09.03.2013 Views

verbatim report of - ConstitutionNet

verbatim report of - ConstitutionNet

verbatim report of - ConstitutionNet

SHOW MORE
SHOW LESS

You also want an ePaper? Increase the reach of your titles

YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.

Edward Aringo: Mimi naweza kupiga asante kwa serikali ya Kenya kuanza mtindo mpya kama huu...

Com. Nunow: Majina yako kwanza, na ukaribie microphone.

Edward Aringo: Jina langu ni Edward Aringo. Nashukuru serikali kufunguka na hii serikali kufunguka ni Mungu ndiye anatoa

mwangaza. Siku Kenya ilipata uhuru, 1963 December, ilikuwa furaha mingi, wakapea President authority and power. Hii ndio

ilikuwa kitu kibaya cha kwanza kumpa Kenya, ikijua namna ya kuendesha serikali. Maana nataja Mungu, amekwisha ona watu

wengi wanaumia. Na yeye ndiye aliumba watu, ndio akatoa mwangaza waanze sheria kuwa kila kitu ikuwe inatumiwa na

sheria. Wananchi wake wafurahie matunda ya uhuru. Kwa maana siku hizi, ni watu wachache wanao furahia matunda ya

uhuru. Maanake katika Kenya a ¼ ya watu katika Kenya wanafurahia matunda ya na ¾ wana-suffer.

Ya pili ni hii; Ukienda katika location, mshtakiwa anatakiwa atoe pesa kwa sub-chief, na yule mwenye kushtaki pia atoe. Sasa

utajua ni nani ameshtakiwa?

Na kwa koti naona mtu mmoja ndiye anashtaki mtu kwa makosa, na huyo mshtakiwa halipi tena kwa koti. Hii ni kinyume cha

sheria na inafanyika, na watu wengi wanaumia. Na pengeni usipotoa wanasema tunahimiza kesi yako haiwezi kufanyika, na

wewe ndio ulishtakiwa. Ndio maanake nashukuru hii sheria mpya ikuwe inaendesha vitu katika sheria bila kufikiria au

kuonyesha mapendeleo.

Ya pili, nasikia watu wanataja mambo ya chang'aa, pombe na polisi Hii sheria nataka ikuwe hivi, polisi wakija kufanya

inspection katika nyumba ya mtu, aliiba chupa au aliiba jembe, wasije kuhangaisha mwenye nyumba ati kila kitu mtu wanataka

receipt, alinunua namna gani. Ikuwe sheria wanakuja kwa ile kitu kinasikika aliiba. Kwa maana wanaingia katika nyumba,

wengine wanachukua yule bwana wanamtia nje kwa room ya kukaa, na wengine wanaingia katika bedroom, wanachafua vitu

huko kumbe hao ndio wanaiba hivyo vitu. Hiyo yote nashukuru, serikali itie katika sheria. Wakija kutafuta jembe ikuwe

jembe. Hapana radio, leta receipt, kitu fulani, lete receipt, hapana.

Ya tatu, katika Bunyore hapa, nasikia wanazungumuza mambo ya Bunyore na Nyanza. Miaka miwili imepita Luanda county

council ilipewa kuzunguka six square miles kutoka Luanda. Wakaanza kutia signboard pale mileage inafika. Na watu wa

Nyanza waling'oa hiyo signboard, wakatupilia mbali. Nikashindwa kujua hiyo kitu walitia halali au walitia kufuatana na sheria.

Kwa sababu walinyamaza. Kama walijua walipewa six square miles, mpaka saa hii, sijaona hiyo signboard. Mimi ni mtu wa

katikati ya mpaka wa Nyanza na Western.

Ya nne...

Com. Nunow: (Inaudible).

74

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!