12.07.2015 Views

verbatim report of constituency public hearings ... - ConstitutionNet

verbatim report of constituency public hearings ... - ConstitutionNet

verbatim report of constituency public hearings ... - ConstitutionNet

SHOW MORE
SHOW LESS

You also want an ePaper? Increase the reach of your titles

YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.

11wakuu kwa sababu tunaona ya kwamba shule inataka ionekane kwenye magazeti ikiwa inaongoza. Kwa hivyo wakati mwingineunaona shule zingine zinafanya maovu kama kusajili au kuwa na vituo viwili katika shule moja. Unakuta ya kwamba walewanafunzi wazuri wanasajiliwa katika kituo fulani, wale ambao sio wazuri, wanaorodheshwa katika sehemu nyingine iliwasiharibu nafasi ya yule. Pia ni vizuri idadi ya wanafunzi ambao wanatakiwa kuwa katika darasa moja lipunguzwe ilikuhakikisha ya kwamba mwalimu anapata nafasi ya kuwahudumia wanafunzi barabara. Wakati mwingine tunaona ya kwambashule zetu sina idadi ya watoto ambao wanapita hamsini katika shule za msingiCom. Bishop Njoroge: - You should go to the point.Thomas Kagambi: Thank you. Asante, pia uteuzi wa waalimu wakuu utekelezwe kupitia ujuzi lakini sio jambo lingine lolote.Ningetaka pia kuzungumzia wasiobahatika katika jamii. Hawa ni raia kama wengine na Haki zao zinatakiwa kupewa kibaombele. Ni sharti pesa maalum zitengwe ili kujengwe makazi maalum ambapo wasio bahatika katika jamii watahudumiwa. Piatunapojenga miji, hospitali, makanisa na nyumba lazima tufikirie juu ya wale ambao ni walemavu, ili wapate nafasi ya kutembea,kuingia kwa nyumba au kanisa bila pingamizi ya vile ambavyo wameumbika.Ni vizuri pia wale ambao hawajabahatika katika jamii watengewe baadhi ya viti katika Bunge ili wawe na nafasi ya kutoa maoniyao na waakilishi wao. Wale ambao kwa kawaida huvunja sheria hasa ya hawa watu ambao hawabahatiki katika jamii, ni vizuriwachukuliwe hatua mwafaka kwa sababu jambo hili linaleta aibu wakati mwingine katika jamii yetu. Kuhusu siasa, ningetakakila MKenya apewe haki ya kupiga kura popote alipo.Pia kuna jambo hili la kujiandikisha kama mpiga kura tuseme sehemu hii, - Halafu baadaye ninasafiri kwenda Kisumu wakati wakupiga kura. Ninatakiwa nipewe ruhusa ya kupiga kura ya kumchagua Rais, kwa sababu hata kama kadi yangu ni ya sehemuhii, na niko Kisumu, bado sitakiwi kupigwa marafuku kupiga kura. Jambo lingine ni kuwa ni vizuri kura zihesabiwe katika vituovya kupigiwa na zitangazwe mara moja hapo bila kusafirishwa pahali pengine.Atakayechaguliwa Rais, ningependekeza awe ametimiza asilimia hamsini na mbili ili atangazwe Rais wa nchi. Jambo lingineambalo ningezungumzia, ni uhuru nchini. Kunatakiwa kuwe na uhuru wa kuanzishwa kwa vituo vya utangazaji bila mapendeleo.Shirika la utangazaji litumikie wanaKenya wote kwa sababu zote ni watu wa kodi. Pia umiliki wa mali uruhusiwe popote katikanchi hii. Sheria isitumiwe kubagua baadhi ya wanaKenya. Madaraka ya Rais yapunguzwe. Uteuzi wa nafasi muhimu, unapaswauidhinishwe na Bunge letu.Dini: Ni vizuri tuwe na uhuru wa kuabudu nchini mradi tu dini hizo ziwe zinatoa maadili mema ama mafunzo yanayozitahili. Pili,dini zisitumiwe kupotosha jamii. Dini hizo ni sharti zizajiliwe ili kuepusha vikundi ambavyo vinachipuka na ambavyo vina maonimengine. Makundi ya dini pia yaruhusiwe kusimamia shule zetu ili kuhakikisha ya kwamba maadili mema yanafunzwa katikashule hizo. Natarajia maoni haya pamoja na mengine, bwana mwenyekiti ambayo yametolewa na wanaKenya mbalimbali

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!