verbatim report of constituency public hearings ... - ConstitutionNet
verbatim report of constituency public hearings ... - ConstitutionNet
verbatim report of constituency public hearings ... - ConstitutionNet
Create successful ePaper yourself
Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.
47

naona. Lakini nyinyi wenyewe mfikirie, siku moja itafika, wewe mama wewe baba, watoto wako watakuuliza swali,

tulitengeneza tukatoa maoni yetu, kwa nini nchi yetu imetupitishia kwa ule moto tu, na zile shida zilikuwa hapo mbeleni. Hiyo

nimewatuma, mjaribu muone vile mambo yanayotolewa, ni ya kutawala nchi hii yetu bila ubaguzi na bila chochote cha

mapendeleo. Basi wacha niende kwa mambo yangu.

Jambo la kwanza ni mambo ya shida ya kuajiriwa kazi, ama lack of employment. Na ningesema kwa kifupi hivi, niseme kwa

kifupi badala ya tafsiri, itakuwa muda mrefu. (Speaks in Kikuyu),……………. Ukabila na undugu, na nyinyi ndio mko katika

pale top. Wale watoto wa masikini hawapati kazi, si ni kweli? Wale watoto wa matajiri wanachukuliwa mbele, hata kama

hawajahitimu mtihani sawa, sawa, anaendesha hiyo ofisi kubwa, kwa sababu baba yake ama mama yake ana uwezo. Ama

ndugu zake ama dada zake wana uwezo. Tunaomba sasa kwa Katiba mpya, muone kwamba hiyo imeondolewa, kusiwe na

ubaguzi kwa mtu yeyote, kazi ziajiriwe watu kulingana na vile wamepita. Wale hawajapita sawasawa watafutiwe mambo

mengine na serikali. Iwekwe katika Katiba.

Shida ya wale ambao wamesoma na wameacha masomo,- yaani school leavers.- Mapendekezo yangu ni hivi: wawe registered

na serikali, kama tu wangekuwa wameandikwa, kutoka standard seven ama eight, form four na university. Na wapewe kazi,

ama training kulingana na vile wamepita. Wale wamepita vizuri hata kama ni mtoto wa masikini, ama kama ni mtu kiwete,

apewe ile ofisi inalingana na yeye. Hiyo ndiyo maombi yangu. Yule anayebaki, kuna kazi ya polisi, kazi ya askari, kazi ya

labour, apatiwe huko, na uwe ni mzigo wa serikali maanake tumesema tumeomba masomo ya bure, kwa nini tupoteze wale

watoto wengine? Na zaidi wale wa masikini? Tunajua kweli, tukiulizwa maswali mengi, watoto wa masikini ni werevu, na

wengine wana akili sana na wanatupiliwa mbali, kwa sababu hawajulikani popote, tunaomba hiyo.

Wakiwa wanachukuliwa kwa register, tuondoe mzigo kutoka kwa wazazi wa watoto. Wakiwa wamemaliza masomo, ni wa

serikali. Mnaelewa vile ninasema? Huu mzigo wa mzazi mwingine ambaye hana elimu, asije akashughulike, nilitaka kumuuliza

nani; – M.P. wetu ni nani nishikilie atanisaidia ama ni ndugu yangu, - awe ni mtoto wa serikali. Apatiwe kazi kulingana na vile

alivyo. Kazi ni nyingi ya kupatia. Na asipotosheka kwenda university aende training, na asipotosheka training, aende kwa kazi

nyingine yeyote ambayo haihitaji watu wa masomo. Lakini kwa wakati huu tunajua, kuna ubaguzi.

Sitaendelea kujifafanua sana. Wacha nimalize hapo.

Mambo ingine, nimesema awe mzigo wa serikali. Ningependa muandike, mmeandika?

Interjection – laughter from the crowd.

Jambo lingine langu ni hili, nimezipeleka haraka sana. Ni mambo ya electon: Imezungumzwa sana. Ili tumalize mambo haya ya

wizi wa kura, Ningewaomba nyinyi Commissioners,- mimi huona ya kwamba, kutoka,- from now onwards, kwa ile election

inakuja karibu, tunafanya polling station hapa kama Njabini kwa hii ofisi. Zihesabiwe hapo, na agent wa yule mtu wa parliament,