1 hotuba ya waziri mkuu, mheshimiwa mizengo peter pinda (mb)

1 hotuba ya waziri mkuu, mheshimiwa mizengo peter pinda (mb) 1 hotuba ya waziri mkuu, mheshimiwa mizengo peter pinda (mb)

parliament.go.tz
from parliament.go.tz More from this publisher
30.08.2015 Views

Check Against Delivery Serikali itaendelea kusimamia mafanikio hayo na kuchukua hatua zaidi zitakazoongeza usindikaji wa ngozi hapa Nchini. Sekta ya Utalii 58. Mheshimiwa Spika, Serikali imeandaa Mpango Mkakati wa kuifanya Mikoa ya Dar es Salaam, Lindi, Mtwara na Tanga kuwa vituo vya utalii wa fukwe. Mikoa hiyo ina fukwe za kipekee zinazovutia watalii na pia zinafaa kwa uwekezaji wa kitalii. Vilevile, Serikali imevitangaza vivutio vya utalii katika soko la ndani na nje ya nchi kupitia Vyombo vya Habari na maonesho ya ndani na Kimataifa. Kutokana na hatua hiyo, idadi ya Watalii walioingia nchini mwaka 2012 imeongezeka na kufikia watalii 930,753 ikilinganishwa na watalii 867,994 mwaka 2011. Aidha, mapato yatokanayo na utalii yameongezeka kutoka Shilingi Bilioni 2,119 mwaka 2011 hadi Shilingi Bilioni 2,183 mwaka 2012. 59. Mheshimiwa Spika, matunda ya juhudi za kutangaza vivutio vya utalii na pia kuhamasisha utalii wa ndani yamedhihirika baada ya Taasisi ya The Seven Natural Wonders yenye Makao yake Nchini Marekani kuijumuisha Tanzania katika zoezi la kutafuta Maajabu Saba ya Asili katika Bara la Afrika. Zoezi hilo lilishirikisha wataalam wengi Duniani na kupigiwa kura na watu kutoka sehemu mbalimbali, wakiwemo Watanzania kwa kutumia Tovuti. Matokeo ya zoezi hilo yalitangazwa tarehe 11 Februari 2013, Jijini Arusha, ambapo Tanzania iliibuka mshindi kwa vivutio vitatu vya Maajabu Saba ya Asili ya Afrika yakijumuisha Mlima Kilimanjaro, Ngorongoro Crater na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti. Napenda kutumia fursa hii kuwashukuru Watanzania wote wa ndani na nje ya Nchi walioshiriki kupiga kura na hatimaye kutuwezesha kupata ushindi huo. Aidha, namshukuru Dkt. Philip Imler ambaye ni mwanzilishi wa Taasisi ya The Seven Natural Wonders aliyesimamia zoezi hilo. Pia, nayashukuru Makampuni yote yaliyofadhili mashindano hayo na kutangaza vivutio vya Tanzania Barani Afrika na Duniani kote. Natoa wito kwa Watanzania wote kuhakikisha kwamba tunavilinda, tunavitunza na kuviendeleza vivutio hivyo kwa manufaa ya Taifa letu. Tutumie pia ushindi huo kutangaza zaidi utalii wetu ili rasilimali hizi nzuri tulizo nazo ziendelee kuvutia watalii wengi na kuongeza mapato yetu. Sekta ya Madini 60. Mheshimiwa Spika, wachimbaji wadogo wa madini wana mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa Nchi yetu. Ili kuwaendeleza wachimbaji hao, Serikali imekamilisha Mkakati, Mpango Kazi na Programu ya Mafunzo pamoja na kuwatengea maeneo wachimbaji wadogo kwa mujibu wa Sheria. Maeneo hayo ni Mpambaa (Singida), Kilindi (Tanga), Dete na Melela (Morogoro), Winza (Dodoma), Songwe (Mbeya), Nyakunguru (Mara), Nyamilonge na Ilagala (Kigoma), Mihama (Katavi), Mwajanga (Manyara), Makanya (Kilimanjaro) na Mbesa (Ruvuma). Aidha, Serikali imekusanya takwimu na taarifa muhimu za wachimbaji wadogo kote Nchini kwa lengo la kuwatambua, kufahamu changamoto walizonazo na kujenga kanzidata (database). 61. Mheshimiwa Spika, Tanzania imekuwa Mwanachama kamili wa Mpango wa Kimataifa Unaohimiza Uwazi katika Sekta ya Madini (Extractive Industries Transparency Initiatives- EITI) baada ya kutimiza vigezo vilivyowekwa kimataifa katika Sekta ya Madini. Hatua hiyo imeiwezesha Tanzania kuwa na mfumo thabiti wa utoaji taarifa za malipo na mapato kutoka katika kampuni zinazojishughulisha na uchimbaji wa Madini, Gesi Asilia na Mafuta ambao unamwezesha mwananchi kufahamu na kujadili mchango wa Kampuni hizo katika Pato la Taifa. 14

Check Against Delivery Katika mwaka 2013/2014, Serikali itaimarisha ukaguzi kwenye uzalishaji na biashara ya madini pamoja na kuimarisha STAMICO ili itekeleze majukumu yake kikamilifu. HALI YA AJIRA NCHINI 62. Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua umuhimu wa kuongeza fursa za ajira kwa vijana wengi wanaoingia kwenye soko la ajira kila mwaka. Kwa mujibu wa matokeo ya Utafiti wa Ajira na Kipato Nchini wa mwaka 2010/2011, Ajira ziliongezeka kutoka 1,276,982 mwaka 2010 hadi Ajira 1,362,559 mwaka 2011, sawa na ongezeko la Asilimia 6.7. Ili kuongeza kasi ya ukuaji wa ajira, Serikali inakamilisha Programu ya Kitaifa ya Kukuza Ajira kwa Vijana. Programu hiyo ya miaka mitatu itaongeza fursa za Vijana 301,100 kuweza kujiajiri au kuajiriwa. Msukumo zaidi utawekwa katika Miradi ya Kilimo, Viwanda Vidogo, Maeneo Maalum ya Kiuchumi (EPZ na SEZ), Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano. Sambamba na hatua hiyo, Serikali itaendelea kutoa mafunzo ya ujasiriamali kwa wanafunzi wa Vyuo vya Ufundi na vya Elimu ya Juu ili kuwawezesha kujiajiri baada ya kuhitimu mafunzo yao. HUDUMA ZA KIUCHUMI Ardhi 63. Mheshimiwa Spika, pamoja na Nchi yetu kuwa na ardhi ya kutosha na inayofaa kwa Kilimo na uwekezaji mwingine, bado hatujakamilisha zoezi la uwekaji mipaka, kupima na kutoa Hati kwa matumizi mbalimbali. Hali hiyo inachangia migogoro ya ardhi na kukwamisha uwekezaji kwa kiasi kikubwa. Serikali imechukua hatua muhimu kwa kutumia teknolojia ya kisasa itakayoharakisha zoezi la upimaji ardhi. Katika kutekeleza kazi hiyo, Awamu ya Kwanza ya usimikaji wa Mtandao wa Alama za Msingi za Upimaji Ardhi Nchini (Geodetic Control Network) imekamilika. Mikoa iliyohusika ni Pwani, Morogoro, Mara, Mwanza, Kagera, Shinyanga, Lindi, Tabora na Dodoma. Tayari majaribio ya matumizi ya Alama hizo yamefanyika katika Wilaya za Ngorongoro na Kilombero na kudhihirisha kuwa gharama na muda wa kupima ardhi zimepungua. Awamu ya Pili ya usimikaji wa Alama hizo utaendelea katika Mikoa iliyobaki na kuanza upimaji wa viwanja na mashamba kwa kutumia utaratibu mpya wa upimaji wa ardhi. 64. Mheshimiwa Spika, ili kuwa na mfumo endelevu wa utunzaji wa kumbukumbu za ardhi, Serikali imeanza ujenzi wa Mfumo Unganishi wa Kuhifadhi Kumbukumbu za Ardhi. Mfumo huo utakaounganisha Ofisi za Ardhi Nchini unategemewa kukamilika mwaka 2014 na utaiwezesha Tanzania kuwa na kumbukumbu sahihi za ardhi. Vilevile, utaharakisha na kurahisisha utoaji wa maamuzi, upimaji na utoaji wa Hati Miliki na hivyo kupunguza migogoro ya ardhi. Katika mwaka 2013/2014, Serikali itaendelea na ujenzi wa Mfumo Unganishi wa Kuhifadhi Kumbukumbu za ardhi na kurahisisha upatikanaji wa ardhi kwa ajili ya uwekezaji. Nishati 65. Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea kusogeza huduma ya nishati ya umeme karibu na Wananchi ili kuharakisha maendeleo yao. Katika kutekeleza azma hiyo, gharama za kuunganisha umeme wa njia moja kwa wateja wadogo Vijijini na Mijini zimepunguzwa kwa wastani wa kati ya Shilingi Milioni 1,311,000 na Shilingi 114,000. Hatua hiyo imewezesha wananchi wengi kumudu gharama ya kuunganisha umeme na kuongeza kasi ya usambazaji umeme Nchini. Serikali pia, imefikisha umeme katika Makao Makuu ya Wilaya za Nkasi na Namtumbo, hivyo kufanya idadi ya Makao Makuu ya Wilaya zenye umeme kuwa 117, sawa na Asilimia 88 ya Wilaya zote Nchini. Vilevile, Serikali inatekeleza Programu Kabambe ya Kusambaza Umeme Vijijini ambapo wateja 8,046 wamelipiwa gharama za kuunganishiwa umeme kupitia Mfuko wa Nishati Vijijini. Aidha, kazi ya kusambaza na kuboresha miundombinu ya umeme katika Mikoa ya Mtwara na Lindi inaendelea kufanyika. 15

Check Against Delivery

Serikali itaendelea kusimamia mafanikio hayo na kuchukua hatua zaidi zitakazoongeza

usindikaji wa ngozi hapa Nchini.

Sekta ya Utalii

58. Mheshimiwa Spika, Serikali imeandaa Mpango Mkakati wa kuifanya Mikoa ya Dar es

Salaam, Lindi, Mtwara na Tanga kuwa vituo vya utalii wa fukwe. Mikoa hiyo ina fukwe za

kipekee zinazovutia watalii na pia zinafaa kwa uwekezaji wa kitalii. Vilevile, Serikali

imevitangaza vivutio vya utalii katika soko la ndani na nje ya nchi kupitia Vyombo vya Habari na

maonesho ya ndani na Kimataifa. Kutokana na hatua hiyo, idadi ya Watalii walioingia nchini

mwaka 2012 imeongezeka na kufikia watalii 930,753 ikilinganishwa na watalii 867,994 mwaka

2011. Aidha, mapato yatokanayo na utalii yameongezeka kutoka Shilingi Bilioni 2,119 mwaka

2011 hadi Shilingi Bilioni 2,183 mwaka 2012.

59. Mheshimiwa Spika, matunda ya juhudi za kutangaza vivutio vya utalii na pia

kuhamasisha utalii wa ndani yamedhihirika baada ya Taasisi ya The Seven Natural Wonders

yenye Makao yake Nchini Marekani kuijumuisha Tanzania katika zoezi la kutafuta Maajabu

Saba ya Asili katika Bara la Afrika. Zoezi hilo lilishirikisha wataalam wengi Duniani na kupigiwa

kura na watu kutoka sehemu mbalimbali, wakiwemo Watanzania kwa kutumia Tovuti.

Matokeo ya zoezi hilo yalitangazwa tarehe 11 Februari 2013, Jijini Arusha, ambapo Tanzania

iliibuka mshindi kwa vivutio vitatu vya Maajabu Saba ya Asili ya Afrika yakijumuisha Mlima

Kilimanjaro, Ngorongoro Crater na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti. Napenda kutumia fursa hii

kuwashukuru Watanzania wote wa ndani na nje ya Nchi walioshiriki kupiga kura na hatimaye

kutuwezesha kupata ushindi huo. Aidha, namshukuru Dkt. Philip Imler ambaye ni mwanzilishi

wa Taasisi ya The Seven Natural Wonders aliyesimamia zoezi hilo. Pia, nayashukuru

Makampuni yote yaliyofadhili mashindano hayo na kutangaza vivutio vya Tanzania Barani Afrika

na Duniani kote. Natoa wito kwa Watanzania wote kuhakikisha kwamba tunavilinda, tunavitunza

na kuviendeleza vivutio hivyo kwa manufaa ya Taifa letu. Tutumie pia ushindi huo kutangaza

zaidi utalii wetu ili rasilimali hizi nzuri tulizo nazo ziendelee kuvutia watalii wengi na kuongeza

mapato yetu.

Sekta ya Madini

60. Mheshimiwa Spika, wachimbaji wadogo wa madini wana mchango mkubwa katika

kukuza uchumi wa Nchi yetu. Ili kuwaendeleza wachimbaji hao, Serikali imekamilisha Mkakati,

Mpango Kazi na Programu ya Mafunzo pamoja na kuwatengea maeneo wachimbaji wadogo

kwa mujibu wa Sheria. Maeneo hayo ni Mpambaa (Singida), Kilindi (Tanga), Dete na Melela

(Morogoro), Winza (Dodoma), Songwe (Mbeya), Nyakunguru (Mara), Nyamilonge na Ilagala

(Kigoma), Mihama (Katavi), Mwajanga (Manyara), Makanya (Kilimanjaro) na Mbesa (Ruvuma).

Aidha, Serikali imekusanya takwimu na taarifa muhimu za wachimbaji wadogo kote Nchini kwa

lengo la kuwatambua, kufahamu changamoto walizonazo na kujenga kanzidata (database).

61. Mheshimiwa Spika, Tanzania imekuwa Mwanachama kamili wa Mpango wa Kimataifa

Unaohimiza Uwazi katika Sekta ya Madini (Extractive Industries Transparency Initiatives- EITI)

baada ya kutimiza vigezo vilivyowekwa kimataifa katika Sekta ya Madini. Hatua hiyo

imeiwezesha Tanzania kuwa na mfumo thabiti wa utoaji taarifa za malipo na mapato kutoka

katika kampuni zinazojishughulisha na uchimbaji wa Madini, Gesi Asilia na Mafuta ambao

unamwezesha mwananchi kufahamu na kujadili mchango wa Kampuni hizo katika Pato la Taifa.

14

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!