of the way to fight global poverty, Public Affairs,2011, sana katika sura ya 4.

Kuhesabu na Kusoma Katika Afika Mashariki 25

Kiambatisho cha 1: Ngazi za Wilaya

Jina la wilaya Viashiria vya uwezo wa wanafunzi Viashiria vya upatikanaji nyenzo shuleni

Ufaulu Darasa

la 3

Ufaulu Darasa

la 3

Uandikishaji

Nafasi ya

ufaulu (*)

Uwiano wa

wanafunzi

kwa

mwalimu

Uwiano wa

wanafunzi

kwa darasa

Uwiano wa

wanafunzi

kwa choo

Nafasi ya

shule (*)

Adjumani 0% 93% 89% 107 66 57 47 78

Amuria 2% 60% 93% 76 69 100 89 131

Amuru 2% 67% 89% 112 70 117 76 130

Apac 3% 80% 89% 94 69 97 65 119

Babati 3% 58% 92% 78 58 58 42 72

Budaka 3% 62% 91% 97 69 101 87 132

Bukoba Vijijini 1% 39% 82% 130 64 78 47 90

Bukoba Mjini 6% 36% 86% 117 36 73 62 71

Buliisa 2% 84% 92% 66 67 173 112 134

Bundibugyo 1% 49% 94% 98 65 83 108 124

Bungoma Kaskazini 7% 78% 91% 48 42 61 31 51

Bunyala 9% 83% 82% 79 43 68 37 55

Buret 25% 85% 81% 46 34 96 81 92

Bushenyi 4% 67% 91% 81 40 47 45 50

Busia 9% 80% 95% 21 48 88 49 88

Busia 2% 79% 87% 109 64 93 90 125

Butere 11% 77% 91% 39 40 45 37 39

Chunya 10% 55% 82% 115 56 73 50 83

Eldoret Mashariki 26% 92% 93% 4 28 34 36 11

Gatanga 38% 89% 94% 1 41 34 14 16

Geita 6% 59% 81% 120 83 108 92 133

Gucha 30% 95% 89% 8 43 57 40 54

Gulu 0% 90% 93% 73 59 78 63 100

Hamis 20% 84% 91% 17 37 39 53 45

Ibanda 3% 66% 91% 91 42 52 54 60

Igembe 11% 91% 89% 26 45 44 24 36

Ijara 19% 94% 79% 44 41 50 154 82

Ilemela 13% 68% 81% 105 87 140 107 135

Iment Kusini 38% 85% 88% 18 25 29 23 1

Imenti Kaskazini 36% 95% 89% 5 28 23 14 4

Kabale 2% 56% 94% 75 41 53 59 61

Kakamega Kati 14% 80% 88% 52 44 90 39 74

Kakamega Kaskazini 14% 79% 79% 85 35 44 45 34

Kaloleni 34% 95% 72% 31 60 59 104 109

Kamuli 0% 74% 92% 95 66 86 110 127

Karagwe 2% 24% 87% 128 65 78 53 99

Kasulu 4% 18% 79% 129 90 77 67 116

Katakwi 0% 88% 95% 64 63 89 84 121

Je Watoto Wetu Wanajifunza? 26

Jina la wilaya Viashiria vya uwezo wa wanafunzi Viashiria vya upatikanaji nyenzo shuleni

Ufaulu Darasa

la 3

Ufaulu Darasa

la 3

Uandikishaji

Nafasi ya

ufaulu (*)

Uwiano wa

wanafunzi

kwa

mwalimu

Uwiano wa

wanafunzi

kwa darasa

Uwiano wa

wanafunzi

kwa choo

Nafasi ya

shule (*)

Keiyo 24% 90% 83% 34 28 58 27 23

Kericho 18% 94% 85% 32 28 35 30 6

Kibaale 2% 82% 87% 113 65 107 70 123

Kibaha 7% 35% 90% 102 37 53 58 56

Kibwezi 21% 90% 91% 9 33 37 40 24

Kikuyu 53% 87% 94% 3 35 31 25 8

Kilifi 19% 96% 70% 42 57 59 68 91

Kilombero 2% 43% 91% 106 55 81 80 112

Kilosa 0% 36% 89% 124 53 85 68 108

Kinondoni 6% 48% 92% 77 38 83 120 98

Kisarawe 1% 46% 91% 114 45 41 29 38

Kisii Kusini 14% 84% 84% 58 39 45 42 41

Kisumu Magharibi 7% 81% 87% 72 35 38 59 46

Kitui Kaskazini 19% 95% 91% 7 49 39 36 47

Koibatek 16% 89% 86% 38 32 32 46 19

Kongwa 4% 46% 91% 100 59 91 82 120

Kotido 1% 14% 44% 134 92 92 52 115

Kuria East 10% 83% 84% 70 52 51 66 81

Kyenjojo 2% 78% 90% 93 64 78 65 107

Kyuso 10% 92% 79% 63 36 36 49 31

Lagdera 2% 69% 82% 118 64 38 65 76

Laikipia Kaskazini 34% 79% 61% 62 38 161 35 65

Lamu 18% 88% 91% 15 32 31 43 17

Lari 17% 59% 93% 22 37 33 13 13

Limuru 23% 66% 87% 50 42 41 78 68

Liwale 0% 16% 79% 135 57 61 50 79

Loitoktok 25% 82% 83% 51 50 46 34 52

Makueni 15% 87% 90% 24 33 37 39 21

Mandera Kati 12% 83% 74% 86 51 47 58 73

Manga 27% 91% 89% 11 31 35 31 12

Marakwet 17% 91% 87% 33 30 33 53 29

Masaba 21% 82% 92% 13 31 38 33 15

Masaka 7% 76% 92% 53 49 67 75 96

Maswa 4% 33% 84% 125 54 61 79 97

Mayuge 1% 61% 93% 87 64 99 100 128

Mbeere 35% 94% 92% 2 27 28 17 2

Mbeya Mjini 0% 50% 95% 99 40 46 51 53

Mbulu 13% 68% 84% 101 45 62 68 85

Meru Kusini 23% 95% 91% 6 28 25 17 3

Misungwi 4% 34% 91% 108 65 68 53 94

Kuhesabu na Kusoma Katika Afika Mashariki 27

Jina la wilaya Viashiria vya uwezo wa wanafunzi Viashiria vya upatikanaji nyenzo shuleni

Ufaulu Darasa

la 3

Ufaulu Darasa

la 3

Uandikishaji

Nafasi ya

ufaulu (*)

Uwiano wa

wanafunzi

kwa

mwalimu

Uwiano wa

wanafunzi

kwa darasa

Uwiano wa

wanafunzi

kwa choo

Nafasi ya

shule (*)

Molo 14% 87% 90% 29 42 45 41 49

Morogoro Vijijini 1% 25% 80% 133 48 67 66 89

Morogoro Mjini 9% 32% 92% 82 49 72 78 101

Moshi Vijijini 16% 54% 87% 92 30 49 33 25

Moshi Mjini 27% 72% 89% 43 41 94 85 106

Moyale 12% 89% 83% 59 56 48 69 86

Mpanda 2% 40% 89% 119 44 90 68 103

Mpwapwa 7% 48% 89% 103 65 87 53 104

Mubende 2% 69% 91% 89 59 76 78 110

Mukono 2% 69% 88% 111 43 65 68 84

Muleba 1% 22% 84% 131 91 83 79 126

Musoma Mjini 13% 52% 91% 68 48 86 66 102

Mwala 14% 82% 93% 19 31 49 25 20

Mwanga 1% 17% 89% 127 45 44 28 40

Naivasha 41% 85% 86% 23 44 78 39 64

Nakapiripirit 2% 90% 65% 123 85 78 55 111

Nakasongoria 5% 78% 94% 49 42 55 55 63

Nakuru Kaskazini 31% 88% 84% 27 36 42 21 22

Nandi Kati 17% 87% 83% 54 33 63 39 44

Nandi Mashariki 32% 91% 88% 14 28 48 37 26

Nandi Kaskazini 37% 96% 85% 12 27 35 38 14

Narok Kaskazini 28% 91% 74% 40 37 52 35 35

Newala 2% 34% 91% 116 78 54 44 80

Ngara 5% 38% 83% 122 69 76 79 118

Njombe 6% 52% 87% 110 65 60 40 75

Nyandarua Kaskazini 18% 79% 89% 35 35 33 17 7

Nyeri Kusini 35% 93% 88% 10 33 28 14 5

Pokot Kaskazini 37% 83% 47% 56 43 93 64 95

Rachuonyo 9% 75% 88% 69 38 63 48 58

Rakai 3% 65% 93% 71 45 69 72 93

Rombo 20% 70% 91% 36 47 68 42 69

Ruiru 27% 80% 84% 45 45 43 29 37

Rukingiri 5% 76% 92% 60 70 80 64 113

Samburu Kati 18% 66% 65% 96 34 35 45 28

Samburu Kaskazini 8% 97% 69% 65 34 31 49 27

SamburuMashariki 5% 95% 56% 88 35 38 57 43

Shinyanga Vijijini 1% 27% 82% 132 71 76 82 122

Singida Vijijini 1% 39% 88% 126 68 66 48 87

Singida Mjini 4% 44% 84% 121 39 74 53 70

Sotik 12% 85% 91% 25 35 57 60 57

Je Watoto Wetu Wanajifunza? 28

Jina la wilaya Viashiria vya uwezo wa wanafunzi Viashiria vya upatikanaji nyenzo shuleni

Ufaulu Darasa

la 3

Ufaulu Darasa

la 3

Uandikishaji

Nafasi ya

ufaulu (*)

Uwiano wa

wanafunzi

kwa

mwalimu

Uwiano wa

wanafunzi

kwa darasa

Uwiano wa

wanafunzi

kwa choo

Nafasi ya

shule (*)

Suba 24% 90% 85% 28 36 38 47 32

Sumbawanga 11% 45% 92% 67 70 101 54 117

Taita 31% 86% 89% 16 38 35 25 18

TanaRiver 17% 92% 66% 57 41 40 70 62

Tanga 6% 29% 93% 84 48 142 59 105

Taveta 23% 88% 86% 30 46 45 59 66

Tharaka 20% 76% 89% 37 29 29 39 9

Thika Magharibi 19% 77% 88% 47 32 66 38 42

Trans Mara 6% 81% 80% 104 41 83 53 77

Trans Nzoia Mashariki 16% 91% 84% 41 37 57 30 33

Urambo 4% 52% 92% 80 86 110 69 129

Wajir Mashariki 7% 92% 84% 55 48 42 63 67

Wajir Kaskazini 21% 69% 52% 83 43 34 51 48

Wakiso 8% 76% 91% 61 40 58 51 59

Wareng 20% 78% 75% 74 31 35 31 10

West Pokot 24% 98% 84% 20 33 40 43 30

Yumbe 0% 78% 92% 90 54 84 80 114

Angalizo: Wilaya za Kenya ni buluu, wilaya za Uganda ni kijani, wilaya za Tanzania ni nyekundu

(*) Faharasa hizi hizi mbili zimetengeneza kwa kujumlisha alama zinazoambatana na nafasi ya wilaya kwa kila kimoja ya viashiria

vitatu vilivyozingatiwa, na kutengeneza faharasa nyingine inayoonesha nafasi ya jumla kuanzia ya chini kabisa hadi ya juu kabisa.

Chanzo cha data: Uwezo

Kuhesabu na Kusoma Katika Afika Mashariki 29

Serikali za Kenya, Uganda na Tanzania zinatekeleza sera za elimu ya msingi kwa wote kuwawezesha watoto

wote kwenda shule na angalau wajue kusoma, kuandika na kufanya hesabu. Katika muongo uliopita nchi hizi

zimeongeza sana bajeti zao za elimu na mafanikio makubwa yameonekana katika kuandikisha wanafunzi.

Lakini wakati watoto wengi sasa wanakwenda shule, je wanajifunza?

Uwezo ilifanya taftishi katika nchi hizi tatu, kwa kuwatembelea maelfu ya watoto majumbani kwao, na

kuwapa majaribio ya kiwango cha darasa la pili kwa somo la Kiingereza, Kiswahili na Hisabati. Watoto

wengi sana walishindwa majaribio haya. Katika nchi zote tatu watoto walipata matokeo ya chini sana

ikilinganishwa na kiwango kinachotarajiwa katika mitaala ya nchi zao. Katika mazoezi yote matatu watoto

wa Kenya walikua juu wakifuatiwa na Uganda.

Nini huchochea ujifunzaji? Taftishi ya Uwezo imegundua vitu vya kushangaza. Hali bora ya uchumi wa

familia imeonekana kushabihiana na umahiri au werevu wa watoto katika stadi za msingi; watoto kutoka

katika familia zenye hali nzuri walifanya vizuri zaidi. Jinsia ya mtoto haikuonekana kuwa na uhusiano na

werevu wa mtoto. Matokeo toka shule binafsi yalileta sura mchanganyiko; zaidi ya kuongeza ufahamu wa

lugha ya Kiingereza katika madarasa ya chini wanafunzi toka shule za binafsi hawakuonesha tofauti kubwa

ya umahiri katika stadi za msingi. Kwa watunga sera matokeo muhimu zaidi ni kuwa uwekezaji katika

miundombinu na uwiano wa mwalimu na wanafunzi si muarobaini wa kuboresha ufahamu wa wanafunzi.

Watoto toka maeneo yenye shule zenye majengo bora hawakufanya vizuri kupindukia kuwazidi wale

wanaosoma shule zenye miundombinu hafifu ama waliorundikana madarasani. Hivyo basi, wazazi, serikali

na wahisani wanaweza tu kujiridhisha kuwa mabilioni ya shilingi wanazowekeza kila mwaka kwenye sekta ya

elimu yametumika vizuri iwapo watoto wakimaliza shule wataingia kutika dunia yenye ushindani wakiwa na

ufahamu wa kiwango cha juu wa kusoma, wakijua Hisabati na wakijiamini.

Uwezo Uwezo Afrika East Africa Mashariki (managed (ikisimamiwa by Twaweza) na Twaweza)

S.L.P. P.O Box 19875, 19875, 00200 00200 Nairobi, Nairobi, Kenya Kenya

Simu: Tel: +254 20 3861372

Baruapepe: Email: info@uwezo.net. Web: Tovuti: www.uwezo.net

Twaweza Afrika East Africa Mashariki

127 Mtaa Mafinga wa Mafinga, Rd, Off Kando Kinondoni ya barabara Rd ya Kinondoni

S.L.P. P.O Box 38342, 38342, Dar es Dar Salaam, es Salaam, Tanzania. Tanzania

Simu: Tel: +255 22 266 4301. Nukushi: Fax +255 +255 22 266 22 266 43084308.

Barua Email: pepe: info@twaweza.org. Web: Tovuti: www.twaweza.org

Barua Email: pepe: info@uwazi.org. Web: Tovuti: www.uwazi.org

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!