SEHEMU YA SITA 49

amani na utulivu bungeni amani na utulivu bungeni

parliament.go.tz
from parliament.go.tz More from this publisher
30.08.2015 Views

. SEHEMU YA SITA AMANI NA UTULIVU BUNGENI 72.-(1) Spika atakuwa na wajibu wa kuhakikisha kuwa, utaratibu bora unafuatwa Bungeni, na uamuzi wa Spika kuhusu jambo lolote la utaratibu utakuwa ni wa mwisho. (2) Mbunge atakayekiuka utaratibu uliowekwa na Kanuni hizi anaweza papo hapo kutakiwa na Spika afuate utaratibu na vilevile Mbunge mwingine yeyote anaweza kusimama na kumfahamisha Spika kuhusu ukiukwaji wa utaratibu huo na katika kufanya hivyo, atalazimika kutaja Kanuni ya Bunge iliyoweka utaratibu uliokiukwa. Mamlaka ya Spika kusimamia utaratibu 49

SEHEMU YA SITA

AMANI NA UTULIVU BUNGENI

72.-(1) Spika atakuwa na wajibu wa kuhakikisha kuwa, utaratibu

bora unafuatwa Bungeni, na uamuzi wa Spika kuhusu jambo lolote

la utaratibu utakuwa ni wa mwisho.

(2) Mbunge atakayekiuka utaratibu uliowekwa na Kanuni hizi

anaweza papo hapo kutakiwa na Spika afuate utaratibu na vilevile

Mbunge mwingine yeyote anaweza kusimama na kumfahamisha

Spika kuhusu ukiukwaji wa utaratibu huo na katika kufanya hivyo,

atalazimika kutaja Kanuni ya Bunge iliyoweka utaratibu uliokiukwa.

Mamlaka

ya

Spika

kusimamia

utaratibu

49

(3) Endapo Mbunge yeyote atatakiwa kuthibitisha ukweli wa jambo

au suala alilolisema Bungeni na hadi kufikia mwisho wa muda

aliopewa amekataa au ameshindwa kutoa uthibitisho huo, Spika

anaweza kumsimamisha Mbunge huyo kuhudhuria vikao vya Bunge

visivyozidi vitano.

(4) Endapo Mbunge atafanya kosa ambalo alikwishawahi

kuadhibiwa kwa mujibu wa fasili ya (2) na (3) ya Kanuni hii, Spika

atalipeleka suala lake kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka

ya Bunge kwa mujibu wa masharti ya Kanuni ya 71 ya Kanuni hizi ili

Kamati hiyo ilishauri Bunge kuhusu hatua za kinidhamu zinazostahili

kuchukuliwa dhidi ya Mbunge huyo.

Adhabu

zinazoweza

kutolewa

na

Spika

kwa

ukiukaji

wa

Kanuni

73.-(1) Mbunge au Waziri atakayezungumzia jambo au mambo

ambayo hayaruhusiwi na Kanuni hizi, anaweza kuamriwa na Spika

au Naibu Spika au Mwenyekiti akatishe hotuba yake na kukaa mahali

pake.

(2) Endapo Mbunge au Waziri atatumia maneno au lugha

isiyotakiwa Bungeni, yaani lugha ya matusi, usafihi, uchokozi au

lugha ya maudhi na akitakiwa na Spika ajirekebishe kwa kufuta

maneno au lugha hiyo atakataa kufanya hivyo, Spika anaweza

kumwamuru Mbunge huyo atoke mara moja nje ya Ukumbi wa

Bunge na abaki huko nje kwa muda wote uliosalia wa kikao cha

siku hiyo.

(3) Endapo Mbunge yeyote atatakiwa kuthibitisha ukweli wa

maneno aliyoyasema na hadi kufikia mwisho wa muda aliopewa,

amekataa au ameshindwa kutoa uthibitisho huo, Spika anaweza

kumsimamisha Mbunge huyo asihudhurie vikao vya Bunge

visivyozidi vitano.

(4) Endapo Mbunge atafanya kosa ambalo alikwishawahi

kuadhibiwa kwa mujibu wa fasili ya (2) na (3) ya Kanuni hii, Spika

atalipeleka suala lake kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka

ya Bunge ili Kamati hiyo ilishauri Bunge kuhusu adhabu inayostahili

kutolewa kwa Mbunge mhusika.

Adhabu

zinazoweza

kutolewa

na

Bunge

kwa

ukiukaji

wa

Kanuni

74.-(1) Spika anaweza kutaja jina la Mbunge kwamba amedharau

Mamlaka ya Spika na kisha kupeleka jina hilo kwenye Kamati ya

Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge ikiwa:-

(a)

kwa maneno au vitendo, Mbunge huyo

anaonesha dharau kwa mamlaka ya Spika; au

50

(b)

Mbunge huyo atafanya kitendo chochote cha

makusudi cha kudharau Shughuli ya Bunge au

Mbunge yeyote anayeongoza shughuli hiyo.

(2) Ikiwa maneno au vitendo vya Mbunge vilivyoainishwa katika

fasili ya (1) ya Kanuni hii vimetokea wakati Bunge likiwa katika

Kamati ya Bunge Zima, basi Mwenyekiti atasimamisha shughuli za

Kamati na ataagiza Bunge kurudia ili kumpatia Spika fursa ya kutoa

taarifa kwa Bunge kuhusu mwenendo wa Mbunge huyo na

kuwasilisha suala hilo kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka

ya Bunge.

(3) Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge itajadili suala

hilo na ikithibitika kuwa Mbunge husika ametenda kosa inaweza

kushauri kwamba:-

(a)

(b)

ikiwa ni kosa lake la kwanza Mbunge huyo

asihudhurie vikao vya Bunge visivyozidi kumi; au

ikiwa ni kosa lake la pili au zaidi Mbunge huyo

asihudhurie vikao vya Bunge visivyozidi ishirini;

(4) Bunge linaweza kuzingatia ushauri mwingine wowote

utakaotolewa na Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge

kuhusu adhabu anayostahili kupewa Mbunge aliyekiuka masharti

ya Kanuni hii.

(5) Bila ya kujali masharti ya fasili ya (4) ya Kanuni hii, Bunge linaweza

kumchukulia hatua nyinginezo za kinidhamu, ikiwa ni pamoja na

kumsimamisha kazi Mbunge yeyote aliyetenda kosa chini ya Kanuni

hii.

(6) Adhabu yoyote itakayotolewa kwa Mbunge aliyekiuka masharti

ya Kanuni hii itatolewa kupitia Azimio la Bunge ambalo litataja

adhabu hiyo pamoja na sababu zake.

75.- Mbunge aliyesimamishwa kazi atatoka katika Bunge na

hataingia tena katika sehemu yoyote ya Ukumbi wa Bunge na

maeneo ya Bunge kwa muda wote atakapokuwa amesimamishwa,

na atalipwa nusu mshahara na nusu posho zinazoambatana na

mshahara huo.

76.-(1) Kwa madhumuni ya kudhibiti fujo endapo itatokea ndani ya

Ukumbi wa Bunge na Spika ataona kuwa kuna haja ya kutumia

51

Masharti

kwa

Mbunge

aliyesimamishwa

kazi

Udhibiti

wa fujo

Bungeni

nguvu, basi anaweza kuahirisha Shughuli za Bunge bila ya hoja

yoyote kutolewa au kusitisha kikao kwa muda atakaoutaja ili fujo

hiyo iweze kudhibitiwa na Mpambe wa Bunge.

(2) Baada ya utulivu kurudia, Spika atalipeleka kwenye Kamati ya

Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge suala ambalo lilisababisha

kutokea kwa fujo ikiwa ni pamoja na jina la Mbunge au majina ya

Wabunge waliohusika na fujo hiyo ili Kamati hiyo iweze kulishauri

Bunge kuhusu adhabu inayostahili kutolewa.

52

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!