verbatim report of constituency public hearings ... - ConstitutionNet
verbatim report of constituency public hearings ... - ConstitutionNet
verbatim report of constituency public hearings ... - ConstitutionNet
You also want an ePaper? Increase the reach of your titles
YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.
32

La pili, ni kuhusu umaskini: Ningependekeza kwamba, tuwe na sheria kwamba, watu ambao ni maskini watengewe angalau hata

kama ni mshahara kwa kila mwezi, wawe wakipewa pesa kila mwezi ya kuweza kuendeleza mahitaji yao ya mara kwa mara.

Kama nchi nyingi tunazo ambazo zinagharimia watu ambao hawajiwezi, ambao sisi hapa tunaita masikini. Wanaangalia masilahi

yao kwa kuwapa at least kila mwezi, kiwango fulani cha pesa ambazo zinaweza kufanya huyu mtu ajiendeleze katika maisha

yake ya kawaida.

Jambo la tatu ni kuhusu mashamba. Watu wengi wameongea kuhusu mashamba hapa, na ni jambo ambalo linagusia kila

Mkenya. Kuna mashamba mengi sana ambayo yanakaa bure; watu wamesema kwamba kuna wanyama ambao wakaa hapo.

Ndio, sio vibaya. Wanyama wanatuletea pesa kupitia kwa watalii, lakini kuna wengine ambao wana mashamba makubwa na ni

mtu mmoja pekee yake. Mimi ningependekeza kwamba, Commission hii irecord chini kwamba, Mkenya yeyote ambaye hana

shamba, ama wale ambao wanaitwa squtters, angalau serikali iangalie na iwape kila mtu acre mbili mbili, ili tusije tukawa na

squatters. Miaka arobaini tukijitawala, ni vibaya sana kuwa bado na jambo la squatters.

La nne ni kuhusu trespass. Hili neno trespass lilikuwa wakati wa ukoloni, na mkoloni alileta neno trespass kwa sababu hakutaka

uingie mahali pake wewe mtu mweusi. Lakini sasa saa hii sisi watu weusi wenyewe ndio tunajitawala, neno ‘trespass’

liondolewe kabisa katika Katiba ya Kenya. Mkenya awe huru, anaweza kuingia mahali popote na ahudumiwe. Ukienda mahali

pengine, kama vile reli, kule ukienda pale ndani ya reli, utaambiwa kwamba umekanyaga reli. Na hata ukikanyaga hiyo reli ni

chuma, haiumii lakini utaenda kushtakiwa. Kwa hivyo hiyo maneno ya trespass iondolewe, kila Mkenya awe huru kutembea

mahali popote.

La tano ni kuhusu elimu- education: Ni hivi tu mwaka huu tulitangaziwa na Rais wetu ya kwamba Primary education iwe free,

lakini sisi wazazi bado tunalipa. Ingekuwa bora iwe kwa Katiba kwamba,- na itiliwe maanani- kwamba elimu ya kutokea

standard one mpaka standard eight iwe ni free, na iwe ni free. Sio eti kwamba tunaambiwa ni bure, na hali sisi wazazi huku

tunaambiwa tutoe shilingi mia tano. Hiyo sio bure. Kwa hivyo iwe ni elimu ya bure, vile tulikuwa tukisoma tu zamani. Zamani sisi

tuliposoma, hakuna siku tuliambiwa kwamba utanunua ruler, utanunua vitabu, hivyo vitu ulikuwa ukivipata darasani, mpaka

rubber unapata. Lakini siku hizi tunaambiwa elimu ni ya bure, lakini mtoto kesho anakuja anakwambia kwamba baba,

nimefukuzwa school fees, unashindwa hii school fees mnasema ni ya bure, inatokea wapi. Tafadhali elimu kama ni ya bure, iwe

ndani ya Katiba ni ya bure.

Jambo la sita,- na nitamalizia hapo-, ni kuhusu vyama vya upinzani. Mimi ninapendekeza kwamba tuwe na vyama vya upinzani

vitatu vyenye nguvu. Vitatu pekee yake vyenye nguvu. Hivi vyama vingine vyote vifagiliwe viwekwe kando. Na hivi vyama

vitatu, serikali iwe ikivigharimia tukienda kwa uchaguzi. Na hiyo pia, tukiwa na vyama vichache kama hivyo, tutapoteza ile neno

ambalo kila wakati tunaimbiwa: “ukabila”. Kwa sababu tukiwa na vyama vitatu, tutajumuisha makibila arobaini na mbili yote ya

Kenya na ambapo neno ‘ukabila’ litapotea. Ukabila unatokea kwa sababu, vyama ni vingi na kila kabila kitakuwa na chama